Charles tylor alikuwa cia

elmagnifico

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
8,260
9,704
Aliyekuwa Rais wa Liberia Charles Taylor
alikuwa na uhusuiano rasmi na shirika la
ujasusi la Marekani, CIA. Mwandishi wa gazeti moja nchini
marekani la Boston Globe, Bryan Bender,
ameiambia BBC kwamba imemchukua
miaka sita kupata jibu hilo kutoka kwa
shirika hilo la CIA Kulingana na mwandishi huyo, Bwana
Taylor alipotoroka kutoka jela moja mjini
Boston Marekani mwaka wa 1985, aliishi
nchini Libya, ambapo aliweza kutafuta
habari kuhusu marehemu Kanali Gadaffi
na kuwasilisha maelezo yake kwa shirika la ujasusi la Marekani la CIA. Bwana Bender amesema serikali ya
Marekani ilithibitisha kuwa uhusuiano
kati yake na Bwana Taylor ulianza miaka
ya themanini. Mwandishi huyo ameiambia BBC kwamba
shirika la ujasusi la idara ya ulinzi
limesema kuna stakabadhi nyingi za siri
zinazothibitisha uhusiano kati yao na
Bwana Taylor. Lakini shirika hilo halikutoa maelezo
zaidi kuhusu yaliyomo katika stakabadhi
hizo. Bwana Bender anasema aliwasilisha
ombi kwa shirika la ujasusi la idara ya
ulinzi na pia shirika la CIA miaka 6
iliyopita, akitaka kuelezwa ikiwa Bwana
Taylor alikuwa na uhusiano wowote na
mashirika hayo.
 
Back
Top Bottom