Elections 2010 Chonde chonde chadema!

reandle

JF-Expert Member
May 6, 2009
11,168
8,142
CHONDE CHONDE CHADEMA, msije mkasahau kutumwagia sera zenu wakati wa kampeni! Wakati nikikumbusha hilo, vilevile napenda kukumbusha kwamba kKuna mwanaharakati mmoja (katika masuala ya upigaji vita rushwa) aliwahi kunukuliwa kwamba kila mtu ananunulika, cha kufanya ni kutafuta bei yake tu! Halikadhalika, mimi naamini kwamba asilimia kubwa kabisa ya wapiga vita rushwa nao wanaweza kuwa wala rushwa wa kutisha endapo watapata nafasi hiyo! Dokta Slaa, ni mmoja wa wapiganaji hodari katika masuala ya kupiga vita rushwa ingawaje sina hakika kama nae akipata nafasi anaweza kuwa mla rushwa wa kutisha!
Nimeleta hoja hii kwa sababu nina hofu! Nina hofu kwamba wakati wa kampeni ukifika, huenda Dr. Slaa na wenzake wakasahau suala zima la sera na kutumia muda mrefu kwenye majukwaa kuzungumzia masula ya rushwa! Si kwamba jambo hilo si la msingi bali ni simulizi ambazo zimezoeleka huku wengi wao wanaishia tu kupiga kelele bila kuonesha ni ya dhati ya kuichukia rushwa. Si kwamba Dr. Slaa na wenzake wasizungumzie masuala ya rushwa bali wabadilishe staili. Wasiishie tu kusema kwamba serikali ya Kikwete na CCM yake inanuka kwa rushwa, bali watuambie wao wakiingia madarakani watafanya nini ili serikali yao isiwe ya wala rushwa! Inawezekana Dokta Slaa akawa mchukia rushwa kwelikweli, vipi kuhusu wana CHADEMA wenzake atakaoundanao serikali!?
Kila mtu ananunulika, tafuta bei yake tu! Kwa jinsi Watanzania tunavyopenda ahsante, ni ishara kubwa ya namna gani wengi wetu tunaweza kuwa wala rushwa endapo tutapata channel hizo! JITU unakuta limekuhudumia, na ni wajibu wake kutoa huduma hiyo lakini bado utakuta linataka ahsante! Ahsante ina-affect maamuzi ya mpokea ahsante kwa cku za usoni hata kama ahsante hiyo hakuiomba! Ni watu wangapi wanakataa ahsante wanapopatiwa baada ya kuwahudumia wateja wao? Mijitu mingine imezoea ahsante hadi inahisi ni haki yao!
Hivyo basi, badala ya kuishia ku-rewind kanda zile zile za serikali ya CCM ni mafisadi, vilevile mje ni vibwagizo vya namna gani wapinga vita ufisadi mtafanya kufutilia mbali ufisadi endapo mtapata ridhaa ya wananchi kuingia madarakani. Si hivyo tu, mtumie muda mwingi kutueleza ni namna gani mtatuondolea umaskini wetu Watanzania badala ya kutumia muda mwingi kuelezea udhaifu wa CCM.
Ingawaje sijawahi kupiga kura, mwaka huu nitapiga na kura yangu ataipata yule atayeeleza ni namna gani atatuondolea matatizo yetu na sio tu ni nani kayaleta matatizo hayo. Wala sitampa kipaumbele mtu atakayeishia kuupiga vita ufisadi kwavile najua Watanzania wengi wanapounda serikali inakuwa ni kama serikali za wanafunzi wa vyuo vikuu ambazo ni hodari kwa kuelezea ufisadi wa waliowatangulia ili nao wapate nafasi ya kufanya ufisadi ule ule!
Kwa kumalizia, na bila shaka ndilo nililokusudia kulisema, chondechonde CHADEMA, msije mkatumia energy kubwa kuelezea ufisadi wa serikali ya Kikwete halafu mkasahau kuelezea sera zenu! WENGI WETU TUNAFAHAMU KWAMBA CCM KUMEJAA UFISADI, HIVYO TUNACHOHITAJI KUSIKIA KWENU NI SERA ZENU NA VIPI MTAPAMBANA NA UFISADI AMBAO KIMSINGI UMEENEA KILA MAHALI, KWA WANA-CCM NA WASIO WANA-CCM!
 
Back
Top Bottom