Chatanda azua tena mvutano CCM, Chadema Arusha

Nimewahi kukutana na Mary Chitanda mara moja mwaka jana akitokea Morogoro kama sikosei kwa nafasi hiyo hiyo ya katibu wa mkoa.

Nina sehemu ya kufanyabiashara eneo la stadium huyu mama alitupandishia kodi 100 % ikabidi nijitose ofisini kwake nikakumbana na dharau ya aiana yake. Nilipodadisi baadhi ya watumishi wa CCM mkoa wote walikuwa wakimuogopa utadhani Mungu mdogo kuanzia madereva mpaka maofisa wa vyeo vya juu walikuwa hawataki kuingia kwenye anga zake. Kila mmoja alikuwa akitoa hadithi mbaya za Mary Chitanda kwamba ni mtu wa karibu sana na mkuu wa nchi, kwamba ni jasusi wa hali ya juu, kwamba alishiriki kumtimua aliyekuwa katibu wa UWT taifa, kwamba kaletwa hapa kuhujumu upinzani ambao umeonekana ukiisumbua CCM tangu mwaka 1995.

Mary Chitanda ni kiongozi mwenye nguvu kubwa sana ndani ya CCM kiasi kwamba alimwambia wazi Dr Batilda Buriani anapaswa kujilaumu mwenyewe kwakuwa alishiriki kuanzisha kambi mbili ndani ya CCM. Mary Chitanda kwa kutumia nafasi yake ya katibu wa CCM mkoa ni mshirika na mwanachama mwaminifu wa kundi la mtandao. Nafasi ya katibu wa mkoa kwa kawaida aina nguvu kubwa sana lakini hali ni tofauti kidogo kwa Chitanda amabae pia ni mjumbe wa kamati kuu UWT na halmashauri kuu ya CCM taifa.

Unaweza kujiuliza kiburi cha Chitanda kinatoka wapi mbona wapo makatibu wa mikoa kibao hatuwasikii wala hawana impact ya maana katika jamii. Mary ni jasusi ndiyo maana alipoona maaskofu wamebaini ubaradhuli wa CCM alitumia taaluma yake kuwachota baadhi ya masheckh ubwaubwa kwamba mgogoro wa umeya Arusha una harufu ya udini kitu ambacho si kweli hata kidogo bahati nzuri Meya wa kuchongwa wa CCM Bwana G Lyimo ni mkristo tena aliyesomea upadri ukamshinda. Mgombea wa CDM naye ni mkristo sasa suala la udini liko wapi kama si ujasusi uchwara wa Mary Chitanda.
 
Mbona hata ndani ya CHADEMA wapo wengi tu, mnawajua na mnawafagilia. Siku watakapomaliza shughuli yao ndio mtajua kuwa system is awake and at work. Muulize Slaa.
 
Haya ndiyo mambo ya uzushi. Kwa kuwa amewaponda maaskofu sasa akiitwa Zuhura wengi ndio wanakubali. Yaani siku hizi, uongo uongo tuuuu. Inamaana ili uishi Arusha unatakiwa ubadili jina lako na watu watakukubali na si competency yako. JF kuna kazi mwaka huu.
 
Nimewahi kukutana na Mary Chitanda mara moja mwaka jana akitokea Morogoro kama sikosei kwa nafasi hiyo hiyo ya katibu wa mkoa.

Nina sehemu ya kufanyabiashara eneo la stadium huyu mama alitupandishia kodi 100 % ikabidi nijitose ofisini kwake nikakumbana na dharau ya aiana yake. Nilipodadisi baadhi ya watumishi wa CCM mkoa wote walikuwa wakimuogopa utadhani Mungu mdogo kuanzia madereva mpaka maofisa wa vyeo vya juu walikuwa hawataki kuingia kwenye anga zake. Kila mmoja alikuwa akitoa hadithi mbaya za Mary Chitanda kwamba ni mtu wa karibu sana na mkuu wa nchi, kwamba ni jasusi wa hali ya juu, kwamba alishiriki kumtimua aliyekuwa katibu wa UWT taifa, kwamba kaletwa hapa kuhujumu upinzani ambao umeonekana ukiisumbua CCM tangu mwaka 1995.

Mary Chitanda ni kiongozi mwenye nguvu kubwa sana ndani ya CCM kiasi kwamba alimwambia wazi Dr Batilda Buriani anapaswa kujilaumu mwenyewe kwakuwa alishiriki kuanzisha kambi mbili ndani ya CCM. Mary Chitanda kwa kutumia nafasi yake ya katibu wa CCM mkoa ni mshirika na mwanachama mwaminifu wa kundi la mtandao. Nafasi ya katibu wa mkoa kwa kawaida aina nguvu kubwa sana lakini hali ni tofauti kidogo kwa Chitanda amabae pia ni mjumbe wa kamati kuu UWT na halmashauri kuu ya CCM taifa.

Unaweza kujiuliza kiburi cha Chitanda kinatoka wapi mbona wapo makatibu wa mikoa kibao hatuwasikii wala hawana impact ya maana katika jamii. Mary ni jasusi ndiyo maana alipoona maaskofu wamebaini ubaradhuli wa CCM alitumia taaluma yake kuwachota baadhi ya masheckh ubwaubwa kwamba mgogoro wa umeya Arusha una harufu ya udini kitu ambacho si kweli hata kidogo bahati nzuri Meya wa kuchongwa wa CCM Bwana G Lyimo ni mkristo tena aliyesomea upadri ukamshinda. Mgombea wa CDM naye ni mkristo sasa suala la udini liko wapi kama si ujasusi uchwara wa Mary Chitanda.
Bravo report, na sasa mambo haya yanazidi kuwa hadharani!

Mkuu, na wewe hukufanikiwa kupata picha yake?

Anyway, kesho nitakuwa na ka-camera kangu kwenye Maombolezo, naombea awepo nim'photo, naihitaji sana picha yake kwa kazi za intelijensia!
 
Kaitika pitapita zangu nimekutana na hii ya zamani kidogo iliyototewa na gazeti la mwanahalisi kwa headline ya

Wanawake UWT wavuana nguo

Katika habari hiyo Mary Chitanda anatajwa kama kinara wa kumshambulia mwenzao na hii chini ni nukuu ya maneno yake dhidi ya Husna Mwilima.

Catherine alifuatiwa na
Mary Chitanda ambaye alisema, "Mwenyekiti wewe ndiye umetuletea huyu mtu… sijui ulimwokota wapi halafu ukamleta humu ndani. Tuondoshee huyu hatumtaki."

Chitanda amenukiliwa akisema, "Yeye … kujipamba tu, hana jingine. Hajui kazi, hana lolote analolijua zaidi ya umbea na kutuibia fedha zetu. Tupishe bibi tufanye kazi zetu."

Taarifa zinasema Chitanda alifika mbali zaidi na kusema, "Hata kama watu watapeleka ujumbe kwa ‘bwana mkubwa,' kikao hiki ni cha mwisho, hakuna mwenye uwezo wa kutuingilia."

Ujumbe kwa "bwana mkubwa" umeelezwa kuwa ni ujumbe wa simu ya mkononi kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete ambao haikuwezekana kuthibitishwa.

Imedaiwa kuwa wakati wa kuporomosha matusi kwa Husna, kuna aliyepeleka ujumbe kwa Kikwete kueleza hali ilivyo ukumbini. Imedaiwa kuwa Kikwete aliandika juu ya ujumbe huo maneno, "Mtendeeni haki Katibu," na kuupeleka kwa kiongozi mmoja wa CCM.

"Mimi ninao hapa, lakini siwezi kukuachia unukuu. Unajua ninyi waandishi mna mengi," ameeleza mmoja wa wajumbe. Imeelezwa kuwa mmoja wa maofisa wa umoja huo aliusambaza kwa wajumbe wengi.

Baadhi ya wanaotajwa kusambaziwa ujumbe huo ni pamoja na Simba, Mary Chitanda, Catherine Nao na Nenburis Kimbele, mjumbe wa Baraza kutoka Arusha.

Hata hivyo Chitanda amenukuliwa akisema, "Haya mambo ni yetu sisi. Watu wanapeleka umbea kwa bwana mkubwa. Baraza hili ndilo lenye uwezo na mamlaka ya mwisho ya kuamua nini kifanyike, mwenyekiti muondoe huyu mtu…"

Ilikuwa baada ya mashambulizi haya, Husna aliomba kujibu tuhuma. Kwa mujibu wa mtoa taarifa, naye alianza kwa jazba akishambulia wenzake, lakini mjumbe Zaria Madabida ndiye amenukuliwa akisema, Husna "Anasakamwa kwa mambo yasiyokuwa ya msingi."

Source: http://www.mwanahalisi.co.tz/wanawake_uwt_wavuana_nguo

My take: Huyu hana elimu ya Ujasusi labda elimu ya umbea.Maneno yake yamekaa kimipasho na kukosa adabu lakini hata hivyo katika CCM kuna watu wengi wa aina hii.
 
My take: Huyu hana elimu ya Ujasusi labda elimu ya umbea.Maneno yake yamekaa kimipasho na kukosa adabu lakini hata hivyo katika CCM kuna watu wengi wa aina hii.
Seems she is such an untouchable and strong stooge!..
Nalilia picha yake tu!..anyone guys??!
 
Waandishi wa habari mliokutana na Chitanda hamjampiga hata picha moja siku zote hizi?
 
Bravo report, na sasa mambo haya yanazidi kuwa hadharani!
Mkuu, na wewe hukufanikiwa kupata picha yake?
Anyway, kesho nitakuwa na ka-camera kangu kwenye Maombolezo, naombea awepo nim'photo, naihitaji sana picha yake kwa kazi za intelijensia!

Mkuu sikuweza kuchukua picha ila sura lake bado liko kichwani nitajitahidi siku mbili tatu labda naweza kuibandika hapa.Unakumbuka ile issue ya Mkwere kukabidhi pikipiki za mafisadi wa EPA ?.Baada ya ile issue Mzee Mbonde aliondolewa akaletwa Mama Chitanda sasa kila mtu ndani ya ofisi ya CCM mkoa na Wilaya alikuwa anaonekana mbaya hata mkuu wa mkoa hakuwa na usemi mbele ya Mama siunajua hata yeye alishiriki kumdanganya mkwere akafungua Hotel baada ya siku moja tu uzio wa Hotel ukabomolewa.

Kiongozi pekee alieonekana ana uwezo wa kuondoa mauza uza ndani ya mkoa wa Arusha ni Mary Chitanda !!!!!.
 
Mary Chitanda kiboko, ha ha ha haaaaaa.

Kama nawaona vile hao waandishi wa habari wanavyotimua mbio baada ya kutimuliwa. hahahaaaaaa. Waandishi wa habari.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom