Cheyo aisulubu CHADEMA

Habarindiyohiyo

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
263
13
Mwenyekiti wa UDP John Cheyo ameisulubu CHADEMA kwa kusema kwamba falsafa yake ya Nguvu ya Umma haina maana yoyote kwa watanzania. Cheyo amesema CHADEMA watambue kuwa Kikwete ndiye Rais halali. Cheyo ameyasema hayo katika mkutano mkuu wa chama hicho unaondelea hivi sasa katika ukumbi wa Sabasaba.

Mkutano huo umemchagua kuwa mwenyekiti wa chama hicho akiwa ni mgombea pekee na kupokea majina ya wajumbe wa kamati kuu aliowateua kuendelea na nyadhifa zao. Wajumbe wa mkutano huo walitoka maeneo mbalimbali ya Dar es salaam, ambapo Cheyo amewashukuru kwa kufika kumsikiliza.

Cheyo ametumia mkutano huo kuwalaumu CHADEMA kwa kuingilia ngome zake za kisiasa katika mikoa ya kanda ya ziwa na kutaka chama hicho kichukuliwe hatua kwa kuvuruga amani ya nchi na kumpongeza Rais Kikwete kwa kubaini hila ya CHADEMA.

.........ndiyohiyo
 
lyatonga+lipumba+cheyo = magalasa.

hakuna haja ya kuyajadili haya magalasa yaliyofulia na kubaki kujipendekeza.

awaambie wanyantuzu hizo pumba
 
Kwamba kikwete ndiye rais pekee halali,kwani kuna mtu aliyesema wapo na wengine halali?uyo cheyo yuko sure na anayosema? Kanda ya ziwa anaijua au anaisikia? Ka bariadi tu ndo anaongelea kanda ya ziwa yote?
 
Kweli sasa tunahitaji damu changa. Wazee wamechoka kufikiri! Matatatizo ya nchi yako wazi wazi lakini hawayaoni?!
 
Huyo nae na hio NGO yake....haya sawa amesema so what???
 
Its OK JK ni rais, hakuna mwenye shida na hilo!
Je ametaja kuwa cdm wanavuruga vipi hiyo amani?
Na je ameongelea makali ya maisha yaliyopo, na kutoa suggestions za kuyapunguza?

Kweli nguvu ya umma ni tishio kwa wengi!
 
UDP chama cha familia?ukitembelea ofisi zake pale mwananyamala kituo cha garage ni aibu kudhania hiki chama kina lengo la kushika dola.
 
Hakuna mapendekezo yoyote anayoweza kutoa coz anajali tumbo lake tu,na yote anayoyafanya sasa ni harakati za kuganga njaa tu
 
UDP chama cha familia?ukitembelea ofisi zake pale mwananyamala kituo cha garage ni aibu kudhania hiki chama kina lengo la kushika dola.
 
UDP chama cha familia?ukitembelea ofisi zake pale mwananyamala kituo cha garage ni aibu kudhania hiki chama kina lengo la kushika dola.
 
Habarindiyohiyo
Join Date : 11th August 2008
Posts : 221
Thanks 0
Thanked 35 Times in 13 Posts
Rep Power : 23
Mkuu uliisahau Avator yako nini, maana naona ni mkongwe lakini ndiyo hivyo! Tuachane na hayo, Cheyo ikitokea Mungu akamuchukua leo basi ndiyon basi tena UDP nayo imekufa! Ni kama chama cha kitapeli ambacho ofisi ipo kwenye briefcase!
Anachojaribu Cheyo saizi ni kutapatapa kutokana na wananchi kuwaona si wapinzani bali wachumia tumbo zaidi.

Vyama vingine hadi aibu akitoka hapo anakwenda Bariadi then anangojea uchaguzi 2015.
 
Sijui kama watanzania wanajua Cheyo ni kiongozi wala ana chama chake peke yake. Huu utumiaji wa siasa kuwaumiza watanzania kwa kufanya miradi ndio kinachomsukuma cheyo kuingia kwenye siasi. Sidhani kama kuna haja ya Chadema kumjibu Cheyo na Lipumba, majibu wanayo wao wenyewe na wanajua Chadema na wananchi wakiingia serikalini hakuna deals tena na biashara wanazotaka wao.

Cheyo iendelea kujiabisha na tunakuingiza kwenye kundi la wasomi wanaowaibisha Taifa​
 
Mwacheni aongee kwani anamdomo kwaiyo ni haki ake kuongea hata kama atasema maneno asiyoeleweka.
Watu kama huyu ni nguo iliyochakaa, hata kama inarangi nuri ndo basi tena.
 
Duh!! wanapeana moyo wao watupu!! hii kali. Mapenzi mabaya, mapenzi mabaya!
 
Kweli Chadema inatisha,kila chama kinaongelea Cdm,yaani kaita viongozi wake,kaacha kuongea jins ya kuimarisha udp,anaongelea cdm,KAZI WANAYO!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom