Chikawe aikabili M4C kwa kugawa sanda Misikitini Nachingwea!

MgungaMiba

JF-Expert Member
Aug 28, 2011
999
815
Mbunge wa Nachingwea Bw Chikawe, alipopata habari kuwa kizaazaa cha M4C kilicholeta maafa makubwa kwa CCM Mkoani Mtwara kitaingia Wilayani kwake leo J'5 likitokea Wilayani Nanyumbu Mkoani Mtwara, basi jana nzima alikuwa akihaha kwenye Misikiti mbalimbali kama vile Misikiti ya Kata za Namapuya, Nditi, Mtonda, Nachingwea nk akigawa Sanda za kuzikia Maiti kwa biidii! Ingawa matangazo ya mikutano ya leo yalishaanza kutolewa, lakini inasemekana Convoy hilo la M4C limebadilisha ratiba na ruti yake hivyo halitafika Nachingwea leo, bali litafika baada ya siku 3 au 4 hivi likitokea Lindi Mjini, hivyo atakuwa amepata nafasi zaidi kwenda kufungasha Sanda nyingine zaidi za kugawa katika Misikiti ya Kata zilizobakia!
 
Yani anagawa sanda inamaana anawatakia umauti watu wake na wanaopokea kweli na hamnazo!!
 
Yani anagawa sanda inamaana anawatakia umauti watu wake na wanaopokea kweli na hamnazo!!

mkuu, mifumo yao yote ya fahamu ilishakufa, uwezo wa kufikiri kwishnei. Anataka wapiga kura wake wafe au anawalaani? watu wanalia maisha magumu, kisha anawapelekea sanda....CCM...LoL!!!
 
Yaanj sanda amabayo haizidi hata 20,000 kwa misikiti isiyozidi hata kumi ndiyo anaweza kujinusuru na M4C? Kama ni kuishwa sera basi huu ndiko kwa mwisho kabisa.
 
Anagawa sanda badala ya kugawa madawa mahospitalini hii ni hatari sana anachuria watu Vifo hafai kabisa. Mwishoni atawagawia sumu ili waweze kutumia hizo sanda
 
Kweli kusini mmedharaulika yaani among all rushwaz nyie mnapewagwa za SANDA????????? Forgive my understanding
 
Sanda!!!! Haiwezekani. Kwani huko kwa siku wanakufa wangapi?
 
Una agenda ya siri,,,, SANDA,,, sidhani kuwa hiyo ni matatizo ya wananchi wa jimbo lake
 
kwa hiyo dar es salaam wanajengewa maghorofa ila wa mtwara wanapewa sanda...kweli watu wa kusini ccm inawaona hamnazo

hivi inawezekana kugawa sanda arusha au MUSOMA?? mbona tunadharauliana ivyo jamani???
 
Poor thinking, poor strategy. huku ni kukurupuka na kutojua nini cha kufanya i.e. kupanic!

Huwezi kwenda kuwagawia wapiga kura wako sanda!!! kwanza ni laana na pili ni kuwaona hamnazo! sidhani kama matatizo ya wananchi wa jimbo lake ni namna ipi ya kuwazika wafu wao.

Kama hao wapiga kura wake hali zao za maisha zimekuwa ngumu kiasi cha hata kuwasitiri wafu wao kwa sanda, basi ni sababu tosha ya kumweka mbunge wao na chama chake pembeni kwa kuwafikisha kwenye ugumu huo wa maisha!!! Poleni sana CCM! Haya ndiyo matokeo ya chama kutokuwa kimoja.

Kila mtu anajiamulia kivyake kwa uwezo wake wa kufikiri ...ingawa akichemka kama alivyochemka waziri huyu wa sheria, itakayoumia ni CCM!!
 
Haya ni matusi kwa wapiga kura wake yaani ameona hakuna msaada mwingine anaoweza kuwa saidia isipokuwa yeye amewaona wao ni wakufa tu.je?.na sanda yake ameiandaa.
 
This is layman solution.
Hakika kuitetea CCM unatakiwa uwe na akili ya maiti.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Duh !! UMASIKINI WAKUKOSA NDOTO NA MAWAZO NI MBAYA SANA!! Kunamsemo "Masikini haishiwi ndoto" sijui huko kusini kama itawasaidia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom