Chimba kisima chako mwenyewe

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,108
18,325
kisima.bmp

Uchimbe kisima wewe mwenyewe unywe maji yako peke yako na usiyashiriki nao wengine ni hatari kubwa eeh!

Maji ya kisima cha watu wengi yameingiliwa na mdudu ukiwa na kiu usiyaonje utaambukizwa eeh.

Na kiu ya maji imeongezeka watu wanayanywa kila wakati na yanauzwa kote barabarani nani atapona eeh?

Kwa sababu maji yana mdudu yanapatikana kirahisi ukipita kote utayaona wacha kuyachota eeh.

Tena na siku hizi na hayo maji yaliyo yaliyoingiwa na mdudu utapewa bure bila kuomba ili mfe wote eeh.

Yapo kwenye chupa kubwa na ndogo watu wanazipenda zile ndogo wanafikiliria zipo salama wamedanganyika eeh.

Wanazifunika nusunusu wamefanya hivyo makusudu ili waamushe kiu ya maji usidanganyjike eeh!

Ndugu jihadhari na maji ya rahisi kachimbe kisima wewe mwenyewe ukiwa na kiu uyanywe maji uliypoyachimba heri.

Dawa ya mdudu hawajaipata wanaitafuta kotekote umwamini Yesu akuokoea amalize kiu.

By Faustin Munishi:
 
sawa malenga lakini hukuwa na haja ya kutumia lugha ya mafumbo hivi huku jamvini hakuna watoto.
 
kisima.bmp

Uchimbe kisima wewe mwenyewe unywe maji yako peke yako na usiyashiriki nao wengine ni hatari kubwa eeh!

Maji ya kisima cha watu wengi yameingiliwa na mdudu ukiwa na kiu usiyaonje utaambukizwa eeh.

Na kiu ya maji imeongezeka watu wanayanywa kila wakati na yanauzwa kote barabarani nani atapona eeh?

Kwa sababu maji yana mdudu yanapatikana kirahisi ukipita kote utayaona wacha kuyachota eeh.

Tena na siku hizi na hayo maji yaliyo yaliyoingiwa na mdudu utapewa bure bila kuomba ili mfe wote eeh.

Yapo kwenye chupa kubwa na ndogo watu wanazipenda zile ndogo wanafikiliria zipo salama wamedanganyika eeh.

Wanazifunika nusunusu wamefanya hivyo makusudu ili waamushe kiu ya maji usidanganyjike eeh!

Ndugu jihadhari na maji ya rahisi kachimbe kisima wewe mwenyewe ukiwa na kiu uyanywe maji uliypoyachimba heri.

Dawa ya mdudu hawajaipata wanaitafuta kotekote umwamini Yesu akuokoea amalize kiu.

By Faustin Munishi:

hi.hi,hi,hi mmm, Hapo penye nyekundu nimecheka!! Kumbe tumegundulika.
 
Mi nishachimba changu ila cjui ninywe yenye tope au masafi?!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom