Chou cha ufundi Veta-DSM chashindwa kuendesha mafunzo

kyoga

Member
Sep 16, 2011
31
11
Nijambo la kusikitisha kuona wanafunzi wanakosa haki yao ya kufundishwa eti ni kwa sababu ya chuo kimeshindwa kuagiza malighafi ya kufundishia kwa wakati, hadi hii leo wanafunzi hawajafundishwa toka wafungue chuo julai mwaka huu kwasababu ya kukosa malighafi ya robo ya kwanza na hii ni robo ya pili ya mwaka kwa sababu ambazo hazina msingi wowote, hadi mkuu wa chuo anadiriki kusema swala la uagizaji malighafi limemshida kabisa haliwezi, wakati yeye ndiye aliyeteuliwa na mamlaka kusimamia shughuli zote za chuo, mkurugezi mkuu wa veta analijua hili kwa kipindi kilefu lakini ameshindwa kuuwajibisha uongozi wa chuo kwa kosa la kuto agiza malighafi kwa muda muafaka wakati tatizo siyo pesa ila ni ukwasi wa chuo. je kwa jinsi hii kweli vijana wetu tutawasaidiaje?. Kuna wanafunzi wanatakiwa wafanye mtuhani mwezi wa 12 lakini hadi hii leo hawaja soma kutokana na tatizo la kukosa malighafi ya kufundishia.
 
Tanzania haichezi kama pele na haina mipango kama kanisa katoliki!!! Ndo hayo ya veta wakati ni chuo muhim kwenye nchi kama hii
 
Back
Top Bottom