Cheti cha degree kikichanika, kikiibiwa, unafanyafanyaje?

Ubungoubungo

JF-Expert Member
Jul 28, 2008
2,502
739
Wakubwa, hivi certificate ikichanika , mtu anaweza kufanya nini ili apate mpya? je, anaweza kupeleka ile iliyochanika akapata nyingine, na je chukulia mfano umeibiwa begi lenye vyeti vyote, au nyumba imeungua, ndo degree yako imeondoka hivihivi au vipi, kuna uwezekano kupata kipya? how...

nimeulizwa swali hili na mtu nikashindwa kumjibu kwa uhakika. naomba wenye uelewa mzuri na hili waeleze hapa kwa faida ya wengi. asante.
 
Huyo aliyekuuliza kwanza angewasilina na chuo alichosoma. Kwa UDSM original transcript huwa haitolewi, unapewa certified copies of the original. Kwa degree certificate/ leaving certificate unatakiwa pia kutoa copies na ku-certify. Sasa mambo hayo yakitokea sijui inakuwaje? Mwambie aende huko alikomaliza watampa majibu sahihi. Hiki cheti ni chake kweli, kwa nini asiende huko alikomaliza? Nionavyo mimi sio mwisho wa degree - kwani degree yake ipo kichwani kwake!
 
amesoma udsm. I don't understand unaposema udsm original transcript huwa haitolewi, ulitaka kusema original certificate au transcript ile inayoelezea somo moja baada ya lingine uliyosoma miaka yote....kwasababu certificate udsm huwa hawaorodheshi masomo uliyosoma.
 
kwanza kitu kama hicho kinapochanika, kuibiwa au kupotea unatakiwa kwanza ukatoe taarifa polisi (kama ukipoteza passport yako au resident permit kama ni mgeni wa nchi)

baadae ndo unakwenda ofsi husika (kwa mfano wako ni chuo ulichomaliza) pamoja na karatasi yako ya polisi.

baadae wakihakikisha kuwa kimeibiwa au kupotea kweli wanakupatia chengine
 
Back
Top Bottom