Chemsha Bongo ya Elimu

mahwelu

JF-Expert Member
Jun 8, 2013
322
252
Hali zenu wakuu,
Nawashukuru katika thread ya last week tulijadili sana kuhusu wako wapi ma TO waliopita? na tulitafakari mengi....

Leo sina hoja ya moja kwa moja bali naomba kila mmoja atafakali haya :-
  1. Jaribu kwenda wizara ya elimu na ufanye tathmini ya wakurugenzi na wakuu wa idara wetu wakuu.....je watoto wao wanawasomesha private/public?
  2. Kabla hujaondoka wapitie makatibu wakuu, manaibu, makamishna nakadhalika nao jiulize swali hilo hilo.... je watoto wao wanawasomesha private/public?
  3. Nenda NECTA, VETA, TCU na taasisi zote zenye kushiriki katika elimu .... je watoto wao wanawasomesha private/public?
  4. Nenda baraza la mawaziri pamoja na ikulu na kunakofanana na huko .... je watoto wao wanawasomesha private/public?
  5. Nenda bungeni na wakague hawa watetezi wa wananchi wa pande zote tawala na upinzani ... je watoto wao wanawasomesha private/public?
  6. Nenda mikoani na wilayani na jiulize kuhusu waimamizi wetu wa elimu .... je watoto wao wanawasomesha private/public?
  7. Usiwasahau wakaguzi wa shule .....je watoto wao wanawasomesha private/public?
  8. Mnaongea value for money ...nenda kwa CAG, je watoto wao wanawasomesha private/public?
  9. Sasa ongeza safari zako binafsi za uchunguzi kada za chini.
Kama unapenda kukaa kijiweni jaribu kupata kahawa na utafakari ...kama itakuwa asilimia kubwa ya watunga sera na wasimamizi watoto wao wako private/public then husisha na kupanda na kushuka kwa elimu...jiulize kunashabihiana au la?

N.B: Naomba msimind kwakua nyie ni great thinkers hapo tutapata uchambuzi wa maana, kila la kheir, tufanyeje?
 
Back
Top Bottom