China support the modernization of Tazara(a great shame)

Kwa jinsi unavyoifagilia kenya katika threads zako nyingi humu international forum nilifikiri wewe ni mkenya. Mistari miwili hii uliyoandika inaashiria wewe ni mtanzania. Pity.
Huyu ni Mkenya usidanganyike tena Mkikuyu maana wana matatizo ya kutamka R hata wenye kuandika pia
 
Nadhani Waafrika, wabantu, tuna kasoro ya akili. Inakuwaje mtu aharibu kitu ambacho anakitegemea kw maisha yake? Sikuambii maisha ya taifa, la, maisha yake binafsi. Kweli watu kama hao ni binadamu timamu? Na hii siyo TAZARA pekee, karibuni sehemu zote.
Ndiyo maana tukauzana hapo kale. Hata hivi sasa tunauzana kwa namna nyingine. Watu wanodiriki kuuza ndugu zao kwa wageni si binadamu, ni wanyama tu wanovaa suti.

the only place we fit best is in the jungle huku kwingine tunajisumbua tu, hao wachina hata sijui kwanini wanajihangaisha watuache tumalize kila kitu, au la watoe msaada na wao wenyewe ndio waimanage
 
post yako nzuri umeiharibu kwa kutumia sana h mahali isipotakiwa,ungeweza ku-edit km huwa unasoma ulichoandika kabla hujapost,lakini kwa kuwa husomi umepost ilivyo,wewe na hao tazara max zenu sawa

MIAFRIKA NDIYO ILIVYO.......Je umeelewa post? kinachofanya ung'ang'anie h ni nini? soma post bana uelewe basi tosha.
 
Hv huwa najiuliza,nin hasa cha kufanya ili twnde sawa?mi nahc cha msngi ni kuwajibshana2.na hawa chadema 2tawapa kura z2 2015 ole wao wabadilike,warai ntkua wa kwnza kuingia msituni,nakupenda sana tanzania.
 
MIAFRIKA NDIYO ILIVYO.......Je umeelewa post? kinachofanya ung'ang'anie h ni nini? soma post bana uelewe basi tosha.

Mkulu, wala husijisumbue kumpe somo huyu, hawezi kukuelewa; we fikilia mtu mwenye attitude kama hizi kama ana elimu ya kutosha (which I doubt) ukimpa responsibility ya ku-run Shirika au Kiwanda kutatokea nini? Haya ndiyo matatizo ya kuwapeleka Sekondari mpaka vyuo vikuu watu walio pass kwa asilimia 40% darasa la saba.
 
Hv huwa najiuliza,nin hasa cha kufanya ili twnde sawa?mi nahc cha msngi ni kuwajibshana2.na hawa chadema 2tawapa kura z2 2015 ole wao wabadilike,warai ntkua wa kwnza kuingia msituni,nakupenda sana tanzania.

BABUKIJANA! Kama hupo, ebu jaribu kusoma post hii ya mwana JF huyu ndiyo utajua nilicho kueleza kuhusu uwezo wa ubongo wa kujaziliza au kuondoa maneno fulani bila kujali staili iliyotumika kuandika sentensi. Swali ni je, Bwana Babukijana unaweza kueleza members kwamba huelewi alicho andika Jaslaws? Sasa hii ndiyo maana halisi ya matumizi ya SOCIAL NETWORKS unaweza kutumia maneno ya mkato kwa kusave time na watu wakakuelewa tu, je kwa mawazo yako unafikili Jaslaws kakosea nini? jibu unalo.
 
nakuunga mkono mchangiaji hapo juu. Nimefanya kazi hilo shirika kwa miaka kadhaa kabla ya kuondoka kutokana na fitina za waliokuwa juu yangu. Uongozi wa tazara ni janga kubwa sana. Kila ulichokisema ni kweli. Umesahau kitu kimoja. Tazara huwa wanapewa mafuta ya ku-run treni hata kwa miezi sita, lakini viongozi wanaiba mafuta kiasi kwamba hata mwezi moja hayatoshi. Kila mtu anachuma. Tazara ina rasilimali za thamani sana wao wanauza tu. Shame on management, shame on governments as well.


Mkuu kilichoua RTC, ATC na mashirika Mengi ya Tanzania ni kile kile. Unachosema kuhusu wizi wa mafuta kiko wazi na wengi wanakiona, lakini hakuna anayejali. Ni vizuri wewe uliyotooka ndani ya TAZARA unasema wazi. Uongozi ndio ovyo kabisa usiseme, kila mtu mwizi, kila mtu anataka mwanaye mjobawe, hawara yake au rafiki yake aajiriwe. fitina juu ya fitna. NI afadhari wapewe wachina waiendeshe toka management hadi mfagiaji, utaona jinsi itakavyokuwa bomba. Mwaka mmmoja tu itakuwa na faida kuliko shirika lolote Tanzania. Nasema hivyo kwa kuwa opportynities za biashara kwa Tazara kwa sasa ni kubwa kuliko zile za miaka 10 au 20 iliyopita.

Kuna siku Mh Kapuya aliwahi kusema "vijana wetu si waaminifu ndio maana wageni wanaajiri vijana wao wanaowaamini"

Kuomba msaada no doubt ni aibu. Lakini Tanzania yetu ina watu wenye utamaduni na mila tofauti. Kuna wengine kuomba msaada ni sifa, tena wanatangaza kuwa nimeomba msaada na nimepata msaada. Wengine wanaona hata aibu kusema kuwa nimeomba msaada. Kwa hiyo inategemea umetoka kona ipi ya nchi yetu, kujua kama hili ni aibu au si aibu. Naingana na wewe ni aibu.
 
post yako nzuri umeiharibu kwa kutumia sana h mahali isipotakiwa,ungeweza ku-edit km huwa unasoma ulichoandika kabla hujapost,lakini kwa kuwa husomi umepost ilivyo,wewe na hao tazara max zenu sawa

"veve ni bouya". kama umeielewa hii sentesi basi kumbe umejifanyisha hapo juu..now gechuaas bak 2 da topic usitupoteze muda.
 
