Chikawe awakemea Mwakyembe na Sitta: Waache kuzungumzia DOWANS

Mnajua hz habar za kufuata utaratibu na nzur lakn zna negatve side,sabab ya majority wins,kwamba wakienda ktk baraza ztapgwa kura na sita na mwakyembe watashdwa,hvyo mi naona ni vzur mtu aongee na kuwaeleza wananch direct through journalist. Ndg chikawe hawa watu (RA.AC,EL)mtajtahd sana na mwaweza tumia maj yote ya bahar lakn hawasafshki.

Safi sana. Huo ndio ukweli, kuna kundi la mawaziri wako tayari kupinga ulipwaji huo wa kifisadi. Lakini kanuni mbovu! Na hizo ndizo zinatufikisha hapa. Nchi za wenzetu Waziri yuko huru kujadili kitu chenye maslahi kwa umma. Sisi hapana, lengo ni kujichumia tu wachache. Kura haziwezi kusaidia. Wazalendo ni wachache!! Ila niseme tu kwamba, kujiuzuru kwao ni wakati mwingine mzuri wa Kiwete kuonja shubiri ya Uongozi
 
na mwakyembe na sitta wasijiuzulu, aliye wateu kama anaona hawafai basi na avunje hilo baraza la mawaziri aanze upya? pia chikawe ana takiwa arejee maneno aliyo toa PM mstaafu Cleopa David Msuya
Hawa jamaa majimbo yao wangeyahamishia CHADEMA ingekuwa poa sana yaani nguvu ya uma ingeongezeka!sitta na mwakyembe!
 
Chikawe anajaribu kulinda serikali ambayo imeshapoteza uhalali wa kuitwa serikali! Wakati wa sakata la EPA, Samwel SITTA aliwahi kumwambia rais apunguze upole katika kuwashughulikia mafisadi, hakuona mabadiliko! Sitta na Mwakyembe wanajua hatuna serikali, kila mtu anapuyanga kivyake! Hata Mkulo, wazri wa fedha na uchumi alisema hazina hakuna hela za kuilipa dowans, labda wizara ya nishati na madini ilipe kwa hela zake! mawaziri hawamwamini kikwete maana ameshindwa kazi yake, ni kama kocha anazidiwa mbinu na wachezaji wake, hawawezi kumsikiliza! Lazima chikawe ajue kwamba kama serikalini kuna watu wanatetea ufisadi na wengne wanatetea wanyonge basi hawawezi kusikilizana kamwe!
 
Hawa jamaa wawili Sitta na Mwakyembe ni wamedhihirisha upuuzi wao katika hili kwa kujifanya waongeaji. Km wao wanaamini katika dhana ya kupambana na ufisadi kwanini wasikae kando? Yaani Uwaziri wanautaka na wakati huohuo wanaishambulia serikali ambapo na wao ni sehem ya serikali.

Mkuu, kumbe ukikubali kuwa waziri lazima uwe unaficha maovu au ukubaliane na kilakitu hatakama unaona ni usanii tu? Ina maana all "presidential appointees" ni mafisadi sababu wamekubali position walizopewa? I think hii ndio inawafanya CCM na serikali yote waonekane mafisadi wakati sio kweli. Kuna watu ndani ya CCM na serikali ambao sio mafisadi, lakini wanaogopa kusema kutokana na dhana hii yakutakiwa kukubali kilakitu e.g Pinda. Kwa mtazamo wangu naona hii issue inaumuhimu kupelekwa kwenye baraza la mawaziri, likazungumzwe kwa undani badala ya ku-rush. Otherwise kila mtu anataka kutoa mawazo yake huwezi kumnyima: ndio fruits za democracy hizi.
 
“Unajua Rais wetu ni mwepesi sana kuwasikiliza mawaziri wake wakati wowote"

He hears but does he listen? Huyu rais ni mwepesi kuSIKIA lakini mgumu kuSIKILIZA... nawasilisha!

I have a feeling "anang'ata na kupuliza" i.e. akiongea na huyu anakubaliana naye, akienda huku anakubali basi anawachang'anya wote. Haiwezekani awe msikivu alafu tuwe hapa tulipo.
 
I have a feeling "anang'ata na kupuliza" i.e. akiongea na huyu anakubaliana naye, akienda huku anakubali basi anawachang'anya wote. Haiwezekani awe msikivu alafu tuwe hapa tulipo.

Comment yako akiongea na huyu anakubaliana naye, akienda huku anakubali basi anawachang'anya wote nimecheka sana!
 
Kwa bahati mbaya hawakulazimishwa na walikuwa na bado wanahaki ya kukataa nafasi zile. Hizi kauli zao zinatofauti gani na wafanyakazi wanaomwibia mwajiri wao? Au marketing officer anayachafua bidhaa za kampuni aliyoajiriwa. Upuuzi wa namna hii haupo. Hapa ninasisitiza aidha watoke serikalini au wafunge midomo yao.

Teh teh! Hisia na ushabiki vimeua akili zako lkn hata macho na masikio pia vimekufa bana anfaal? Nenda japo kenya tu apo ukaone mfumo huo unavyosaidia kui-sharpen kenya. Usiongozwe na hisia bali uhalisia!
 
Sitta na mwakyembe wanapenda vyeo na sifa

Kama wanaona kuna shida serikali wajiuzulu kuonyesha usafi..can they dare kuacha shanginfi? wapi
 
wazir Clara wa uingereza alimupinga waziri mkuu ton blair ambaye ni sawa na Rais wa Uk kuhusu BE kuiuzia Tz rada .To Blai alikuwa anaunga ufisadi lakini mpaka sasa mtazamo wa Clara ndio kweli , kipindi Waziri Clara anapinga hakujiuzuru!!!
Serikali ya Kikwete inalinda mafisadi hivyo kuipinga ni kosa ,tunataka hoja wanazo toa zichunguzwe!!!
Wanaodai kujiuzuru ni kundi linalo nufaika na wizi huo
 
Wao (mwakyembe na sitta) wangejiondoa kwenye baraza la mawaziri ili wawe huru zaidi kutoa mawazo yao
 
SAKATA la malipo ya kampuni ya kufua umeme ya Dowans, limeingia hatua mpya baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utawala Bora, Mathias Chikawe, kusema mawaziri wawili waliompinga Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kutangaza serikali kuilipa kampuni hiyo, walikiuka utaratibu wa serikali.

Aidha, amewataka mawaziri hao, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kuacha kutoa maelezo ya sekta zisizowahusu kwani si utaratibu wa utawala bora na ni kuwachanganya wananchi.

Akifafanua kuhusu kauli zilizompinga Waziri Ngeleja, Chikawe alisema mawaziri hao walipaswa kufuata utaratibu wa kufikisha hoja zao kwa Mamlaka husika, au wajiondoe serikalini kabla ya kupingana na waziri mwenzao.

Alisema Waziri Sitta ni mzoefu na wa siku nyingi, hahitaji kufundishwa, kwa kuwa ameshika nyadhifa mbalimbali serikalini na anafahamu namna za kutoa maoni kwa mawaziri bila kuathiri utaratibu.

Kuhusu Mwakyembe, alisema ingawa ni mpya katika uwaziri, lakini ni mwanasheria wa siku nyingi na anajua utaratibu wa sheria ulivyo, hivyo pia hakuhitaji kufundishwa kuhusu namna ya kutoa mawazo yake kuhusu Dowans wakati akiwa serikalini tena Naibu Waziri.

“Umefika wakati Sitta na Mwakyembe waache kuendesha mambo kisiasa, bali waangalie sheria zaidi katika suala la Dowans,” alisema Chikawe.

Alisema kitendo cha mawaziri hao kumkosoa Waziri Ngeleja, kutokana na kutangaza hadharani kuilipa kampuni hiyo Sh bilioni 94, kimetoa picha kuwa kuna mgongano ndani ya Baraza la Mawaziri.

Alisema jambo zito kama hilo, halikupaswa kutolewa maelezo magazetini, bali wangetumia utaratibu wa kumfuata waziri husika na kutoa maoni na ushahidi walionao na iwapo wangeona waziri huyo hawatilii maanani, wangekwenda kwa Waziri Mkuu au Rais.

“Unajua Rais wetu ni mwepesi sana kuwasikiliza mawaziri wake wakati wowote, sasa iwapo wangeona waziri husika hawasikilizi, wangepeleka hoja yao kwake ambaye kama angeridhishwa na hoja zao, angeitisha kikao cha Baraza la Mawaziri kutoa uamuzi wa pamoja,” alisema Chikawe.

Chikawe alisema kuna utaratibu wa aina mbili, ambao waziri anaweza kuutumia kutoa uamuzi wa Serikali; kwanza ni kutoa uamuzi unaohusu wizara yake na mwingine, uamuzi wa pamoja.

Alifafanua kuwa waziri wa sekta husika, ana jukumu la kutoa uamuzi wowote wa wizara yake bila kuingiliwa na akiona kuna jambo zito linaloathiri sera za nchi, ndio hupeleka kwenye Baraza la Mawaziri ili lijadiliwe kabla ya kutoa uamuzi wa pamoja.

Chikawe alisema Waziri Sitta na Naibu Waziri Mwakyembe, walikuwa na nafasi ya kumwona Rais na kutoa ushahidi wao na iwapo Rais angeona kuna umuhimu wa kuitisha Baraza la Mawaziri, angefanya hivyo na si kutoa siri za Baraza kuwa hawajalijadili suala hilo.

Alisema maoni binafsi kwa mawaziri hao si tatizo, ndiyo maana katika Baraza la Mawaziri, kikao kinaweza kujadili suala moja kwa siku nzima mpaka wanafikia uamuzi wa pamoja, lakini kuyazungumzia hadharani ni kosa, kwa kuwa wamekiuka utaratibu wa utawala bora kwa kutoa siri za Baraza hilo.

Chikawe alimtetea Ngeleja kuwa inawezekana hakuona sababu ya kupeleka suala la kuilipa Dowans kwa Baraza la Mawaziri kwa kuwa alishirikisha wataalamu mbalimbali wa sheria na
kujiridhisha katika kufanya malipo kwa kampuni hiyo.

Wiki iliyopita, Waziri Sitta alipinga tamko la Waziri Ngeleja la kuilipa kampuni ya Dowans na kusema kuwa inashangaza waziri kutoa tamko hilo kabla hata Baraza la Mawaziri halijalijadili.

Juzi pia Naibu Waziri Mwakyembe, aliibuka na kusema anashangaa kusikia kampuni hiyo aliyoiita ya kitapeli, inalipwa kwa madai kuwa ilirithi mkataba wa kufua umeme kutoka katika kampuni hewa ya Richmond LCC Ltd.

Katika Bunge lililopita chini ya Spika Sitta, Mwakyembe aliongoza Kamati Maalumu iliyochunguza suala la kampuni ya kufua umeme ya Richmond hata kusababisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na mawaziri wawili, Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha, kujiuzulu kutokana na kashfa ya kampuni hiyo.

HabariLeo | Dowans ‘yawatafuna’ Sitta na Mwakyembe
chikawe ?????? sina hakika kama hayo unayoyasema nikweli unamsaidia RAIS NA KAMA NDIYO HASWAA UTAWALA BORA AU UTAWALA MASLAHI BINAFSI, TAFADHALI BADILIKA
 
Sasa Chikawe na wewe si ungewaambia kimyakimya wao wenyewe mbona na wewe umeenda kwenye vyombo vya habari sasa!!!!

Ungewaita na uwape ushauru huo kimyakimya!!!kwa mtazamo wangu na wewe umetereza au umetumwa uwasafishe watu kwa mjadala huo!

Wazo zuri kweli tena wewe chikawe ndiyo umetuonesha kumbe kuna Tatizo kubwa katika uongozi na pia umemsahau na Mkulo nae alisema hakuna pesa ya kuwalipa au yeye ulivyotumwa uliambiwa usimtaje nini! Du kazi tunayo safari hii.
 
SAKATA la malipo ya kampuni ya kufua umeme ya Dowans, limeingia hatua mpya baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utawala Bora, Mathias Chikawe, kusema mawaziri wawili waliompinga Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kutangaza serikali kuilipa kampuni hiyo, walikiuka utaratibu wa serikali.

Aidha, amewataka mawaziri hao, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kuacha kutoa maelezo ya sekta zisizowahusu kwani si utaratibu wa utawala bora na ni kuwachanganya wananchi.

Akifafanua kuhusu kauli zilizompinga Waziri Ngeleja, Chikawe alisema mawaziri hao walipaswa kufuata utaratibu wa kufikisha hoja zao kwa Mamlaka husika, au wajiondoe serikalini kabla ya kupingana na waziri mwenzao.

Alisema Waziri Sitta ni mzoefu na wa siku nyingi, hahitaji kufundishwa, kwa kuwa ameshika nyadhifa mbalimbali serikalini na anafahamu namna za kutoa maoni kwa mawaziri bila kuathiri utaratibu.

Kuhusu Mwakyembe, alisema ingawa ni mpya katika uwaziri, lakini ni mwanasheria wa siku nyingi na anajua utaratibu wa sheria ulivyo, hivyo pia hakuhitaji kufundishwa kuhusu namna ya kutoa mawazo yake kuhusu Dowans wakati akiwa serikalini tena Naibu Waziri.

"Umefika wakati Sitta na Mwakyembe waache kuendesha mambo kisiasa, bali waangalie sheria zaidi katika suala la Dowans," alisema Chikawe.

Alisema kitendo cha mawaziri hao kumkosoa Waziri Ngeleja, kutokana na kutangaza hadharani kuilipa kampuni hiyo Sh bilioni 94, kimetoa picha kuwa kuna mgongano ndani ya Baraza la Mawaziri.

