Cheo ni dhamana - Viongozi lindeni heshima ya future yenu

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,884
6,885
Cheo ni dhamani, sitakitumia cheo changu au cha mtu mwingine kwa faida ya....
Kuwa kiongozi ni dhamani kubwa aliyopewa kiongozi toka kwa raia waliomdhamini kuwaongoza. Ni wajibu wa kiongozi kulinda heshima hiyo kwa manufaa ya waliomchagua na kulinda heshima yake na future yake.

Hali kwa sasa nchini inatisha na kuleta wasiwasi, si kwa Tanzania tu, ila nchi nyingi barani Afrika. Tangu nchi za kiafrika zipate uhuru viongozi wake hawaendani na wakati ambapo raia wanazidi kukomaa kidemokrasia na elimu ya maisha na ya kiraia kuzidi kushika kasi. Kasi ya uelewa wa raia inawapa taabu viongozi kwa vile wangali na ndoto za mfumo wa uongozi wa miaka 50 iliyopita nchi zilipopata uhuru.

Kizazi cha walichokulia viongozi wa leo (informal education) ni kile ambacho mtoto huwezi kumwuliza kitu au kumdadisi baba kitu vinginevyo utaonekana huna adabu na kuchapwa bakora. Kizazi cha leo kimekulia zaidi katika mfumo wa formal education, mfumo ambao ni wa utandawazi unaofanya vijana wa leo waonekane kuwa wenye fikra pevu na wazi na wa kweli, na hawataki mfumo wa kuendesha mambo kwa siri.

Tatizo hapa ni dhana ya viongozi wetu licha ya kuona ishara za nyakati na uelewa mkubwa wa wananchi katika masuala ya haki zao na wajibu wa viongozi kwa raia bado viongozi wamekuwa wazito wa kuwa wawazi na hoja za msingi zinapoibuliwa na wananchi viongozi wanabuni mbinu ya ububu katika masuala wanayowajibika kutolea ufafanuzi au kuridhia haki za wananchi. Kwa ububu wa viongozi haishangazi kuona kauli kinzania ndani ya viongozi wenyewe kwa vile ukimya hufumba mengi ambayo angepaswa kuyatolea ufafanuzi hadharani.

Uongozi una hatima yake, na jinsi unavyoongoza wananchi na kulinda vema jina na heshima yako kwa wananchi waliowachagueni ndivyo viongozi wanavyojenga vema future ya hatima ya maisha yao katika jamii. Adhabu ya uongozi mbaya, au ujanja ujanja wa kujitwalia haki za msingi katika demokrasi inaweza viongozi kuwageukia kitanzi chao. Tumeshashuhudia viongozi wengi waliohujumu demokrasi na hatima yao inavyokuwa. Kama si kiboko cha Mungu basi kuna mengi ambayo yatakukosesha raha.

Sifikirii kiongozi baada ya kuwatumikia vema raia wake aishie kupata adhabu toka kwa Mungu ya kuwa kipofu. Na pengine haipendezi badala ya kufurahia raha ya kupumzika baada ya kustaafu unaishia kuwa kiwete au kiziwi, yote hayo ni adhabu zinazoanzia hapa hapa duniani kwa wanaochezea haki za wananchi. Kuna mengi lakini tukumbuke haki za raia zikipotoshwa ni kitanzi cha viongozi, na hata kutoishi kwa amani katika maisha yao baada ya kustaafu maana amani imekosekana ndani ya mioyo yao na dhamira zitawasuta daima.
 
Nchi hii imeingiwa na ugonjwa mbaya sana wa mmong'onyoko wa misingi ya utawala bora,
umoja na mshikamano wa kitaifa; maadili na utu wema, jambo linalowatumbukiza walio wengi
katika umasikini.


Huko nyuma tulizoea kuambiwa kuwa cheo ni dhamana na kwamba uongozi ni utumishi,
lakini siku hizi kupata cheo ni kuula! Neno 'kuula' limeanza kama lugha ya mtaani ambayo ina
tafsiri pana kidogo. Moja ya tafsiri ni 'mambo kuwa mazuri (kunyooka)'.


Miaka ya hivi karibuni wazo la cheo ni dhamana limepotelea mbali na kusahauliwa kama
lilivyosahauliwa Azimio la Arusha. Tunawezaje kupata viongozi wazuri kama kila mmoja
anafikiri nafasi aliyonayo ni haki yake, ni mali yake, na ni stahili yake?

Zama hizi mtu anaruhusiwa kuwa na kampuni na akajipa tenda ya kutoa huduma ofisini kwake,
zama ambazo kufikishwa mahakamani kwa ubadhirifu inategemea umekwapua kiasi gani, kama
ni kikubwa, dola yenyewe inatamka kuwa hukamatiki!

Ni zama ambazo ukiwa mtumishi wa umma mwenye cheo kikubwa unaweza kusomesha mwanao

nchi yoyote uitakayo bila mawazo ya karo, si hivyo tu kutibiwa nje si kwa magonjwa ya moyo tu
bali hata mafua, muhimu cheo kizuri cha kuhudumia umma.
 
Huo usemi uliishia kwa Hayati Nyerere,hauko tena,na sa hivi cheo si dhamana tena.

KWELI KABISA MKULU

DHANA ZA Cheo ni dhamana iliondoka na JK Nyerere wa Ukweli......ikazikwa kule Zenj walipokuja na AZIMIO LA ZANZIBAR.....na DHANA MPYA IKAWA CHEO NI DILI (UTAJIRI).....NA NDIYO MAANA TANGU WAKATI HUO MTU AKIWA NA CHEO KATIKA NGAZI YEYOTE NCHINI LAZIMA AWE TAJIRI....
 
cheo sasa ni utajiri! hasa ukiwa mtumishi wa umma na una cheo kikubwa "umeula" sio kama zamani, marehemu Mwalimu ni kama aliondoka na Maadili ya utumishi wa umma kwani fisadi ndio anatetemekewa na serikali na hata viongozi wa juu kabisa wenye dola wanasema hakamatiki! usipoiba nchi hii unachekwa unaonekana *****..na jamii nayo imebadilika ukiiba unasifiwa, mfano jamaa baada ya mradi kaporomosha bonge ya jumba na gari mbili kali..utasikia wananchi wakisema jamaa mjanja! hata kama huo mradi ukidumu kwa miaka 2 hakuna anayejali..
 
Toka enzi ya Mwinyi na Azimio la Zanzibar ambalo liliondoa miiko na maadili ya viongozi, ili kuacha miaya ya conflict of interest ktk uongozi kuwa sii makosa tena ktk nguzo za uongozi bora.
 
Misemo katika jamii huashiria fikra za jamii hiyo. Kwa kutumia na kukubali neno la 'kaula', jamii imehalalisha kitendo cha ubadhirifu na kuwajibika kazini ili mradi tu yule aliyepewa jukumu lile afaidike kwa njia yeyote ile.
 
Nchi hii imeingiwa na ugonjwa mbaya sana wa mmong'onyoko wa misingi ya utawala bora,
umoja na mshikamano wa kitaifa; maadili na utu wema, jambo linalowatumbukiza walio wengi
katika umasikini.
.
Mimi nadhani hata kwenye masomo ya menejiment topic ya decision making process imefutwa, ndiyo maana maamuzi hakuna. bila maamuzi sahihi hata neno CHEO NI DHAMANA haina nafasi tena
 
mwalimu alipokufa amekwenda navyo vyote, yale mafundisho yake watu hawayafuati tena.
 
Hakuna ubishi kuwa sasa taifa limefika na linapita katika kipindi kigumu sana kutokana na mambo mengi ya utendaji ndani ya serikali kuwa yanafanyika kinyume na maadili.

Kila mtu kuanzia viongozi wa ngazi za juu hadi yule mwananchi wa kawaida akiwa analalamika jambo ambalo linaashiria kuwepo kukata tamaa na hivyo kumfanya kila mmoja kulia kivyake.

Mgomo wa madaktari ambao umeleta maafa makubwa kwa wananchi wanyonge, umeendelea kutikisa nchi, huku wahusika wakuu na watu wa kada nyingine wakigawanyika, wengine wakiunga mkono na wengine wakipinga.

Watu wanayo haki ya kuulaumu uongozi wa nchi, kwa kuangalia baadhi ya mambo kijuujuu na kuacha kuangalia mizizi ya suala lenyewe ili kuyapatia ufumbuzi matatizo ya wnanchi.

Kwa walio wengi taswira inayojionesha hapa ni kwamba tumeacha kuwa na utu, badala yake tunafanya mambo yanayotufurahisha wenyewe na kuona kuwa tumeridhika na kusahahu kuwa sehemu kubwa ya jamii inaendelea kuumia.

Watu wanakwenda makanisa na misikitini kwa wingi kila siku, lakini ni hao hao tunaoiba, kudhulumu na kuwatendea vibaya wenzetu.

Nenda katika uongozi wowote uwe wa serikali ya mtaa ama kijiji, aliyepewa nafasi ya uongozi hawezi kutoa huduma bila kutaka kwa lazima ama kwa kukuzungusha hadi utoe chochote.

Nenda katika zahanati zetu ambako hata kama kuna dawa zimeletwa kwa ajili ya wagonjwa, ni wahudumu hao hao watazikwapua na kumuuzia mmiliki wa duka la dawa ili naye awauzie wagonjwa. Unalipia kuanzia kumwona daktari hadi kitanda. Mama anayetaka kujifungua anaagizwa kununua hata wembe.

Nenda ofisi za serikali ambako kuna watu wameajiriwa na wanalipwa, kama huna ndugu, lazima utoe kitu ndio upate huduma. Hali ni hiyo hiyo hadi ngazi ya juu serikalini. Kila mmoja ni mwongo, ni fisadi katika eneo lake.

Mtu mwaminifu anachukiwa sana na kupigwa vita hata na wakubwa wake. Ataitwa mnoko na matusi ya kila aina. Utashangaa hata ndugu zake watamwita ----- kwa sababu kwa miaka yote aliyofanya kazi hana chochote wakati vijana walioanza kazi miaka miwili wana nyumba na magari.

Uaminifu, kujali mali ya uuma, kuthamini na kulinda heshima ya kazi kwa wengi ni ujinga. Utaona mtu mzima, anashiriki kuiba mtihani ili mtoto wake afaulu! Mzazi wa aina hii, ana tofauti gani na fisadi? Mtu mzima na akili zake, anafanya kampeni hadi anahonga fedha ili achaguiliwe kuwa kiongozi katika kanisa ama msikiti..

Mwingine anajifanya kusali sana kumbe lengo lake ni kupata mwanya wa kuiba sadaka au kuiba fedha za miradi ya ujenzi wa makanisa na misikiti. Katika hali hiyo kumekuwepo wizi mtindo mmoja hata aibu hakuna.

Cheo ni dhamana yamekuwa ni maneno yaliyopitwa na wakati. Kila mtu ni mimi kwanza! na sio Tanzania kwanza, kwa maana ya kila mtu kujali na kuheshimu haki ya mwingine.

Hakuna dawa mbadala itakayotuokoa na majanga haya, kama kila mmoja anatakiwa kufanya maamuzi ili kurudi na kuishi kulingana na maadili ya utu, heshima na kutanguliza maslahi ya nchi kwanza!

Ubabaishaji, ujanja ujanja wa kimaadili hautaliokoa taifa hili. Kila mmoja aone anahusika kwa namna moja ama nyingine na kuirudisha heshima na hadhi ya Tanzania.

Hali hiyo itawezekana kwa kurejea kwenye kauli hii, Cheo ni dhamana sitakitumia cheo changu kwa faida yangu bali kwa manufaa ya wote.
 
Unapopewa madaraka, tenda Haki, usilewe madaraka, usijivune, iko siku utaondoka madarakani au utaondolewa.

Sasa kama ulilewa madaraka, ukajisahau kwamba iko siku utaondoka, ukafanya ujinga kibao, ndo pale unapoona sasa hivi hivi unaondoka. Kila mbinu unayofanya kupambana ubakie ni kama nyani kwenye miti itelezayo. Hivi hivi unarudi uraiani, wale wote uliowafinya, kuwatisha, kuwanyanyasa.. waoooo Karibu ukutane nao sasa. WANAKUNGOJA..WAKO WENGI SANA AISEE..NJOO UWAFACE MWENYEWE..

Na haya mabaya unayozidi kuyafanya ndo unajiharibia zaidi. Wenzako wakifikia UKINGONI hutengeneza mahusiano mema na jamii wanayokwenda kuishi nayo, wewe hadi Leo bado unazidisha ubaya juu ya ubaya. Mabaya hayataisha Kwako aisee.

Hao wenzako wanao kufundisha mabaya wakati wao ulisha kwisha. Watakufundisha ubaya..watakutosa..

Sms SEND...
 
Watu wa zamani sijui walifikiri nini ,utakuta mtu wakati wa kuomba kura anapiga magoti anakuwa mpole kabisa kimbembe anapokipata kile cheo basi hapo ndipo balaa uanza,kauli ubadilika utasikia Mimi ndiye amiri mkuu wa jeshi yeyote atakayeleta fyokofyoko atanitambua sasa ndugu yangu wewe ulipigiwa kura na jeshi hau sisi mbona umetubadilikia
 
Kinachotokea ni kama kibaka /mwizi sugu mtaani ashinde milioni 10 za Biko/Tatu Mzuka kisha katika mahojiano aulizwe atazifanyia nini zile pesa atoe majibu kwamba "Atapanua shughuli zake" sasa kwakua mtaani mnamjua kwamba ni mwizi kifuatacho Itv? ni kuhama mtaaa...tafakari!
 
Kamwe usikitumie cheo chako kuwaonea walio chini yako

Kamwe usitumie cheo chako kuwaumiza walio chini yako

kamwe usitumie cheo chako kuwaharibia wezako kazi

Tutumie vyeo vyetu vizuri, tusiwaumize wengine, tusiwe na roho za kinyama/kishetani, maana kuna baadhi ya viongozi walio pewa madaraka ni hatari kuliko hata wanyama.

Kazi iendelee

tuendelee kujenga nchi yetu kwa nguvu zetu zote na maarifa yetu yote
Pongezi kwa wateuli wote haswa Mama Tax kwa kuaminiwa ktk wizara nyeti kabisa.
Mama Tax ni Mfano mzuri sana wa kuigwa na viongozi/mawaziri wengine, ni kiongozi ambaye unaweza muweka ktk nafasi yoyote na akafiti.
 
60% hawana uwezo katika nafasi zao prof ASSAD

Sababu hiyo ili tuendelee kuishi ofisini inabidi tufanye uliyotaja hapo juu.
Sio kweli.
ukifanya hivyo ni ujinga.
tumia taaluma yako vizuri, kama huwezi acha au utumbuliwe.
 
Back
Top Bottom