Chonde chonde wabunge wangu wa CHADEMA

Ikiwa bado siku 5 kuanza kwa bunge la bajeti, ni masikitiko makubwa kwa wakazi wa majimbo ya
1. Kawe,
2. Mbeya Mjini
3. Hai
4. Nyamagana
5. Ubungo,
6. Singida Mashariki

Wabunge wa majimbo husika wameshindwa kukutana na wananchi ili kupata maoni yao kuyafikisha bungeni BADALA yake wametumia pesa na marupurupu yatokanayo na ubunge kufanya mikutano ya chadema nje ya majimbo yao.
Tafadhali wabunge wa majimbo niliyoyataja geukeni nyuma na kukumbuka nyinyi ni wawakilishi wa wapiga kura ambao mnatakiwa kuweka mbele mahitaji ya wapiga kura. BADILIKENI mtumikie wana jimbo wenu!!

Kila siku twawasikia kiguu na njia mara Mtwara, Masasi, Newala wakati Sugu ukitamba Dar Live badala ya kupita maeneo ya Mwanjelwa, Soweto, masite nk. kuongea na wapiga kura; HIYO NI HAKI, MTAFAKARI!!!

TEMBELEA Joseph Mbilinyi (Mr II - SUGU) halafu simuoni zitto hapo kwenye list, yeye alishakutana na wananchi?
 
Ikiwa bado siku 5 kuanza kwa bunge la bajeti, ni masikitiko makubwa kwa wakazi wa majimbo ya
1. Kawe,
2. Mbeya Mjini
3. Hai
4. Nyamagana
5. Ubungo,
6. Singida Mashariki

Wabunge wa majimbo husika wameshindwa kukutana na wananchi ili kupata maoni yao kuyafikisha bungeni BADALA yake wametumia pesa na marupurupu yatokanayo na ubunge kufanya mikutano ya chadema nje ya majimbo yao.
Tafadhali wabunge wa majimbo niliyoyataja geukeni nyuma na kukumbuka nyinyi ni wawakilishi wa wapiga kura ambao mnatakiwa kuweka mbele mahitaji ya wapiga kura. BADILIKENI mtumikie wana jimbo wenu!!

Kila siku twawasikia kiguu na njia mara Mtwara, Masasi, Newala wakati Sugu ukitamba Dar Live badala ya kupita maeneo ya Mwanjelwa, Soweto, masite nk. kuongea na wapiga kura; HIYO NI HAKI, MTAFAKARI!!!

Wewe uliwachagua kupitia majimbo hayo wakati kura ilikuwa siku moja? Hangaika na maisha yako mwenyewe, Wabunge unaowasema wanafanya kazi za kibunge sehemu wanapoenda ila kwa UELEWA wako mdogo hujui kinachofanyika.
Maisha magumu hayapo kwenye majimbo uliyotaja ndio maana wanaenda kama timu kuelezea hali halisi kwa Watanzania, labda wewe mbunge wako amekufanyia nini tangu achaguliwe?
 
MAFILILI, hii issue lazima tuiangalie kwa darubini, jamaa wamekuwa watalii, unajua ile michango yetu ya toka Arumeru imewachanganya sasa kila mbunge anataka apate gawio.

Jamaa wamekuwa watalii. yaani 2015 ni mbali sana, majaribio ya kuchagua upinzani yanatutokea puani.
Nina mashaka na utafiti wako kwani
mbuge wangu SUGU wa Mbeya Mjini amezunguka karibu vitongoji vyote vya jiji la Mbeya akifanya mikutano ya hadhara, akiulizwa maswali na kuyajibu

labda kwa taarifa yako hawa jamaa wa CDM wako busy sana wao muda wote wapo kazini ili kuwaelimisha watanzania hawana muda wa kupoteza.
 
Mkuu wangu, ingawa mimi si CCM ni mwanachama wa ADC, ila unapaswa uelewe kuwa system ya CCM ni tofauti sana na vyama vingine, wana hadi mabalozi wa nyumba 10, kwa hiyo mfumo wa mawasiliano wa hiki chama ni tofauti na vyama vingine.
mkubwa!mtajificha mwaka huu,umeanza kukikana chama chako mchana kweupe,na bado mpaka mtakimbia nchi
 
Mbunge wa Bahi (Badwel?) yuko jimboni mwake, au unataka kusema alichaguliwa na mahabusu na wafungwa wa Ukonga?
 
MAFILILI, hii issue lazima tuiangalie kwa darubini, jamaa wamekuwa watalii, unajua ile michango yetu ya toka Arumeru imewachanganya sasa kila mbunge anataka apate gawio.

Jamaa wamekuwa watalii. yaani 2015 ni mbali sana, majaribio ya kuchagua upinzani yanatutokea puani.

Nape kakupa sh. ngapi?
 
Last edited by a moderator:
Kuna ofisi za wabunge ambapo ndio sehemu ya kupeleka kero na matatizo,kisha hupewa mbunge na kuyafanyia kazi.....hata kama ni mkutanoni bado wa kuchukua kumbukumbu ya kero zilizotajwa ni katibu wa mbunge!
Kwetu ubungo,tuna utaratibu wa kufikisha kero zetu.
Afterall,mbunge wetu yuko active hata online na ameshachelewa bungeni mara nyingi kwa kutatua kero jimboni kwanza....hivi karibuni ameongea na kiongozi wa jumuiya ya bodaboda na kuahidi kukutana nao mapema kabla ya kikao cha bunge!
Huyu ndie JJ Mnyika!
 
Mkuu wangu, ingawa mimi si CCM ni mwanachama wa ADC, ila unapaswa uelewe kuwa system ya CCM ni tofauti sana na vyama vingine, wana hadi mabalozi wa nyumba 10, kwa hiyo mfumo wa mawasiliano wa hiki chama ni tofauti na vyama vingine.

Mabalozi wametengwa na wala hawajui chochote kuhusu chama zaidi ya kununuliwa pombe kiongozi akipita....kuna ugumu wa kupitisha maazimio bungeni kwa upinzani na hii inatokana na uchache wao,hivyo wanakijenga chama kiwe na mizizi ila walau next election wawe wengi kupangua hoja bungeni kwa manufaa ya Taifa....tofauti na ugumu wanaopata sasa kutokana na wingi wa wanaozomea tuuuuu!
 
Ungemshauri na kikwete apunguze safari za nje maana toka awe rais ameenda kigoma mara moja ila usa mara mia.
 
Badala ya kuwashangaa wabunge wa CDM ungemshangaa kwanza Mh. NAHODHA Waziri wa Ulinzi ambaye ni mwakilishi kule ZNZ. Kwanza haishi ZNZ anaishi DSM miezi yote. Pili wakati vikao vya baraza la wawakilishi, Yeye anakuwa Dodoma kuhudhulia vikao vya bunge la JMT. Je hao wananchi wake wanawakilishwa nani kwenye BLW?
 
MAFILILI, hii issue lazima tuiangalie kwa darubini, jamaa wamekuwa watalii, unajua ile michango yetu ya toka Arumeru imewachanganya sasa kila mbunge anataka apate gawio.

Jamaa wamekuwa watalii. yaani 2015 ni mbali sana, majaribio ya kuchagua upinzani yanatutokea puani.

Huyu sasa ndiye ameshindwa kufichama kabisaaaaa. Magamba at work, live! Wabunge tajwa wanashughulika na maslahi mapana ya nchi. Nchi hii inahitaji ukombozi muhimu kutoka mikononi mwa magamba. Na 'majembe' yaliyotajwa ndiyo yako kazini tena kwa kujitolea. Juhudi zenu Magamba kutaka kuwakatisha tamaa wapiganaji hawa, nakuapia hakiyamama, hazitafanikiwa kamwe! Shame upon you, pambaf!!!!
 
Nadhani huyu mtoa maada hajui anachozungumza, namuona kama hajafurahishwa na kazi wanayofanya wabunge hao huko, ninapenda kukutaarifu kwamba wabunge wa mkoa wa dar es salaam kwa tiketi ya chadema kupitia kwa katibu wao john john mnyika siku ya tarehe 26 pale jangwani a.k.a chadema squire alijiridhisha kwa wananchi tena akasema namnukuu "nikiwa kama katibu wa wabunge mkoa wa dar es salaam napenda kuwaomba wananchi mturuhusu kwenda kwenye oporesheni lindi na mtwara, mnaokubali kwamba wabunge wa chadema twende mtwara na lindi nyosheni mikono juu" kwa mantiki hiyo walipata political legality sasa tatizo ni nini?
Pili, wanachama na wapenzi wa chadema tunajua kuwa wabunge wetu hufanya kazi nchi nzima lakini pia wakiwa bungeni tunajua uwezo wao na wanajua ni nini matatizo ya wananchi wao.
Tatu, viongozi wabunge wa ccm na cuf, tlp na vyama vingine wamekwenda kwa wananchi wao au tunatazama kwa cdm tu?
Mwisho nakupongeza kwa kukubali kwamba wanaotakiwa kutatua matatizo ya wananchi ni wabunge wa chadema tu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Ikiwa bado siku 5 kuanza kwa bunge la bajeti, ni masikitiko makubwa kwa wakazi wa majimbo ya
1. Kawe,
2. Mbeya Mjini
3. Hai
4. Nyamagana
5. Ubungo,
6. Singida Mashariki

Wabunge wa majimbo husika wameshindwa kukutana na wananchi ili kupata maoni yao kuyafikisha bungeni BADALA yake wametumia pesa na marupurupu yatokanayo na ubunge kufanya mikutano ya chadema nje ya majimbo yao.
Tafadhali wabunge wa majimbo niliyoyataja geukeni nyuma na kukumbuka nyinyi ni wawakilishi wa wapiga kura ambao mnatakiwa kuweka mbele mahitaji ya wapiga kura. BADILIKENI mtumikie wana jimbo wenu!!

Kila siku twawasikia kiguu na njia mara Mtwara, Masasi, Newala wakati Sugu ukitamba Dar Live badala ya kupita maeneo ya Mwanjelwa, Soweto, masite nk. kuongea na wapiga kura; HIYO NI HAKI, MTAFAKARI!!!
Mkuu Mafilili, mbona unawasahau wapiga kura wa jimbo la Bahi ambao mbunge wao badala ya kwenda kuchukua hoja zao azipeleke bungeni yeye akaishia Mkuranga kwa mama Spora Liana kumdai rushwa ya milioni! au tuseme ile milioni ya rushwa angeitumia kuleta maendeleo ya jimbo la Bahi?
 
Silence is sometimes the best answer.Mijitu kama hii si yakuielimisha dawa yao ni M4C.Hizi ni propaganda watuweke busy tusiendelee kupokea kadi za Magamba.
 
mafilili, hii issue lazima tuiangalie kwa darubini, jamaa wamekuwa watalii, unajua ile michango yetu ya toka arumeru imewachanganya sasa kila mbunge anataka apate gawio.

Jamaa wamekuwa watalii. Yaani 2015 ni mbali sana, majaribio ya kuchagua upinzani yanatutokea puani.

wewe fisadi umemchagua nani?acha longolongo zako.
 
Last edited by a moderator:
Fuatilia bunge kwa makini ndio utajua nani anawakilisha wananchi kwa dhati..
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom