Chikawe awakemea Mwakyembe na Sitta: Waache kuzungumzia DOWANS

kiduku+jk.jpg


Rais Mwizi aende Chalinze kucheza mdundiko atuachie wenyewe tuijenge nchi yetu.
Tuwasafishe mafisadi papa na aiache Tanzania kama ambavyo aliikuta.



Mwenzio alikuwa anatafuta kura za UWT na akapata
 
Mimi binafsi naona CHIKAWE anahaki ya kutueleza kile kilichomo moyoni mwake. Hapa Tutaona nani amewafuga hao Dowans. Na sasa wanazidi kuongezeka Pembe zao zimeanza kuyeyuka. Hivyo kama Chikawe Ametumwa kuwaondoa Mwakyembe na Sitta basi atangaze tu kuwa na yeye ni FISADI MKUU.
 
Dowans ... Dowans ..... Dowans;

Kwanza timing ya hukumu yenyewe, months after Uchaguzi inaharufu ya mipango. Bila shaka hawa watu walijua baada ya uchaguzi watakuwa na mandate ya kufanya wanachokitaka! Kwa hiyo wakawaambia washirika wao wakae kimya mpaka baada ya uchaguzi ndo hukumu itoke; kweli hukumu imetoka lakini kuna ambayo hawakuyatarajia!

Jambo la kwanza ambalo hawakulitarajia ni aina uchaguzi ulivyofanyika na matokeo yake yaliyomwacha mkuu akiwa na majeraha kibao. Hilo hawakulitarajia asilani, si 2010. Majeraha aliyoyapata mkuu kwenye uchaguzi yamemfanya akose mandate ya kuunda baraza lake, akalazimika kuokoteza hapa na pale ili mambo yaende, ila suala hili la Dowans linaonekana lilishapangwa vizuri sana kwani wizara ile haikuguswa!

Aliyevunja mkataba wa Dowans ni aliyekuwa bosi wa Tanesco kipindi kile, na wakati anavunja ule mkataba haikuwepo amri ya Bunge au ya mtu mwingine yeyote kumtaka auvunje ule mkataba. Ulivunjwa kwa kupangwa? Kuwa vunja mkataba tutapeleka kesi mahakamani, baada ya uchaguzi hukumu itatoka na tutalipwa fasta! Kama kutakuwa na mjadala yatakuwa ya baadaye!

Kuna watanzania kama Kina Mramba wanahenyeka mahakamani na kesi za kutumia vibaya madaraka na kuisababishia serikali hasara kubwa! Kina Liyumba wako gerezani! Lakini kisu hicho hicho kilichowachinja kina Mramba na kina Liyumba kinashindwa kuwapeleka walioshiriki kwenye mkataba wa Dowans, kwa nini? Ikiwa serikali inataka kutumia kisingizio cha kufuata sheria, basi ifungue kesi mahakamani mara moja ya kuwadai wote walioshiriki katika mkataba wa Dowans kwani mkataba huo ambao serikali imepata hasara kubwa hauwezi kuwa mkataba halali. Walioshiriki wote wafunguliwe mashitaka na fedha za kuilipa Dowans zitoke kwao. Mbona wezi wa EPA waliamuliwa kurudisha fedha walizokwapua? Walioshiriki mkataba wa Dowans wote wahusike kuzilipa hizo fedha, watu tutaridhika kuwa serikali inafata sheria na taratibu.

Vinginevyo serikali haina heshima yoyote mbele ya macho ya watazamaji. Haina heshima ya kufuata taratibu. Ni ujinga wa wazi wazi kuhamishia lawama kwa akina Mwakyembe na Sitta ambao Mchango wao kwenye suala hili ilikuwa ni kuishauri serikali imwajibishe nani na nani kwenye huu mkataba. Mwakyembe na Sitta ndo walioingia mkataba au ndo walio vunja mkataba? give me a break!

Serikali hii haina face kwenye Dowans kama ilivyokosa face kwenye EPA na vikesi vyao vya ze Komedi. Je wanataka Dowans iiangushe serikali hii?? Mambo ambayo hayajawahi kutokea huwa yanatokea na Dowans inaweza kuiangusha serikali ambayo tayari ni dhaifu mno kutokana na uchaguzi ambao matokeo yake yanatiliwa shaka na kila mtu.

Kina Ngeleja inaelekea walishapangwa ku clear mess ya Dowans ila wawe makini. Kuna wale wasio na Kinga mess hii inaweza kuja kuwala siku yoyote. We are counting on them!
 
Ndugu zangu wa JF,

Habari Leo limetoka na habari kuwa waziri wa utawala bora mathias chikawe amepingana na kulaumu kauli za mhe. Sitta na mhe. Dr. Mwakyembe za kutaka serikali isiilipe Dowans kwani ni kampuni ya kitapeli.

Anachosema kina mantiki kwamba wao kama mawaziri wana channels zao za kufikisha uamuzi wowote wanaoupinga ndani ya serikali badala ya kutumia vyombo vya habari.

Binafsi siwalaumu mzee sitta na dr. Mwakyembe kwani pamoja na uelewa wao wa taratibu zinazozungumzwa na chikawe lakini wameshindwa kuvumilia kukaa kimya kutokana na uzalendo kwa nchi yao. Wote wawili wanalifahamu vizuri suala la Dowans na wana uhakika kuwa ni utapeli tena mbaya zaidi unaofanywa na watanzania wenzetu. Suala la Dowans linatia uchungu tena mkubwa sana.

Kwa mtazamo wangu, ni bora viongozi wetu hao (sitta na mwakyembe) ili kulinda heshima yao kwa kujiondoa kwenye serikali inayotetea na kusimamia maamuzi ya kunyonga wananchi wao maskini.
 
- Well, my very good friend Mh. Chikawe, sometimes unafika wakati kwenye maisha enough inakuwa enough, serikali haieleweki nani ni nani, sheria haziheshimiwi I mean it is almost a Sodoma & Gomorah Nation, hata Mungu had to destroy his own works, sembuse Mwakyembe na Sitta kukemea tu serikali wanayoiongoza?

- Now why don't you do us wananchi na taifa zima a big favor by resigning badala ya kujaribu kunyamazisha sauti ya Mungu kuhusu wizi wa hela za wananchi? It is very simple, hukubaliani na kitendo cha Mwakyembe na Sitta kuuliza kuhusu wizi wa hela za wananchi, then just pack up and go! Tanzania hatuna sheria inayowakataza mawaziri kuuliza wanapoona hela za wananchi zinaibiwa tena mchana kweupee as this Dowans thing!

- Enough is enough!
Bravo Mwakyembe & Sitta keep up the good works!, Wewe mtumzima na akili zako timamu unaona hela za wananchi zinaibiwa, eti unahitaji kusubiri kikao cha baraza la mawaziri kukemea Mh. Chikawe are you kidding me or what?

William.
 
wapo wengi wanaoweza kuzungumza lakini ni hizo kanuni sheria zinawabana
 
Sana hawa jamaa wameshachemka kumfunga mdomo sitta na mwakyembe pia mama malecela mbona siku hizi asikiki kabisa au ndio wameshamtia kapuni!
 
Mnajua hz habar za kufuata utaratibu na nzur lakn zna negatve side,sabab ya majority wins,kwamba wakienda ktk baraza ztapgwa kura na sita na mwakyembe watashdwa,hvyo mi naona ni vzur mtu aongee na kuwaeleza wananch direct through journalist. Ndg chikawe hawa watu (RA.AC,EL)mtajtahd sana na mwaweza tumia maj yote ya bahar lakn hawasafshki.
 
''wewe unayejiita Anfaal, kokote ulipo, UZALENDO WAKO UMEUPOTEZEA WAPI??? unafurahishwa na umasikini wa watanzania waziwazi kwa manufaa unayoyapata kupitia mafisadi,. ni rahisi kufikiri ndio waliokufikisha hapo ulipo..
kwa nini binadamu wa kizazi cha sasa hatutamani hata kwenda mbiguni angalau kwa kutenda yaliyo haki mbele ya Mwenyenzi Mungu na viumbe wote kwa ujumla!!!
Tutaangamia na moto jamani
 
Je Chikawe kwa kuwakosoa Sitta na Mwakyembe kwenye vyombo vya habari si na wewe unarudia kosa kama lao?

Kila mtu anafanya atakavyo nini katika serikali ya sasa. Kama wamevunja sheria basi mkuu wa kaya awavue uwaziri kwani tatizo ni nini?

Kama Chikawe anatakatuamini Suala la kuilipa DOWANS ni dogo na hivyo waziri peke yake anaweza kulitolea maamuzi basi kazi ipo!

Je lipi litafanya baraza la mawaziri likutane????
 
Chikawe ni mmoja kati ya wengi tunaowazungumzia ambao wamelewa tu na madaraka ya kuteuliwa yasiyotoa mwanya wa wenye uwezo na badala yake kujuana kikitumika km kigezo cha uteuzi....Ni imani yangu katiba mpya itamulika maadili na ukomo wa maamuzi wa watu aina ya Chikawe
 
Chikawe ni mmoja kati ya wengi tunaowazungumzia ambao wamelewa tu na madaraka ya kuteuliwa yasiyotoa mwanya wa wenye uwezo na badala yake kujuana kikitumika km kigezo cha uteuzi....Ni imani yangu katiba mpya itamulika maadili na ukomo wa maamuzi wa watu aina ya Chikawe
Enzi na mzee kipara alikua asikiki huyu sijui alikua wapi kipindi hicho!
 
mi nashauri wa tanzania wote tusimame imara kutolipwa dowans, na hapa jf tutoe mawazo thabit yatakayosaidia jinsi ya kutolipwa dowans maana imeanza kutucost kwa kupandishwa maumeme na gas, wa tz ni wavumilivu sana sasa sisi tunaoamini tunaonambali hebu tusaidie njia za kusimamisha ulipwaji huu haramu.
 
Nina hakika Sitta na Mwakyembe hawakuomba uwaziri/naibu waziri. Walipewa ili kuwaziba midomo. Wanajua fika hilo suala la uwajibikaji wa pamoja lakini wameona bora waseme ukweli. Kikwete sasa ana uamuzi wa kuwatimua au la. Akiwatimua kama anavyoshauriwa na mafisadi na vikaragosi vyao cha moto atakiona mbele ya safari na hao hao mafisadi watasema hafai!
 
Kumbe kila waziri yuko kivyakevyake hata ktk malipo makubwa kama haya?

Exactly! Na tutajuaje hao wataalamu aliowashirikisha sio watu "incompetent" kama wale anaowasema wa Tanesco??? Nakumbuka Mwakyembe alisema yeye anachangia hoja kama mwanasheria: I think kama mtanzania mwingine yeyote ana haki yakuuliza maswali.
 
Mimi binafsi naona CHIKAWE anahaki ya kutueleza kile kilichomo moyoni mwake. Hapa Tutaona nani amewafuga hao Dowans. Na sasa wanazidi kuongezeka Pembe zao zimeanza kuyeyuka. Hivyo kama Chikawe Ametumwa kuwaondoa Mwakyembe na Sitta basi atangaze tu kuwa na yeye ni FISADI MKUU.

Very true. This is the time to know who is who.
 
kama tuna zungumzia utawala bora, basi chikawe na aliye mtuma wamekosa hiyo sense ya utawala bora, na wanatakiwa waelewe maana ya kuwepo kwa kikao cha baraza la mawaziri.
kiwango cha pesa kinacho ongelewa ni juu ya uwezo wa waziri husika kukiongelea bila kukipeleka kwenye baraza la mawaziri, ila ikiwa nia ni kujaribu maji ya moto ya baridi, kwa maana nyingine ikiwa kuna nia mbaya ndio utaratibu kama huu hutumika.
hii ni sawa sawa kwenye kampuni kuna level ya kusaini shs 10m, halafu 100m na kuendelea mpaka issue ya bodi nk nk.
jingine je utawala bora ulifuatwa katika kuingia huu mkataba? sheria zilifuatwa? au utawala bora unakuwepo pale mtawala/watawala wanapo waibia wananchi?
 
Sasa Chikawe na wewe si ungewaambia kimyakimya wao wenyewe mbona na wewe umeenda kwenye vyombo vya habari sasa!!!!

Ungewaita na uwape ushauru huo kimyakimya!!!kwa mtazamo wangu na wewe umetereza au umetumwa uwasafishe watu kwa mjadala huo!

HAHAHAHAHAHAHA NIMEIPENDA HII!
 
na mwakyembe na sitta wasijiuzulu, aliye wateu kama anaona hawafai basi na avunje hilo baraza la mawaziri aanze upya? pia chikawe ana takiwa arejee maneno aliyo toa PM mstaafu Cleopa David Msuya
 
na huyo chikawe na waliomtuma kama katumwa waelewe wahisani na trading partners wetu wanatuangalia.
 
Back
Top Bottom