Alisema jambo zito kama hilo, halikupaswa kutolewa maelezo magazetini, bali wangetumia utaratibu wa kumfuata waziri husika na kutoa maoni na ushahidi walionao na iwapo wangeona waziri huyo hawatilii maanani, wangekwenda kwa Waziri Mkuu au Rais.

"Unajua Rais wetu ni mwepesi sana kuwasikiliza mawaziri wake wakati wowote, sasa iwapo wangeona waziri husika hawasikilizi, wangepeleka hoja yao kwake ambaye kama angeridhishwa na hoja zao, angeitisha kikao cha Baraza la Mawaziri kutoa uamuzi wa pamoja," alisema Chikawe.

Chikawe alisema kuna utaratibu wa aina mbili, ambao waziri anaweza kuutumia kutoa uamuzi wa Serikali; kwanza ni kutoa uamuzi unaohusu wizara yake na mwingine, uamuzi wa pamoja.

Alifafanua kuwa waziri wa sekta husika, ana jukumu la kutoa uamuzi wowote wa wizara yake bila kuingiliwa na akiona kuna jambo zito linaloathiri sera za nchi, ndio hupeleka kwenye Baraza la Mawaziri ili lijadiliwe kabla ya kutoa uamuzi wa pamoja.

Chikawe alisema Waziri Sitta na Naibu Waziri Mwakyembe, walikuwa na nafasi ya kumwona Rais na kutoa ushahidi wao na iwapo Rais angeona kuna umuhimu wa kuitisha Baraza la Mawaziri, angefanya hivyo na si kutoa siri za Baraza kuwa hawajalijadili suala hilo.

Alisema maoni binafsi kwa mawaziri hao si tatizo, ndiyo maana katika Baraza la Mawaziri, kikao kinaweza kujadili suala moja kwa siku nzima mpaka wanafikia uamuzi wa pamoja, lakini kuyazungumzia hadharani ni kosa, kwa kuwa wamekiuka utaratibu wa utawala bora kwa kutoa siri za Baraza hilo.

Chikawe alimtetea Ngeleja kuwa inawezekana hakuona sababu ya kupeleka suala la kuilipa Dowans kwa Baraza la Mawaziri kwa kuwa alishirikisha wataalamu mbalimbali wa sheria na

kujiridhisha katika kufanya malipo kwa kampuni hiyo.

Wiki iliyopita, Waziri Sitta alipinga tamko la Waziri Ngeleja la kuilipa kampuni ya Dowans na kusema kuwa inashangaza waziri kutoa tamko hilo kabla hata Baraza la Mawaziri halijalijadili.

Juzi pia Naibu Waziri Mwakyembe, aliibuka na kusema anashangaa kusikia kampuni hiyo aliyoiita ya kitapeli, inalipwa kwa madai kuwa ilirithi mkataba wa kufua umeme kutoka katika kampuni hewa ya Richmond LCC Ltd.

Katika Bunge lililopita chini ya Spika Sitta, Mwakyembe aliongoza Kamati Maalumu iliyochunguza suala la kampuni ya kufua umeme ya Richmond hata kusababisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na mawaziri wawili, Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha, kujiuzulu kutokana na kashfa ya kampuni hiyo.

HabariLeo | Dowans ‘yawatafuna' Sitta na Mwakyembe
Hakuna cha channel wala nn..as long as media ipo waseme tu...tena kama wanajua na issue zingine watuambie tu...cuz channel zinazosemwa ni za kulinda maslah ya mafisadi na uongozi ulioo oza...OVA!
 
Unajua mtu asiye akili timamu akikuvua nguo ukamkimbiza weye ndio punguani au hazitoshi. Chikawe kamkimbiza asiye akilil timamu akiwa uchi. Nani kichaa?
 
Sasa Chikawe na wewe si ungewaambia kimyakimya wao wenyewe mbona na wewe umeenda kwenye vyombo vya habari sasa!!!!

Ungewaita na uwape ushauru huo kimyakimya!!!kwa mtazamo wangu na wewe umetereza au umetumwa uwasafishe watu kwa mjadala huo!

nimeipenda sana hii, hivi wapi mnampa thanks
 
Unajua mtu asiye akili timamu akikuvua nguo ukamkimbiza weye ndio punguani au hazitoshi. Chikawe kamkimbiza asiye akilil timamu akiwa uchi. Nani kichaa?

Hiyo nimeipenda. Thanks Mwakyembe na Sita for taking the risk. Lakini my feeling yako mengine zaidi Mwakyembe na Sita wanayajua hawajatuambia. Hapo ndio ujasiri wao utakuwa na tija.
Hakuna heshima iliyobaki kwa serikali ya JK ya kulinda tena.
 
Back
Top Bottom