Chenge huru!

Huu ndio utawala wa sheria. Tunamwomba mwendesha mashitaka akate rufaa. Halafu wana Familia wafungue kesi ya madai. Nadhani wadai compensation ya USD million 2 kwa kila marehemu. Halafu dereva wa bajaji ajitokeze naye adai kama USD laki saba hivi.

Kidogoo mjomba wangu ndio ataona ubaya wa alichokifanya.
 
That only happens in Tanzania...and he still keeps his driving licence?Yaani kwa kupatikana na hatia ya makosa yote hayo hakupaswa kuachwa aendeshe kwa muda fulani...leseni ingeweza kufungwa kwa wakati fulani...au kuwekea restrictions.

Mimi nafikiri sheria za usalama wa barabarani na hukumu zinatokana na makosa yake zinapaswa kurekebishwa maana inatoa mwanya wa kuwa na madereva wengi wazembe.Maaskali wetu wajifunze,watembelee nchi nyingine na waweze ku-introduce mifumo kama hiyo right away!
 
tatizo hapa sio status ya chenge, ni sheria mbovu zinazofatwa na hii inchi ya kusadikika!!
mtu ukimpiga kibao mke wako unafungwa miezi sita ila ukiua laki saba.
 
Usiharakishe kumsafisha anayo makosa mengi........matatu.........hivi..........................moja kuua bila ya kukusudia.....................kuendesha gari bila ya bima kwa zaidi ya miaka mitatu.....na la tatu..............kusababisha ajali ya gari..............

sasa haya yote adhabu yake ni faini tu?

Si kila kosa lilipaswa hukumu yake? Hawezi kuendelea kuwa Mbunge kama atakubali kulipa faini hiyo kwa sababu atakuwa amekubali kutumikia kifungo cha miaka mitatu ambayo ni sawa na hiyo faini aliyolipa......................................

Ubunge ni kwa wale tu ambao hawajawahi kutumikia vifungo vya zaidi mwaka mmoja.........hiyo mitatu ......it is over 4 him......labda akakate rufani

Kosa la kwanza na la pili...KUENDESHA GARI KWA UZEMBE NA KUSABABISHA AJALI ILIYOPELEKEA VIFO VIWILI @TShs 250,000(Total 500,000)

Kosa la tatu.......KUSABABIBSHA UHARIBIFU WA MALI ...Tshs 100,000
Kosa la nne.......KUENDESHA GARI LISILO NA BIMA ...Tshs 100,000

Mkuu Chenge hakuwa na kesi kubwa sana kama wengi wanavyodhani. Kama kesi ya kuua ukiwaunaendesha ingekuwa kesi kubwa kwa sheria za Tanzania then wengi wangekuwa wamefungwa.

Simtetei huyu mzee wa vijisenti, ila nashangaa Wadanganyika tulivyokuwa tumekomalia tukidhani kuna la maana out of that case. Muhimu tukomae afikishwe mahakamani kwa tuhuma za kula rushwa kwenye RADAR,pale tunaweza kupata chochote maana rushwa kifungo likely zaidi kama mtu atakutwa na hatia.
 
Haya ndio mambo ya TZ.Naamini kabisa angekuwa kapuka kama mimi angeambaiwa aende jela miaka 3 na si laki saba.Unaona sasa hata hukumu yenyewe alishaambiwa kuwa itakuwaje.Je kwako wewe kapuka ungeambiwa ujiandae na hela hiyo?
 
So you kill someone while driving drunk in an uninsured vehicle and you pay a fine of less than $500 and walk away. A persons life is now worth less than $500 in Tanzania?

WOW!!!!!

I'm telling you there will be no change in this country until there is a bloody revolution.

Tanzanians WAKE UP!!!
 
Bariadi wana mbunge batili!
Mkuu fafanua, sheria inasemaje? Je, suala la mtu anayefungwa zaidi ya miezi sita anapoteza sifa ya kuwa kiongozi inakuwaje hapa? Au mpaka akae jela? Kuna watu wanasema "HUKUMU" inatosha hata kama atalipa faini lakini amehukumiwa zaidi ya miezi sita ni kigezo tosha cha nafasi kuwa wazi.
 
..................
Simtetei huyu mzee wa vijisenti, ila nashangaa Wadanganyika tulivyokuwa tumekomalia tukidhani kuna la maana out of that case. Muhimu tukomae afikishwe mahakamani kwa tuhuma za kula rushwa kwenye RADAR,pale tunaweza kupata chochote maana rushwa kifungo likely zaidi kama mtu atakutwa na hatia.

uko sahihii kabisa hii ndiyo kesi watanzania, NGO wana JF wanatakiwa kukomalia sababu ina maslahi ya taifa.

kama aliweza kuchomoa kwenye mambo ya radar wala sikutegema maajabu zaidi kwenye kesi hii rahisi. Naona hata hizo laki 7 huyo hakimu anaweza kunyimwa promotion
 
hhahahaha

miaka mitatu haina thamani ya hizo laki 7

we unadhani miaka mi3 ilitakiwa iwe thamani kiasi gani?lazima uangalie hiyo sheria imetungwa mwaka gani?na kwa wakati huo laki 7 ilikuwa na thamani kiasi gani?ndo maana nasema sheria zifanyiwe marikebisho kama inawezeka fine iendane na kipato cha mtu.
 
Chenge ametiwa hatiani kwa makosa manne ya Kusababisha vifo vya wasichana wawili, Kugonga Bajaji, Kuendesha gari kwa uzembe na kuendesha gari isiyokuwa na Bima. Makosa yote hayo amepigwa faini ya shilingi za Kitanzania laki saba! (700,000/=) na amelipa

Source: Global Publisher

Jamani naomba kuuliza wadau ina maana hawa watu ni OUTLAWS au? Mana kwakweli ni jambo lisiloingia akili kuona mtu ana makosa yote hayo analipa faini tu.

Ila kuna watu wakitenda makosa hata madogo zaidi ya haya wanafungwa miaka na miaka jela. Mfano yule dereva wa chacha wangwe na hawa madereva wa mabasi ya abiria wanao fungwa kila siku kwa kuendesha kwa uzembe na kusababisha ajili. Ila huyu anaachiwa kwa kulipa faini.

Haya ndo mambo ya kina mkapa na madudu yake yote tunaogopa kumshitaki, mambo ya kina rostam aziz na kagoda na deep green tunashindwa kumshitaki. Me nadhan kile kipengele cha kusema kua kua everyone is under the law katika katiba kifutwe tu,ijulikane kuna watu wengine ni outlaws
 
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/98510-hukumu-ya-chenge.html
 
Karibu Bongo where Money and Political Status are more than the damn laws
 
Hiyo laki saba mbona hata hainunui bajaji aliyoigonga akiwa kalewa chakali from disco? Mi nilijua tu kwa kuwa ni trafiki case Chenge atashinda na kulipishwa kafaini. Hiyo mizimu alioiua itamfata daima.
 
kumbe ukimchoka mtu mgonge na gari kisha jisalimishe, subiri kesi lipa faini, kula maisha.

Hi ni kwa wenye visasi, hakuna haja ya kutafuta watu kufanya ushenzi wako.
 
Bwana CHENGE mbunge wa Bariadi leo hukumu yake imetoka na imedhihirisha ni jinc gani viongozi wa ngazi za juu walivyo juu ya sheria.Sheria c msimeno tena maana imeshindwa kumkata mheshimiwa huyo. Baada ya kesi yake ya mauaji ya wanawake wawili kuendeshwa kwa muda mrefu na yeye kupatikana na hatia,amehukumiwa miaka 3 jela,au kutoa faini ya sh laki 7 ambayo mbunge huyo hakuwa na shida kuitoa na kuachiliwa huru tayari kwa kuhudhuria bunge lijalo.Sasa yuko huru kwa sh.laki 7 uhai wa watu ukiwa umekwishapotea.
 
Back
Top Bottom