Wasegesege
Senior Member
- Oct 22, 2009
- 107
- 10
Hebu jamani watu ambao ni wataalamu wa Sheria wanisaidie hapa. Mhe. Chenge ameonekana ana hatia na kahukumiwa kifungo cha Miaka mitatu (3) au kulipa faini ya Tshs laki saba [700,000/-] kwa TAFSIRI YANGU ANAITUMIKIA MIAKA 3 KWA KULIPA FAINI YA TSHS 700,000
Sasa hoja yangu:
kwa mujibu wa Ibara ya 67.-(2) (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyorekebishwa mwaka 2005 kinasema nanukuu:
"(2) Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge-
(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu;"
mwisho wa nukuu.
Sasa Mhe. Chenge amehukumiwa kifungo cha Miaka 3 na badala yake amelipa faini, yaani Hakimu kasema unakwenda Miaka 3 jela ama ulipe faini, kwa maana hiyo iwapo angekosa kuwa na fedha Tshs, 700,000 angekwenda gerezani kutumikia adhabu ya miaka 3.
Sasa wanasheria na wataalamu wa Katiba hapa mnasemaje Chenge bado ni Mbunge halali wa Bariadi? au siyo Mbunge halali?
Hebu tusaidieni hapo.