Chatu ammeza dreva, aacha gari porini!

Nyani Ngabu, mwaka jana niliona chatu nyamaume kule Ruvu, urefu wa futi 12 na unene wake ni kama lilikuwa limemeza mbuzi watatu. Wajuvi walisema lina uwezo wa kumeza mtu Pepe Kale style, kwa makadirio uzito wake ulikuwa nia around Kg 250. Kwenye sehemu lilipopita ni kama mtu alikuwa anaburuza gunia la mahindi. Ni kweli linapomeza mtu huwa linavyunnjavunja mbavu, na mabega then linameza, so kuna chatu wakubwa Tanzania wengi tu, hasa maeneo ya mkoa wa Tabora na Morogoro. Lakini you are right, they are not even close to South American amazonian giants.

Hata Anaconda wa futi 45 hawezi kummeza mtu wa saizi ya Kabasele Yampanya. Huo ni uongo mtupu.
 
Natumia common sense bana.....

Ni vyema siku hizi kutilia shaka kila kitu maana hakuna vitu halisi tena..si watu, si picha...yaani ni full usanii tu siku hizi

Heshima kwako Nyani Ngabu,

Mkuu mimi nimewahi kumwona Chatu maeneo ya Kilindi Tanga amemeza Swala 50 kg mzima sasa atashindwaje kummeza mwanadamu ?.Chatu mwenye uwezo wa kummeza Mbuzi,Swala kwa hakika hashindwi kummeza mwanadamu.
 
Heshima kwako Nyani Ngabu,

Mkuu mimi nimewahi kumwona Chatu maeneo ya Kilindi Tanga amemeza Swala 50 kg mzima sasa atashindwaje kummeza mwanadamu ?.Chatu mwenye uwezo wa kummeza Mbuzi,Swala kwa hakika hashindwi kummeza mwanadamu.

Sawa lakini tunazungumzia mwanadamu gani? Mtoto mdogo? Kwa sababu mtoto mdogo naye ni mwanadamu vile vile lakini ukija na habari za chatu kuweza kummeza mtu wa saizi ya Pepe Kale nitakuona unaniletea habari za Nyangumi kupindua meli......
 
Nawajua sana hao wanyama. Kwanza sisi Tanzania hatuna chatu wakubwa. Chatu wakubwa, reticulated pythons wanapatikana Asia. Na majoka makubwa kwa girth ni ma Anaconda ya South America.

Kwa hiyo inaniwia vigumu sana kuamini kuwa vichatu vyetu vinaweza kumeza mtu. Acheni uzushi

Sikatai kuwa ni wanyama hatari kwa sababu wanaweza kabisa kuua mtu. Lakini kummeza mzima mzima.....uuuuum try again

Guku mhola hene?
Yeah Chatu kummeza mtu ni kitu cha kawaida sana: Huko vijijini tumeshuhudia chatu wakimeza mbuzi, ndama n.k. Anachofanya chatu ni kukutaimu na kukuchoma mwiba wake kisha kujiviringisha kwenye mwili wako na kujivuta na hapo anakuwa anavunjavunja mbavu ili iwe rahisi kumeza. Kitendo cha kumeza si cha haraka huwa ni cha polepole sana na akishameza huishia kwenye shingo na kukaa hapohapo mpaka kichwa kioze kidondoke ndo aendelee na safari yake.
 
Guku mhola hene?
Yeah Chatu kummeza mtu ni kitu cha kawaida sana: Huko vijijini tumeshuhudia chatu wakimeza mbuzi, ndama n.k. Anachofanya chatu ni kukutaimu na kukuchoma mwiba wake kisha kujiviringisha kwenye mwili wako na kujivuta na hapo anakuwa anavunjavunja mbavu ili iwe rahisi kumeza. Kitendo cha kumeza si cha haraka huwa ni cha polepole sana na akishameza huishia kwenye shingo na kukaa hapohapo mpaka kichwa kioze kidondoke ndo aendelee na safari yake.
Kwa picha hiyo hapa chini naonekana alianza kummeza mtu kwa kuanzia kichwani

 
Wakuu nimeona niwashirikishe kisa cha kweli kilichotokea hivi karibuni, ili kisaidie kufanya maamuzi sahihi wakati wote.

Dreva wa magari yanayo safirishwa nje ya nchi kupitia bandari ya Dar es salaam yenye namba 'IT' amekumbwa na kifo baada ya kumezwa na chatu, pale alipo patwa na haja kubwa na kuamua kuacha gari (silensa) na kuingia porini ili achimbe dawa. Kumbe Chatu mkubwa akiwa na njaa yuko mawindoni akafanikiwa kumkamata na kummeza!.

Madreva wenzie, walio kuwa na magari ya aina hiyo wakisafiri kwa pamoja, walishangaa baada ya kuona kuwa yeye na gari yake hawaonekani, wakati wanampigia simu inaita mpaka inakata bila kupokelewa. Mwanzo walidhani kuwa kuchimba dawa ni starehe hivo, akimaliza kuchimba dawa, atajibu simu zao. Mara wanaona kimya! hapo ilikuwa kama saa 2 usiku na walikuwa wanakaribia kufika mpakani Zambia.

Baadhi yao (Madreva wenzake) wakaamua kurudi nyuma kuona kulikoni. haikuwachukua muda, mara wakarikaribia gari na bado liko( on) yaani limepack na liko kwenye 'silensa' wakaangalia huku na huku, na kuna giza, pia wakiita, bila mafanikio.

Iliwalazimu kwenda kuwaambia wenzao walio kuwa wametangulia mbele. Kwakuwa usiku ulikuwa unazidi, wakaamua kuelekea karibu na mpakani mwa TZ na Zambia kutoa taarifa Polisi. Kilicho fanyika, Polisi na baadhi ya madreva hao, walirudi kwenye eneo la tukio na kuamua kuchukua gari hilo mpaka kituoni, ili kesho waanze zoezi la kumtafuta huyo dreva.

Asubuhi na mapema waliondoka na polisi wawili wakiwa na silaha kwenda kweye eneo la tukio. wakaanza kuzungukia maeneo hayo, ghafla kama hatua kumi kutoka kwenye tukio wakamwona Chatu mkubwa akiwa amejilaza na asiweze hata kusogea.! Mmoja wao akapiga yowe na kusema Jamani ni chatu ndiye aliye leta balaa! Askari ammoja aliye kuwa karibu, akatoa msaada wa kumuua chatu kwa risasi.

Baada ya kumuua Chatu huyo wakapasua tumbo wakamkuta maskini dreva kesha kufa, na simu yake iikakutwa na missed call walizokuwa wakimpigia!

USHAURI' TUNZA MAZINGIRA NA ACHA UBAHILI WA SH. 200 UOKOE MAISHA. - KISA HIKI NI CHA KWELI KABISA.

Habari nyepesi nyepesi hizi. Kwa kawaida magari haya makubwa huwa yana dereva na utingo. Unataka kutuambia kuwa na utingo naye alimezwa na chatu mwingine au? Iweje mpaka madereva wa magari mengine ndiyo wagundue kuwa huyu jamaa amemezwa na chatu? rubbish.

Naunga mkono hoja ya kutunza mazingira lakini sidhani kuwa kunya porini ni kuchafua mazingira. Unapokunya porini unaacha mbolea na kusadia mimea iliyopo jirani na unakuwa huna tofauti na mnyama yeyote anayekunya porini.
 
Back
Top Bottom