"Chemsha bongo enzi zile"

Homemade

Member
Jun 2, 2011
17
1
Wanajf tujikumbushe zile chemsha bongo za primary mfano; 1. Kati ya kilo 1 ya mawe na kilo 1 ya manyoya ya kuku ipi nzito?=mawe 2.mtini kulikuwa na ndege 100 Juma alirusha jiwe na kuua ndege 3 je,mtini walibaki ndege wangapi?=97.Tililika nayo..
 
1. Ndege kutoka Kenya kuja Tanzania inaanguka mpakani mwa Tz na Kenya.

Je majeruhi watazikiwa wapi?.................................

2. Train la TGV yaani la umeme linatoka Berlin kwenda Bonn. Upepo mkali sana unapiga kutoka upande wa Bonn kwenda Berlin. Sasa swali hapa linakuja ni hili, je moshi wa train utaelekea upande upi?

3. Kwa kawaida upepo unavuma kutoka upande wa Dar kuelekea Mwanza. Katika utafiti wangu, nimegundua kuwa ndege ikitoka Dar kwenda Mwanza inachukua saa moja na nusu na ikitoka Mwanza kuja Dar inachukua dakika 90 tu, kwa nini?..........
 
1. Ndege kutoka Kenya kuja Tanzania inaanguka mpakani mwa Tz na Kenya.Je majeruhi watazikiwa wapi?.................................2. Train la TGV yaani la umeme linatoka Berlin kwenda Bonn. Upepo mkali sana unapiga kutoka upande wa Bonn kwenda Berlin. Sasa swali hapa linakuja ni hili, je moshi wa train utaelekea upande upi?3. Kwa kawaida upepo hunavuma kutoka upande wa Dar kuelekea Mwanza. Katika utafiti wangu, nimegundua kuwa ndege ikitoka Dar kwenda Mwanza inachukua saa moja na nusu na ikitoka Mwanza kuja Dar inachukua dakika 90 tu, kwa nini?..........
Duuu,mwanangu hiyo ya tatu imeniona!hebu nikumbushe!
 
Mpira wa mguu katika mechi ulitumbukia nda ya shimo lilitosha mpira pekee kuingia...na refa(refree) alibakiza dakika 3 amaliza mechi...watafanyaje ili kuwahi muda?
 
1. Ndege kutoka Kenya kuja Tanzania inaanguka mpakani mwa Tz na Kenya.Je majeruhi watazikiwa wapi?.................................2. Train la TGV yaani la umeme linatoka Berlin kwenda Bonn. Upepo mkali sana unapiga kutoka upande wa Bonn kwenda Berlin. Sasa swali hapa linakuja ni hili, je moshi wa train utaelekea upande upi?3. Kwa kawaida upepo unavuma kutoka upande wa Dar kuelekea Mwanza. Katika utafiti wangu, nimegundua kuwa ndege ikitoka Dar kwenda Mwanza inachukua saa moja na nusu na ikitoka Mwanza kuja Dar inachukua dakika 90 tu, kwa nini?..........
Mkuu kumbukumbu unayo duh!
 
Mpira wa mguu katika mechi ulitumbukia nda ya shimo lilitosha mpira pekee kuingia...na refa(refree) alibakiza dakika 3 amaliza mechi...watafanyaje ili kuwahi muda?
Hapo si ndio tunamwaga maji kwenye shimo bhanaaa!
 
Au hii,una machungwa matano kapuni.kuna watoto watano wamekuzunguka na inabidi kila mmoja apate chungwa moja.Utawezaje kuwapatia kila mmoja chungwa moja na chungwa moja libaki kapuni?
 
Au hii,una machungwa matano kapuni.kuna watoto watano wamekuzunguka na inabidi kila mmoja apate chungwa moja.Utawezaje kuwapatia kila mmoja chungwa moja na chungwa moja libaki kapuni?
utatoa machungwa manne na kuwapa watoto wanne. Alafu utawaambia wale wanne kila mmoja amkatie robo yule aliyekosa. Kwa kuwa robo ziko nne, na yule wa tano atapata chungwa zima. Lile chungwa moja litakuwa limebaki kapunihapo vp?
 
k kila mtoto apate chungwa moja ale peke yake!
 
Kuna kuku wa5 wanakula pumba,kisha ikapita ndege juu.je,macho mangapi ya kuku yataangalia juu?
 
jogoo alitoka tanzania kwenda kenya alipofika mpakani mwa tanzania na kenya akataga yai litakuwa la kenya au tanzania
 
Wanajf tujikumbushe zile chemsha bongo za primary mfano; 1. Kati ya kilo 1 ya mawe na kilo 1 ya manyoya ya kuku ipi nzito?=mawe 2.mtini kulikuwa na ndege 100 Juma alirusha jiwe na kuua ndege 3 je,mtini walibaki ndege wangapi?=97.Tililika nayo..
Hawawezi kubaki hata ndege mmoja mtini kwa sababu wote 97 waliobakia wataruka.
 
Back
Top Bottom