"Chenga twawala na twawafunga Bara"

GAMBLER

JF-Expert Member
Nov 22, 2009
303
11
Kuna msemo mmoja ambao ni maarufu sana wanautumia ndugu zetu wa znz unaosema "Kufungwa twafungwa lakini chenga twawala". Kwa nini wa znz wanapenda kuutumia huu msemo? Ukweli ni kwamba znz wako nyuma sana ki soka ukilinganisha na bara. Bara kuna viwanja vingi sana vya mpira ukilinganisha na znz, vilabu vya bara na timu ya taifa huwa wanapata wadhamini, ambapo znz hawana wadhamini, znz hakuna serengeti na makampuni kama ya bara. Bara wana makocha kutoka ulaya na Brazil wakati znz wana makocha wazawa tu. Bara ni kubwa zaidi ya mara 100 kwa znz! Pamoja na mapungufu yote hayo ya znz, bado znz wanakuja kuitandika bara katika kombe la cecafa na kuchukua ubingwa wa tatu! hii ni aibu na fedheha kubwa sana kwa bara,nawashauri wabara wenzangu tuache usanii, serekali yetu ya kisanii, basi mpaka michezoni tunafanya usanii! siku zote lawama kubwa ktk soka zinamwendea kocha, kocha anapofanya vibaya huwa yeye mwenyewe amevunja mkataba na anatakiwa atimuliwe, huu ni mwaka wa ngapi tunamlea maximo? kwa nini maximo anaogopewa? kwa sababu huyu kocha yuko tz kisiasa, ameletwa na JK na usanii hapo umetumika, mkataba wake ni wa kifisadi, Maximo analijuwa hilo na ndio maana pamoja kuboronga amekuwa na jeuri sana na anaogopewa mpaka na TFF!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom