CHINA kutoa Dola bilioni 20 kwa Africa: Pigo kwa US na ULAYA?

Pasco_jr_ngumi

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
1,802
282
Rais Hu Jintao, Uchina ameziahidi serikali za Afrika mkopo karibu dola za Marekani bilioni 20 kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Amesema kuwa mkopo huo utasaidia katika ujenzi wa miundombinu, kilimo na maendeleo ya biashara. Rais Jintao aliyasema hayo wakati wa mkutano wa ushirikiano baina ya Uchina na viongozi wa Afrika mjini Beijing.

Kuanzia barabara mpya za mjini Nairobi hadi wauza kuku katika soko la Zambia ni dhahiri kwamba Uchina imeweka nyayo zake katika kuinua uchumi wa Mataifa mengi barani Afrika.

Miundombinu ni mojawapo ya sehemu ambazo Uchina imewekeza vilivyo barani Afrika.

Biashara kati ya Bara Afrika na Uchina imeongezeka kutoka dola bilioni 10 miaka kumi iliyopita na kufikia takriban dola bilioni mia moja na sitini hii leo.

Nchi hiyo imetoa mikopo zaidi kuliko Benki ya Dunia. Baadhi ya viongozi wa mataifa ya Afrika wamefurahia uhusiano huu wakisema kuwa utakomesha tabia na hali ya kukaliwa na Mataifa ya magharibi kiuchumi na kisiasa kwa masharti
yanayoambatana na mikopo hiyo.

Kwa upande mwingine Uchina imeshutumiwa na nchi za magharibi kama yenye tamaa, hali inayoifanya kupuuza haki za utu na kupendelea maendeleo ya kiuchumi na mahitaji yake ya nishati.

Mataifa ya magharibi hayajasita kuinyooshea kidole Uchina kama Mkoloni mpya wa Afrika, kwa kutangaza rekodi yake ya ukiukaji wa haki za binadamu kwa kisingizio cha kuitojiingiza katika masuala ya ndani ya nchi wanakoendesha shughuli zao.

Mfano uliopo ni nchini Sudan ambako mashirika ya kutetea haki za binadamu yamekosoa uhusiano na Uchina, licha ya vitendo vya unyanyasaji vinavyoendelea huko Darfur.

Mashirika hayo yanaongezea kusema kuwa Uchina imesaidia katika kuchochea ghasia kupitia msaada wake wa fedha, silaha na sera. Kwa upande wake Uchina imesisitiza kuwa itaendelea na sera yake ya kutoingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine.

Mpango wa Uchina kwa Afrika ni bayana. Ina hamu ya maliasili kutoka Bara hilo pamoja na soko la bidhaa zinazotengenezwa Uchina. Vilevile, Uchina inataka kudhibiti ushawishi wake wa kibalozi ulimwenguni kwa msaada wa Afrika. Hivyo ndivyo hali ilivyo kuhusu miradi ya Uchina kwa Afrika ambapo watu wengi hudhani kuwa Uchina ndiyo inayodhamini miradi yote.

Benki ya Maendeleo ya Afrika, ADB huenda ikahisi kuwa Wachina wameipokonya hadhi yake kutokana na kwamba watu wengi wanaonelea hata miradi ya Benki hiyo na kudhani imedhaminiwa na Wachina, ingawaje fedha zimetoka kwenye Benki hiyo lakini
wahandisi na wajenzi ni Wachina.

Viongozi wa Kiafrika hukumbushwa kuhusu mshirika wao mpya wanapokwenda Addis Ababa kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika. Jengo kabambe la kisasa lililojengwa kwa vioo na mawe kwa gharama ya dola milioni 200 lilidhaminiwa na Uchina, bila shaka.
 
Hapa Kiuchumi, jamaa anakamata makoloni AFRIKA... Akitupilia mbali Demokrasia ya magharibi, yeye anawaza zaidi UCHUMI na harakati ya kuotawala dunia...

Pembeni USA akihangaika kuitawala dunia KISIASA, wacha tuishi miaka mingi tuone mambo mengi!!!!!!!
 
Ndugu yangu US na jamaa wa Ulaya wanazikodolea macho hizo hela wanatamani wangepewa wao...Ulaya si Ulaya tuijuayo tena ndio inaelekea kwisha. Leo hii hata Angola wanakwenda ku-bailout nchi iliyokuwa inawatawala kimabavu, South Africa wanaikopesha IMF ....China, Brazil, India na Russia ndio tegemeo lililobaki. Huko Ulaya Ujerumani imezidiwa kila mtu anataka msaada....:hat:

Ni kweli tutaona mengi safari hiii....:hat:
 
Ahsante kwa kunidadavulia kiundani,

Mchina anawavuta kama na wanavutika vilivyo!! Nguvu na ubavu hawana, wanatapatapa tuuu
 
Pigo ni sisi wajinga wa Kiafrika ambao tumekubali kuwa shamba la bibi. Kama tungekuwa na akili timamu wala tusingekuwa tunajadili misaada ya Uchina, Amerika au Ulaya. Tunapokuwa na mijadala kama hii inakuwa kama vile tumeshakubali sisi Waafrika kuwa malaya ambaye kila bwana anampitia, ila sasa tunajadili ni bwana yupi mwenye dau kubwa. Disgusting.
 
Bahati mbaya hatuna mikakati ya kujinasua hivi karibuni la hili zimwi la ukoloni mambo leo.
 
Pigo ni sisi wajinga wa Kiafrika ambao tumekubali kuwa shamba la bibi. Kama tungekuwa na akili timamu wala tusingekuwa tunajadili misaada ya Uchina, Amerika au Ulaya. Tunapokuwa na mijadala kama hii inakuwa kama vile tumeshakubali sisi Waafrika kuwa malaya ambaye kila bwana anampitia, ila sasa tunajadili ni bwana yupi mwenye dau kubwa. Disgusting.

Msikilize huyu alisemaje?
 
Last edited by a moderator:
120719044804_hu_jintao_304x171_reuters_nocredit.jpg

Rais Hu Jintao, Uchina ameziahidi serikali za Afrika mkopo karibu dola za Marekani bilioni 20 kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Amesema kuwa mkopo huo utasaidia katika ujenzi wa miundo mbinu, kilimo na maendeleo ya biashara.

Rais Jintao aliyasema hayo wakati wa mkutano wa ushirikiano baina ya Uchina na viongozi wa Afrika mjini Beijing.

Kuanzia barabara mpya za mjini Nairobi hadi wauza kuku katika soko la Zambia ni dhahiri kwamba Uchina imeweka nyayo zake katika kuinua uchumi wa Mataifa mengi barani Afrika.

Miundo mbinu ni mojawapo ya sehemu ambazo Uchina imewekeza vilivyo barani Afrika.

Biashara kati ya Bara Afrika na Uchina imeongezeka kutoka dola bilioni 10 miaka kumi iliyopita na kufikia takriban dola bilioni mia moja na sitini hii leo.

Nchi hiyo imetoa mikopo zaidi kuliko Benki ya Dunia.

Baadhi ya viongozi wa mataifa ya Afrika wamefurahia uhusiano huu wakisema kuwa utakomesha tabia na hali ya kukaliwa na Mataifa ya magharibi kiuchumi na kisiasa kwa masharti yanayoambatana na mikopo hiyo.
Kwa upande mwingine Uchina imeshutumiwa na nchi za magharibi kama yenye tamaa, hali inayoifanya kupuuza haki za utu na kupendelea maendeleo ya kiuchumi na mahitaji yake ya nishati.

Mataifa ya magharibi hayajasita kuinyooshea kidole Uchina kama Mkoloni mpya wa Afrika, kwa kutangaza rekodi yake ya ukiukaji wa haki za binadamu kwa kisingizio cha kuitojiingiza katika masuala ya ndani ya nchi wanakoendesha shughuli zao.

Mfano uliopo ni nchini Sudan ambako mashirika ya kutetea haki za binadamu yamekosoa uhusiano na Uchina, licha ya vitendo vya unyanyasaji vinavyoendelea huko Darfur.

Mashirika hayo yanaongezea kusema kuwa Uchina imesaidia katika kuchochea ghasia kupitia msaada wake wa fedha, silaha na sera.

Kwa upande wake Uchina imesisitiza kuwa itaendelea na sera yake ya kutoingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine.

Mpango wa Uchina kwa Afrika ni bayana. Ina hamu ya maliasili kutoka Bara hilo pamoja na soko la bidhaa zinazotengenezwa Uchina. Vilevile, Uchina inataka kudhibiti ushawishi wake wa kibalozi ulimwenguni kwa msaada wa Afrika.

Hivyo ndivyo hali ilivyo kuhusu miradi ya Uchina kwa Afrika ambapo watu wengi hudhani kuwa Uchina ndiyo inayodhamini miradi yote.

Benki ya Maendeleo ya Afrika, ADB huenda ikahisi kuwa Wachina wameipokonya hadhi yake kutokana na kwamba watu wengi wanaonelea hata miradi ya Benki hiyo na kudhani imedhaminiwa na Wachina, ingawaje fedha zimetoka kwenye Benki hiyo lakini wahandisi na wajenzi ni Wachina.

Viongozi wa Kiafrika hukumbushwa kuhusu mshirika wao mpya wanapokwenda Addis Ababa kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika.

Jengo kabambe la kisasa lililojengwa kwa vioo na mawe kwa gharama ya dola milioni 200 lilidhaminiwa na Uchina, bila shaka.
 
Pigo ni sisi wajinga wa Kiafrika ambao tumekubali kuwa shamba la bibi. Kama tungekuwa na akili timamu wala tusingekuwa tunajadili misaada ya Uchina, Amerika au Ulaya. Tunapokuwa na mijadala kama hii inakuwa kama vile tumeshakubali sisi Waafrika kuwa malaya ambaye kila bwana anampitia, ila sasa tunajadili ni bwana yupi mwenye dau kubwa. Disgusting.

Umewahi kumsikia kiongozi wa Afrika akizungumzia hili?

Au hapa

Last edited by a moderator:
Pigo ni sisi wajinga wa Kiafrika ambao tumekubali kuwa shamba la bibi. Kama tungekuwa na akili timamu wala tusingekuwa tunajadili misaada ya Uchina, Amerika au Ulaya. Tunapokuwa na mijadala kama hii inakuwa kama vile tumeshakubali sisi Waafrika kuwa malaya ambaye kila bwana anampitia, ila sasa tunajadili ni bwana yupi mwenye dau kubwa. Disgusting.

Ni kweli kabisa na hii sio tu kwamba inatia "KINYAA" bali ni "AIBU" na "FEDHEHA" kubwa kwa serikali za nchi za kiafrika!
 
Kukiwa na power shift, at least waAfrika tutaweza kutoka kwenye minyororo ya nchi za magharibi. Tulishakosea tokea awali, sasa tukiendelea kuwakumbatia hawa westerns hatutapiga hatua yoyote, vile vile mikopo ya china ni nafuu ukilinganisha na ile ya majambazi WB na IMF...
 
CHINA inatupatia another option. Kama ushindani (competition) ni mzuri kibiashara/kiuchumi ndani ya nchi zetu kama tunavyohubiriwa na nchi za Magahribi, kwa nini usiwe mzuri katika mahusiano yetu ya kimataifa kiuchumi na kibiashara? Wacha Wachina waje washindane na hao wa magharibi. Tutanunua au kumfuata anayetoa nafuu kwetu. Lakini tunahitaji uongozi mpya. Viongozi ambao akili zao hazijafumgwa kwenye box la imani kuwa bila Marekani, Ulaya, IMF, WB, WTO, n.k. Afrika kama bara hatuwezi kumudu maisha. Hawawezi kuona ukweli kuwa bila Afrika hizo nchi/taasisi ndizo zitaumia zaidi. Hawana thubutu ya kuicheza hiyo turufu. Ni ubwege.
 
Hii ni hatua nzuri sana kwa ustawi wa socialism ikiwa ndio mfumo bora wa maisha...Mmataifa ya magharibi yamebaki na propaganda yao ya demekrasia ...
 
Kukiwa na power shift, at least waAfrika tutaweza kutoka kwenye minyororo ya nchi za magharibi. Tulishakosea tokea awali, sasa tukiendelea kuwakumbatia hawa westerns hatutapiga hatua yoyote, vile vile mikopo ya china ni nafuu ukilinganisha na ile ya majambazi WB na IMF...
Huyu Kanali alikuwa anawabembeleza wenzake wa Afrika lakini kasumba ya wazungu ilishawaingia sana. Tunaanza zero baada ya simba wa kweli kupotezwa. Bonyeza link
 
Last edited by a moderator:
Pigo ni sisi wajinga wa Kiafrika ambao tumekubali kuwa shamba la bibi. Kama tungekuwa na akili timamu wala tusingekuwa tunajadili misaada ya Uchina, Amerika au Ulaya. Tunapokuwa na mijadala kama hii inakuwa kama vile tumeshakubali sisi Waafrika kuwa malaya ambaye kila bwana anampitia, ila sasa tunajadili ni bwana yupi mwenye dau kubwa. Disgusting.

Ni ukweli unayo yasema toka Mababu ze kihistoria tumenyonywa na mpaka hii leo akili zetu zimedumaa. Mie naona viongozi wetu wa afrika wote ni ******* na hawana uelewa na uzalendo wao. Ndo maana kila siku wanataka kwenda ulaya,amerika na huko uchina kufanya umalaya wao. Hawana lolote. Mazunghu masenge kweli yanapenda tuchapane yawe yanafanya biashara. Huu ni upuzi. Say no to AIDS and aids.
 
Pigo ni sisi wajinga wa Kiafrika ambao tumekubali kuwa shamba la bibi. Kama tungekuwa na akili timamu wala tusingekuwa tunajadili misaada ya Uchina, Amerika au Ulaya. Tunapokuwa na mijadala kama hii inakuwa kama vile tumeshakubali sisi Waafrika kuwa malaya ambaye kila bwana anampitia, ila sasa tunajadili ni bwana yupi mwenye dau kubwa. Disgusting.

Ni ukweli unayo yasema toka Mababu ze kihistoria tumenyonywa na mpaka hii leo akili zetu zimedumaa. Mie naona viongozi wetu wa afrika wote ni waseeeenghe na hawana uelewa na uzalendo wao. Ndo maana kila siku wanataka kwenda ulaya,amerika na huko uchina kufanya umalaya wao. Hawana lolote. Mazunghu masenge kweli yanapenda tuchapane yawe yanafanya biashara. Huu ni upuzi. Say no to AIDS and aids.
 
Baada ya kuishtukia misaada kutoka nchi za kimagharibi sasa wameanza kutumia uchina. **** me for being under these african governance.
 
China wanajitahidi kujipanua zaidi Afrika maana wanajua kuwa bado kuna rasilimali nyingi ambazo wanazihitaji katika maendeleo yao.
 
Anapoteza nguvu zake Jintao, hizo pesa kama atatoa in cash naziona atleast 50% zinaenda kwenye mifuko ya mafisadi. Mikopo I believe should be in kind, otherwise watakonufaika watakuwa wachache.

Its good news and bad new at the same time, misaada, misaada kila siku tutaendelea au tutaendeshwa hivi mpaka lini. Siku zote sisi watu wa kufikiriwa, hapo hapo tunakaa tukijua tuna all resources so what is lacking.........
 
Back
Top Bottom