Cheche: Ya Mboma, Meremeta, na Apson!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,460
39,928
toleola16.jpg


Karibuni tena! Kuna habari nyeti ambazo zimefichwa kwenye nakala hii ambapo ukiipata siyo tu utashangaa lakini hautaamini kama tunachoshuhudia ni kitu chenyewe kweli au ndio mazingaombwe! Habari hiyo nyeti hujaisoma mahali pengine popote na kijarida chako kinakuwa cha kwanza kukudokeza! Ukijua usimwambie mtu unaweza kujikuta unavunja sheria!

Ukikigundua ibakie siri yako. Ukitaka kusema lolote nitumie PM!
 

Attachments

  • TOLEOJIPYA16.pdf
    421.5 KB · Views: 882
Last edited by a moderator:
hiki kijarida huwa kinapatika wapi.... i mean hard copy!!!
 
sasa huku ndio nini ikiwa habari zipo kwenye kijarida na kijarida ni cha bure ,hapo peke yake kumetanuka wigo wa habari ,aidha ikiwa kijarida kimebeba habari nyepesi au nzito kama wananchi hawatatumia redio kifua kueneza habari hizo nguvu ya kudai kioja hicho kijadiliwe kitaifa itakuwa chini ni lazima hiyo hadi kopi iwekwe hapa kwa wale wasio na ubavu wa kukipata hicho kijarida bila ya shaka yeyote watajisomea na hivyo upo uwezekano wa kuwaamsha ndugu na jamaa zao waliolala na mazingahombe ya EPA kuwa kuna mbuzi mwengine ameanza kupigiwa gitaa ,weka hizo nyaraka hapa ,yaani tunaweza kuziita nyaraka za JF. Au bado mnahogopa ,jamani dunia ya leo si ya kuogopana tumaamini kabisa wenye madaraka wamewekwa na sisi wapiga kura kama ni hivyo tusione taabu kuwatolea uvivu.
Maana kama mkuu wa jeshi kuna ushahidi alikuwa anajilimbikia mabilioni kwa njia ya wizi wakati askari wake wanavaa ndara na hata wanapostaafu bado huwa wanababaika,yaani nilimkuta Kapteni wa Jeshi ambae wakati nikiwa kazini alikuwa rafiki yangu mkubwa sana kikazi na tukifahamiana tu japo yeye alikuwa mkiristo na mimi ni muisilamu ,lakini dini zetu hazikutufanya tuwe na mirengo mikali kiuhusiano.
Mimi niliacha kazi baada ya kupata matatizo ambayo yalinikuta tukiwa kwenye mazoezi ya risasi za moto na hivyo sikuweza na sikuruhusika kuendelea tena kwani kiafya nilikosa sifa za kuendelea na hata yeye alinishauri nirudi uraiani kwani kuendelea huko ni kujizidisha madhara ,kwa ufupi nilitakiwa niwe mwenye kutulia na kutofanya harakati zozote za nguvu,nilitenguka tindi ya mgongo wakati tukipakia zana nzito kwenye gari na hapo ndipo ulipokuwa mwisho wa shughuli zangu za kijeshi ,ingawa madaktari walifanikiwa kunisaidia na walisema niliwahi kukurupuka ndio athari hazikunilemaza.
Okay baada ya hapo na miaka kupita kwa bahati nilikutana na yule kapteni ambae alikuwa mkuu wangu wa kazi na bosi ,nilishangaa sana nilivyomkuta anaendesha baiskeli na viatu ni kanda mbili zilizokwisha kabisa na hana hata nyumba ya maana ,nilipomuuliza aliniambia amestaafu lakini baada ya hapo hakuweza tena kupata ushirikiano wa kutoka kazini,na alizidi kueleza kuwa kinachowafanywa wawe wanahangaika ni mpangilio mzima wa kikazi huwa hauna mshiko wa kuweza kufanya kitu cha baadae muda wote unakuwepo kambini na familia yako na huna maisha ya uraiani.Hivyo wanashindwa hata kujiendeleza kwa maisha ya kustaafu inakuwa kama ni watu wepya kwenye jamii yao ya kijijini.
 
once again big up mwnkjj..............
hiki kijarida huwa kinapatika wapi.... i mean hard copy

mwanakijiji amefanya part yake nawe unaweza kusaidia kwa kutoa print out na kuzisambaza kwa kadri uwezavyo, mie nafanya hivyo sasa hivi!
 
Mkuu M.M.M, shukrani kwa watendaji wote.... Kaaz kweli kweli.... Nchi imekwisha jamani, ni wapi tuendako??
 
Mkuu Mzee mwanakijiji kazi nzuri sana,nitapaje hard copy.


Hatma ya safari ya ukombozi wa Wadanganyika si endelevu kuelekea kuikomboa jamii kifikra na kiuchumi. Mawazo mgando yaliyokomazwa na fikra za “Hakuna Msaada, Hakuna Maendeleo” yanaonekana kuwa laana hadi kizazi cha nne.

Ee Mungu tushushie tena Musa. Maana ulipotupatia ardhi ya kutosha yenye rutuba na kutunyeshea mvua wanadamu waliuliza majembe yako wapi?!
Na baada ya kubariki uzao wa wanyama wa kondeni, maziwa na nyama Vikapatikana kwa wingi, binadamu hao hao wakauliza mbona hujawapatia vyombo vya kukamulia maziwa na kupikia nyama?!
 
Mkuu MJJ
Kama ukitoweka jamvini unarudi na makali haya, basi we kaa huko porini tu maana kuna mengi kuliko hapa mjini. Kazi nzuri saaaaaaaaaana, by the way kuna watu walikuwa hawaamini habari za mtandao, siku hizi ndio wakuu wa fwd kijarida cha Cheche. Taratibu tutafika
 
Hey M.M.M,
Asante sana kwa kazi yako nzuri. Naomba maelezo ya ziada juu ya mahusiano kati ya Andy Chande, Ruhinda na Mkapa katika mfumo wa utatu wa kifisadi.

KWA HABARI ZILICHAMBULIWA NA ZA UKWELI UNANIACHA MWAKA MMOJA NYUMA. NAAFIKI HU-NABII MWENYE MAONO YA MBALI. MOJA YA ISHARA, SIKU ZOTE NABII HUPINGWA HASA NYUMBANI KWAO. NAOMBEA AMANI NA UPENDO.
 
So we have now gone to talking about the untouchables who it was said that when they are touched the country will be ungovernable. Ukweli sasa umefikia mwisho. Ufisadi ule wote wa jeshi na wa usalama sasa unaanza kuzungumzwa, kweli vita imefika penyewe hasa.
 
Mwanakijiji,

Freedom of information and education in Africa far outweighs in importance some well prioritized issues such as foreign aid .

However obstacled, your initiative is well noted.
 
Mwanakijiji,

Freedom of information and education in Africa far outweighs in importance some well prioritized issues such as foreign aid .

However obstacled, your initiative is well noted.

unajua kabisa you are singularly responsible for this! it is you my friend that I'm eternally grateful for lighting that flame within me. I hope our little contribution to the the expansion of freedom of speech and information will not be forgotten.
 
Jamana ni mimi tu asiyeweza ku-download "Cheche" au wapo wengine wenye tatizo kama langu?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom