Chemsha Bongo; Simba, Chui na Fisi nani ataruka futi sita?

Mzizi wa Mbuyu

JF-Expert Member
May 15, 2009
7,323
6,810
Ilikuwa katika hifadi ya wanyama ya kreta ya Ngorongoro.
Twiga mmoja aliekuwa amegongwa na gari la watalii, alikuwa anachechemea na kuangalia pande mbalimbali za nchi akiogopa kushambuliwa na wanyama wakali wala nyama.
Ghafla wakatokea Simba, Chui na Fisi,... kwa kujitahidi Twiga aliruka juu ya jiwe kuubwa lenye urefu wa futi6 kwenda juu.
Sasa swali, katika wanyama hao watatu (Simba, Chui na Fisi) yupi anauwezo wa kuruka juu futi6?
 
Duuh, ina maana sijawa sahihi 100% ? Basi natoa lingine, nikikosa nakupa mji! Simba, Chui na Fisi hawawindi/hawaui Twiga. Hapo je?
 
Duuh, ina maana sijawa sahihi 100% ? Basi natoa lingine, nikikosa nakupa mji! Simba, Chui na Fisi hawawindi/hawaui Twiga. Hapo je?

Mh, kweli wewe mpiganaji mkuu, hukati tamaa! Kunasiku utakuja kuwa tajiri sanaaaa!.....
Lakini bado siyo sahihi
 
Haa haa haa!! Utajiri wa Bongo haupo kwa wapiganaji, upo kwa mafisadi. Sasa ni nini? Hebu usijibu kwanza labda nikipata lunch akili itafanya kazi. Saa hizi njaa inauma, I'll be back!
 
Haa haa haa!! Utajiri wa Bongo haupo kwa wapiganaji, upo kwa mafisadi. Sasa ni nini? Hebu usijibu kwanza labda nikipata lunch akili itafanya kazi. Saa hizi njaa inauma, I'll be back!

Mh, usiende kuuliza mtu lakini mkuu! endelea kujaribu mwenyewe bwana.
Haya sijibu naenda Tandika kununua maembe ya juisi, kule bei rahisi mno! waifu kajifungua anahitaji sana juisi.
 
Huo mzigo utakuwa wa fisi maana kipindi ameruka futi 6 alipotua chini alitua juu ya kinywa cha Fisi
 
Jamani hongera kwa woote mliojaribu, mlijitahidi kiasi chenu....natoa jibu sasa;...............
.........
Katika hifadhi ya kreta ya Ngorongoro hakuna Twiga......(yaani hakuna mnyama Twiga aneishi mle mbugani)
 
Sijajua fani yako ila ungekuwa Mwalimu ungeishia kuwapa wanafunzi wako alama 20 kwa 20 kama swali lilikuwa na Alama hizo. Maana swali lenyewe halieleweki na ukiliangalia vizuri halina uhusiano na Watalii, Ngorongoro, jiwe la futi 6 na hao wanyama. Liangalie na ulitunge upya vinginevyo ukitengeneza Marking Scheme yako itakuwa na mapungufu mengi.

Salamu.
 
Hii ni chemsha bongo baba!! Chemsha bongo! uanapenda mambo marahisi rahisi ee? shauri yako ubongo wako utaendelea kulala hivyo hivyo, kuna kichwa maisha yamejifungafunga, yafungue kwa kutumia ubongo wako.
 
Jamani hongera kwa woote mliojaribu, mlijitahidi kiasi chenu....natoa jibu sasa;...............
.........
Katika hifadhi ya kreta ya Ngorongoro hakuna Twiga......(yaani hakuna mnyama Twiga aneishi mle mbugani)

duh! kwa hiyo thread ndio imeishia hapa?
mKuu umetoa jibu mapema sana
 
Back
Top Bottom