Cheyo hakustahili kuongoza kamati ya matumizi ya serikali.

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Kulingana na mfumo unaotumika katika mabunge ya "commonwealth", mwenyekiti wa kamati ya matumizi ya serikali anapashwa kutoka kwenye chama kilichoshika nafasi ya pili nyuma ya kile kinachounda serikali, ambacho ni CDM. Katika hali hiyo kumteua mtu kama Cheyo, ambaye idadi ya kura zilizopigwa kwa chama chake hazifikii hata asilimia moja, ni sawa na kuinyima sauti ya umma fursa ya kusimamia serikali katika matumizi ya rasilimali ya umma.
 
halafu inawezekanaje chama chake kiko Bariadi tu, hakijapanuka nje ya hapo miongo kadhaa sasa. Au akishakwaa ubunge anakuwa amefunga kazi hadi baada ya miaka 5 tena.
By the way, katibu mkuu wa hicho chama cha Cheyo anaitwa nani?
 
knye bold ni mdogo wake yule wa kiume aligombea na chenge akashindwa hiki ni cha cha familia
 
halafu inawezekanaje chama chake kiko Bariadi tu, hakijapanuka nje ya hapo miongo kadhaa sasa. Au akishakwaa ubunge anakuwa amefunga kazi hadi baada ya miaka 5 tena.
By the way, katibu mkuu wa hicho chama cha Cheyo anaitwa nani?

Sio katibu mkuu tu, mimi sijawahi kusikia kiongozi yeyote!!:twitch:
 
Niwakumbushe tu kwamba, Mh. Cheyo ni mdaiwa sugu wa pesa na madeni ya serikali. Kumbukeni nyumba yake ni moja ya rasilimali zake zilizo kwenye orodha ya kupigwa mnada ili kurudisha fedha za serikali ambazo alizifuja kwenye zabuni zake za ujenzi wa barabara. Jambo hili lilitulia baada ya kuonyesha hisia chanya kwenye mrengo wa utawala uliopo, vinginevyo ilikuwa kila kitu kiende.

Je, kwa mazingira ya aina hii unategemea ufanisi wa aina gani watanganyika wautarajia katika kuiongoza kamati hii? Bila shaka haihitaji kuwa na digrii kulijua jibu la swali hili.

Kifupi, tuandike maumivu wakuu.

Nilikuwepo.
 
Back
Top Bottom