Cheyo asimamishwa usemaji kambi ya upinzani

PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,599
3,673
Leo hii kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, Mhe. Hamad Rashid Mohamed amemuondoa Mhe. Cheyo kutokuwa tena msemaji wa upinzani katika wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi na hii inafuatia ukigeugeu wa Cheyo hadi jana akaenda kinyume na wapinzani wenzake kwa kuunga mkono bajeti ya serikali ya CCM
 
is it true?je kwa mujibu wa Katiba ya Upinzani Hamad Rashid ana mamlaka hayo?na je hata kama angekataa kuunga mkono Bajeti ile je inga add any value kwa mtu mmoja?maana yake waliounga mkono walikuwa 220 na waliokataa 37 tu je kura moja ya Cheyo ingebadilisha chochote?Simtetei Cheyo ila najaribu kutafakari kwa kina kama kweli kumfukuza kutaleta impact yeyote.
 
leo hii kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, mhe. hamad rashid mohamed amemuondoa mhe. cheyo kutokuwa tena msemaji wa upinzani katika wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi na hii inafuatia ukigeugeu wa cheyo hadi jana akaenda kinyume na wapinzani wenzake kwa kuunga mkono bajeti ya serikali ya CCM

...kwa wanayemjuwa cheyo wa mwaka 1995 ..hawataon ajabu...daima cheyo amekuwa akila kwa ajili ya usaliti wake....sina uhakika kama anaipenda ccm..laini daima anajulikana kama MPINZANI MASLAHI!!!

KWA WAnaokumbuka 1995 pale kilimanjaro hotel...tanzanikulikuwa na mhahara mmoja maarufu sana....kwenye mhadhara cheyo kwa kulipwa alienda pale kwa lengo noja tu la kumchokaza mrema....wakati mwenzake lipumba akitoa hoja za maana ...cheyo alifanya kazi kubwa ya ku mu undermine mrema.....hakutoa hoja hata moja dhidi ya ccm..matokeo yakawa mrem akataharuki na kushindwa kuendelea na mtiririko aliokuwa ameaandaliwa na mshauri wake prof .mwasega abaregu...akaanguka kwenye mtego wa cheyo..

kwenye ule muhadhara aliyefanya vema kuliko wote alikuwa lipumba....mkapa alisomaa tu kila kitu alichoandaliwa na campagne team yake ...wakati huo mkapa alikuwa hajaiva sana kwa siasa za jukwaani....kila kitu alichokuwa akiongea ilikuwa ni lazima asome.....mrema hakufanya vema...lakini cheyo alitia aibu upinzani....kwani hata baada ya mdahalo lipumba na mrema walisusia chakula kwa kudai kuhujumiwa kwenye mdahalo kwa spika zao kutosika vema ....na hata wakati wakiongea kutkea mawimbi redioni........CHEYO ALIWACHEKESHA WAANDISHI WA HABARI PALE ALIPOWAMBIA KUWA YEYE HAWEZI KUSUSA CHAKULA...NI LAZIMA AENDE AKALE MEZA MOJA NA MKAPA......

KWA WASIOMJUWA Cheyo amekuwa akiishi kwa ujanja ....ni wazi wengi hawajuwi kuwa amepata kupigwa PI Kule swissland........na majuzi nyumba yake imeokolewa kupigwa mnada kimaajabu[so lazima alipe fadhila].....mdogo wake cheyo pia alifaidika na fedha za benki kuu.......

so sioni kwa nini HAMAD hajaangalia historia na kumuonea huruma.....labda hata huo uwaziri kivuli asingempa!!
 
The title is very deceiving. Cheyo "haja fukuzwa kambi ya upinzani" ni kaondolewa kama msemaji kwa mujibu wa habari yenyewe.
 
The title is very deceiving. Cheyo "haja fukuzwa kambi ya upinzani" ni kaondolewa kama msemaji kwa mujibu wa habari yenyewe.

bora mwanafalfasa umerekebisha. sisi wengine hatujui kinachoendelea, tunapokea tu kilichowekwa mezani na kuanza kujadili..
 
is it true?je kwa mujibu wa Katiba ya Upinzani Hamad Rashid ana mamlaka hayo?na je hata kama angekataa kuunga mkono Bajeti ile je inga add any value kwa mtu mmoja?maana yake waliounga mkono walikuwa 220 na waliokataa 37 tu je kura moja ya Cheyo ingebadilisha chochote?Simtetei Cheyo ila najaribu kutafakari kwa kina kama kweli kumfukuza kutaleta impact yeyote.

TUnachoangalia ni Umoja na one Voice regardless kama kura yake inge-add ama kuto ku-add value.
 
is it true?je kwa mujibu wa Katiba ya Upinzani Hamad Rashid ana mamlaka hayo?na je hata kama angekataa kuunga mkono Bajeti ile je inga add any value kwa mtu mmoja?maana yake waliounga mkono walikuwa 220 na waliokataa 37 tu je kura moja ya Cheyo ingebadilisha chochote?Simtetei Cheyo ila najaribu kutafakari kwa kina kama kweli kumfukuza kutaleta impact yeyote.

Naamini alichofanya Hamad hajaingilia uhuru wa mtu kutoa maoni, bali ameangalia grounds za kutolewa maoni na impact yake katika utangamano kwenye 'kambi' ya upinzani. Ana haki na namuunga mkono....
 
is it true?je kwa mujibu wa Katiba ya Upinzani Hamad Rashid ana mamlaka hayo?na je hata kama angekataa kuunga mkono Bajeti ile je inga add any value kwa mtu mmoja?maana yake waliounga mkono walikuwa 220 na waliokataa 37 tu je kura moja ya Cheyo ingebadilisha chochote?Simtetei Cheyo ila najaribu kutafakari kwa kina kama kweli kumfukuza kutaleta impact yeyote.

Gender sensitive, I dont think kuna 'katiba ya upinzani'. I stand to be corrected if I thought wrong....
 
Jamani kwani Cheyo hammujui ni ndumila kuwili anachojali ni biashara zake basi upinzani ni subset kwake hana tofauti kabisa na Mrema siku akishindwa ubunge safari ya kurudi CCM itakuwa imewadia.
 
Hawa ndiyo wale aliowasema Liundi, tusishangae wapo wengi ndani ya upinzani wanatuharibia sana.
 
Hamad kaonyesha mfano mzuri wa kuwajibisha wanaoenda kinyume na wanachopaswa kufanya. Action on the spot, hakuna kurembaremba. Kama hata serikali yetu ingekuwa inawawajibisha viongozi wake wanaokwenda kinyume na maadili ya kazi zao palepale bila kusita au kuoneana aibu, nchi ingekuwa mbali na uoza uliopo ungepungua kama sio kwisha kabisa.
 
maaan kubwa ya kua mpinzani ni ku exploit upungufu kwa serikali ili either ijirekebishe au mwisho wa siku waondoke madarakani ili wapinzani watekeleze pale waliotoka waliposhindwa! sasa kama mpinzani unachukua upande wa ccm unakua maana nzima umeipoteza, kwanza lazima ijulikane hakuna mswada usio na mapungufu hata uwe mzuri vipi, idea ni kwa upinzani kuya point out ili serikali iyarekebishe, unaweza uo muswada overall ni mzuri lakini mapungufu na some concerns lazima upinzani uzi iron out na iyo ndio idea ya kua mpinzani! cheyo has lost that caliber kwa interest zake binafsi, mara nyingi unamuona akicome before kikwete defence hadi unajiuliza, who is cheyo represent!
 
Cheyo loses portfolio for backing budget

Polycarp Machira
16th June 10


The Bariadi East MP, John Cheyo (UDP) was yesterday dropped from the portfolio of shadow minister for Lands, Housing and Human Settlement for supporting the 2010/2011 budget estimates.

His removal was announced by the leader of the opposition camp, Hamad Rashid Mohamed, when he spoke to reporters here yesterday.

But Cheyo who talked to journalists later rubbished the decision, saying: "The opposition leader does not have such powers as this was an individual decision."

It all started on Monday evening when members of parliament were required to vote for or against the 2010/2011 budget estimates tabled by the minister for Finance and Economic Affairs, Mustafa Mkulo.

Speaker of the National Assembly, Samwel Sitta reminded the legislators that it was time for roll call vote as the minister had wound up his speech.

Every member of parliament' was called one by one and they were to respond as per their wish.

Some members of the opposition camp opposed the budget, but when Cheyo's turn came he responded in the affirmative, going against the opposition stand, amid uproarious applause from CCM legislators.

This did not go down well with the opposition camp which had apparently decided to take collectively vote against the budget.

In their earlier meeting which Cheyo also attended, they faulted the government budget terming it ‘cheap politics'.

Addressing a press conference yesterday, Hamad Rashid Mohamed said the opposition reached the decision to relieve the Bariadi MP of his duties as shadow minister, saying this was the second time the legislator had gone against an opposition stand.

Last year, Cheyo also supported the budget though he later apologized for the stand.

"We resolved that John Cheyo should take political responsibility for his action, by being moved out of office. We have decided to relieve him of his duties as shadow minister after he failed to respond appropriately," said Hamad Rashid.

He said the Ziwani MP, Ali Said Salim (CUF) who was until yesterday Cheyo's deputy shadow minister will assume responsibilities in that portfolio.

Hamad explained that according to the Commonwealth parliamentary rules, party caucuses always come up with one voice, adding that even the ruling party always follows suit and supports the budget in one voice.

He cited section 15/2 of the parliamentary standing orders that gives him powers to appoint and fire any shadow minister.

Cheyo who talked to reporters later said he decided to go his way in appreciation of the government acceptance to incorporate his demand to give the Controller Audit General (CAG)'s office some eight billion shillings that were earlier slashed from the estimates.

The Bariadi MP had sought explanation why the government decided to reduce CAG budget estimates, saying this would deprive the chief auditor with the autonomy to improve his work.

"How did they expect me to say ‘NO' when money I wanted returned to the CAG budget was returned? They ought to understand that, this is a difficult time; we must all support the government budget," he said.

He said he has in this parliament requested the government to build bridges in his constituency. Thus he was forced to support the budget as his electorate would ask him: "Where will you get the money to fulfill these election pledges when you disapproved the government budget?"


THE GUARDIAN
Cheyo loses portfolio for backing budget
 
Ingekuwa kwa kiswahili ingekuwa nzuri sana hii!Lakini asubuhi TBC wameonyesha malumbano ya wazi kati ya John Cheyo na Hamad, ambayo kibinafsi yamenichukiza na kunihuzunisha sana!We stop fighting a common anemy and rise against each other in public!..inatisha hii!...Ni msambaratiko wa kambi ya upinzani, ambapo CCM wanachekelea sana!
 
Hakuna Upinzani uliyojibizana on public, cheyo si mpinzani bali ni kipandilizi cha sisiemu - uthititisho ni kauli na mwenendo wake tata.

UDP = CCM tawi.
 
Nadhani hilisomo la kujifunza kukubaliana na kutakubaliana na mambo bado lina fanya upinzani waonekane wao kwa wao ni maadui, sidhani kwa kipindi hichi kuanza kutimuana hadharani kuna jenga upinzani, lazima tufike mahali tukubali kutokukubaliana kwetu kwa njia ya vikao. sija ipenda hii
 
Kwani hata hiyo UDP ni chama cha siasa basi! Hakuna vikao, hakuna uchaguzi, Cheyo lazima awe mwenyekiti, mnamkumbuka Jidulamabambasi? Tendwa wala hasemi kitu kwa UDP!
 
Nadhani tunakosea kidogo kumhukumu Cheyo (Mapesa) kwa uamuzi wake wa kuunga mkono hoja. Ni dhahiri kuwa kila Mbunge ana haki ya kutoa mchango wake kulingana na anavyoona na hakuna sheria au kanuni inayomkataza kufanya hivo.

Tutambue kuwa Upinzani sio kukataa kila kitu kinacholetwa na serikali, bali ni kukosoa kile ambacho hakifai na kuunga mkono kinachofaa na pengine kuipongeza pale inapofanya vizuri.

Hivyo basi, nionavyo mie Cheyo alitumia haki yake kikatiba kama mbunge kutoa maoni yake na sio lazima yafanane na ya Rashid Hamad au anachotaka Rashid Hamad.

Hata wabunge wa CCM huwa wanakataa mambo ambayo hayako sawa, Je tutawaita nao ni wapinzani???. Hivo basi nahitimisha kwa kusema "Upinzani sio kupinga kila kitu kinacholetwa na serikali" Tunahitaji kubadilika kifikira
 
cheyokichwachauma.jpg


Cheyo atemwa uwaziri kivuli Send to a friend
Wednesday, 16 June 2010 09:14
Exuper Kachenje
KAMBI ya upinzani kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano imemvua mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo cheo cha Waziri Kivuli wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi baada ya kupiga kura ya kuunga mkono bajeti ya serikali ya mwaka 2010/11.

Cheyo, ambaye ni mwenyekiti wa UDP, pamoja na Shoka Hamisi Shoka wa CUF waliungana na lundo la wabunge wa CCM kuipigia bajeti hiyo ya Sh11.1 trilioni kura ya kuipitisha licha ya kuwepo mapungufu kadhaa yaliyolalamikiwa na kambi ya upinzani.

Pamoja na kwamba mkutano huu ni wa mwisho kwa Bunge hili, kambi hiyo imeshamteua Ali Said Salim, ambaye ni mbunge wa Ziwani (CUF), kuchukua nafasi ya Cheyo. Awali Salim alikuwa naibu waziri katika wizara hiyo.
Kambi hiyo ya upinzani imesema imeamua kumwondoa Cheyo kwenye wadhifa huo kwa kuwa amesaliti makubaliano ya ya kupinga bajeti ya serikali ambayo ilipitishwa na wabunge 220 juzi jioni.

Katika kura ya wazi iliyopigwa bungeni juzi jioni, Cheyo alipotakiwa kueleza anaikubali au kuipinga, alijibu "ndiyo" na hivyo kuwa mmoja wa wabunge 220 waliopitisha bajeti hiyo, inayolaumiwa kwa kutoweka vyanzo vipya vya mapato huku ikiweka misamaha ya kodi kwa makampuni ya migodi.

Shoka Hamisi Shoka wa jimbo la Micheweni kwa tiketi ya CUF, pia alichukuliwa kuwa ameipitisha bajeti hiyo, jana alikanusha akisema kuwa alijibu "siyo" na hivyo kunukuliwa vibaya.

KiutarCheyo habari kamili soma pembeni
atibu, mbunge hutakiwa kutoa jibu la "ndiyo" anapokubaliana na bajeti hiyo au jibu la "hapana" anapoipinga.

Hata hivyo, Cheyo amepinga uamuzi wa kumvua wadhifa wake akisema kuwa kiongozi huyo wa kambi ya upinzani hana mamlaka hayo.

"Hamad hana uwezo wa kuniondoa... mimi si CUF. Muungano ndio unaniweka pale na si Hamad... tuligawana majukumu... sababu aliyotoa ni ‘nonsense' (haina msingi)".

Alisema amepokea nakala ya barua ya Hamad aliyoiandika kwenda kwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta ikieleza uamuzi huo, lakini akasema anaandaa barua kwenda kwa kiongozi huyo wa Bunge kuelezea suala hilo na kusisitiza kuwa yeye ndiye msemaji wa kambi ya upinzani kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

"Naandika barua kwenda kwa spika kwa kuwa hili limefanyika kinyume," alisema Cheyo.

Lakini kiongozi huyo wa kambi ya upinzani, Hamad Rashid Mohamed (CUF) alisema amefanya mabadiliko kwa mujibu wa sheria ya Bunge.

"Maamuzi ya baraza la mawaziri ni ya kikatiba. Usipokubaliana nayo unajiuzulu, usipojiuzulu unawajibishwa. Cheyo amekwenda kinyume na maamuzi ya kambi ya upinzani hivyo kwa mamlaka niliyonayo kwa kutumia kanuni ya 15(2) ya Bunge, nimemwondoa Cheyo katika nafasi yake ya Waziri Kivuli wa Ardhi," alisema Hamad.

Hamad, ambaye alikuwa pamoja na na naibu kiongozi wa kambi hiyo Dk Willibrod Slaa na Shoka Hamis Juma wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari, alisema hatua ya kumuondoa Cheyo inaonyesha jinsi walivyo makini katika kutekeleza makubaliano wanayojiwekea kwenye utendaji wao.

Cheyo alionekana kufahamu mapema uamuzi wa kumuondoa na alidhihirisha hilo hata kabla ya kutangazwa kuvuliwa madaraka wakati alipodokeza suala hilo aliposimama kuchangia muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2010/2011 iliyowasilishwa bungeni jana.

Alisema: "Najua naweza kuondolewa kwenye kambi ya upinzani, lakini nataka kusema, tujifunze kuweka mbele maslahi ya taifa. Hii ni ‘vote' (hoja) yangu, haiwezekani nipiganie kurejeshwa kwa Sh8bilioni za CAG, zirudi nami nipinge bajeti."
Naibu spika wa bunge Anne Makinda

alimwambia Cheyo kuwa "watu walichukia sana jana".
Lakini Cheyo alijibu: "Shauri yao, najua naweza kuondolewa kambi ya upinzani."

Baadaye mbele ya waandishi wa habari, Cheyo alisema suala la yeye kupiga kura ya kupitisha bajeti hiyo ni la mtu binafsi na siyo la kambi ya upinzani.

Alikejeli kuwa waliopiga kura ya kuikataa, hawakufanya kitu kilichotoka moyoni na kwamba haitashangaza kuona walioipinga ndio wakiwa wa kwanza kwenda kudai mafao ya ubunge.

"Ukiondoa UDP hakuna kambi ya upinzani; "no yao" (hapana) yao haitoki moyoni bali ndiyo yangu. Na wao ingawa walipinga, watakuwa wa kwanza kwenda kudai mafao yao ya kustaafu ubunge," alisema Cheyo.

Naibu kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, Dk Willibrod Slaa alieleza kushangazwa kwake na hatua ya Cheyo kulalamika bungeni hatua ya kuvuliwa wadhifa huo.

"Tangu nikue na kupata akili, ni mara ya kwanza kuona, waziri (Cheyo) akiondolewa, anaenda kulalamika bungeni," alisema Dk Slaa.
 
Back
Top Bottom