CHEDEMA kufutwa, Kibamba, Nkya na Wanaharakati kufungwa; Warema kasema leo Bungeni!

Mr. Clean

Senior Member
Aug 7, 2006
194
44
Wanajamiiforums,

Kutokana na kifungu (19) kilichoongezwa katika mswada kama alivyosoma mwanasheria mkuu wa CCM-warema, ni kuwa atakayepinga au kuzungumzia maamuzi ya mswada ulopitishwa bunge la CCM leo, adhabu yake ni miaka mitatu jela au faini milioni tano!

Well n' good, wanaharakati wetu na chadema mtasalimika kwa hili? Au ndo mambo yashakuwa level hivyo?

HECHE, KAFULILA, KIBAMBA, bado j'2 kitaeleweka?

.....wameshika mpini je atakayethubutu kushika makali ya sime nani.....?

 
CCM wana hofu gani hadi waje na na vitisho ?Hivi hawa CCM wanadhani wanamkomoa nani na watoto wao au hata wajukuu wanawaweka wapi baadaye ?
 
Hicho kifungu ni illegal kinapingana na katiba ya sasa inayompa mamlaka mtanzania kutoa maoni yake kwa uhuru na kama kipengele hicho kipo kweli basi moja kwa moja tumeanza na mguu mbaya kwa kuwafunga watu kutoa maoni yao wakati mswahada safi ni ule unaotoa uwanja mpana wa wananchi kutoa maoni yao na siyo ule ambao UNA LIMIT FREE SPEECH KWAHIYO TUNA KILA SABABU ZA KUTOKA MTAANI KUPIGA MSWADA KWA MAANA UNAANZA KWA KUTUNYANGANYA OUR BASIC RIGHT OF SPEAKING AGAINST WHAT WE THINK IS WRONG.
 
Hilo bomu tayari limeshatengenezwa CCM wasubiri litakapo walipukia hapo baadaye
 
CCM si na wao walisema watawaachia wananchi waamue wenyewe, sasa hofu yatoka wapi. Wanataka kutuvurugia nchi hawa ccm, WATANZANIA TUSIKUBALI.
 
CCM wasidhani kwamba wananchi wa Tunisia, Libya, na Misri walipoandamana hapakuwa na katiba. ilikuwepo katiba tena ilikuwa inapinga maandamano ya aina yoyote, na ilisomeka kwamba yeyote atakayeandamana, lakini watu waliandamana na wakawaondoa wahafidhina.
 
Hawa dawa yao ni kupambana nao hadi mwisho!Haki yetu haiwezi kunyang'anywa kirahisi hivyo!!!!!!!!!!!!
 
Mie naona kama wamechelewa kuipitisha hiyo katiba na kuweka vifungu uchwara. Waipitishe tuone ni magereza ngapi hapa nchini zitakuwa sustainable na wafungwa watakaotokana na kukiuka hiyo katiba. Hata mimi na familia yangu tutakuwemo kwa sababu ninaipinga hata kabla hawajaipitisha.
 
Kwa sisi wapigania haki siku zote sheria za kipumbavu huvunjwa kwa gharama yoyote hata kama ni jela na hata kifo.Mwisho ukweli utashinda.
 
Hivi jamani nauliza chama kingine kikiingia madarakani halaf kianze kuwanyanyasa ccm na hyo katiba waliyoitunga wao itakuwaje??? Wao ccm wana uhakika gani kuwa watatawala tanganyika maisha??kuna siku tu tutapata uhuru!!
 
hii nchi inatia hasira!! ipo siku tutajua nani mtawala na nani mtawaliwa
 
Back
Top Bottom