Chonde chonde wabunge wangu wa CHADEMA

MAFILILI

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
2,377
1,194
Ikiwa bado siku 5 kuanza kwa bunge la bajeti, ni masikitiko makubwa kwa wakazi wa majimbo ya
1. Kawe,
2. Mbeya Mjini
3. Hai
4. Nyamagana
5. Ubungo,
6. Singida Mashariki

Wabunge wa majimbo husika wameshindwa kukutana na wananchi ili kupata maoni yao kuyafikisha bungeni BADALA yake wametumia pesa na marupurupu yatokanayo na ubunge kufanya mikutano ya chadema nje ya majimbo yao.
Tafadhali wabunge wa majimbo niliyoyataja geukeni nyuma na kukumbuka nyinyi ni wawakilishi wa wapiga kura ambao mnatakiwa kuweka mbele mahitaji ya wapiga kura. BADILIKENI mtumikie wana jimbo wenu!!

Kila siku twawasikia kiguu na njia mara Mtwara, Masasi, Newala wakati Sugu ukitamba Dar Live badala ya kupita maeneo ya Mwanjelwa, Soweto, masite nk. kuongea na wapiga kura; HIYO NI HAKI, MTAFAKARI!!!
 
magamba at work.....kazi wanyofanya ni zaidi ya kupokea maoni.....
 
MAFILILI, hii issue lazima tuiangalie kwa darubini, jamaa wamekuwa watalii, unajua ile michango yetu ya toka Arumeru imewachanganya sasa kila mbunge anataka apate gawio.

Jamaa wamekuwa watalii. yaani 2015 ni mbali sana, majaribio ya kuchagua upinzani yanatutokea puani.
 
Last edited by a moderator:
Magamba bwana. Hasara tupu. Nipo jimbo linaloongozwa na Gamba. Mara ya mwisho kuonekana huku ni mwaka jana mwezi wa 9.. Na siku hyo aliwapelekea mipira mitatu ya soka..

Wabunge wa Chadema wote wamekuwa wakiu2mia muda mwng majimboni kwao. Na hata jnc walvyo kwenye hyo miku5 ya chama wananch wanajua kuwa ukomboz unapelekwa kwngne hvyo wametoa baraka.. Wananch wa majimbo yaliyochn ya Chadema wanataka kila mtz awe mjanja kwa kuichagua Chadema.
 
wabunge wa chadema ni wabunge wa watanzania yote. wanachokifanya ni kuwapa watanzania elimu ya uraia ili kujua haki zao. Na si kweli kwamba wamesahau majimbo yao bali wanafanyakazi usiku na mchana kwa faida ya watanzania.
 
Tume ya katiba ulikuwa ukiiponda cdm kuwa ipo kaskazini tu,ONA SASA UNAKUJA NA HOJA ZA MFA MAJI..KWELI GAMBA LAKO GUMU
 
MAFILILI, hii issue lazima tuiangalie kwa darubini, jamaa wamekuwa watalii, unajua ile michango yetu ya toka Arumeru imewachanganya sasa kila mbunge anataka apate gawio.

Jamaa wamekuwa watalii. yaani 2015 ni mbali sana, majaribio ya kuchagua upinzani yanatutokea puani.

Pole sana ndugu yangu!! Mbunge wa CHADEMA siyo mbunge wa jimbo lake la uchaguzi....ni mbunge wa Watanzania wote ambao wamekosa wa kuwasemea na kutambua mahitaji yao hasa yanayosababisha UMASKINI!!!

Usilete ushabiki hapa jamvini....mi nipo Moshi vijijini, mbona sijamsikia Chami akichukua maoni ya wananchi wa huku kuyapeleka bungeni? We umewaona Mbowe, Sugu, Mnyika na Lissu ndiyo wabunge peke yao? Najua kinawauma kuwaona wanafanya kazi ya kuwababidilisha wana ccm kuwa wana CHADEMA....mtakoma mwaka huu!!!!!
 
Mkuu wangu, ingawa mimi si CCM ni mwanachama wa ADC, ila unapaswa uelewe kuwa system ya CCM ni tofauti sana na vyama vingine, wana hadi mabalozi wa nyumba 10, kwa hiyo mfumo wa mawasiliano wa hiki chama ni tofauti na vyama vingine.
 
mkuu hapo kwenye bold,maeneo mengi wamegoma kuchukua fomu mpaka sasa hivi uchaguzi haujafanyika!
 
Ikiwa bado siku 5 kuanza kwa bunge la bajeti, ni masikitiko makubwa kwa wakazi wa majimbo ya
1. Kawe,
2. Mbeya Mjini
3. Hai
4. Nyamagana
5. Ubungo,
6. Singida Mashariki

Wabunge wa majimbo husika wameshindwa kukutana na wananchi ili kupata maoni yao kuyafikisha bungeni BADALA yake wametumia pesa na marupurupu yatokanayo na ubunge kufanya mikutano ya chadema nje ya majimbo yao.
Tafadhali wabunge wa majimbo niliyoyataja geukeni nyuma na kukumbuka nyinyi ni wawakilishi wa wapiga kura ambao mnatakiwa kuweka mbele mahitaji ya wapiga kura. BADILIKENI mtumikie wana jimbo wenu!!

Kila siku twawasikia kiguu na njia mara Mtwara, Masasi, Newala wakati Sugu ukitamba Dar Live badala ya kupita maeneo ya Mwanjelwa, Soweto, masite nk. kuongea na wapiga kura; HIYO NI HAKI, MTAFAKARI!!!

ndg.yangu mleta uzi.uongo sio kitu chema.mwezi may sugu alifanya mikutano kwa kata zote pale mbeya mjini.mpaka kule juu kata ya iziwa,majengo.kule mwanjelwa ,iyunga,nzovywe.nk.watu wa mbeya mjini watakuwa mashahd na watanisapoti.kwa maana hata ratib za mikutano ya ndani ya mbunge niliiona nami nilihudhuria mkutano wa ukombozi wa fikra kule iziwa.so mod,mleta uzi huyu kwa upand wa sugu hajui alic.hoandika.
 
cdm hawawezi kwenda kusini,wameenda mmegeuka tena,kweli ukiwa gamba ni kazi pevu kwenye ubongo....................
 
Kama rais anavyotamba kwenye majimbo ya uchaguzi ya nje ya nchi?
 
Hawa watu wa Chama Tawala sidhani kama huwa wanawaza. Hivi kujua matatizo ya wananchi watanzania unahitaji kufanya utafiti?
 
Wamekusikia! Hata hivyo taarifa yako si sahihi Ubungo kumefanyika mikutano mingi tu hivi karibuni na kusikiliza hoja
 
Tatizo lako umezoea hao wenu wa Magamba wakiondoka ndo kwaheri, huku kwetu Singida Mashariki ameacha kila kitu Murua na unavyomuona yuko huko wenzio hazipiti wiki mbili tuko naye kwa jinsi anavyotumia posho yake kwaajili ya nchi yote. Haya tueleze hao wengine walioko huko wamefanya lipi hasa
 
Ikiwa bado siku 5 kuanza kwa bunge la bajeti, ni masikitiko makubwa kwa wakazi wa majimbo ya
1. Kawe,
2. Mbeya Mjini
3. Hai
4. Nyamagana
5. Ubungo,
6. Singida Mashariki

Wabunge wa majimbo husika wameshindwa kukutana na wananchi ili kupata maoni yao kuyafikisha bungeni BADALA yake wametumia pesa na marupurupu yatokanayo na ubunge kufanya mikutano ya chadema nje ya majimbo yao.
Tafadhali wabunge wa majimbo niliyoyataja geukeni nyuma na kukumbuka nyinyi ni wawakilishi wa wapiga kura ambao mnatakiwa kuweka mbele mahitaji ya wapiga kura. BADILIKENI mtumikie wana jimbo wenu!!

Kila siku twawasikia kiguu na njia mara Mtwara, Masasi, Newala wakati Sugu ukitamba Dar Live badala ya kupita maeneo ya Mwanjelwa, Soweto, masite nk. kuongea na wapiga kura; HIYO NI HAKI, MTAFAKARI!!!

Usituzingue hapa mnafiki wewe,kaa kando uwe mtazamaji kama magamba wenzio,mtaumia sana na magamba yenu,propaganda za mtindo wako are too low for us! kachukue posho yako,sadistic
 
Back
Top Bottom