Chifu Mwangupili wa Unyakyusa na Ibara 29:3,4

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Na Mwandishi Maalum, (Habari Leo)
Kyela, Mbeya

mwangupili.jpg

Rais Jakaya Mrisho Kikwete Jumamosi Oktoba 11, 2008) ametawazwa kuwa chifu wa Kabila la Wanyakyusa na amepewa jina rasmi la Chifu Mwangupili.
Rais amepewa heshima hiyo na wazee wa Wilaya ya Kyela, mkoa wa Mbeya, kwenye Uwanja wa Michezo wa mji wa Kyela wakati alipotembelea wilaya hiyo akiwa katika siku ya tatu ya ziara ya Mkoa huo.

Tangazo la Rais Kikwete kuwa Chifu Mwangupili limetolewa kwenye Uwanja wa Michezo wa Kyela mbele ya maelfu ya wananchi ambako pia alivalishwa wazi rasmi la kichifu na kupewa zana nyingine kukamilisha heshima hiyo.

Wazee wa Wilaya hiyo wamesema kuwa wameamua kumpa heshima hiyo Rais Kikwete kwa sababu ya uhodari wa utawala wake na kwamba Chifu Mwangupili alikuwa babu wa Chifu Magombe Mwakyusa ambaye alikuwa chifu wa eneo la Kyela.

Akizungumza mara baada ya kuwa ametawazwa kuwa chifu wa kabila hilo, Rais Kikwete amewashukuru wazee na wakazi wote wa wilaya hiyo kwa uamuzi wake wa kumtunukia heshima ya kuitwa Chifu Mwangupili.

Baada ya hapo, ametumia muda wa kutosha kuelezea utekelezaji wa ahadi za Serikali zake kitaifa na katika wilaya ya Kenya katika maeneo ya elimu, afya, miundombinu na hasa ujenzi wa barabara, uwezeshaji wa wananchi.

Kwa mara nyingine amesisitiza kuwa Serikali Kuu imekuwa inatoa fedha nyingine kwa serikali za mitaa kwa ajili ya maendeleo, lakini mara nyingine fedha hizo zimekuwa hazisimamiwi vizuri na madiwani.

Amesisitiza kuwa ni wajibu wa madiwani kusimamia vizuri fedha hizo ili matunda ya fedha hizo yaonekane katika mabadiliko ya maisha ya wananchi iwe kwa njia ya elimu, afya ama hata miundombinu.

Wilaya ya Kyela imepewa sh bilioni 12 kwa ajili ya kuendeleza miradi mbali mbali wilayani humo kwa mwaka huu.

"Kama ninavyosema kila mara, tunatoa fedha nyingi mno kuliko wakati mwingine wowote tokea tupate uhuru, lakini lazima matumizi ya fedha hizi yasimamiwe na madiwani ambao ndiyo wabunge wetu kwenye ngazi ya Serikali za Mitaa."

Mapema akipokea taarifa ya wilaya hiyo ya Kyela, Rais Kikwete amewaonya wakazi wa wilaya hiyo kuvusha dawa kutoka Tanzania na kuzipeleka kwa jamaa zao katika nchi jirani ya Malawi.

Kwenye taarifa hiyo iliyotolewa katika eneo la mpakani kabisa mwa Tanzania na Malawi la Kasumulu, ilielezwa kuwa hospitali za wilaya hiyo zimekuwa zinakabiliwa na matatizo makubwa ya sekya ya afya ikiwa ni pamoja na ukosefu wa dawa za kutosha kiasi cha kwamba baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo wamekuwa wakitafuta huduma za afya katika wilaya jirani ya Rungwe.
"Naambiwa sasa tatizo limepatiwa ufumbuzi, lakini pia naambiwa kuwa mmekuwa mnachukua dawa katika hospitali zetu na kuzipeleka kwa jamaa zenu Malawi.

"Hapa tunayo matatizo makubwa ya afya. Tunalo tatizo kubwa la malaria. Msipeleke dawa hizo kule nchi jirani ya Malawi. Hawa wajomba wenu kama wanataka kutibiwa wavusheni mpaka na kuwaleta huku," amesema na kuongeza:
"Watu wa ajabu nyie. Dawa mnapeleka Malawi, halafu nyie mnakwenda Rungwe kutibiwa. Kweli ujanja mwingi huondoa maarufu."

My Take:
Ibara ya 29:3,4 ya Katiba yetu inasema hivi:
(3) Raia yoyote wa Jamhuri ya Muungano hatakuwa na haki,
hadhi au cheo maalum kwa misingi ya nasaba, jadi au urithi
wake.
(4) Ni marufuku kwa sheria yoyote kutoa haki, hadhi au cheo
maalum kwa raia yeyote wa Jamhuri ya Muungano kwa misingi
ya nasaba, jadi au urithi.
 
Na Mwandishi Maalum, (Habari Leo)
Kyela, Mbeya

mwangupili.jpg

Rais Jakaya Mrisho Kikwete Jumamosi Oktoba 11, 2008) ametawazwa kuwa chifu wa Kabila la Wanyakyusa na amepewa jina rasmi la Chifu Mwangupili.
Rais amepewa heshima hiyo na wazee wa Wilaya ya Kyela, mkoa wa Mbeya, kwenye Uwanja wa Michezo wa mji wa Kyela wakati alipotembelea wilaya hiyo akiwa katika siku ya tatu ya ziara ya Mkoa huo.

Tangazo la Rais Kikwete kuwa Chifu Mwangupili limetolewa kwenye Uwanja wa Michezo wa Kyela mbele ya maelfu ya wananchi ambako pia alivalishwa wazi rasmi la kichifu na kupewa zana nyingine kukamilisha heshima hiyo.

Wazee wa Wilaya hiyo wamesema kuwa wameamua kumpa heshima hiyo Rais Kikwete kwa sababu ya uhodari wa utawala wake na kwamba Chifu Mwangupili alikuwa babu wa Chifu Magombe Mwakyusa ambaye alikuwa chifu wa eneo la Kyela.

Akizungumza mara baada ya kuwa ametawazwa kuwa chifu wa kabila hilo, Rais Kikwete amewashukuru wazee na wakazi wote wa wilaya hiyo kwa uamuzi wake wa kumtunukia heshima ya kuitwa Chifu Mwangupili.

Baada ya hapo, ametumia muda wa kutosha kuelezea utekelezaji wa ahadi za Serikali zake kitaifa na katika wilaya ya Kenya katika maeneo ya elimu, afya, miundombinu na hasa ujenzi wa barabara, uwezeshaji wa wananchi.

Kwa mara nyingine amesisitiza kuwa Serikali Kuu imekuwa inatoa fedha nyingine kwa serikali za mitaa kwa ajili ya maendeleo, lakini mara nyingine fedha hizo zimekuwa hazisimamiwi vizuri na madiwani.

Amesisitiza kuwa ni wajibu wa madiwani kusimamia vizuri fedha hizo ili matunda ya fedha hizo yaonekane katika mabadiliko ya maisha ya wananchi iwe kwa njia ya elimu, afya ama hata miundombinu.

Wilaya ya Kyela imepewa sh bilioni 12 kwa ajili ya kuendeleza miradi mbali mbali wilayani humo kwa mwaka huu.

“Kama ninavyosema kila mara, tunatoa fedha nyingi mno kuliko wakati mwingine wowote tokea tupate uhuru, lakini lazima matumizi ya fedha hizi yasimamiwe na madiwani ambao ndiyo wabunge wetu kwenye ngazi ya Serikali za Mitaa.”

Mapema akipokea taarifa ya wilaya hiyo ya Kyela, Rais Kikwete amewaonya wakazi wa wilaya hiyo kuvusha dawa kutoka Tanzania na kuzipeleka kwa jamaa zao katika nchi jirani ya Malawi.

Kwenye taarifa hiyo iliyotolewa katika eneo la mpakani kabisa mwa Tanzania na Malawi la Kasumulu, ilielezwa kuwa hospitali za wilaya hiyo zimekuwa zinakabiliwa na matatizo makubwa ya sekya ya afya ikiwa ni pamoja na ukosefu wa dawa za kutosha kiasi cha kwamba baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo wamekuwa wakitafuta huduma za afya katika wilaya jirani ya Rungwe.
“Naambiwa sasa tatizo limepatiwa ufumbuzi, lakini pia naambiwa kuwa mmekuwa mnachukua dawa katika hospitali zetu na kuzipeleka kwa jamaa zenu Malawi.

“Hapa tunayo matatizo makubwa ya afya. Tunalo tatizo kubwa la malaria. Msipeleke dawa hizo kule nchi jirani ya Malawi. Hawa wajomba wenu kama wanataka kutibiwa wavusheni mpaka na kuwaleta huku,” amesema na kuongeza:
“Watu wa ajabu nyie. Dawa mnapeleka Malawi, halafu nyie mnakwenda Rungwe kutibiwa. Kweli ujanja mwingi huondoa maarufu.”

My Take:
Ibara ya 29:3,4 ya Katiba yetu inasema hivi
:

Lakini hii si ni symbolic tu....Kwani atakuwa mtawala halali atakayetumia uchifu wake huo aliopewa kutawala? Ataondoka hapo na kurudi Ikulu na kuvua hiyo mitambara aliyovaa kichwani, hilo limkuki litawekwa stoo, atavaa suti yake ya Brooks Brothers halafu huyo atapanda G5 yake kwenda kiwanja....
 
Nafahamu wanachoashiria lakini sicho wanachosema; Katiba haina utata, soma hicho kipengele cha pili. Najaribu kukumbuka mahali ambapo Nyerere alikuwa anakubali kuvikwa mavazi haya ya uchifu, inawezekana ilikuwepo lakini nimetafuta sana picha sijaziona.
 
Mi nadhani wanachosema ni uchifu utakaokuwa na authoritative powers na sio huu wa kuvikwa migwanda kwenye sherehe halafu mkimaliza hakuna atakayekumbuka tena kuwa wewe ni chifu wa sehemu fulani. Mbona Fundikira aliendelea kuwa na hiyo title ya uchifu hata wakati wa Nyerere. Labda basi wangeweka wazi kwenye katiba kuwa hata uchifu wa ishara ni marufuku.
 
Nafahamu wanachoashiria lakini sicho wanachosema; Katiba haina utata, soma hicho kipengele cha pili. Najaribu kukumbuka mahali ambapo Nyerere alikuwa anakubali kuvikwa mavazi haya ya uchifu, inawezekana ilikuwepo lakini nimetafuta sana picha sijaziona.[/QUOTE]

mzee Mwanakijiji Unakosea kama Nyerere hakuvaa labda yalikuwa matashi yake tu lakini isiwe kigezo cha rais mwingene kutokuvaa.
Kuna vitu vingi tu Mwalimu hakufanya alipokuwa madarakani lakini viongozi wengine wamefanya na haikuwa kosa, nafikiri tujaribu kuangaria hilo la katiba tu, tusimchukulie mzee wa watu kama SI unit ya matendo ya Ikulu
 
Katiba imeweka wazi kabisa kuwa:

(3) Raia yoyote wa Jamhuri ya Muungano hatakuwa na haki,
hadhi au cheo maalum kwa misingi ya nasaba, jadi au urithi
wake.
(4) Ni marufuku kwa sheria yoyote kutoa haki, hadhi au cheo
maalum kwa raia yeyote wa Jamhuri ya Muungano kwa misingi
ya nasaba, jadi au urithi.

Kimsingi kwangu siyo huo uchifu wa ishara wa mtu asiye na nasaba au urithi wa uchifu; kwangu ni hilo la watu ambao wanatambulishwa katika jamii kuwa ni machifu kutokana na nasaba zao au urithi wao. Kikatiba watu hao hawapo na ni makosa kwa kiongozi wa serikali kuwatambua hivyo au kuwatambulisha hivyo.

Lakini Katiba katika hilo halina utata kuwa inasema "hakutakuwa"... sasa mbona wapo?
 
Nyerere aliwahi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tena wa kwanza, hivyo kumtumia mfano si kosa. Au unataka tumfute hata kwenye historia na mtu yeyote asilinganishwe naye ambaye ataupata Urais baadaye?
 
Mzee Mwanakijiji,

Mbona Nyerere alishavaa sana hayo manguo ya jadi? Binafsi nilishaona picha za Nyerere mara nyingi tu akivishwa hayo manguo.

Kitu ambacho sikumbuki ni kama yalikuwa ya kijadi au kichifu.
 
Katiba imeweka wazi kabisa kuwa:

(3) Raia yoyote wa Jamhuri ya Muungano hatakuwa na haki,
hadhi au cheo maalum kwa misingi ya nasaba, jadi au urithi
wake.
(4) Ni marufuku kwa sheria yoyote kutoa haki, hadhi au cheo
maalum kwa raia yeyote wa Jamhuri ya Muungano kwa misingi
ya nasaba, jadi au urithi.

Kimsingi kwangu siyo huo uchifu wa ishara wa mtu asiye na nasaba au urithi wa uchifu; kwangu ni hilo la watu ambao wanatambulishwa katika jamii kuwa ni machifu kutokana na nasaba zao au urithi wao. Kikatiba watu hao hawapo na ni makosa kwa kiongozi wa serikali kuwatambua hivyo au kuwatambulisha hivyo.

Lakini Katiba katika hilo halina utata kuwa inasema "hakutakuwa"... sasa mbona wapo?

Kwa hiyo mimi nikianza kujiita Chifu Nyani na baadhi ya watu wakaanza kuniita hivyo na nika design vazi langu mwenyewe na kila sehemu nitakayoenda watu watakuwa wakiniita Chifu Nyani McCain nitakuwa nimevunja katiba?

Halafu kwenye hiyo habari sijaona chifu yeyote yule. Wamesema ni wazee ndio waliompa hicho cheo.
 
Who cares anyway? Watu wanataka na kujali maisha bora na sio ku-mind migwanda na mitambara anayovaa au kuvalishwa kiongozi fulani kwenye hafla ambaye baada ya hafla atarudi nyumbani na kumpa hiyo kitambara housebirl au houseboy kupigia deki. Come on people......
 
Mwanakijiji,

..kwa kweli hapa tulipofika Kikwete inabidi abadili jina sasa.

..tena nadhani jina Mwangupili linamfaa.

..Raisi ameharibu kwelikweli. inabidi aanze upya.

..kutuhakikishia kwamba ameachana uzembe na tarbia zake za zamani, na pia kutupa imani mpya, inabidi abadili jina.

NB:
 
Kwa hiyo mimi nikianza kujiita Chifu Nyani na baadhi ya watu wakaanza kuniita hivyo na nika design vazi langu mwenyewe na kila sehemu nitakayoenda watu watakuwa wakiniita Chifu Nyani McCain nitakuwa nimevunja katiba?

Halafu kwenye hiyo habari sijaona chifu yeyote yule. Wamesema ni wazee ndio waliompa hicho cheo.

kwenye origina story huyo anayemvika hayo magwanda ni Chifu of sort..
 
Who cares anyway? Watu wanataka na kujali maisha bora na sio ku-mind migwanda na mitambara anayovaa au kuvalishwa kiongozi fulani kwenye hafla ambaye baada ya hafla atarudi nyumbani na kumpa hiyo kitambara housebirl au houseboy kupigia deki. Come on people......

Nyani, it matters a lot.

Unajua kwanini wamarekani walikataa George Washington asiwe mfalme wa aina fulani na Katiba yao (kama ya kwetu) inamkataza Mmarekani yeyote yule kupokea cheo chochote kinachotolewa kwa kurithishana.
 
kwenye origina story huyo anayemvika hayo magwanda ni Chifu of sort..

Original story ndiyo hiyo uliyoiweka wewe au? Maana nimerudia tena kusoma na hakuna sehemu inayoonyesha huyo anayemvika magwanda Kikwete kuwa ni chifu of sort unless umefikia hiyo conclusion kwa sababu na yeye kavaa hiyo migwanda.... Sana sana kilichosemwa ni kwamba Chifu Mwangupili (Kikwete) alikuwa ni babu wa Chifu Magombe Mwakusya ambaye "alikuwa" chifu wa eneo la Kyela......
 
Katiba imeweka wazi kabisa kuwa:

(3) Raia yoyote wa Jamhuri ya Muungano hatakuwa na haki,
hadhi au cheo maalum kwa misingi ya nasaba, jadi au urithi
wake.
(4) Ni marufuku kwa sheria yoyote kutoa haki, hadhi au cheo
maalum kwa raia yeyote wa Jamhuri ya Muungano kwa misingi
ya nasaba, jadi au urithi.

Kimsingi kwangu siyo huo uchifu wa ishara wa mtu asiye na nasaba au urithi wa uchifu; kwangu ni hilo la watu ambao wanatambulishwa katika jamii kuwa ni machifu kutokana na nasaba zao au urithi wao. Kikatiba watu hao hawapo na ni makosa kwa kiongozi wa serikali kuwatambua hivyo au kuwatambulisha hivyo.

Lakini Katiba katika hilo halina utata kuwa inasema "hakutakuwa"... sasa mbona wapo?

Mkuu hii ukiipeleka mahakamani utashindwa kesi kufuatana na misingi ya tafsiri ya sheria katika korti. Ibara ya 29(4) inasema "ni marufuku kwa sheria yoyote kutoa haki, hadhi au cheo...". Hakuna sheria hapo iliyotoa haki, hadhi au cheo maalum kwa Mwangulupi. Pia Ibara ya 29(3) inasema "...kwa misingi ya nasaba, jadi au urithi wake". Hapo Mwangulupi hakupewa uchifu kwa misingi ya nasaba yake ya Uafrika, jadi yake ya Kikwere au urithi wake wa Kichifu. Kesi imefungwa.
 
Kwa hiyo Wanyakyusa (akina Mtanzania) wamekubali Mwangupuli (Kikwete) kuwa Chifu wao!!!!............my God!........i don't want to believe this......kwi kwi kwi kwi kwi
 
......and this is very interesting.........

Na Mwandishi Maalum, (Habari Leo)
Kyela, Mbeya

mwangupili.jpg

Wazee wa Wilaya hiyo wamesema kuwa wameamua kumpa heshima hiyo Rais Kikwete kwa sababu ya uhodari wa utawala wake na kwamba Chifu Mwangupili alikuwa babu wa Chifu Magombe Mwakyusa ambaye alikuwa chifu wa eneo la Kyela.

Na hapa Chifu Mwangupuli (Kikwete) anawaambia wafuasi wake...........
"Hapa tunayo matatizo makubwa ya afya. Tunalo tatizo kubwa la malaria. Msipeleke dawa hizo kule nchi jirani ya Malawi. Hawa wajomba wenu kama wanataka kutibiwa wavusheni mpaka na kuwaleta huku," amesema na kuongeza:
"Watu wa ajabu nyie. Dawa mnapeleka Malawi, halafu nyie mnakwenda Rungwe kutibiwa. Kweli ujanja mwingi huondoa maarufu.".................

eeeeehhhhh!!!......kwi kwi kwi kwi kwi
 
Nyani, it matters a lot.

Unajua kwanini wamarekani walikataa George Washington asiwe mfalme wa aina fulani na Katiba yao (kama ya kwetu) inamkataza Mmarekani yeyote yule kupokea cheo chochote kinachotolewa kwa kurithishana.

So it matters because the Americans didn't want to?

My point is this: kisheria machifu hawatambuliwi na hawana mamlaka yoyote yale. Lakini kama watu wa sehemu fulani wakiamua kukuita wewe Mwanakijiji Chifu Mwanakijiji kuna ubaya gani? Haina maana utakuwa unatawala watu na haina maana watoto wako watarithi hicho cheo na hata na wao wakiamua kujiita Chifu Mwanakijiji Jr.....hey what's wrong with that?
 
Mkuu hii ukiipeleka mahakamani utashindwa kesi kwa kufuata misingi ya tafsiri ya sheria katika korti. Ibara ya 29(4) inasema "ni marufuku kwa sheria yoyote kutoa haki, hadhi au cheo...". Hakuna sheria hapo iliyotoa haki, hadhi au cheo maalum kwa Mwangulupi. Pia Ibara ya 29(3) inasema "...kwa misingi ya nasaba, jadi au urithi wake". Hapo Mwangulupi hakupewa uchifu kwa misingi ya nasaba yake ya Uafrika, jadi yake ya Kikwere au urithi wake wa Kichifu. Kesi imefungwa.

We utamuweza Mwanakijiji.....
Yaani hata hii anataka kuishikia bango....naona kaboreka leo...
 
Back
Top Bottom