Nadhani Waafrika, wabantu, tuna kasoro ya akili. Inakuwaje mtu aharibu kitu ambacho anakitegemea kw maisha yake? Sikuambii maisha ya taifa, la, maisha yake binafsi. Kweli watu kama hao ni binadamu timamu? Na hii siyo TAZARA pekee, karibuni sehemu zote.
Ndiyo maana tukauzana hapo kale. Hata hivi sasa tunauzana kwa namna nyingine. Watu wanodiriki kuuza ndugu zao kwa wageni si binadamu, ni wanyama tu wanovaa suti.

Mkuu you are a megatimes right unacho zungumza hapa, mtu ukiyafikilia sana mambo ya sisi Wafrica unaweza ukasema maneno ya kufuru - tunashangaza sana! Swali ni je kama sisi tunajishangaa je wafadhili wanatuonaje.

Swala la TAZARA tukitaka ufumbuzi wa haraka haraka wafanye yafuatayo FASTA:


  • Managing Director awe Mchina Mwenyewe na awe na kauri ya mwisho katika uendeshaji wa Shirika. Deputy wake siyo lazima awe Mtanzania ua Mzambia awe mtu yeyote mwenye uwezo hata akiwa Mzungu na afanye kwa contract ya miaka mitatu mitatu, akifanya umangameza afumuliwe fasta na hiyo iandikwe kabisa kwenye contract yake.



  • Chief Engineer Mechanical awe Mchina.



  • Chief civil Engineer awe mchina. (Note:post hii anaweza kupewa Mtanzania au Mzambia ambaye ana a proven experience katika field hii-wafanyiwe interview na an Independet Recruitment Argency)


  • Supplies Manager awe Mchina.



  • Chief Signallling and Telecommunication Engineer awe Mchina, na idara hii iunganiswe na ICT. Idara hii iwe independent hisichanganwe na CIVIL. (Note:post hii anaweza kupewa Mtanzania au Mzambia ambaye ana a proven experience katika field hii-wafanyiwe interview na an Independet Recruitment Argency)



  • Finance Director awe Mchina, na actually hii ni ya pili katika umuhimu wa kufanyiwa kazi na Serikali zetu FASTA.



  • Idara ya TRAFFIC apewe Mchina hili Mambo yanayohusu rolling stock-yaani mabehewa ya aina zote closed/open/flat na Fuel/Oil tanks, na kuwepo na uwezo wa kuya-track anytime yajulikane yako wapi kama yako nchini au yamekwisha kwenda Zambia au Congo, kumbuka reli hizi gauge zake ni sawa kwa hiyo ni rahisi mabehewa kupelekwa kokote mpaka South Africa au Zimbabwe bila kujulikana yalipo, kuna wakati Fuel Tanks za TAZARA zilipo kuwa zinapelekwa Congo, wa Congomani wanazigeuza kuwa underground fuel TANKS kwenye vituo vya kuhuzia mafuta (nakwambia kuna visanga vya ajabu sana TAZARA). La pili hili kupunguza ujanja(wizi) unaotumiwa na wakubwa kukosesha Shirika mapato, tracking system ya mabehewa ifufuliwe-iliuwawa kimaksudi hili kuwe na urahisi wa kuchezea mabehewa, tatizo hili la kugombania mabehewa ni SUGU sana katika shirika hili na bila kujua mabehewa yako wapi na yako mikononi mwa nani at any given time, bila Serikali zetu mbili kuwa wakali katika hilo usugu wa ukata hautakwisha TAZARA. Kitanzi cha ukata wa TAZARA kinatokana na ku-abuse sector hiyo muhimu lakini watu wa Wizarani hilo hawalioni au ku-question, maanake bila mabehewa kutumika kiufanisi bila mambo ya ujanja ujanja (siyo ujanja ni wizi) TAZARA haiwezi kupata mapato ya kuiwezesha ku-run ki-ufanisi, kumbuka mabehewa ndiyo yana generate REVENUE. Revenue zinazo patikana kwa kusafirisha abiria ni negligible inabaki kuwa service tu. Mabehewa ya mizigo ndiyo uti wa mgongo wa TAZARA wahusika mlikumbuke HILO.



  • Weighbridges zote zifanyiwe Calibration na watu wahadirifu siyo marafiki zao - ku-overload mabehewa kumeharibu sana ma-springs za mabehewa na infrastructure za PERMANENT WAY kwa kuitia hasara kubwa TAZARA siyo springs tu hata ku-under declare uzito wa bidhaa zilizobebwa na mabehewa hivyo kuipotezea mapato TAZARA, minzani hii inachezewa SANA. Metal fartique za springs za mabehewa uchagia sana kwenye ajali za kila mara wakati mabehewa yanapo kosa balance yakiwa kwenye mwendo kasi. Sijuhi kama accident analysis wasifanyazo kila kikicha kuna kitu chochote wamewahi kujifunza maana naona makosa haya huwa yanajirudia rudia.

Serikali zetu hasipashwi kuleta Wachina lukuki kama enzi za kujenga reli ya TAZARA, Serikali zikichezesha karata nilizo taja hapo juu kutatokea mabadiriko ya ajabu in no TIME, haya ni mambo ya kisakolojia tu nina maana wafanyakazi wakisha juwa kwamba watu waliopo madarakani ni wahadirifu na wazalendo au wageni nakuhakikishia watafanya kazi kwa bidii na ufanisi bila ya kusimamiwa.

Tusiende mbali kuangalia sakolojia inavyo fanya kazi - chukulia mfano wa barabara inayojengwa ya kuanzia Mwenge kwenda Tegeta inajengwa kwa ufanisi mkubwa sana na kasi ya ajabu-ebu angalia watu wanao fanya kazi za kuendesha mashine kujenga madaraja kuweka lami ni wakina nani? Waswahili! Wasimamizi ni Konoike lakini ni mara chache kuwakuta kwenye site, foremen na mainjinia wa ki-Tanzania ndiyo wanafanya kazi zote zile kufuatia michoro.

Sasa wachukuwe ma-Foremen wote pale, mashine zote na Mainjinia wote na wafanyakazi wote, wape barabara nyingine wakaijenge bila ya kusimamiwa na wa Japan/Wachina uone kitakacho tokea. Kwanza wafanya kazi wata angalia uhadirifu wa wakubwa zao na kama wanawajali shida zao au la, kama wakubwa zao hawafanyi mambo ya wizi wizi au la! Wakisha jilidhisha kwamba mambo yote swali watachapa mzigo bila ya mizengwe, lakini wakigundua kwamba wenzao wamewazidi kete, hakuna litakalo fanyika kiufanisi wataboronga kimaksudi kila kitu; na hili ndilo tatizo letu kubwa wa Tanzania, tunapashwa kubadilika. Wachina wakirudi na kufanya niliyo pendekeza hapo juu kuhusu TAZARA mtaona maajabu. God bless TANZANIA na Jakaya.
 
Mheshimiwa Nundu ambaye nina imani naye, kwamba ana nia thabiti ya kujaribu kuleta ufanisi kwenye reli hii ambayo aina mfano we katika Africa nzima save Egypt na South Africa. Tatizo kubwa la shirika hili ni Uongozi mbovu uliyo jaa majungu wizi na kupigana vita na blantant nepotism, TAZARA is more of scientific entity lakini imegeuzwa na viongozi wake ambao hawana uchungu na reli hii na wengi wao wanawekwa pale kwa shinikizo la marafiki zao HUKO JUU. Wanacho sahau ni kwamba it takes ages to train a railwayman - Wachina hawakuwa wajinga! Huwezi kumleta mtu kutoka barabarani ukafanya make shift on the job training alafu ukategemea kwamba kiumbe huyu atafanya miujiza, how? Mambo ya TAZARA yanashangaza sana; we fikilia Wachina walikuwa na uzoefu wa zaidi ya miaka sabini na ushee katika uendeshaji wa Reli nchini mwao, walipomaliza ujenzi wa reli ya TAZARA waliacha wame-establish ORGANIZATION CHART(ORGANOGRAM) ya jinzi ya ku-run TAZARA kwa ufanisi; Wachina walipo ondoka TOP Management ikaona CHART inawabana sana wakafanya mbinu za kutafuta consultant of "questionable merit" hili waifumulie mbali, nini kilitokea baadae - viongozi waliambiwa kila kiongozi atafute mfanyakazi ambaye ataelewana nanaye kikazi!!! Dunia ya leo mtu unawezaje kutoa a skewed directive kama hizo, matatizo ya TAZARA yalianzia tangu hapo na chati imebadilishwa mara lukuki kutegemea who is in POWER - Mh Waziri Nundu (MB) wambie uongozi wa TAZARA ukupatie ORGNOGRAM iliyo achwa na Wachina, wasikuletee zao za kuhunga hunga - nalisema hila kwa nia safi kwa sababu niko attached na shirika hili morally na wala simsemi mtu vibaya.

Juzi juzi nilimsikia Mheshimiwa Raisi wa JMT Mh.JK akisema wazi wazi kwamba tatizo la TAZARA ni Uongozi si kitu kingine, hiyo ni kweli tupu. Kwa nini Wizara inakubali kulete mtu kutoka nje ya Shirika au mtu ambaye hajawahi kukaa kwenye shirika kwa muda mrefu na wala hana handon experience ya kuendesha reli (ambaye si-railman perse) mkakubali kumkabidhi reli bila ya kufikilia mara mbili! Unategemea nini mtu ambaye hana ujuzi wowote katika uendeshaji wa reli kawekwa tu pale kwa kujuwana na Higher Authority bila ya merit zozote katika uendeshaji wa reli; watu wa aina hiyo at the end of the day wanakuwa obssed kuangalia ni mtu gani ambaye ni tishio kwake hili amuondoe kwa mbinu zozote zile kwa kuwa ajiamini aliwekwa pale kwa upendeleo tu. Tatizo hili limei-cost sana TAZARA, kuna wafanyakazi ambao wanajulikana kwa ubunifu wao mkubwa lakini wamewekewa kibano au wanatupwa tu in the middle of nowhere. We viongozi wambie mambo ya TENDER na kuhuza mali za TAZARA kwa bei chee mpaka viwanja na majengo kidogo wahuze karakana, wamekazania kuhuza mali za shirika upande wa Tanzania lakini upande wa Zambia mali zao ziko intact; shirika limekuwa shamba la bibi no accountability hawana ubunifu wowote KIBIASHARA zaidi ya political rhetoric, kuwalaumu Wazambia kila saa as if wakiondoka wao basi Shirika lita anza ku-tic, Uwongo mtupu. Call Zambians anytime of the day utakuta wote wako highly organised na ndiyo maana wanakuwaga na hoja za kuwapiku waswahili-take a look kwa Watanzania ukihitisha mkutano wa kushtukiza say, utasikia kila mtu anazungumza la kwake completely out of SYNCH, wenzetu wanakaaga kila wiki kupanga mikakati i.e the way forward, waswahili walaa! wako kupigana vita wenyewe kwa wenye na kuharibiana sifa; Wazambia wanacho fanya ni ku-exploit to maximum kutoelewana kwa Watanzania kwa Watanzania, we are not justified kuwalahumu Wazambia-kumbe wafanyeje?

Wapunguze endless production meetings ambazo huwa hazina tija na nyingine hazina minutes, na cha kushangaza Serikali zetu zinaonekana kusuwa suwa katika swala la ku-address ombwe la Uongozi katika Shirika, aibu tupu maika hii 30 plus tangu kuanzishwa kwa TAZARA bado tunakwenda kukinga bakuri kwa Wachina!

Siku nyingine ntazungumzia karakana ya Tazara ambayo ni one of the biggest in Eastern and Southern Africa save Egypt and South Africa, inahuwezo wa kuhunda kuanzia sindano ya kushonea nguo mpaka a BATTLESHIP, nenda kaingalie sasa hivi imukuwa kama mahame, ubunifu wa kuitumia kwa ufanisi hakuna! wanashindwa na vijikarakana vya wasomali vinavyo hunda Fuel/Oil Tanks, matrailer and what have you, mashine za ku-fabricate vitu hivyo ziko idle TAZARA karakana, they have a modern laboratory ya (Metallugy,metrology, Chemical na Insrumentation) a modern forge and foundary Shop - mtu mwenye ubunifu akiwa na hazina kama hiyo atahunda kitu chochote Duniani, inauma sana. Niliwahi kutembelea kiwanda cha kutengeza magari ya FORD kule Liverpool na cha Landrover Solihull Midland - nakwambia eneo la viwanda hivyo aliwezi kuzidi Tazara karakana-all Chinese efforts have gone to waste under our watch- tatizo letu ni nini hasa!


si tatizo la TAZARA tu, hata Rais mwenyewe akitaka kuteua wakuu wa mikoa, wilaya, mabalozi wa nchi za nje mara nyingi anawateua rafiki zake na si wale walio katika mifumo au idara husika. Kwa mfano wizara ya mambo ya nje utakuta mtu ameitumikia wizara maisha yake yote mpaka kufikia kiwango cha kuwa msaidizi wa balozi na ana uzoefu mkubwa tu, lakini wakati wa kuteua mabalozi wapya utakuta watu hao hawapewi promotion na kuwa mabalozi kamili badala yake Rais anatafuta marafiki zake walioshindwa kura za maoni au nyakati za uchaguzi mkuu. Hili ni tatizo kubwa linaloanzia Ikulu na si TAZARA tu,
 
I greatly appriciate the support and friendship of people of china,but i am sometimes suprised,walitujengea reli ya Tazara (kwa wale wanaoifahamu au walishasafiri kwenye reli hiyo watakiri kwamba ilijegwa kwa ustadi mkubwa) wachina walitumia fedha zao nyingi sana na watu wake wengi walipoteza maisha.leo ni aibu sana kupewa msaada wa kuifufua.tulishindwa kuitunza na kuiendeleza iendane na wakati,binafsi naona hii ni aibu kubwa kwetu tanzania,tuwe wazalendo tuwajibike kulinda mali zetu wanatushangaa sana

Nakubaliana na wewe 100% ni aibu kubwa sana, tumeshindwa kila nyanja. Viwanda tumeua, reli tumeua, mashamba tumeua. Wakipewa wawekezaji tunalalamika.

Toka lini mtumwa akawa master? labda maandiko yabadilike. Tutabaki kuwa watumwa daima, in one way or another.

Omba omba wa kungoja kila kitu tufanyiwe, hata tukikosa fedha za kujikimu tunalalamika kuwa Serikali haijatufanyia, itufanyie nini zaidi ya kutuwekea viwanda, reli, mashamba na sisi wenyewe ndio tunashindwa kuyaendesha.

Hiyo reli hata wachina wakiifufuwa na kuifanya ya kisasa zaidi, bila wao kukaa kui manage, itakuwa ni kazi bure tu, tutaifanya kama mavi baada ya muda si mrefu.
 
Mkuu you are a megatimes right unacho zungumza hapa, mtu ukiyafikilia sana mambo ya sisi Wafrica unaweza ukasema maneno ya kufuru - tunashangaza sana! Swali ni je kama sisi tunajishangaa je wafadhili wanatuonaje.

Swala la TAZARA tukitaka ufumbuzi wa haraka haraka wafanye yafuatayo FASTA:


  • Managing Director awe Mchina Mwenyewe na awe na kauri ya mwisho katika uendeshaji wa Shirika. Deputy wake siyo lazima awe Mtanzania ua Mzambia awe mtu yeyote mwenye uwezo hata akiwa Mzungu na afanye kwa contract ya miaka mitatu mitatu, akifanya umangameza afumuliwe fasta na hiyo iandikwe kabisa kwenye contract yake.



  • Chief Engineer Mechanical awe Mchina.



  • Chief civil Engineer awe mchina.



  • Supplies Manager awe Mchina.



  • Chief Signallling and Telecommunication Engineer awe Mchina, na idara hii iunganiswe na ICT. Idara hii iwe independent hisichanganwe na CIVIL.



  • Finance Director awe Mchina, na actually hii ni ya pili katika umuhimu wa kufanyiwa kazi na Serikali zetu FASTA.



  • Idara ya TRAFFIC apewe Mchina hili Mambo yanayohusu rolling stock-yaani mabehewa ya aina zote closed/open/flat na Fuel/Oil tanks, na kuwepo na uwezo wa kuya-track anytime yajulikane yako wapi kama yako nchini au yamekwisha kwenda Zambia au Congo, kumbuka reli hizi gauge zake ni sawa kwa hiyo ni rahisi mabehewa kupelekwa kokote mpaka South Africa au Zimbabwe bila kujulikana yalipo, kuna wakati Fuel Tanks za TAZARA zilipo kuwa zinapelekwa Congo, wa Congomani wanazigeuza kuwa underground fuel TANKS kwenye vituo vya kuhuzia mafuta (nakwambia kuna visanga vya ajabu sana TAZARA). La pili hili kupunguza ujanja(wizi) unaotumiwa na wakubwa kukosesha Shirika mapato, tracking system ya mabehewa ifufuliwe-iliuwawa kimaksudi hili kuwe na urahisi wa kuchezea mabehewa, tatizo hili la kugombania mabehewa ni SUGU sana katika shirika hili na bila kujua mabehewa yako wapi na yako mikononi mwa nani at any given time, bila Serikali zetu mbili kuwa wakali katika hilo usugu wa ukata hautakwisha TAZARA. Kitanzi cha ukata wa TAZARA kinatokana na ku-abuse sector hiyo muhimu lakini watu wa Wizarani hilo hawalioni au ku-question, maanake bila mabehewa kutumika kiufanisi bila mambo ya ujanja ujanja (siyo ujanja ni wizi) TAZARA haiwezi kupata mapato ya kuiwezesha ku-run ki-ufanisi, kumbuka mabehewa ndiyo yana generate REVENUE. Revenue zinazo patikana kwa kusafirisha abiria ni negligible inabaki kuwa service tu. Mabehewa ya mizigo ndiyo uti wa mgongo wa TAZARA wahusika mlikumbuke HILO.



  • Weighbridges zote zifanyiwe Calibration na watu wahadirifu siyo marafiki zao - ku-overload mabehewa kumiharibu sana ma-springs ya mabehewa na kuitia hasara kubwa TAZARA, mizani hii inachezewa SANA,
    na hii huwa inachagia sana kwenye ajali za kila mara wakati mahehewa yakikosa balance kwa kuvunjika springs, sijuhi accident analysis wasifanyazo zanasaidiaga nini kupunguza ajali hizi! hukuna.

Serikali zetu hasipashwi kuleta Wachina lukuki kama enzi za kujenga reli ya TAZARA, Serikali zikichezesha karata nilizo taja hapo juu kutatokea mabadiriko ya ajabu in no TIME, haya ni mambo ya kisakolojia tu nina maana wafanyakazi wakisha juwa kwamba watu waliopo madarakani ni wahadirifu na wazalendo au wageni nakuhakikishia watafanya kazi kwa bidii na ufanisi bila ya kusimamiwa.

Tusiande mbali kuangalia sakolojia inavyo fanya kazi - chukulia mfano wa barabara inayojengwa ya kuanzia Mwenge kwenda Tegeta inajengwa kwa ufanisi mkubwa sana na kasi ya ajabu-ebu angalia watu wanao fanya kazi za kuendesha mashine kujenga madaraja kuweka lami ni wakina nani? Waswahili! Wasimamizi ni Konoike lakini ni mara chache kuwakuta kwenye site, foremen na mainjinia wa ki-Tanzania ndiyo wanafanya kazi zote zile kufuatia michoro.

Sasa wachukuwe ma-foremen wote pale mashine zote na mainjinia wote na wafanyakazi wote wape barabara nyingine wakaijenge bila ya kusimamiwa na wa Japan uone kitakacho tokea. Kwanza wafanya kazi wata angalia uhadirifu wa wakubwa zao na kama wanawajali shida zao au la, kama wakubwa zao hawafanyi mambo ya wizi wizi au la! Wakisha jilidhisha kwamba mambo yote swali watachapa mzigo bila ya mizengwe, lakini wakigunduwa kwamba wenzao wamewazidi kete hakuna litakalo fanyika kiufanisi wataboronga kila kitu; na hili ndilo tatizo letu kubwa wa Tanzania, tunapashwa kubadilika. Wachina wakirudi na kufanya niliyo pendekeza hapo juu kuhusu TAZARA mtaona maajabu. God bless TANZANIA.

Mkuu ukweli ni kuwa matatizo tuliyonayo Tanzania hayatokani na kukosa akili au kuwa wavivu. Kama kukiwa na proper management and administration, kuna mifano mingi tu inayoonesha kuwa watanzania can do things. Yes kuna watanzania wavivu, kuna watanzania wezi, lakini pia kuna watanzania wengine wengi tu wanaoweza kufanya kazi vizuri. Mzizi wa fitina uko kwenye uongozi na usumamiaji wa utekelezaji wa kazi.
 
Mkuu ukweli ni kuwa matatizo tuliyonayo Tanzania hayatokani na kukosa akili au kuwa wavivu. Kama kukiwa na proper management and administration, kuna mifano mingi tu inayoonesha kuwa watanzania can do things. Yes kuna watanzania wavivu, kuna watanzania wezi, lakini pia kuna watanzania wengine wengi tu wanaoweza kufanya kazi vizuri. Mzizi wa fitina uko kwenye uongozi na usumamiaji wa utekelezaji wa kazi.

Nakubaliana nawe 100% Mkuu na ndiyo maana nikatoa mfano wa Ujenzi wa barabara ya Mwenge kwenda Tegeta kwamba wajenzi ni wa Tanzania, ninacho zungumza humu ni kule kukosa uhadirifu siyo kwamba wa Tanzania ni mbumbumbu au wote ni wavivu la asha, actually wa Tanzania ni wabunifu sana na wanaheshimika sana nchi za nje kama vile Botswana, Namibia nk. Ukweli wa mambo ni kwamba watu wenye uwezo hawatakiwi nchi hii, watakufanyia vitimbwi mpaka uhache kazi au uhame kabisa nchi. Ukiangalia utaona nilisema tangu mwanzo nakuweka wazi kwamba wa Tanzania wenye uwezo wa kui-run TAZARA kiufanisi wapo. List niliyoweka hapo juu kuhusu Wachina watakao saidia kufufua TAZARA aina maana kwamba ndiyo basi Watanzania na Wazambia hawatakiwi kwenye top Management, hilo siyo lengo langu mimi nawajua wa China ni watu wadadadisi sana na wanajua watu wanaojua kazi na wenye uwezo na watu wababaishaji, nakuhakikishia ndani ya mwaka mmoja Wachina watakuwa mamekwisha juwa ni Mswahili gani au Mzambia aende wapi na kwa wadhifa gani - jamaa hawa ni mahili sana katika hilo - wala usiwe na wasi wasi.
 
Ukitafiti kwenye majarida ya kitaalamu unaambiwa kuwa Tazara ni reli bora zaidi kujengwa duniani baada ya Vita Kuu ya Pili (1945). Ina maana kuwa zile reli zote kabambe za Ulaya na Amerika zilijengwa zamani. Lakini kwa reli zote za nusu ya pili ya karne ya 20 na hii karne tuliyonayo, Tazara ndiyo reli bora zaidi kwa usalama na miundombinu. Bado inaendelea kuelezwa kuwa stesheni ya Dar es Salaam ni kubwa zaidi kuliko stesheni zote Afrika. Namaanisha kubwa kijengo. Lakini ni reli yenye huduma mbovu kabisa. Jana nimesikia redioni kuwa safari iliyokuwa ifanyike jana 13.50hrs imeahirishwa hadi leo 13.50hrs. Delay ya masaa 24. Wananchi wanateseka vipi?

Tuje kwenye hali za wafanyakazi. Ukitazama hali zao unaweza toa machozi. Wafanyakazi huko Lumumwe, Uchindile, Kidunda, Mzenga, Yombo, Makambako na kwingineko wana maisha ya dhiki sana. Mishahara yao inaishia kulipa madeni. Shirika haliwajali kabisa wafanyakazi wake. Hawasikilizwi. Hawapewi nafasi. Mfanyakazi akifanya jitihada ajiinue kidogo kwa juhudi binafsi, viongozi watamwandama sana. Viongozi wa Tazara hawataki mfanyakazi hata ajiendeleze kitaaluma. Wakisikia unasoma lazima upewe uhamisho kwenda stesheni za mbali huko porini. Shirika limejaa chuki na ubinafsi.

Kwa maisha hayo tija itatoka wapi? Tazara kuna miungu-watu. Watu wanaogopwa kuliko Mungu aliye hai muumba wa mbingu na dunia. Uongozi wa Tazara umejaa roho mbaya kuliko maana yenyewe ya neno mbaya.

Tazara walikuwa na rasilimali nyingi. Zote wameuza. Pale Kurasini kulikuwa na Material Base, yadi kubwa ya kuhifaddhia mizigo. Kubwa kuliko hata bandari. Wamemwuzia mhindi wa Tanzania Road Haulage (TRH). Leaders club ilikuwa mali ya Tazara, wameuza. Lile jengo la Tanzania Heart Institute lilikuwa hostel ya Tazara, wameuza. Wameuza mali nyingi mno hado aibu. Tazara inasikitisha.

Leo Tazara wanakodi mabehewa toka Railways System of Zambia (RSZ) shirika la Zambia wakati wao wana mabehewa zaidi ya 1400. Wanakodi hadi injini (locomotives) kutoka RSZ wakati injini za Tazara ni U30C zenye horse power 3000 zilizotengenezwa na General Electric ya USA na Krupp ya German. Ni injini zenye nguvu kuliko zozote zinazotumika Afrika. Tazara imelaaniwa.
Mabehewa ya Tazara yanatia huruma. Tazama mabehewa ya abiria yaliyoletwa 1995 leo ni scrapper na mitambo ya tetanus. Tazara haioni aibu kwa Rovos Train ya South Afica ambayo mabehewa yake ya miaka ya 1947 lakini bado ni mazuri sana.

Nina mengi sana ya kueleza juu ya Tazara. Nitaeleza wakati mwingine nitakapopata nafasi. Mara nying nafikiria kuandika kitabu kuelezea hili shirika ambalo waasisi wake Mwalimu Nyerere, Kaunda na Mwenyekiti Mao walikuwa na dhamira nzuri sana ya kulianzisha.
 
"By Tukuyu' Tazara ndiyo reli bora zaidi kwa usalama na miundombinu. Bado inaendelea kuelezwa kuwa stesheni ya Dar es Salaam ni kubwa zaidi kuliko stesheni zote Afrika. Namaanisha kubwa kijengo. Lakini ni reli yenye huduma mbovu kabisa. Jana nimesikia redioni kuwa safari iliyokuwa ifanyike jana 13.50hrs imeahirishwa hadi leo 13.50hrs. Delay ya masaa 24. Wananchi wanateseka vipi?

Mkuu kuna wakati nilitembelewa na rafiki yangu kutoka nchi ya ng'ambo, wakati tuko garini kutoka kiwanja cha ndege alipo liona jengo la station ya TAZARA akaniuliza eh Bwana eh, hivi hapa Dar-Es-Salaam mna International Airports ngapi! Nikamwambia ni moja tu-kaniuliza kwani jengo hili kumbe ni la kitu gani nikamwabia hilo ni jenga la station ya TRAIN siyo Airport. We fikilia wageni wanasifia mchango mkubwa na azina kubwa tulio achiwa na Wachina, lakini sisi hilo atulioni - tumekazana ku-uproot kila kitu. Tukija kuhusu kuahirishwa kwa safari ya TRAIN jana, siwezi kushangaa nikisikia tatizo lilikuwa na kukosekana (kukosekana kwa fedha za kununulia mafuta on time) ni ajabu na kweli.

"By Tukuyu" Mfanyakazi akifanya jitihada ajiinue kidogo kwa juhudi binafsi, viongozi watamwandama sana. Viongozi wa Tazara hawataki mfanyakazi hata ajiendeleze kitaaluma. Wakisikia unasoma lazima upewe uhamisho kwenda stesheni za mbali huko porini. Shirika limejaa chuki na ubinafsi.

Kwa maisha hayo tija itatoka wapi? Tazara kuna miungu-watu. Watu wanaogopwa kuliko Mungu aliye hai muumba wa mbingu na dunia. Uongozi wa Tazara umejaa roho mbaya kuliko maana yenyewe ya neno mbaya.

Nakuhunga mkono katika hilo, inasikitisha sana na hii limechangia vile vile kudumaza hari/wafanyakazi kuwa frustrated unnecessarily, niliwahi kushudia vijana zaidi ya mmoja wakipewa majibu ya kimkato na ujeuri kutoka kwa Human Resorces Manager as if kwenda kwao kujiendeleza ki-elimu hakuwezi kuinufaisha chochote TAZARA, kumbuka hao wote walikuwa wana taaluma za kiufundi! Si hilo tu mfanyakazi anaweza kuhamishiwa HQ kwa mfano lakini HRM kama ana chuki nawe unaweza kukaa pale bila ya kupata barua yoyote ya uhamisho hata kama Head wa Dpt husika amukumbushe vipi anakaa kimya au kuficha faili lako, mtu huwezi kuamini mambo haya! Walikuwa wanafikia hatua ya kuficha mafaili ya watu chini ya carpet, and he didn't give a damn! lakini Mungu mkubwa naye alikuja kuondolewa pale kwa shinikizo la wafanya kazi, lakini alikuwa amejisahau mno mtu ungefikili labda na yeye ni share holder wa TAZARA-very arrogant.

'By Tukuyu' Tazara walikuwa na rasilimali nyingi. Zote wameuza. Pale Kurasini kulikuwa na Material Base, yadi kubwa ya kuhifaddhia mizigo. Kubwa kuliko hata bandari. Wamemwuzia mhindi wa Tanzania Road Haulage (TRH). Leaders club ilikuwa mali ya Tazara, wameuza. Lile jengo la Tanzania Heart Institute lilikuwa hostel ya Tazara, wameuza. Wameuza mali nyingi mno hado aibu. Tazara inasikitisha.

Mkuu we fikilia walikazania kuhuza mali karibu zote za TAZARA upande wa TANZANIA na siyo Zambia kwa nini? mimi wala si walahumu Wazambia, kumbe wafanye nini kama sisi Watanzania hatujali mali zilizo upande wa kwetu. Mkuu unajua dalali mkubwa aliyesuka deal hizi, kwa kushirikiana na viongozi ambao hawajali mali za TAZARA upande wa TANZANIA wakahuza mali hizi kwa bei ya chee! Je mtu huyu alikuwa ni nani?- MTANZANIA aliye ajiliwa TAZARA, kwa sasa hivi amekwisha ondoka lakini mtu mwenyewe alikuwa na eti "taluma ya SHERIA!"

Sasa kama Serikali zetu ziko serious na jambo hili la kuhuza mali ya SHIRIKA ki holela na kwa bei ya sawa na kutupwa, basi wa-revisit procedures zote zilizo tumika ku-despose off mali za shirika-watafute an indepedent mthamini (Govt Agency preferrably) a go-through mali zote zilizo kwisha huzwa aone kama fedha zilizo lipwa na watu/makampuni kwa TAZARA zinalingana na thamani halisi za mali hizo. Nakuhakikishia watakuta mambo ya hajabu sana, alafu mtu na akili zako timamu unawezaje kuhuza Kurasini material BASE? Mimi sijuhi Wachina watatuona sisi ni binadamu wa aina GANI! Kuhuza Kurasini material base nijanga la kitaifa lakini naona Serikali zetu hilo hawalioni au sijuhi hawajuhi hiyo Material Base alijengwa pale na Wachina kwa madhumuni GANI! Ignorance wakati mwingine inaweza ku-cost an arm and leg; bila BASE hile unafikili uendeshaji wa Shirika utakwenda sawa sawa kweli? Nachelea kusema kwamba uhuzaji wa Kurasini ni hujuma na kosa la jinai, wote walio husika na hujuma hiyo wanapashwa kufikishwa kwa Pilato. Huyo Mhindi anapashwa kuwekwa to-task mpaka aeleze alivyo huziwa Kurasini na ni nani walihusika hili wachukuliwe hatua FASTA. Nchi hii haiwezi kuendelea huku inahujumiwa na watu wasio wahaminifu na ukosefu wa UZALENDO. Kurasini ni janga la kitaifa lakini sijawahi kusikia mtu yeyote analizumgumzia hilo.

'ByTukuyu' Leo Tazara wanakodi mabehewa toka Railways System of Zambia (RSZ) shirika la Zambia wakati wao wana mabehewa zaidi ya 1400. Wanakodi hadi injini (locomotives) kutoka RSZ wakati injini za Tazara ni U30C zenye horse power 3000 zilizotengenezwa na General Electric ya USA na Krupp ya German. Ni injini zenye nguvu kuliko zozote zinazotumika Afrika. Tazara imelaaniwa.

Mkuu wala hilo husilishangae Wazambia ni wajanja wanataka kunufaisha Taifa lao, kwani mabehewa na locomotives zikikodishwa kutoka shirika la Zambia (RSZ) wanao faidi ni nani - Wazambia of course. Nakwambia hawa jamaa walisha tusoma siku nyingi na kujua hulka zetu sisi Watanzania za kutokua makini sana kwa kuhoji mambo yanayo kwenda ndiyo sivyo. Kwani kazi ya Deputy Managing Director ni nini si kuangalia maslahi ya Tanzania kwanza alafu TAZARA, huyu ni mtu mwenye akili sana lakini sijuhi Wazambia huwa wanamzidi kete kivipi au na yeye anajikuta yuko peke yake nini? Kwa nini swala kama hili alifikishi Serikalini! Kuna wakati fulani mtu na mkewe wakawa among ya ma-signatory wa cheque za TAZARA-wewe uliwahi kusikia wapi dunia hii ethics za ajabu kama hizo kikazi, hilo linafanyika wakati Deputy Managing Director Mtanzania (ambaye amekwisha retire) yupo lakini alikaa kimya anaona kitu kama hicho ni sawa tu.

Titizo kubwa lingine ni hili la kupoteza muda mwingi kwenye mambo ya witch hunting kwa ku-instigate trade union kuleta vurugu kwamba Wazambia hawafahi as if wakiondoka ndiyo TAZARA itafanya kazi ki-ufanisi hiyo siyo kweli (nakubali kuna baadhi ya Wazambia kama ilivyo kwa Watanzania wanafanya mambo ya kulihujumu shirika lakini si wote), nakwambia bila ya attitude za sisi Watanzania kubadilika hakuna kitakacho endelea. Trade unions zinapashwa kuwa makini sana, watu crafty wanaweza kuwatumia bila ya wao kujijuwa kwa ajili ya maslahi yao binafsi na wala si kwa manufaa ya TAZARA, mimi nilisha fanya analysis kuhusu hili kwa muda mrefu sana nikagundua kwamba kunaweza kuwa na tatizo kweli lakini mambo mengi ni kwa ajili ya ku-serve self interests za watu fulani na si kitu kingine; kuweni wangalifu.


'By Tukuyu' Mabehewa ya Tazara yanatia huruma. Tazama mabehewa ya abiria yaliyoletwa 1995 leo ni scrapper na mitambo ya tetanus. Tazara haioni aibu kwa Rovos Train ya South Afica ambayo mabehewa yake ya miaka ya 1947 lakini bado ni mazuri sana.

Mkuu wewe si unajua karakana ya TAZARA ya DSM licha ya ku-repair mabehewa na ma-coach ina huwezo mkubwa wa kuhunda mabehewa kuanzia kwenye super structure, si wana kila kitu pale in terms of machinary a modern carpentary shop and what have you, kitu ambacho wangeagiza nje ni wheel sets tu labda na shock absorbers lakini springs za aina zote wana machine za kuzi-coil na kuzi-heat treat(komaza), kupiga rangi etc, Wachina walikuwa wamefundisha watu ufundi wa hali ya juu sana kwani nani anajali hilo? hapa tunazungumzia wagons zote including Tanks za mafuta, nazo zinaweza kuhudwa pale Karakana machine za kukunja mabati ya saizi zote zipo, hawashindwi chochote pale - kinacho takiwa ni ubunifu na kuona mbali.

'By Tukuyu' Nina mengi sana ya kueleza juu ya Tazara. Nitaeleza wakati mwingine nitakapopata nafasi. Mara nying nafikiria kuandika kitabu kuelezea hili shirika ambalo waasisi wake Mwalimu Nyerere, Kaunda na Mwenyekiti Mao walikuwa na dhamira nzuri sana ya kulianzisha.

Katika hilo tutasaidiana Mkuu, kama tunayo eleza humu yanaweza kumaliza umangameza wa TAZARA na Shirika likafanya kazi ku-ufanisi mbona ntafurahi sana-tusiwachie watu wachache wasiyo wazalendo kulifanya shirika kama shamba la BIBI. Mungu ibarika Tanzania na Jakaya kwa kuona mbali, maanake bila effort zake Wachina wasingetia mguu TAZARA eti "KUIFUFUA" - niliwahi kuzungumza na mama mmoja Professor wa Kichina aliye kuwa ameolewa na Managing Director (Mchina) counterpart wa MD wa TAZARA, aliniambia wazi wazi kwamba Chinese Govt haiko interested na kuhiendesha TAZARA kwa hali ilivyo, akasema China haina kipingamizi kama watapatikana watu Private wakuliendesha Shirika - well and good. Wachina walisha fikia kukatishwa tamaa na undeshaji husiyo ridhisha wa TAZARA.

Kwa hiyo nikisema Jakaya must have played a big role kubadirisha mawazo ya Wachina najuwa ninacho zungumza, nimelisema hili maanake watu wanaweza kuleta mambo ya siasa kwenye mambo serious kwa kudhani nampigia debe Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, huyu mtu anaona mbali sana ingawa watu wengine wanamfikilia vitu vingine tofauti kabisa.
 
Bukyanagandi ahsante sana kwa mchango wako. Tazara itakombolewa na watu wenye mawazo ya kimaendeleo na kimapinduzi kama yako. Nadhani tunapaswa sasa kukaa chini na kutoa michango yetu ya kifikra ili hili shirika ambalo ni lulu kubwa kwa Watanzania likombolewe.

Umenikumbusha kuhusu Karakana ya Dsm. Hiyo ni karakana ya aina yake hapa Afrika Mashariki. Ni karakana yenye uwezo wa kutengeneza hata vipuri vya magari. Kama uonggozi wa Tazara ungekuwa na mawazo endelevu leo hii Tazara lingekuwa shirika linalofanya biashara zaidi kuliko shirika lolote. Leo hii Tazara ingeweza hata kuzalisha umeme na kuiiuzia Tanesco. Leo Tazara ingeweza hata kumiliki ndege zake. Leo Tazara ingekuwa mbali.

Tuje kwenye majengo ya Tazara pale DSM station, TCPC na Head Office. Nilishawahi mshauri bosi moja wa idara ya commercial kabla sijaondoka Tazara. Nikamwambia hakuna haja ya matumizi mabaya ya maofisi kwenye yale majengo. Unakuta kuna maofisi kibao yamegeuka stoo za makapeti mabovu na uchafu mwingine.

Unakuta kila mtu ana ofisi yake tena kwa position zisizo na tija. Nikashauri kuwe na mfumo wa office sharind. Kwa mfano labda ofisi moja inatumiwa na watu wawili ama watatu kwa kuwa ni ofisi kubwa sana zile. Tuache tu wakuu wa idara. Tena kwa mfano watu wa Operations na Commercial wote wanapewa maofisi kule DSM station. Wanabaki labda HO, Regional Controller na Control Office. Then, kwa mfano pale TCPC wanakuwa wamesevu upande moja mzima wa lile ghorofa. Upande unaobaki wanapangisha maofisi kwa makampuni mengine.

Nakuhakikishia wateja wengi sana watapatikana kwa kuwa Tazara ina eneo la parking kubwa sana. Makampuni mengi hayapendi kuwa na ofisi kule Posta kutokana na msongamano. Tazara ingetoa alternative nzuri sana. Tazara ipo eneo very potential. Junction ya airport, bandari, posta na ubungo.

Vivyo hivyo ingekuwa kule Head Office. Tatizo umangimeza kila mtu anataka awe na ofisi ya kwake peke yake ili afanye ushirikina na uzinzi kwa uhuru zaidi.

Tuna mengi ya kujadili. Tunapaswa kuyajadili sana.

Ahsante sana kwa mchango wako mkuu.
 
Back
Top Bottom