China yakana kuuza nyama ya binadamu Afrika

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
China yakana kuuza nyama ya binadamu Afrika
160523164936_china_corned_meat_512x288_bbc_nocredit.jpg

Nyama ya mkebe kutoka nchini China
Wizara ya maswala ya kigeni nchini China imekana ripoti kwamba kampuni za chakula nchini humo zinaweka nyama ya binaadamu na kuuza barani Afrika kama nyama ya ng'ombe.

Chombo cha habari nchini humo Xhinua kimesema kuwa jarida moja nchini Zambia lilimnukuu kimakosa mwanamke mmoja ambaye hakutajwa anayeishi China.

Alisema kuwa kampuni za China zilikuwa zikichukua miili ya wafu kuitia katika viungo na kuiweka katika mikebe.

Msemaji wa China Hong Lei amesema kuwa ripoti hizo hazina uwajibikaji.

160523165133_cornedbeef2.jpg

Nyama ya mkebe kutoka China
Balozi wa China nchini Zambia,Yang Youming ,amesema kuwa ripoti hizo zililenga kuharibu uhusiano mzuri kati ya mataifa hayo mawili.

''Leo jarida moja linasambaza uvumi ,likidai China inatumia nyama ya binaadamu ambayo uihifadhi katika mikebe na kuiuza Afrika.

''Hii ni dhulma ya makusudi ambayo haiwezi kukubalika kabisa kwetu sisi''.
chanzo.China yakana kuuza nyama ya binaadamu Afrika - BBC Swahili
 
Wakati nikiwa chuo Mzumbe enzi hizo kuna jamaa pale moro town bar ya Snacks Heartz
alikuwa ana vimishkaki vidogo vitaamu kweli kwa kushushia na Pilsner Ice ya enzi hizo

Dah mwaka juzi nikaja sikia jamaa alikamatwa kumbe alikuwa anatengeneza ya paka daah nilijitapisha balaa
Ila ndo nikawa nishakula hivyo
 
Vyakula vya kwenye makopo sitokuja kula tena tangu mwenzetu mmoja akute kijidole cha binaadam kwenye kopo la nyama aliyokuwa anakula. Ilikuwa kipindi tupo OP's mojawapo kule nyanda za chini kusini. Na hiyo nyama pamoja na magaragwe yalitoka huko huko China. Tangu siku hiyo mimi nacheza na mzabuni tu, au karanga na maji katika vipindi vigumu kama hivyo.
 
China yakana kuuza nyama ya binadamu Afrika
160523164936_china_corned_meat_512x288_bbc_nocredit.jpg

Nyama ya mkebe kutoka nchini China
Wizara ya maswala ya kigeni nchini China imekana ripoti kwamba kampuni za chakula nchini humo zinaweka nyama ya binaadamu na kuuza barani Afrika kama nyama ya ng'ombe.

Chombo cha habari nchini humo Xhinua kimesema kuwa jarida moja nchini Zambia lilimnukuu kimakosa mwanamke mmoja ambaye hakutajwa anayeishi China.

Alisema kuwa kampuni za China zilikuwa zikichukua miili ya wafu kuitia katika viungo na kuiweka katika mikebe.

Msemaji wa China Hong Lei amesema kuwa ripoti hizo hazina uwajibikaji.

160523165133_cornedbeef2.jpg

Nyama ya mkebe kutoka China
Balozi wa China nchini Zambia,Yang Youming ,amesema kuwa ripoti hizo zililenga kuharibu uhusiano mzuri kati ya mataifa hayo mawili.

''Leo jarida moja linasambaza uvumi ,likidai China inatumia nyama ya binaadamu ambayo uihifadhi katika mikebe na kuiuza Afrika.

''Hii ni dhulma ya makusudi ambayo haiwezi kukubalika kabisa kwetu sisi''.
chanzo.China yakana kuuza nyama ya binaadamu Afrika - BBC Swahili
KUTILIWA SHAKA TU INATOSHA, HASWAHASWA IKIZINGATIWA DHARAU ZAO NA KUTOTHAMINI KWAO MAISHA YA BINAADAM WENZAO!
KWA KIFUPI SILI TENA CHAKULA KILICHOANDALIWA CHINA!
 
Watz mmejaa ujinga kichwani kila habari mnaichukua kama ilivo..haingiii akilini kabisaaa
Ni wapuuzi tuh au wenye akili za kijinga wanaeza zania kuna kiwanda cha kuchakata nyama ya binadamu...
 
Wanachimbua makaburi au izo maiti zinatolewa wapi ili nyama ipatikane??
 
Ili ipatikane nyama ya kutosha wazani watu wangapi wataitajika nyama yao
Kwa haraka haraka kila cku watu wasiopungua 1000 kwa cku
Aya izo maiti zitatokea sehem gani
Maana kila mtu akifiwa lazima azike ndugu yake
..watu sio mbuzi au kuku
 
Back
Top Bottom