Chonde chonde kina dada

mdhama

Member
Apr 11, 2011
48
19
Jamani hiki kisa kimenifanya niwaze sana! Kuna bishost mmoja (tupo nae ofisi moja) yamemkuta makubwa! Bidada alikua na boyfriend hapa ofisini. Mambo yalionekana kuwa sawa baina yao mpaka majuzi mkaka alipopigiwa simu na mtu aliedai kuwa ni boyfriend wa mdada na amepata number yake ya simu toka kwenye simu ya mdada. Kwa hiyo nadhani kwenye mazungumzo wakakubaliana wakutane (Yaani hawa wanaume wawili).Basi walipokutana, of course huyu boyfriend wa hapa ofisini akawa haamini kama kweli binti alikua na mtu mwingine. Basi wakakubaliana wamtafute huyu bint ili wajue msimamo wake. Binti akakimbilia kwao, kina kaka hao wakaenda mpaka home kwa kina binti. Binti akagoma kabisa kutoka nje akidai anaumwa pressure! Sasa katika kukaa kaa pale yule jamaa ambaye alimpigia simu mwenzie akaanza kufunguka kwamba huyu bidada anawachanganya, na pia ana jamaa mwingine ambaye wamezaa nae na kamnunulia gari na kiwanja (kweli mdada ameanza ku drive sio siku nyingi)! Mara ghafla wakati wale kina kaka wanaendelea kumsubiri binti, akatoakea mshkaji mwingine ambaye ni wa ofisini pia na akadai kwamba yeye ni boy frend wa mdada muda mrefu! Basi kwa hasira hawa kina kaka watatu wakaamua kwenda zao baa ya karibu wakanywa pombe weee na kuendelea kushare story za binti! binti bila aibu akawa anawatumia msg kila mmoja kwa wakati wake! Chonde chonde kina dada na kina kaka, hii lifestyle ya kuchanganya wapenzi sio kabisa! mwisho wa siku ni kuumbuka tu sio ujanja wala nini!
 
Mh! Huyu dada ana tisha! Naona kila kaka hapo alikuwa na majukumu yake...lol
 
Jamani kuna watu hawana vinyaa na kidudu kawapangia ratiba pia pheewwwwww,ukitoka hapo una majasho na viporo hata ukioga hutakati.
 
Inauma sana pale unapojiwekewa kichwa kizima halafu mwenzio amwapanga mpo kama kumi hivi...atleast wamejua mapema ili waanze mchakato wa kuendelea na maisha.
 
yalishanikuta kama haya miaka ya 2002 hivi, bahati nzuri jamaa mwenzangu alikuwa muelewa tukanawa mikono.
 
Yani we acha tu nasikia kati ya hao wa kaka mmoja alikua ana do bila, kapata mawazo ile mbaya!
 
Na hao wanaume wauni pia. Sasa walienda kumsuta, kumfanyizia au kumuonesha kama wamejuana? Ndio maana wameingizwa mjini. Kama umegundua mwanamke sio muaminifu unabwaga manyanga unaendelea na shughuli zako za muhim,
 
Nafikili kichwa kingekuwa chondechonde akina kaka maana ndio waliopatwa na mkasa dada kasepa home kimya na hamjui wangapi wengine anao!
Hivi vi dada vya siku hizi ni vilaghai sana! Na viko after money
 
Wadada wa siku hizi tamaa zinawaponza sana. Yaani kuna binti alitafutiwa kazi na boyfriend wake kwenye kampuni moja hivi. Aliporipoti hapo kazini, kwa kuwa ni mzuri watu wakaanza kumtongoza. Lakini kwa ustaraabu kwa kumuuliza kama ana commitments zozote kwenye mahusioano. Binti akasema yeye yuko single and searching. Just imagine, mtu unayempenda mpaka kumtafutia kazi anajitambulisha hivyo kwenye ofisi mpya.

Yaliyotokea hapo ni balaa, maana jamaa alikuja kugundua na wakamwagana na binti. Na mafisi kadhaa waliompitia pale ofisini nao wakammwaga vile vile! TAMAA mabinti wa siku hizi tamaa mbele. Asione mwanaume ana gari zuri, tayari chupi imelowa. Asione mwanaume ana vijisafarii vya nje mara kwa mara anaanza kujipendekeza kwa kuagiza vijizawadi kama designer perfumes na underwear! Yaani kwa kifupi mabinti wengi wa humu maofisini ukiwa mwanaume usiyepitwa na sketi mbele yako unaweza kujaza hata Scandinavia la kwenda Songea kwa idadi ya utaowatafuna!
 
Ha ha haaaaa du huyo dada kwenye logistics yupo juu,kuchanganya vichwa vitatu at a time na kuvipa job description inaonekana kichwa chake kipo safi kwenye upangaji na usimamiaji.Kingine hao mbuzi wake wameonyesha ukomavu wa kisiasa kukaa meza 1 na kunywa bia na uhakikia ingekuwa wakidada/mama hapo ni ngumi mtindo mmoja .......lol.
 
Wadada wa siku hizi tamaa zinawaponza sana. Yaani kuna binti alitafutiwa kazi na boyfriend wake kwenye kampuni moja hivi. Aliporipoti hapo kazini, kwa kuwa ni mzuri watu wakaanza kumtongoza. Lakini kwa ustaraabu kwa kumuuliza kama ana commitments zozote kwenye mahusioano. Binti akasema yeye yuko single and searching. Just imagine, mtu unayempenda mpaka kumtafutia kazi anajitambulisha hivyo kwenye ofisi mpya.Yaliyotokea hapo ni balaa, maana jamaa alikuja kugundua na wakamwagana na binti. Na mafisi kadhaa waliompitia pale ofisini nao wakammwaga vile vile! TAMAA mabinti wa siku hizi tamaa mbele. Asione mwanaume ana gari zuri, tayari chupi imelowa. Asione mwanaume ana vijisafarii vya nje mara kwa mara anaanza kujipendekeza kwa kuagiza vijizawadi kama designer perfumes na underwear! Yaani kwa kifupi mabinti wengi wa humu maofisini ukiwa mwanaume usiyepitwa na sketi mbele yako unaweza kujaza hata Scandinavia la kwenda Songea kwa idadi ya utaowatafuna!
na wengìne utawaombea lift kwenye ngorika.b careful ppo!
 
Back
Top Bottom