Chopa ya JWTZ yaanguka na Kuua..

kama ni hivyo ufisadi una gharama zake! ni vema tukaungana sASA KATIKA NYANJA ZOTE KUUPIGA VITA, HAKUNA ALIYE SALAMA
 
Phillemon... kwanini unafikiri ni "chopa" hiyo? Nilikuwa na mawazo hayo lakini sina pa kuanzia.. kwanini isiwe ni nyingine..


mwanakijiji ....baada ya vita vya kagera ..jeshi halikubakiwa na helicopter nzima ...zote walizokuwa nazo zilikuwa grounded...zikihitaji overhaul kutoka urusi ...bahati mbaya cccp ikavunjika ...ikashindikana....jeshi lilinunuliwa helicopter 6 mwaka 2004 ,kati ya hizo hadi leo huyu mjanja ameleta 4 tu... 3 bado hajazileta...na wakanunuliwa transport DC 10 airfreght 2 zinazobeba watu 120 kila moja....kabla ya hapo helicopter pekee zilizokuwa zimebakia zilikuwa za polisi 3 ...zote zilinunuliwa enzi ya mwalimu...na hadi majuzi polisi walikuwa wamebakiwa na moja anayotumia afande TOSSI...baada ya ile ya kiooo kuwa grounded...

ile ndege iliyoanguka KIZOTA tulipewa msaada na mfalme wa saudi arabia mwaka 2004....inatoka IRELAND ....labda tuseme wa saudi arabia walitupa zawadi ndege WRITTEN OFF....

ISHU YA HELICOPTER INAUMA SANA ....NA HILI LAZIMA MAOFISA WA NGAZI ZA JUU ZA JESHI WANAOHUSIKA NA QUALITY ASSUARANCE washitakiwe COURT MARTIAL ....vipi walikubali kupokea helicopter ya kiraia kwa kazi za kijeshi...wakati yule supplier kutoka uarabuni alikuwa tayari kutuuzia GUNSHIP HELICOPETERS ..THE LATEST MILLITARY VERSION....wakamkatalia!!!!!
 
Phillemon.. bado jeshi letu sidhani kama liko fully to a civilian control. Hivi majuzi Waziri wa Majeshi wa US Gates amewafukuza kazi majenerali kwa uzembe... hivi leo Hussein Mwinyi ana ubavu wa kumwajibisha yeyote?
 
Phillemon.. bado jeshi letu sidhani kama liko fully to a civilian control. Hivi majuzi Waziri wa Majeshi wa US Gates amewafukuza kazi majenerali kwa uzembe... hivi leo Hussein Mwinyi ana ubavu wa kumwajibisha yeyote?[/QUOTE]

Akithubutu atazabwa vibao hadi ashike adabu!!!! Bongo wajeshi wanajiona miungu watu......when in reality they are humans just like the rest of us.
 
loh my tanzania,ufisadi kila konaaaa??!!hadi angani nako kuna ufisadi?!duh sasa wapi kuko salama jamani?!!
 
Phillemon.. bado jeshi letu sidhani kama liko fully to a civilian control. Hivi majuzi Waziri wa Majeshi wa US Gates amewafukuza kazi majenerali kwa uzembe... hivi leo Hussein Mwinyi ana ubavu wa kumwajibisha yeyote?

Thubutu?! ajaribu akione cha moto.
Hata hivyo jamani wafiwa nawapa pole kwa msiba huu mzito.
 
Phillemon.. bado jeshi letu sidhani kama liko fully to a civilian control. Hivi majuzi Waziri wa Majeshi wa US Gates amewafukuza kazi majenerali kwa uzembe... hivi leo Hussein Mwinyi ana ubavu wa kumwajibisha yeyote?

.......kinachochangia ufisadi jeshini ...ni huu usiri ..nashangaa jeshi la marekani au russia wako wazi..wakinunua MISSILE inajulikana walau hata kama ni siri vipi bunge kupitia DEFENCE AND SECURITY watakuwa briefed and it is up for scrutiny....

..nchi hii ingalikuwa pesa zinazotengwa kununua zana kila mwaka kwa mabilioni zinatumika inavyopasa leo hii tungelikuwa na kila kitu na hata vita ingetokea ghafla tusingenunua hata tairi la gari..kila kitu kingekuwa AMALI....lakini hapo kwenye zana imedhibitika ndipo ufisadi umejaa...KWA HIZI CHPPER KUDONDOKA KAMA PANZI....majirani wetu wote wana helicopter nzuri ...tena nyingi zinazobeba hadi askari 30 kwa wakati mmoja....sisi zetu mbovu na hazibebi zaidi ya watu 8 ...kama kenya wanayo hadi presidential air force fighter chopper ..ambayo humbeba rais wao wakati wa peak time ku avoid traffic jam au kuendea remote areas.......sasa assume hiyo yetu ingekuwa imembeba MUHASHIMIWA RAIS INGAKUWAJI...sometimes hukatumia..

lazima utafiti ufqanywe..tupewe helicopter mpya 6....waliokufa wafidiwe..na maafisa waliozidhibitisha WAFUNGWE!!!!
 
Phillemon.. bado jeshi letu sidhani kama liko fully to a civilian control. Hivi majuzi Waziri wa Majeshi wa US Gates amewafukuza kazi majenerali kwa uzembe... hivi leo Hussein Mwinyi ana ubavu wa kumwajibisha yeyote?


I am always amazed na resilience uliyonayo mwenzetu

endelea na moyo huo huo nchi inawategemea watoto wa Kijamaa kama wewe. Sie wengine tuko njiani kuachia ngazi
 
Phillemon.. bado jeshi letu sidhani kama liko fully to a civilian control. Hivi majuzi Waziri wa Majeshi wa US Gates amewafukuza kazi majenerali kwa uzembe... hivi leo Hussein Mwinyi ana ubavu wa kumwajibisha yeyote?

Mwanakijiji!, nadhani kumbukumbu zangu za vyombo vya habari vya marekani vinaonyesha kwamba Majenerali wale wa US Airforce (one Maj. Gen. + Civilian US Airforce Secretary) hawakufukuzwa, bali walijiuzulu wenyewe kwa kuwajibika kufuatia kashfa hiyo ya uzembe iliyopelekea mabomu ya nyuklia kusafirishwa kwa ndege B-52 na kupelekwa Taiwan kwa makosa na bila marubani kuwa na taarifa.

Kuna tofauti ya kufukuzwa na kuwajibika (I am right?)
 
Inasikitisha sana kusikia upotevu wa maisha ya watu bila ya sababu za msingi.

Kwa maelezo ya mkuu FM, inaonesha kamba tatizo hapo ni la kiufundi, kwamba huwezi ukaiweka helicopter hewani kwa muda mrefu bila mapumziko, helicopter ambayo kwanza, zimenunuliwa zikiwa zimekwishatumika na pili hazifai kwa kazi ya kufanya doria kwa wiki nzima au zaidi bila ya kupumzishwa na kufanyiwa uchunguzi (maintenance).

Kuna maaswali mengi najiuliza.

Je helicopter hizo zinazunguka maili ngapi kwa saa na ni kiasi gani cha mafuta kinaunguzwa?

Shughuli za Sullivan ndizo kweli zimeiangusha hio helicopter? Je ingekuwaje kama shughuli hio ingedumu kwa mwezi mzima?
 
Mwanakijiji!, nadhani kumbukumbu zangu za vyombo vya habari vya marekani vinaonyesha kwamba Majenerali wale wa US Airforce (one Maj. Gen. + Civilian US Airforce Secretary) hawakufukuzwa, bali walijiuzulu wenyewe kwa kuwajibika kufuatia kashfa hiyo ya uzembe iliyopelekea mabomu ya nyuklia kusafirishwa kwa ndege B-52 na kupelekwa Taiwan kwa makosa na bila marubani kuwa na taarifa.

Kuna tofauti ya kufukuzwa na kuwajibika (I am right?)

Hapana.

Kuwajibika na kujiuzuku kuna kutokufafana kusiko na tofauti, au distinction without a difference. Wenyewe wanaita "requested resignation."

Yule mura, Generali Moseley, na mwezake waliombwa kiustaarabu, watoweke wenyewe jeshini haraka iwezekanavyo! Ukikataa kujiuzulu unafukuzwa na ukijiuzulu maana yake umejiondokea mwenyewe kwa kufukuzwa. Ukikimbia nchale, ukisimama nchale. Yaani, lala chini!

Kwa hiyo walifukuzwa kwa kujiuzulu!

Air Force's top leaders are fired
Defense Secretary Robert Gates cites errors in caring for the nuclear arsenal.

By Julian E. Barnes and Peter Spiegel,
Los Angeles Times June 6, 2008



39657649.jpg


Air Force Secretary Michael Wynn, left, with Air Force Chief of Staff Gen. Michael Moseley,
testifies on Capitol Hill in Washington in March. They were fired today by Defense Secretary Gates.


WASHINGTON -- In an unprecedented action in a time of war, Defense Secretary Robert M. Gates simultaneously fired the civilian and military leaders of the Air Force on Thursday, saying that oversight standards for the U.S. nuclear arsenal had deteriorated on their watch.

The immediate reason for the requested resignations of Gen. T. Michael "Buzz" Moseley, the Air Force chief of staff, and Air Force Secretary Michael W. Wynne was a report on the accidental shipment of nuclear triggers to Taiwan.

http://www.latimes.com/news/la-na-airforce6-2008jun06,0,2409700.story?track=rss
 
hii chopa imeangushwa na watu wa ccm au ?? kama ndio basi mie najiunga chadema sasa hivi !

......there is no reason to think or say kuwa chopper imeangushwa kwa uzembe wa serikali ya ccm ,no way..as long as we know ..jeshi is an independent entity ..ambapo wanao wataalamu wa kununua vifaa wanavyoitaji ..kwa kadiri ya uwezo wa nchi na technolojia ya kivita iliyopo na at no point wanapoweza kulazimishwa kununua zana na maafisa wa kiraia unless kuna corrupt situation....huu msalaba ni wa jeshi na lazima maafisa husika wawajibike...malalamiko kuhusu hizi chopper yalikuwapo miongoni mwa maafisa wa ngazi za chini na kati tangia zinakuja ....wengi wakisema VITHLANI amechomeka chopper za kiraia ...wakati mahitaji ni za kijeshi zenye uwezo wa kujipanga kimapigano na usafirishaji!!!

.....nchi nyingi duniani maafisa wa kijeshi hufanya ufisadi wa OVERPRICING....lakini NO COMPROMISE WITH QUALITY...kwani quality ikiwa mbovu ni kifo.....sasa maafisa waliokwenda kufanya pre shipment inspection kwa influence wanayoijua ...waliamua ku CMPROMISE TO POOR QUALITY AND SPECIFICATIONS....sasa tazama wanauwa wenzao...poor men!!!
 
Katika kila helicopter ama ndege ya kijeshi inayoanguka TZ tunaambiwa kulikuwa na fundi ndani. Hivi jamani hamuoni kuna matatizo hapa? Tunatumia technology ya karne gani mpaka kuweka fundi katika kila helicopter ama ndege za jeshi? Do we have maintenance plans ama quality assurance systems in place kwa kweli? Maana, kama kweli kuna hivyo vitu, then matatizo yote ambayo yanayotufanya tuambatane na mafundi kila mara ndege/helicopter zinaporuka, yangeweza gunduliwa in advance.

Nakubali sisi ni wadanganyika. Ila kwa mwendo huu, I think we are more than wadanganyika.

Jeshi linabidi liweke fresh blood ili waweze ku-update systems zao. Kuendelea kuwakumbatia waliopigana vita ya Kagera hata kama hawana mapya, ndio kunasababisha hata helikopta "mpya" ziwe treated as "spana mkononi" na kuruka na fundi mida yote. Jeshi lingekuwa more efficient kama wange-develop quality systems zinazoendana na wakati; Haya yote yatawezekana kama wakiajiri qualified new blood. Tusiseme kwamba hawapo; Wapo wengi tuu.. Wengine wamejichimbia kwa "Uncle Joji" kama senior engineers kwenye jeshi.. Tunawafahamu....

Hussein Mwinyi, tunakuelewa kwamba wewe ni mwanasayansi... Endesha wizara na jeshi kisayansi mkuu. We know you can.
 
Helikopta ya Jeshi la Wananchi Tanzania yaua sita Arusha
*Ni ile iliyokuwa ikifanya doria wakati wa Sullivan
*Iliwaka moto na kutetea angani


Na Mussa Juma, Arusha


HELKOPTA ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), iliyokuwa inafanya doria wakati wa Mkutano wa Leon H Sullivan katika maeneo mbalimbali ya Arusha imeanguka jana mchana na kuua watu sita, wanne miongoni mwao wakiwa wanajeshi.


Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Matei Basilio alithitibisha jana kutokea kwa ajali hiyo katika eneo la Matevesi Wilayani Arumeru jirani kidogo na Uwanja Mdogo wa Ndege wa Arusha na kueleza kuwa watu wote sita waliokuwemo kwenye helikopta hiyo wamekufa.


''Ninachoweza kusema sasa ni kweli ajali hiyo imetokea na wote sita wamefariki baada ya helikopta hiyo kuwaka moto baada ya kuanguka,'' alisema Basilio.


Kamanda Basilio alisema kuwa helikopta hiyo ilianguka ikiwa safarini kwenda Dodoma jana baada ya kumaliza kazi maalum ya kuimarisha ulinzi wakati wa mkutano wa Leon H Sullivan.


Hata hivyo, Kamanda Basilio alisema majina ya wanajeshi ni kanali Makele, Meja Sinda, Luteni Kirunga na PT Mambe. Wengine ni mtoto mdogo Diana Mzirai na Irine Jitenga. Miili yote imehifadhiwa chumba cha maiti cha Hospitali ya Mount Meru jijini Arusha.


Baadaye taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari Makao Makuu ya Jeshi ilisema helkopita hiyo ya JWTZ yenye namba 9507 iliyokuwa inarejea Dar es Salaam, ilianguka saa 6.40 mchana katika eneo la Oljoro nje kidogo ya Jiji la Arusha.


Taarifa hiyo ilitaja waliofariki katika ajali hiyo ni marubani wawili, mafundi ndege wawili na abiria wawili. Ndege hiyo ilikuwa kati ya ndege mbili zilizokuwa zikitumika kwa shughuli za ulinzi, wakati wa mkutano wa Sullivan.


''Uchunguzi kuhusu ajali hiyo umeanza kufanyika kwa ushirikiano kati ya JWTZ na vyombo vingine,'' ilisema taarifa hiyo.


Umati wa wakazi wa Arusha jana walikuwa wakihaha kupata taarifa za tukio hilo na kupiga simu mara kwa mara kwa waandishi wa habari hasa kutokana na kutotolewa mapema taarifa kamili za tukio hilo.


Tukio hili limekuja wakati bado wakazi wa Arusha, hawajasahau heka heka za ndege hiyo iliyokuwa ikiranda juu ya anga wakati wote wa mkutano wa Leon H Sullivan.


Juni 3 mwaka jana, watu 13 walijeruhiwa katika ajali ya ndege ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yenye namba JW 9036 iliyoanguka eneo la Kizota mjini Dodoma baada ya kupata dhoruba angani.


Ndege hiyo aina ya SD33 Sherpa, yenye uwezo wa kubeba abiria 40 ilianguka saa 7:20 mchana katika eneo hilo baada ya injini zake mbili kushindwa kufanya kazi.
 
Tanzania nayo sasa itageuka kama DRC kwa kutumia ndege zilizo zeeka na kuzifanyia matengenezo yaani service lazima ufisadi ufanyike wa kupiga panga fedha za service sasa hapo hiyo chopa itaruka kweli>??na hata ikiruka siku zake zitakuwa zinahesabika tu lazima ije iue tu.Chopa kibao zimesha jifia kilicho baki ni kuleta vilio tu kwa wa TZ.
 
Mungu awaweke mahali pema peponi. Hatuna miundo mizuri ya uokoaji,na hilo pia ni tatizo chukulia mfano mzuri tu wa zimamoto. Yaani ni kama hawapo. Kwa hiyo hata wale wanaojiita mafisadi na wengineo wakiwa kwenye hayo madege especially hizi za domestic wajue roho ni mkononi. Nadhani wakati umefika wa kukifanyia overhaul kikosi cha zimamoto pamoja na kuweka mifumo madhubuti wa uokoaji.
 
Chopa yenyewe iliyo kula mweleka hii hapa chini.
JWTZ chopa.jpg
Hapa ikiwa uwanja wa ndege Arusha saa chache kabla ya kuanguka.
 
Kutoka kwenye website (http://www.haki-hakingowi.blogspot.com) ya HAKI NGOWI kumewekwa majina yanayosemwa ndiyo ya marehemu wa janga hili. Nami naitundika tu kama nilivyoiona. Ni tumaini langu kuwa ni habari za kweli kwani zimekuwa quouted toka kwa Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Matei Basilio.


Helikopta ya JWTZ yaanguka,
Yaua 6..


HELKOPTA ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), iliyokuwa inafanya doria wakati wa Mkutano wa Leon H Sullivan katika maeneo mbalimbali ya Arusha imeanguka jana mchana na kuua watu sita, wanne miongoni mwao wakiwa wanajeshi.

Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Matei Basilio alithitibisha jana kutokea kwa ajali hiyo katika eneo la Matevesi Wilayani Arumeru jirani kidogo na Uwanja Mdogo wa Ndege wa Arusha na kueleza kuwa watu wote sita waliokuwemo kwenye helikopta hiyo wamekufa.

''Ninachoweza kusema sasa ni kweli ajali hiyo imetokea na wote sita wamefariki baada ya helikopta hiyo kuwaka moto baada ya kuanguka,'' alisema Basilio.

Kamanda Basilio alisema kuwa helikopta hiyo ilianguka ikiwa safarini kwenda Dodoma jana baada ya kumaliza kazi maalum ya kuimarisha ulinzi wakati wa mkutano wa Leon H Sullivan.
Hata hivyo, Kamanda Basilio alisema majina ya wanajeshi ni kanali Makele, Meja Sinda, Luteni Kirunga na PT Mambe. Wengine ni mtoto mdogo Diana Mzirai na Irine Jitenga. Miili yote imehifadhiwa chumba cha maiti cha Hospitali ya Mount Meru jijini Arusha.Habari na Juma Musa/Arusha.


Source: http://www.haki-hakingowi.blogspot.com/
 
Back
Top Bottom