Chikawe awakemea Mwakyembe na Sitta: Waache kuzungumzia DOWANS

Chikawe hana madaraka wala uwezo wa kulazimisha nidhamu kwa waziri yeyote. Kama yeye aliona kuwa wenzake wamekosea kwanini na yeye asimwambie Waziri Mkuu au Rais yeye mwenyewe? Sasa kesho kina Mwakyembe nao wakimjibu kwa magazeti ataona wamemvunjia heshima au wamevunja kanuni?
 
Hawa jamaa wawili Sitta na Mwakyembe ni wamedhihirisha upuuzi wao katika hili kwa kujifanya waongeaji. Km wao wanaamini katika dhana ya kupambana na ufisadi kwanini wasikae kando? Yaani Uwaziri wanautaka na wakati huohuo wanaishambulia serikali ambapo na wao ni sehem ya serikali.

hujui ulisemalo, kwa hiyo wakae kimya? Rudi kwenu India we Rostam na ni bora utumie identity yako ili hujibu tuhuma dhidi yako!
 
Sitta na Mwakyembe wanajaribu kuficha aibu. Najua hawachomoki katika hili. They were supposed to foresee the repucation of breaching the Dowans contract. Were are paying Dowans b'se of Bunge fail to foresee!!

It's shame to have those kind of people!

Unajua wakati mwingine uszungumzie tu mkataba ulivunjwa bali ututajie kama mkataba ulikuwa halali au la na kama kweli Tanzania tulifanya makosa katika kuvunja mkataba uliokuwa halali na kama tunastahili kulipa fidia hiyo. Fikiria Dowans ilirithishwa mkataba na Richmond iliyokuwa kampuni feki, kampuni feki itarithishaje mkataba? Kuhusu Dowans SA Costarica tumeambiwa kuwa hiyo kampuni haipo kwenye orodha ya makampuni kule Costarica na wao ndio wenye asilimia 54 ya hisa katika Dowans Tanzania. Tuambie kama kuna utata katika hilo kuna haja gani ya kulipa fidia?

Wewe unadhani mkataba ni mkataba tu hata kama si halali?
 
Hawa jamaa wawili Sitta na Mwakyembe ni wamedhihirisha upuuzi wao katika hili kwa kujifanya waongeaji. Km wao wanaamini katika dhana ya kupambana na ufisadi kwanini wasikae kando? Yaani Uwaziri wanautaka na wakati huohuo wanaishambulia serikali ambapo na wao ni sehem ya serikali.
mi nadhan wapo sawa cz hwz kuta2a matatz ukiwa mbal nayo "fimbo ya mbali haiui nyoka",acha waendelee kubaki na positions zao hk wakiendelea kupamban na ufisad wa ndg zao kwa ukarb zyd "juen kweli,nayo kwel itawaweka huru"
 
Tatizo JK hakuwapa uwaziri hawa SITTA na MWAKYEMBE kwa roho moja ...aliwapa kwa lengo la kuwaziba mdomo tu ...na wao wanajuwa ...ndio maana hawataacha kuongea pale ambapo wanahisi maoni yao kupuuzwa barazani.

midomo mingine haizibiki hata kwa super glue! Wanalo babu
 
Kwa bahati mbaya hawakulazimishwa na walikuwa na bado wanahaki ya kukataa nafasi zile. Hizi kauli zao zinatofauti gani na wafanyakazi wanaomwibia mwajiri wao? Au marketing officer anayachafua bidhaa za kampuni aliyoajiriwa. Upuuzi wa namna hii haupo. Hapa ninasisitiza aidha watoke serikalini au wafunge midomo yao.

Sisi ndotuliowaajili simafisadi unataka wateteeakinanani? zaidiyamwajiliwake
 
Mimi nadhani tafsiri ya uwajibikaji wa pamoja inakosewa. Sidhani maana yake nsio hiyo ya kufanya uppuuzi wote ni siri ya Baraza la mawaziri. Kwanza mnasema siri ni siri zipi hizo wakati ni mambo yanayoihusu nchi na watanzani kwa ujumla wake? Ni usiri gani huo wa maamuzi mnao usema kuwa baraza la mawaziri lazima ufuate? Hayo mambo ya sirisiri ndiyo yameifikisha nchi hapa ilipo. Sidhani kama mawaziri wanaotoa maoni yao hadharani wanakuwa wamekosea. Kwani kuna ubaya gani wananchi wakijua kuwa Mawaziri wanatofautiana ktk baadhi ya mambo na maamuzi? Huo si ndio uongozi bora? Kwanini Mzee Mwinyi wakati ule akiwa mambo ya ndani alijiudhuru baada ya mauaji, na kwa nini Baraza zima lisijiudhuru kwani ni uwajibikaji wa pamoja?

Mimi nadhani hawa mawaziri wapo sahihi kabisa, hata kama wametoa maoni yao hadharani, huo ndio msimamo wao hata ktk baraza la mawaziri, hawatabadirika. Unajua watanzania tuymejisahau sana na hawa viongozi wanadhani kuwa wakisha kuwa viongozi wanauwezo wa kujiamulia tu mambo kwa vile ni mawaziri. Juzi mzee Msuya kasema, uongozi ni kujitoa kafara kuwahudumia wananchi, na ukiamua kuwa kiongozi ni lazima ujitoa muhanga huo, ndio maana anasema hata watoto wake ameamua kuwaeleza wajipime kwanza kama wanataka kuwa viongozi. Sasa hiyo ndiyo tafsiri sahihi ya uongozi na sio usiri usiri uliokidhiri. Kama yataendelea hayo ya usiri na mawaziri wetu hawatabadilika, ya Tunisia yanawezekana.
 
Kombani, Werema na Membe wakikurupuka na baadaye kusema ni mawazo yao binafsi hatujamsikia Chikawe kuwakemea au hakuwa na masilahi nayo asitufanye wote wajinga, kwenye suala la Dowans ndiyo kakumbuka kwa sababu ana maslahi nalo, nawashauri Sitta na Mwakyembe nao waseme yalikuwa ni mawazo binafsi si ya baraza la mawaziri full stop.
 
Hawa jamaa wawili Sitta na Mwakyembe ni wamedhihirisha upuuzi wao katika hili kwa kujifanya waongeaji. Km wao wanaamini katika dhana ya kupambana na ufisadi kwanini wasikae kando? Yaani Uwaziri wanautaka na wakati huohuo wanaishambulia serikali ambapo na wao ni sehem ya serikali.
:A S thumbs_up:
 
SAKATA la malipo ya kampuni ya kufua umeme ya Dowans, limeingia hatua mpya baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utawala Bora, Mathias Chikawe, kusema mawaziri wawili waliompinga Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kutangaza serikali kuilipa kampuni hiyo, walikiuka utaratibu wa serikali.

Aidha, amewataka mawaziri hao, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kuacha kutoa maelezo ya sekta zisizowahusu kwani si utaratibu wa utawala bora na ni kuwachanganya wananchi.


Akifafanua kuhusu kauli zilizompinga Waziri Ngeleja, Chikawe alisema mawaziri hao walipaswa kufuata utaratibu wa kufikisha hoja zao kwa Mamlaka husika, au wajiondoe serikalini kabla ya kupingana na waziri mwenzao.


Alisema Waziri Sitta ni mzoefu na wa siku nyingi, hahitaji kufundishwa, kwa kuwa ameshika nyadhifa mbalimbali serikalini na anafahamu namna za kutoa maoni kwa mawaziri bila kuathiri utaratibu.


Kuhusu Mwakyembe, alisema ingawa ni mpya katika uwaziri, lakini ni mwanasheria wa siku nyingi na anajua utaratibu wa sheria ulivyo, hivyo pia hakuhitaji kufundishwa kuhusu namna ya kutoa mawazo yake kuhusu Dowans wakati akiwa serikalini tena Naibu Waziri.


“Umefika wakati Sitta na Mwakyembe waache kuendesha mambo kisiasa, bali waangalie sheria zaidi katika suala la Dowans,” alisema Chikawe.


Alisema kitendo cha mawaziri hao kumkosoa Waziri Ngeleja, kutokana na kutangaza hadharani kuilipa kampuni hiyo Sh bilioni 94, kimetoa picha kuwa kuna mgongano ndani ya Baraza la Mawaziri.


Alisema jambo zito kama hilo, halikupaswa kutolewa maelezo magazetini, bali wangetumia utaratibu wa kumfuata waziri husika na kutoa maoni na ushahidi walionao na iwapo wangeona waziri huyo hawatilii maanani, wangekwenda kwa Waziri Mkuu au Rais.


“Unajua Rais wetu ni mwepesi sana kuwasikiliza mawaziri wake wakati wowote, sasa iwapo wangeona waziri husika hawasikilizi, wangepeleka hoja yao kwake ambaye kama angeridhishwa na hoja zao, angeitisha kikao cha Baraza la Mawaziri kutoa uamuzi wa pamoja,” alisema Chikawe.


Chikawe alisema kuna utaratibu wa aina mbili, ambao waziri anaweza kuutumia kutoa uamuzi wa Serikali; kwanza ni kutoa uamuzi unaohusu wizara yake na mwingine, uamuzi wa pamoja.


Alifafanua kuwa waziri wa sekta husika, ana jukumu la kutoa uamuzi wowote wa wizara yake bila kuingiliwa na akiona kuna jambo zito linaloathiri sera za nchi, ndio hupeleka kwenye Baraza la Mawaziri ili lijadiliwe kabla ya kutoa uamuzi wa pamoja.


Chikawe alisema Waziri Sitta na Naibu Waziri Mwakyembe, walikuwa na nafasi ya kumwona Rais na kutoa ushahidi wao na iwapo Rais angeona kuna umuhimu wa kuitisha Baraza la Mawaziri, angefanya hivyo na si kutoa siri za Baraza kuwa hawajalijadili suala hilo.


Alisema maoni binafsi kwa mawaziri hao si tatizo, ndiyo maana katika Baraza la Mawaziri, kikao kinaweza kujadili suala moja kwa siku nzima mpaka wanafikia uamuzi wa pamoja, lakini kuyazungumzia hadharani ni kosa, kwa kuwa wamekiuka utaratibu wa utawala bora kwa kutoa siri za Baraza hilo.


Chikawe alimtetea Ngeleja kuwa inawezekana hakuona sababu ya kupeleka suala la kuilipa Dowans kwa Baraza la Mawaziri kwa kuwa alishirikisha wataalamu mbalimbali wa sheria na

kujiridhisha katika kufanya malipo kwa kampuni hiyo.

Wiki iliyopita, Waziri Sitta alipinga tamko la Waziri Ngeleja la kuilipa kampuni ya Dowans na kusema kuwa inashangaza waziri kutoa tamko hilo kabla hata Baraza la Mawaziri halijalijadili.


Juzi pia Naibu Waziri Mwakyembe, aliibuka na kusema anashangaa kusikia kampuni hiyo aliyoiita ya kitapeli, inalipwa kwa madai kuwa ilirithi mkataba wa kufua umeme kutoka katika kampuni hewa ya Richmond LCC Ltd.


Katika Bunge lililopita chini ya Spika Sitta, Mwakyembe aliongoza Kamati Maalumu iliyochunguza suala la kampuni ya kufua umeme ya Richmond hata kusababisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na mawaziri wawili, Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha, kujiuzulu kutokana na kashfa ya kampuni hiyo.


HabariLeo | Dowans ‘yawatafuna’ Sitta na Mwakyembe

Ijapokuwa kweli Sitta na Mwakyembe walikiuka taratibu, ni muhimu watanzania wakafahamu kuwa wajibu wa kwanza wa kiongozi kama waziri ni kulinda na kuendeleza maslahi ya taifa na wananchi wake. Huu utaratibu wa waziri kuwa na ruhusa ya kushauriana na wachache na kutolea maamuzi mambo bila baraza zima la mawaziri kukaa unatoa mwanya kwa waziri ku-conspire na wenzake wachache akiwemo raisi kuuza nchi. Kama mambo ni hivi ipo siku tutakuta raisi au waziri akishirikiana mafisadi wawili watatu ametuuza watz wote. Katika hali hiyo, ni lazima waziri mwenye uchungu na nchi yake akiuke utaratibu wa collective responsibility akemee mambo kunusuru nchi. Ndiyo Sitta na Mwakyembe wamekosea utaratibu, lakini yaangaliwe pia mazingira ya kukosea kwao jamani.

Ikumbukwe kuwa taratibu huwekwa kwa ajili ya watu, sio watu kwa ajili ya taratibu. Tatizo la baadhi ya viongozi ni kwamba wao huenzi taratibu badala ya watu. Wako tayari kulinda taratibu hata kama ni kwa gharama ya taifa zima! Shame. Wakati Lowassa alipolazimika kujiuzulu, nilishangaa kuwasikia wanasiasa wakongwe kama Kingunge wakilalamika eti utaratibu umekiukwa kwa kutokumuuliza Kwanza Lowassa ili ajitetee, huku akipuuza kabisa hoja mama iliyokuwa mezani ya kuhujumiwa uchumi wa nchi na Richmond. Yaani kwa Kingunge na wenzake hujuma kwa nchi aliyosababisha Lowassa halikuwa tatizo ila kutokulindiwa heshima kwa kupewa kwanza nafasi ya kujieleza ndio waliloliona ni issue!!! Hii ndiyo hali ya ccm ya kulindana iliyotufikisha hapa tulipo leo.

Cha ajabu watu hawa hawa hawasikiki kamwe zinapokiukwa taratibu kwa lengo la kujinufaisha. Ziko taratibu nyingi tu zilizokiukwa katika kusaini mikataba mibovu ambazo hawa watu hawazisemi. Kwao taratibu zinazowauma zikikiukwa ni zila zinazowaumbua tu. Unless Tz, learn a new culture of transparency and accountability we will not make it as a nation. Arise Tanzania, unaliwa mchana mchana.
 
JK awatoe basii kwani wao wanabembeeleza kuwemo serikali chafu??wewe chikawe unakiuka kiapo chako cha uwt???unasafisha upuuzi...mamama weee nchi imekwisha ona Membe alivyokuwa shujaaa....kumbuka kiapo chenu kimoja nyie usije ukayalamba matapishi yako siku ifikia??

we ckilz,unaota?haya taja ushujaa wa membe hapa,ume2mwa ee
 
Sitta na Mwakyembe wanajaribu kuficha aibu. Najua hawachomoki katika hili. They were supposed to foresee the repucation of breaching the Dowans contract. Were are paying Dowans b'se of Bunge fail to foresee!!

It's shame to have those kind of people!
Ni aibu gani hiyo wanayoificha tuambie seems you are speaking the opposite nani kati ya kina Sitta na mnaotetea Dowans wanaojaribu kuficha aibu, jaribuni kumwogopa Mungu hata siku moja, nyie ndio mlioleta madudu how comes wanaopinga hayo madudu wawe ndio waficha siri tena.
 
Chikawe kuwakemea mawaziri wenzake anatumia mamlaka yake vibaya (ultra vires).

Wenzangu, haya mambo yoote yanayoendelea ni maandalizi ya 2015. Kila aliyepo kwenye nafasi sasa anaangalia mbele na anaangalia pia ajiunge na mtandao gani kujihakikishia nafasi in 2015. Alianza mwana sheria mkuu, akawakataza wadanganyika kuwa suala la dowans limefungwa, na hakuna mjadala. As if yeye ni Muumba, akawaambia Wadanganyika, keep your mouth shut, we are going to pay Dowans, whether you like it or not. Huyo ni mwanasheria mkuu wa nchi, katili na kichwa ngumu

Akaja huyu Ngeleja, ninavyomfahamu Ngeleja, yeye hana maamuzi, kaletewa tu minute mezani kuwa lipa. Kwanza nashangaa, suala la kulipa si la Ngeleja, ni suala la hazina. Ngeleja hana bajeti hiyo, na kama ni kulipa, alitakiwa aseme Waziri mwenye dhamana ya hazina au mkuu wa Tanesco, sio Waziri. But ni jinsi anavoona upepo wa 2015 kuwa ajiunge na mtandao upi, kila mtu anangalia upepo.

Kama hilo halikutosha, akaja wakili anaitwa Fungamtama, akatisha sana kuwa nchi itayumba Dowans wasipolipwa. In my life sikuwahi kuona wakili wa kujitegemea akifanya hivyo, huyu naye kasukumwa na ulafi na uchu wa fedha. Akamshambulia waziri Sita na kusema ana chuki binafsi. Loh, nikashangaa, Sita ana chuki binafsi na wale watu wa nje waliotajwa na Ngeleja kuwa ndio wamiliki wa Dowans. Sita ana haja gani ya kuwa na chuki binafsi na wamalysia? Wenye akili wakajua mmiliki halali wa Dowans ni nani, na si shaka huyo mmiliki Sita anamjua na ndio maana ana bifu naye

Sasa kaja naye Chikawe, ambaye sijui kama anajua maana ya utawala bora, manake alivyofafanua kuhusu Sitta na Mwakyembe, si maana halisi ya utawala bora. Utawala bora ni ule unashirikisha jamii katika maamuzi mazito ya nchi, mfano kuilipa Dowans. Ngeleja na kikundi kidogo cha wanasheria hawawezi kufanya matumizi ya fedha za walipa kodi ya shs hizo bila walipa kodi kuelezwa na kukubaliana na jambo hilo. Wawakilishi wa wananchi ni wabunge, ipelekwe legislation bungeni kuomba kibali cha kuilipa Dowans-- hup ndio utawala bora.
Chikawe, with due respect Nadhani unatakiwa uende Ngurdoto ujifunze maana ya utawala bora. Kubariki mikataba hewa, si utawala bora, kufanya matumizi bila ridhaa ya walipa kodi kama kuwalipa dowans, si utawala bora. Sita kutoa maoni yake, hakuna muingiliano na utawala bora, Sita kusema bila kumshauri boss wake hakuna uhusiano na utawala bora, hiyo inaweza kuwa ni insubordianation. Chikawe, please unabore, kwa sababu kama waziri wa utawala bora hajua maana ya utawala bora, anazungumzia insurbodination kuwa ni kukosa utawala bora, hafai
 
Hiyo ndiyo serikali ya JK, kila mmoja na lwake, anakuja huyu anasema hili, mwenzake anamrushia upupu ili aweze kumpiku kumbe ni urojo tu na akili mgando kama kawaida yao.

Chikawe atambue kuwa Sitta na Mwakyembe wametoa faraja kwa umma kuwa angalau wanapata uchungu kwa wizi wa mchana unaohalalishwa na Ngeleja kumlipa mwajiri wake wa zamani RA.

Chikawe ni kipofu na 'nyani asiyeona kundule' maana asiwalaumu wanaowaeleza umma ukweli eti wanakiuka utawala bora. ni porojo na kufilisika.

Yeye atupe ukweli toka ktk wizara yake kuhusu mali za vigogo ambao kwa mamia wamegoma kutaja utajiri wao na yeye hana kauli au lolote la kueleza umma. je huo ndio utawala bora?
asimtishe yeyote! hapo alipo naye kawekwa ili kuficha ufidhuli wa wakuu wake akiwepo JK na RA na mfano halisi ni kama hili la DOWANS. Apotelee mbali asizidishe uchungu na hasira kwa umma unaodhulumika kila uchao.
 
Chikawe hana madaraka wala uwezo wa kulazimisha nidhamu kwa waziri yeyote. Kama yeye aliona kuwa wenzake wamekosea kwanini na yeye asimwambie Waziri Mkuu au Rais yeye mwenyewe? Sasa kesho kina Mwakyembe nao wakimjibu kwa magazeti ataona wamemvunjia heshima au wamevunja kanuni?


Mimi naona hawa wanatunishiana misuli.

Ningetamani kumsikia Sitta na Mwakiembe wakimnjibu Chikawe. Na kama wanaona kauli ya chikawe inapingana na mawazo yao, basi wajiuzulu ili waungane na wanachi na wanasheria wengine wapinge haya malipo mahakamani.
 
Chikawe hana akili hata chembe na sijui Kikwete aliwatoa wapi wa aina hii?? ni bora tu kikwete akawaingiza akina maralia sugu, mtu wa pwani nk watanzania tukajua moja, kuliko kuingiza mbunge sjui wa wapi ambaye anawaibisha waliomchagua!!! Hakika kama nchi hii ingelikuwa ni kenya kwa katiba mpya, wananchi wange petition na kumvua ubunge wake!!!
 
Wanachokifanya Sitta na Mwakyembe ni kama mtu mzima anapoona mtoto mdogo ametumbukia kwenye ndoo ya maji na wakachukua hatua ya kumtoa kumuokoa na baadaye kumtafuta mama yake (ni logic than sheria) kwa sababu ukimtafuta mama yake ili aje amuokoe huenda akawa ameshakufa. Uzalendo wa Mwakyembe na Sitta umewafanya kuona taratibu za kupeleka isshu kwenye baraza la mawaziri ni upotezaji wamuda ambao wizi wa Dowans huenda ukawa umeshafanyika
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom