Chenge kujivua gamba leo?

Status
Not open for further replies.
Mliokuwa sambamba huko magamba wanakogawana fito turushieni mengineyo kama yapo. Kazi kweli kweli!

Naona wamekuwa kimya, huenda kutokana na wajumbe kutokea mlango wa nyuma. labda bado wanakimbizana nao. Basi mkisettle kidogo tupeni na sisi tulio mbali ili tupate updates hizo.

kuna watu hawatakiwi kuleta tetesi JF lakini wanajishusha hadi kiwango cha "tetesi"

Kulikuwa na sababu gani kuweka huu uzi kivyake? Naona contents hazitofautiani na mada kuu. We makwato (paw) muvuzisha hii kitu bana.

kikao hakijaisha wacha kupotosha. Imebaki agenda ya Igunga. Malecela kashauri watu waliobaki wafukuzwe leo, lakini hakuna aliyeunga mkono wala kukataa. wameipotezea tu.

- According to the datas, Chenge ameachia ngazi rasmi leo ndani ya CC inayoendelea sasa hivi Dodoma!
Willie @ NYC, USA.

Je kwa vipi Chenge ameweza kuachia ngazi rasmi ndani ya CC ? Unataka kutuambia kuwa mkono wa binadamu umeweza kudondoka kama alivyokuwa akitamani fisi ? Kama kuna ubavu kwa nini isisemwe CC yamtimua Chenge ? Kuna datas zingine zimepinda kweli kweli !

kikao hakijaisha wacha kupotosha. Imebaki agenda ya Igunga. Malecela kashauri watu waliobaki wafukuzwe leo, lakini hakuna aliyeunga mkono wala kukataa. wameipotezea tu.

we unaongea upo Mtwara

Chama la magamba linanuka,baada ya kuvuana magamba.ss naona yameoza.WE HATE U CCM.MAY U REST IN HELL FOREVER

we unaongea upo Mtwara
Acheni kudanganya watu,, nilichosema nina uhakika asilimia mia. Kikao kinaendelea na sasa wanajadili agenda ya Igunga. Hoja ya Malecela ya kuwafukuza waliobaki hakuna aliyesema chochote kuunga ama kupinga. Kikao kiinaendelea na mimi nipo hapa, acha kupotosha wattu, acha kutafuta sifa za kijinga kwa kudanganya watu, ni mjinga tu anaweza kuamini eti wametokea mlango wa nyuma! This guy is not here at all.. anataka sifa tu

- According to the datas, Chenge ameachia ngazi rasmi leo ndani ya CC inayoendelea sasa hivi Dodoma!

Willie @ NYC, USA.
Ha ha ha haaaa mtu wa NYC leo data zimepinda Tetesi na Rasmi wapi na wapi,
MODS hebu ziunganisheni hizi thread kumfichia aibu Malecela.

Acheni kudanganya watu,, nilichosema nina uhakika asilimia mia. Kikao kinaendelea na sasa wanajadili agenda ya Igunga. Hoja ya Malecela ya kuwafukuza waliobaki hakuna aliyesema chochote kuunga ama kupinga. Kikao kiinaendelea na mimi nipo hapa, acha kupotosha wattu

Unachojua ni kumfagilia Masha tu wewe. Sasa kama upo mkutanoni mbona unashindwa kusema kama EL na AC wameshatimuliwa?

Unachojua ni kumfagilia Masha tu wewe. Sasa kama upo mkutanoni mbona unashindwa kusema kama EL na AC wameshatimuliwa?
Usitoke nje ya topic hapa. Hatumuongelei Masha hapa,, unawadanganya watu kujifanya eti una data kumbe you are just a bit of a bore,, tunaongelea CC ya CCM, kikao hakijakwisha hapa na agenda iliyopo ni ya Igunga,, January ame present paper yake safi kuhusu hali ya kisiasa. Hoja ya Malecela ya kufukuza waliobaki, haijapingwa wala kuungwa mkono hapa. Waungwana wa JF kama naongopa mtaona ukweli kwenye media,, na kuanzia hapo please note jina la huyu PHILANDERER kwamba ni MUONGO na anatafuta umaarufu tu hapa. Mark my words........kikao kinaendelea

KAMATI Kuu ya CCM, (CC) jana ilikutana mjini Dodoma huku mpango mkakati wa kujivua gamba na uchaguzi mdogo katika jimbo la Igunga mkoani Tabora, zikiwa ni agenda moto katika kikao hicho kilichoketi chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete.Mkutano huo wa CC umefanyika kipindi ambacho chama hicho tawala, kimepigwa na mawimbi mazito ya kisiasa kutokana na mpango huo wa kujivua gamba, ambao unaungwa mkono na baadhi ya makada wa chama hicho huku wengine wakipinga jinsi unavyotekelezwa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vya ndani, kikao cha jana ambacho kilitanguliwa na Kamati ya Maadili iliyokutana juzi, pamoja na ajenda nyingine kilijikita zaidi katika mpango mkakati huo wa kujivua gamba.

Hata hivyo hadi jana jioni Katibu wa Itikadi na Uenezi mwenye dhamana ya kueleza umma ajenda sahihi zilizojadiliwa alikwepa jukumu hilo huku akidai kutofahamu chochote ambapo alirudia kauli aliyoitoa juzi kwamba, "ajenda hazijapangwa."

Lakini kauli hiyo ya Nape ambayo haikuwa na nguvu za kimantiki kwa kuwa kikao kilishaanza na kisingeweza kuendelea bila ajenda kuwapo.

Kadhalika kauli hiyo ya Nape ilitofautiana na vyanzo vingine ndani ya kikao hicho ambavyo vilifafanua zaidi kwamba katika sehemu ya kwanza ya kikao hicho “kuliibuka mvutano mkali” kuhusu utekelezaji wa mpango huo wa kujivua gamba ambao wapo waliotaka utejelezwe lakini wengine wakipinga.

Mwananchi ilidokezwa zaidi kwamba, kundi linalopinga linaona utekelezaji wa mpango huo ni sehemu ya kuendeleza mpasuko ndani ya chama kwani wanaotakiwa kuchukuliwa hatua nao wana wafuasi wao.

Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa hizo, wajumbe waliounga mkono utekelezaji wa mpango huo walijenga hoja kwamba ni hatua muhimu kwa chama kujisafisha ili kiweze kusonga mbele kwani hatua ya kurudi nyuma ingeweza kuwa na athari kubwa zaidi.

Chanzo hicho kilifafanua zaidi kwamba, hadi jana majira ya saa 10:00 jioni wakati wajumbe walipokwenda mapumziko, haikuwa imepatikana suluhu ya makubaliano ya pamoja kuhusu kujivua gamba ili yaweze kuwasilishwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (Nec).

Nec ya CCM iliyoketi mwezi Apirili ndiyo ilitoa azimio la kuwataka watuhumiwa wote wa ufisadi ikiwemo Rada, wizi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT) wenye uhusiano na Kampuni ya Kagoda Agriculture na Richmond, wajiuzulu nyadhifa zao kabla ya utekelezaji wa mpango huo wa kujivua gamba.

Tayari aliyekuwa mbunge wa Igunga Rostam Aziz, alikwishafanya uamuzi wa kuachia nafasi zake zote na kwenda mbali zaidi hadi ubunge lakini mwenyewe, akipinga kwamba uamuzi huo ni sehemu ya kujivua gamba.

Mbali ya ajenda ya gamba, ajenda nyingine ilikuwa ni namna ya kuweka mikakati ya kushinda uchaguzi mdogo katika jimbo la Igunga liliachwa wazi na Rostam, ambalo linatarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na wapinzani nao kujipanga kulitwaa.

Ajenda ya tatu kwa mujibu wa chanzo hicho, ni bajeti ya chama kwa mwaka
huo wa 2011/12 kama ilivyo bajeti kuu ya serikali kwa ajili ya makadirio ya mapato na matumizi.

Kikao hicho kilianza mnamo takriban saa 6 mchana na kwenda hadi muda huo wa jioni na kuatarajiwa kwenda hadi usiku kutegemea mjadala wa ajenda ambavyo ungekwenda.

Hadi ilipofika mchana, Nape aliwaambia waandishi, “Kwa sasa sina cha kuwapa kwa kuwa kikao bado kinaendelea na hata kama mngenitaka niseme nini kilichozungumzwa siwezi kuwaambia,’’alisema Nape na kuongeza:

“Lakini naomba muamini kuwa kikao hiki ni lazima kiishe leo kwa muda wowote na katika kipindi hicho nitatoa taarifa kwenu kwa kuwa nimewaambia wajumbe wangu wawe wanaandaa taarifa hiyo hatua kwa hatua hivyo msitoke hapa kwa kuwa zege halilali."
Katika mkutano wa jana, Katibu Mkuu wa CCM Willson Mukama alisema kuwa wajumbe 33 walikuwa wamehudhuria katika kikao hicho idadi ambayo inakipa uhalali kikao hicho kufanyika.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa taarifa kuwa wajumbe waliotakiwa kuhudhuria humu ndani ni wajumbe 39, lakini hadi sasa jumla ya wajumbe 33 wamekwisha hudhuria na hivyo kikao hiki ni halali,’’alisema Mukama akimkaribisha Mwenyekiti kufungua Mkutano.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi na Mukama kwa Vyombo vya habari, kikao hicho pamoja na mambo mengine kilitarajia kupokea taarifa ya utekelezaji wa maamuzi mbalimbali ya Halmashauri Kuu ya April mwaka huu.

Miongoni mwa wajumbe waliohudhuria jana ni pamoja na Mzee Alli Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Zanzibar Aman Abeid Karume, Rais wa sasa wa Zanzibar Dk Ally Mohamed Shein, Makamu wa Rais Dk Mohamed Ghalib Bilali pamoja na viongozi waandamizi ndani ya chama hicho, akiwemo Makamu mwenyekiti Pius Msekwa.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa hakuwemo kwenye chumba cha mkutano wakati wa ufunguzi na hata mchana hakuonekana katika eneo la makao makuu ya CCM Dodoma hali inayoashiria kwamba hakuhudhuria mkutano huo.Hata hivyo hakuna taarifa yoyote rasmi ambayo ilitolewa kuhusu kutokuwepo kwa mtangulizi huyo wa Rais Kikwete.

Source: Mwananchi

Ok, sasa kikao kimekwisha rasmi na wajumbe wanatoka .......Mwigulu Nchemba ndiye aliyepewa mikoba kuongoza kampeni Igunga.. EL, na Chenge watajadiliwa NEC ijayo. yuko wapi huyu PHILA.......?? Shame on you!! kwa kuwapotosha watu hapa. Wee umejisajili jana,, elewa JF watu wako makini,,,, siku nyingine ujipange kuleta mada hapa chundu mkubwa weee

Ok, sasa kikao kimekwisha rasmi na wajumbe wanatoka .......Mwigulu Nchemba ndiye aliyepewa mikoba kuongoza kampeni Igunga.. EL, na Chenge watajadiliwa NEC ijayo. yuko wapi huyu PHILA.......?? Shame on you!! kwa kuwapotosha watu hapa. Wee umejisajili jana,, elewa JF watu wako makini,,,, siku nyingine ujipange kuleta mada hapa chundu mkubwa weee

Kikao kingine cha NEC lini? Baada ya miezi mitatu tena? Slogan ya kikao cha jana soma maandishi kwenye picha.

07_11_shsfqg.jpg

CCM Secretary General Wilson Mukama reads out procedures to be followed by delegates during the Central Committee' s (CC) meeting in Dodoma on Sunday. On his right is the party's Chairman, President Jakaya Kikwete, Vice-Chairman (Isles), Dr Amani Abeid Karume and Zanzibar President, Dr Ali Mohamed Shein. (Photo by Ramadhan Othman)

Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom