Chonde chonde tusifike huku watanzania wenzangu!

Ipo siku atasema ukweli wa nani aliyemmwagia. Kwa sasa namuomba awe kimya, kwani wahusika wanaweza kumtosa kwa matibabu yaliyosalia.
 
Dhurma ni Kitu kibaya na Tamaa inaweza kukuua... RA ameacha historia kuondoka kwake Igunga... hizi ndio haswa Siasa Uchwara RA Atakuwa anajua kila kitu...

Wacha tumsubiri D. Balali hiyo August atakapo kuja naye sijui watamfanyia hivi hivi then Wasingizie ni CDM.
 
ingekua ni chadema wamemmwagia ungekuta wameshakamatwa, fungua akili baba huo ni mchezo wao wenyewe, unakumbuka huko huko igunga walichoma nyumba halafu wakaacha barua eti " ni sisi chadema" kweli inakuingia akilini kuwa kweli ni chadema au ni siasa za maji taka za kubabikiziana kesi?, vipi ile kesi ya dc igunga kuvuliwa ushungi na matamko kibbao misikitini,yameishia wapi? Ccm na washirika wao waache kufanya mambo ya kinyama kwa uchu wa madaraka na waache kuchezea hela zetu kufidia maovu yao.

ni kweli kabisa inasikitisha sana. Nami nakuunga mkono, ni kweli kama wangekuwa ni chadema wangekuwa wamekamatwa tayari. Je, ni nani aliyekamatwa na polisi mpaka sasa kutokana na kuuawa kwayule kada wa cdm kule igunga mpaka sasa? Japo kulikuwa na taarifa za awali za gari na kundi lililotumika kumteka yule kijana? Jiulize haya maswali, then utapata jibu ni kwanini ccm tunamalizana sisi kw sisi. Angalia yanayomkuta dr. Mwakyembe, prof.mwandosya, n.k. Na bado, kuja kufikia mwaka 2015 oktoba sijui hali itakuwaje.
 
Kinachonisikitisha mimi ni kitendo cha CCM kuendelea kumjaza maneno huyu muathirika ili aseme waliomfanyizia ni CDM na siyo wana-CCM wenzake aliowadhulumu hela za kubandika mabango ya Kamfumu.

Hii haitasaidia kitu, wananchi on the ground wanaujua ukweli. Wale makada wa CDM waliouwawa Igunga na green guards pia CCM watawaambia nini watanzania?. Njia pekee ya kurejesha amani ni kuzifanya chaguzi zetu kuwa na integrity. Masuala ya ushindi lazima au kwa vyovyote hayana nafasi tena katika kujenga Tanzania yenye amani ila ya nafasi katika kujenga Tanzania yenye chuki. Mbunge ni mwakilishi wa wananchi tuwaache wananchi wachague wamtakaye then wampime kwa miaka mitano wakimuona hafai wanachagua mwingine.

Huyu Mwigulu na kundi lake waliuingia uchaguzi wa Igunga kana kwamba ni kipimo cha kwanza cha uongozi waliokabidhiwa na kushindwa uchaguzi kwao ilikuwa ni kama failure mbele ya waliowapatia ulaji huo. Sasa njia pekee waliona ni bora kutoa kafara watu ili kulinda ulaji wao. Katika vitu vinavyowachanganya vichwa CCM kwa sasa ni neno 'Uchaguzi' na hasa uchaguzi huo ukiwa unaoshirikisha wananchi ambao wamechoka na ngojera zao.

Tukiacha wananchi waamue hata sisimizi hatachubuka. Ila tukitaka kuweka matakwa yetu mbele ya yale ya wapiga kura basi tujue kuwa hakuna atakaye salimika kama siyo leo kesho. Propaganda kama hizi hazikisaidii chama chochote zaidi ya kukifanya kionekane kituko mbele ya wananchi. Mbona CDM hawapublish makada wao waliotolewa uhai?, It doesn't serve for the country, it serves for the evil only. It incites vangeance minds. Ninamshauri Mwigulu na wenzake kuwa wamwache Mussa sasa aishi maisha yake mwenyewe, wasimfanyia PR kwani haitakisaidia chama chao bali kitaongeza hasira za wananchi kuwa wao wanatoa watu kafara ili kupata huruma ya umma.
 
Lakini wanasema ni wafuasi wa chadema ndio wanahusika na siasa hizi za kishenzi....kama kweli cdm ndugu zangu tubadilike hii sio siasa hivi ni vita!Katika hali ya kawaida ccm wasingeweza kumuumiza kada hadharani,wanao umafia lakini sio huu wa hadharani,hii wamefanya wapinzani wa ccm tu,kama c chadema basi ni nccr ama cuf,huo ndio ukweli tuache upotoshaji kwenye mabo serious!
Acha kujidanganya ndugu! kwani mwakyembe nae kapewa sumu na upinzani? Tabia ya kudhuru na kuu ni ya watu wanoshindwa na ambao ni ccm, umesahau skendo ya meya wa mwanza aliyemuua mwanaccm mwenzake, umesahau wakina Imran kombe na kolimba nao unadhani waliuwawa na upinzani? Umemsahau kamanda wa CHADEMA alivyouwawa na CCM kule igunga? Huyo kamwagiwa na ccm wenzake ambao wamedhulumiwa. CCM ndiko mahali watu wanauwana maana hakuna mwenye dhamira ya kujitolea huko. Usiombe CHADEMA waanze mchezo huo maana kwa jinsi wanavyojua kujipanga ccm haitachukua round.
 
inahuzunisha sana lakini mbona............ dhuluma mauaji ftna na kila aina ya udhalilishaji VIPO NDANI YA CCM .........hebu watwambie kilicho muua DAUDI balali KILICHOMUUA ...sokoine.............kigoma malima na kinacho muangamiza........ MWAKYEMBE NA MWANDOSYA....ccm ndio serekali ccm ndio polisi ccm ndio usalama wa taifa MBONA watuhumiwa wa mauaji ya Gnr kombe wameachiwa alie waachia nani !!.........CCM ACHENI PROPOGANDA.........acheni kuuana.......hii sio siasa!!
CCM noma, hata EL afya yake nowadays si njema sana. anaonekana yuko weak kiaina. sijui ndo washa mmwakyembe?
 
Ukikuta kuna kosa limefanyika na hakuna mtu anakamatwa ujue ni wanaccm wamefanya. Angalia walioiba EPA, waliochakachua mikataba ya Tanesco, waliokiuka kanuni za uchaguzi wa meya Arusha, waliochakachua mgodi wa kiwira, waliosimama na bastola kiunoni jukwaani, wanaochakachua BOT, waliomteka kamanda masoud wa chadema igunga na kumuua. Hamuoni wamefumbiwa macho akina; Jairo, mwakapugi, mwakosya, Hosea, Lowassa, Rostam, Shimbo na wengine wengi? Kwahiyo CHADEMA sio wahusika bali wahusika ni CCM ndo maana wanashindwa kupelekana mahakamani.
 
TAARIFA TOKA IGUNGA ZINASEMA YEYE HAKWENDA ALIKOTUMWA NA BOSI WAKE CCM BADALA YAKE AKAENDA KUPATA KILAJI (POMBE) HIVYO WENZAKE WALIPOMALIZA KAZI YA KUSHUSHA BENDERA ZA CHADEMA WAKAMWAMBIA ARUDISHE MGAO KWANI KAZI HAKUIFANYA AKAGOMA NDIPO WAKAMSHUGULIKIA.


ZAIDI YA HILO WOTE WALIOKAMATWA NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA HILO ,TESHA ALIWAKATAA NA WALIACHIWA HURU(ILIKUWA SHANGWE NA FURAHA IGUNGA) CCM WATAFUTE MCHAWI WAO NA BONA HAWSEMI WALIPOTAKA KUCHOMA OFISI YAO ILIWASINGIZIWE CHADAMA POLISI WAKALIONA MAPEMA ??????
:shock:
 
CDM ilistahili kufutwa kwa kitendo hiki.
Amkeni watanzania.
OTIS
CHADEMA wangehusika wangekuwa wamekwishakamatwa zamani sana!! Lakini watu wengi wanajua kisa na mkasa wa kijana kutokwa magamba usoni ni CCM kudhulumiana posho. Hilo ni funzo na kielelezo tosha kwa CCM kwamba ni vema ijivue magamba kikwelikweli!! Kijana ni mfano hai kwa CCM kujivua magamba, fuateni nyayo!
 
Pole sana!!
hao hao chadema wamemlisha sumu Mwakyembe; hao hao chadema walimshughulikia kolimba; hao hao chadema walichoma nyumba wakaacha waraka; hao hao chadema walimtishia magufuli kumuuwa; hao hao chadema; ................................................... nawe ongeza mabaya yaliyowahi kutokea dhidi ya watanzania ili tuwabebeshe hawa chadema! maana angalau sasa tumepata sehemu ya kupeleka lawama zetu!!
HAKIKA NINASEMA MIAKA MICHACHE IJAYO HATA MVUA ZITAKAPOGOMA KUNYESHA AU KUNYESHA KUPITA KIASI, BASI USISHANGAE KUSIKIA INALAUMIWA CHADEMA KWA KULETA HAYO MAAFA!!!
Hata mafuriko ya Dar es Salaam yalisababishwa na viongozi wa CHADEMA!
 
Sunday, January 15, 2012

MWANA-CCM ALIYEMWAGIWA TINDIKALI IGUNGA AREJEA NCHINI BAADA YA MATIBABU INDIA



1+%281%29.jpg

MKAZI wa Igunga, Kada wa CCM, Mussa Tesha aliyekuwa katika matibabu nchini India baada ya kumwagiwa tindikali usoni na watu wanaodaiwa kuwa wa CHADAEMA, wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo jimboni humo mwaka jana, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam, baada ya kurejea nchini.
Kulia ni Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba ambaye alikuwa Meneja wa Kampeni za CCM jimboni humo.

3.jpg


Na Mwandishi Wetu


KADA wa CCM, mkazi wa Igunga, Tabora, Mussa Tesha (24)aliyekuwa akipatiwa matibabu India, baada ya kuwagia tindikali na watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Chadema wakati wa kampeni za uchagfuzi mdogo jimboni humo mwaka jana, amerejea nchini.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba alisema leo kwamba, Tesha amerejea juzi, akiwa amepona kiasi cha kuweza kuzungumza na kuona jicho moja huku lingine likiwa bado halioni vizuri kutokana na athari alizopata.

Akizungumza nyumbani kwake Tegeta Mwisho, Dar es Salaam, Mwigulu ambaye alikuwa Meneja wa Kampeni za CCM Igunga, alisema amemhifadhi Tesha nyumbani kwake wakati akisubiri kwenda tena India kuendelea kuendelea na matibabu madogo yaliyosalia.

Mwigulu alisema, Chama Cha Mapinduzi ambacho kiligharamia matibabu yote, hadi sasa kinaendelea kumhudumia Tesha mpaka atakapopona kabisa na kuwa na uwezo wa kufanya kazi.

"Hadi sasa tunashukuru kwamba amepona anaweza kuzungumza, kusikia na kuona walau jicho moja, tofauti na mwanzo alivyokuwa mara alipomwagiwa tindikali, hata hivyo hali yake haijaweza kuwa ya kufanya kazi mbalimbali kama za juani, hivyo CCM tunaendelea kumsaidia mpaka ajenge uwezo wa kujitegemea", alisema.

Alisema, CCM imefanya mpango wa kuwaugnanisha wabunge wa CCM kumtayarishia mtaji ambao utamsaidia Tesha kuendesha maisha yake baada ya kukumbwa na madhara hayo.

Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu amwagiwe tindikali, Tesha amewashukuru Watanzania kwa kumuombea wakati wote alipokuwa mgonjwa na kwamba anaamini dua zao ndizo zimemwezesha kubakia hai hadi sasa.

Tesha alisema, baada ya kumwagiwa tindikali Septemba 9, mwaka jana, hakujitambua hadi alipokuwa katika hospitali ya KCMC ambako alipatiwa matibabu na baadaye kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alikaa wiki tatu kabla ya kupelekwa India.

Akiwa India kwenye Hospitali ya Apollo, Tesha alikuwa chini ya uangalizi wa baba yake mdogo, Samwel Bethwel ambaye pia gharama za kuwa huko zimebebwa na CCM. Anatarajia kwenda tena India baada ya miezi mitatu.

Duu! Kafumu anaiangaliaje picha hii?
 
Pole sana!!
hao hao chadema wamemlisha sumu Mwakyembe; hao hao chadema walimshughulikia kolimba; hao hao chadema walichoma nyumba wakaacha waraka; hao hao chadema walimtishia magufuli kumuuwa; hao hao chadema; ................................................... nawe ongeza mabaya yaliyowahi kutokea dhidi ya watanzania ili tuwabebeshe hawa chadema! maana angalau sasa tumepata sehemu ya kupeleka lawama zetu!!
HAKIKA NINASEMA MIAKA MICHACHE IJAYO HATA MVUA ZITAKAPOGOMA KUNYESHA AU KUNYESHA KUPITA KIASI, BASI USISHANGAE KUSIKIA INALAUMIWA CHADEMA KWA KULETA HAYO MAAFA!!!

nimeipenda hii sana tu chadema ndo limekuwa jalala,kweli wadanganyika wanambo sana
 
inahuzunisha sana lakini mbona............ dhuluma mauaji ftna na kila aina ya udhalilishaji VIPO NDANI YA CCM .........hebu watwambie kilicho muua DAUDI balali KILICHOMUUA ...sokoine.............kigoma malima na kinacho muangamiza........ MWAKYEMBE NA MWANDOSYA....ccm ndio serekali ccm ndio polisi ccm ndio usalama wa taifa MBONA watuhumiwa wa mauaji ya Gnr kombe wameachiwa alie waachia nani !!.........CCM ACHENI PROPOGANDA.........acheni kuuana.......hii sio siasa!!

Na wao wanaweza kuhoji kilichomtoa roho chacha wangwe,je mtakua kwenye nafasi ya kujibu?sidhani,mi nadhani binadamu amezaliwa na siku moja atakufa bila kujali nafasi yake,tusiingilie kazi ya mungu,najuamengi yatasemwa sana akifa mtu mashughuli lakini mola ndie anaejua siri ya vifo vyote.
 
Hujafa Hujaumbika...pole sana kaka...tuishie tu hapo, dah!!


Ni kweli Michelle, jana au juzi niliiona picha hii kwa Michuzi lakini kusema kweli ilinishinda kuiangalia mara mbili, hata hapa nimeepuka kuiangalia. Pole zake nyingi.
 
Acha kujidanganya ndugu! kwani mwakyembe nae kapewa sumu na upinzani? Tabia ya kudhuru na kuu ni ya watu wanoshindwa na ambao ni ccm, umesahau skendo ya meya wa mwanza aliyemuua mwanaccm mwenzake, umesahau wakina Imran kombe na kolimba nao unadhani waliuwawa na upinzani? Umemsahau kamanda wa CHADEMA alivyouwawa na CCM kule igunga? Huyo kamwagiwa na ccm wenzake ambao wamedhulumiwa. CCM ndiko mahali watu wanauwana maana hakuna mwenye dhamira ya kujitolea huko. Usiombe CHADEMA waanze mchezo huo maana kwa jinsi wanavyojua kujipanga ccm haitachukua round.

Haya ni madai tu ambayo hayana ushahidi wowote ni sawa na ile "ajali" ya chacha wangwe ambayo wapinzani wa cdm waliihusisha na fitna za kisiasa za vigogo wa cdm hususan mbowe lakini wenye akili tuliidharau kwa kuwa hakukua na ushahidi,hii ya huyu bwana kumwagiwa tindikali angalau ina mashiko kwa kuwa mhusika yupo an yeye yuko katika nafasi nzuri zaidi ya kueleza kilichojiri kuliko tunaotumia nguvu nyingi na maneno mengi,ukweli ni kwamba hatuwezi kujua kilichotokea kuliko yeye mwenyewe anavyojua,wengi hatuwepo igunga tulikua hapa hapa jf wakati harakati za uchaguzi zikiendelea na tulikua tunapeana moyo kwamba hali ni nzuri upande wa chadema na tutashinda kwa kishindo,kumbe tulikua mbali sana na hali halisi.Pia mnapojaribu kufananisha hii issue na ya mwakyembe sielewi kwanini mnafanya hivyo na kujaribu kumsemea mwakyembe ambae yuko hai!kwanini mwakyembe hajasema ni ccm ndio walimtenda kama huyu anavyosema kwamba waliomuumiza ni watu wa chadema?msipende kuwawekea watu maneno midomoni,huo sio u great thinker,ongeeni reality..chadema wamehusika na hili ni lazima tukemeane kama tunataka haya mambo yasiendelee otherwise tukiyafumbia macho huko kwenye vyama vyetu tukaacha kuambiana ukweli mambo ndio utakua utamaduni wetu huko mbele kila zitakapokuwa zinatokea chaguzi.Tujifunze kufanya siasa za kistaarabu,huu mchezo pia waliwahi kuwa nao cuf,kuvamiwa wapinzani wao usiku na kuchoma nyumba zao halafu kudai ni ccm wenyewe!
 
Hivi yale mamilioni aliyolipwa yule kada wa CCM aliyemegewa mke wake na huyu Mwigulu yalitoka kwenye fungu gani vile?
 
chadema ni mafia ..proved

Angalia walinzi wa slaa na jinsi walivyoburuza mkuu wa wilaya..

Hatari sana hawa...fujo fujo...
 
Kwa kweli hii inasikitisha sana,hiki chama sasa wengine licha ya kuwa wanachama wake itabidi tunaze kufikiria mara mbili kuendelea kuwamo ndani yake,wengi tulidhani ndio kitakua mkombozi wa kutusaida kuiondoa ccm madarakani baada ya nccr ya kina mrema na cuf kutuangusha,sasa kwa siasa za dizaini hii bwana mmmm!hapana ni kweli tunaichukia ccm na tungependa iondoke hata kesho madarakani lakini si kwa njia hii,tunayotaka kuizoea kwa kuteteana,wanachadema wenzangu tukiitetea hii kitu itatutafuna huko mbele,wote tusimame imara kulaani hii kitu na kushinikiza viongozi wetu wa kitaifa tuliowatuma igunga pamoja na cdm igunga kama sio tabora wanawajibika kufuatia tukio hili la kinyama linalokiaibisha chama na kuchafua taswira yake mbele ya jamii,nani ataipenda chadema baada ya kuona hii picha?si ndio wapinzani wetu sasa watakua wanatembea na huyu jamaa kila pahala nchini kama kielelezo cha vurugu zetu?tuchukue hatua ili wananchi waone hata sisi tumechukizwa na watu wachache ndani ya chadema wanaotaka kukipaka matope chama hiki imara cha upinzani kwa sasa.Tuache jazba ndugu zanguni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom