Chezea mume wa mtu??

aisee acheni tu haya mambo yapo believe kuna dada alikuwa anaenda mwenzini kila siku mpaka kwenda kumpigia magoti mama wa kizaramo

Kwa ufupi uku kwetu uswahilini jina nahifadhi kulikuluwa na baba la kihaya la haja watoto walisoma st Mary's enzi hizo wote wanne yani alikuwa na fuba si unajua sisi tukishachezwa sijui miemuko inazidi basi libaba likavamia binti na binti akakubali jamaa likasahau mpaka ada za watoto watoto wakafukuzwa na kurudi shule za serikali mama mwenye mume si akamuendea bagamoyo dah binti alikuwa atoki ndani tangu siku ya kufahamu hayo sikwenda kusuka kwa yule mama nilimuogopa sana mama mzazi wa binti na binti wakaenda omba msamaha bahati mbaya mama kagoma sijui kilichofata maana nilihamishwa mkoa sikufatilia zaidi

swali hv ni kutojiamini , tamaa , roho mchafu anayetupelekea kuchua mume wa mtu kama hajui sawa lakini wengine tunajua lakini bado ....ee Mungu nipe wangu loh ingawa nakaribiaa menopose kwa mbali dah

Yaaani hilo jibaba naona lilisubiri hadi basi kitu kimelowa tuuu hiii no noma...kila la heri mwaya Mungu na akutane na haja za moyo wako.
 
NATA shogaangu ndo kawa chizi hivi tunavyoongea babake kaja kumchukua wanampeleka kwao kanda ya ziwa huyo mwenye mume anaishi mtaani kwetu.sina mazoea naye kivilee ntaanzaje?

Sasa umejuaje kama kamloga?

Wawezakuwa wachuma dhambi bure, shoga ako anamaradhi mengine .lol!
 
Hayo yalimkuta class mate wetu o'level miaka ya mwanzo mwa 90. Alikuwa na viela huyo mdada kuteketeza laki kwa siku kwenye vipodozi kwake haikuwa tabu; miaka hiyo laki pesa. Tukaja kuzinasa kuwa anatembea na baba jirani yao na ni baba wa rafiki yake (umri wa kumzaa). Tukamaliza o level fresh; baada ya kama mwaka nikaja sikia dada kachizika. Wanavyosema yule mama jirani alimfata akamuuliza "unatembea na mume wangu" dada kakataa kata kata; akamwambia sasa tutaona mjanja nani.

Nasikia ndugu zake walikuja kupata dawa baada ya kumpeleka mikoa yote inayoaminika kwa uganga. Lakini nilikuja kumuona amechakaa mbaya si unajua mtu akiwa chizi hawezi tena kuwa normal; sad enough alikuwa very bright lakini kwa kuwa alikuwa chizi hakuendelea na shule.

Wanawake ambao mume kwao ni kila kitu wanaloga aisee ukiingia kwenye kumi na nane zao; maana wakiachika wataenda wapi. Mume ndo kila kitu including ajira.

Wanakazi kwelikweli!
Maana hawa wanaume vipanga hawaishi kutongoza, so wanaloga kila kukicha?
 
Ila jamani acheni tu, kuiba nako kutamu dah! Wenzangu humu jamvini niambieni hakuna ambaye ameiba kweli??
 
DERICK2000: Usiseme mwanamke amepata ndoa kwa bahati :hiyo si bahati ikiwa their love was pure and naturally sababu kumbuka huyo mumewe ndio ubavu wake na hakuna alikoahidiwa ubavu wa pili(watakuwa mwili mmoja)kosa ni hilo kuchizisha kwa uchawi lakini kulinda ndoa ni haki ya kila mwanamke

My dear, ni weredi mdogo tu wawanawake, na kuona mwanaume ndio kila kitu, hivi vyote vinapita tu,
ndoa ngapi zimevunjika na waliapa kuwa kifo ndio kitawatenganisha?

So ni mwanamke kujua adui wake hasa ni huyo mwanaume na si wanawake anaokutana nao HUYO MWANAUME . UKIZINGATIA KUWA WANAWAKE WENGI WANATONGOZWA HAWATONGOZI NA PIA huyo mumewe ndio anajua kuwa ameahidi nini na anatakiwa kulinda na kusimamia nini?

Wanaume wengine ni waongo sana, so anaweza akawa amemdanganya huyo dada kuwa hana mke.
 
Hivi ule usemi wa sikio la kufa halisikii dawa nadhani hapa inaweza kuwa quoted lol

Halafu we biggirl: Yaelekea si rafiki mwema, kwani inaonekana unashabikia yaliyomkuta shogaako badala ya kusikiika.
Wewe si rafiki mzuri kabisa!
 
wabongo wanapenda sana kula vya watu....juzi kati tu huko kenya kuna jamaa kanasa kwa my waifuu wa mwenzake

Check kitu live hii hapa...hapa ndio utaamini Jina la Yesu linafanya kazi na Mungu ni Mungu wa rehema...kwasababu amewarehemu hata hawa waliogandani kiunoni .....baada ya Maombi ya mchungaji on the spot kitandani

Mke au Mume wa mtu sumu acha kabisa!!!!
 
Last edited by a moderator:
Halafu we biggirl: Yaelekea si rafiki mwema, kwani inaonekana unashabikia yaliyomkuta shogaako badala ya kusikiika.
Wewe si rafiki mzuri kabisa!

NATA;kikweli ni rafiki yangu ila mambo kama hayo sipendi best na hata akipona nitamwambia lol we unataka mi nikawe kuni kwa matendo yake akuuuu kayataka mwenyewe mi nilimkataza hakuniskia na hata wewe Nata usidhani ni marafiki wote wanaokuchekea usoni moyoni wanafurahia baadhi ya matendo yako lol
 
Wanajf,mimi nina rafiki yangu mmoja alikuwa na tabia ya kuiba waume za watu nimemkanya mara nyingi lakini akawa hanisikii sasa kakutana na kiboko yake kafanywa chizi kabisa anakimbia ovyo mitaani ,namhurumia ila sina cha kufanya .wadau mnaojihusisha na hii mambo nawashauri acheni!!!!!!!!

Acha kuwatisha wenzio wewe...
Inaonekana unamlinda mmeo kwa kutoa vitisho kwa wanaJF...

Umehisi anammega __________ hapa nini?
Ila kasema ameacha...
 
Acha kuwatisha wenzio wewe...
Inaonekana unamlinda mmeo kwa kutoa vitisho kwa wanaJF...

Umehisi anammega __________ hapa nini?
Ila kasema ameacha...

Tuko taratibu nimtishie nani wakubwa wazima humu ?kwanza watamuweza mume wangu sa hizi yuko zake huko anavua samaki wake ukimuona unadhani utamtamani hiyo kurudi yenyewe shombo tupu anakuja ogea nyumbani nimfaidi mwenyeweee lol habari ndio hiyo
 
Back
Top Bottom