Chenge bado hujasafika

nguluvisonzo

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
515
71
Taarifa ya kujisafisha kwako bado inawalakini sisi watanzania ili uwe msafi pamoja na yote na taarifa kuwa ushaidi umeshindwa kubaini kama ulihusika,tunachohitaji ni kupata taarifa kamili ya kipato chako ulipokuwa mtumishi wa umma,matumizi yako,mali zako ulizonazo katika hayo yote pamoja na mapato mengine halali,Je ulikuwa na uwezo wa kuweka ziada ya vijisenti vyoko hivyo kisiwani na kwa nini usiweke hapa kwenu?usipo fafanua kwa kina bado wewe si msafi kabisa.
 
Chenge anadhani watu ni wajinga. Usione kunyamaza watu tunajua ukweli. Subiri siku ikifika kama sio wewe watoto wako watalipa hela za walalahoi. Hela zilizokisiwani ulizipataje kwa mshahara wako na huna biashara yoyote. Mungu hamfichi mnafiki.
Kwa heri chenge wadanganye wadanganyika, sio mungu
 
Tatizo si Chenge, tatizo ni waandishi wa habari wa bongo. Ebu tujiulize, je alipo wahutumbia aliwapa ushahidi wowote kutoka kwa hao waliokuwa wanamchunguza unaosema wazi ya kuwa hawakubaini kosa lolote linalomhusu? Je hicho kitengo cha upelelezi wa makosa makubwa cha uingereza, hiyo kauli waliitoa lini? Mtu akipitia hukumu iliyotolewa huko uingereza juu ya suala hilo inaonekana wazi kwamba kitengo hicho kilidhibitisha kililipa malipo ya kamishna kupitia offshore accounts ili kurahisisha ulipaji wa mrungula kwa maafisa wa Tanzania waliofanikisha upatikanaji wa tenda hiyo.
 
Haswaa! Waandishi hao walioitwa walikuwa wameshapewa chao. Huyu bwana anajitahidi kujisafisha haraka haraka kwa ajili ya uchaguzi wa CCM mwaka kesho. Lakini ukweli ni kwamba huyu bwana hajijui ni mchafu kiasi gani na hajui kwamba hakuna kiwango cha maji, sabuni na manukato vinavyoweza kuondoa uozo anaotembea nao. HATUDANGANYIKI!
 
Mbona hii njemaba inatumia nguvu sana kujisafisha? Shida nini hasa au anataka nini zaidi? Mbona alikimbia maswali ya waandishi!
 
Kwanini Chenge ajitangazie usafi, why not let the ones who accused him say that he is clean? What does he want anyways?
 
Back
Top Bottom