Jinsi ya kupika chapati laini na zenye ladha nzuri

Ha ha ha ha, mie nikipika zinasimama kama mfuniko wa sefuria

Nikimbambula nazo mtu anapata ngeu

Habari jf chefs,ninatatzo moja kila nikipika chapati za kusukuma zinakua ngumu nawakati mwingne znakatikakatika nataman nipike chapati yani ukiiweka mdomoni ufurah mwenyewe.plz nsaidieni nimsuprize huyu shemej yenu weekend hii afu namwekea na rost la maini
 
Umenchekesha kweli kongosho yani ata zangu znakuaga ngumu hadi aibu.nimeamua nanunua za mtaani cku hzi mana ni noma
 
Nashukuru sana kwa kumletea huu uzi manake uliexhost kila kitu.

ila kwa faida ya mtoa mada mapish kila siku huongezeka ufundi, na hapa nakupa dokezo tu ambalo nimeligundua kwenye upish wa chapati ni hili.

kandia mafuta ya moto hasa ukipata Kimbo, ama Kasuku yale ya mgando. pia tumia maji ya baridi wakati wa kukada. na kumbuka kukunja mistari midogo midogo ili upate layers wakati wa kupaka mafuta. na wakati wa kupika tumia moto mdogo sana usiwe mkali zikababuka. pia usukumapo basi sukuma kwa kuizungusha na izungushe kwa njia moja yaani toka ndani kwenda nje so ivutike kwa stail ambayo itachora duara lenye kontua toka ndani kwenda nje.
 
nashukuru sana kwa kumletea huu uzi manake uliexhost kila kitu.

ila kwa faida ya mtoa mada mapish kila siku huongezeka ufundi, na hapa nakupa dokezo tu ambalo nimeligundua kwenye upish wa chapati ni hili.

kandia mafuta ya moto hasa ukipata Kimbo, ama Kasuku yale ya mgando. pia tumia maji ya baridi wakati wa kukada. na kumbuka kukunja mistari midogo midogo ili upate layers wakati wa kupaka mafuta. na wakati wa kupika tumia moto mdogo sana usiwe mkali zikababuka. pia usukumapo basi sukuma kwa kuizungusha na izungushe kwa njia moja yaani toka ndani kwenda nje so ivutike kwa stail ambayo itachora duara lenye kontua toka ndani kwenda nje.

Asante sana kwa ushauri.ntaufanyia kazi
 
Chapati za kusukuma ni mtihani, nilishagaacha kuzipika mie lol
But kwa ushauri huu hapa nitajaribu tena

Umenchekesha kweli kongosho yani ata zangu znakuaga ngumu hadi aibu.nimeamua nanunua za mtaani cku hzi mana ni noma
 
Kuna njia tofauti za kukanda chapati zako zikawa laini, lakini siri kubwa ya kupata chapati nzuri ni kuukanda huo unga vizuri na ulainike.

Mahitaji basic:

1. Unga wa ngano
2. Chumvi
3. Sukari kidogo sana kwa ajili ya seasoning
4. Mafuta kidogo ya kukandia kulingana na unga wako, usijaze mafuta kibao
5. Maji - hapa inategemea na ukandanji wako mimi natumia maji ya baridi sana ikiwezekana nayaweka kwenye freeza kidogo yazidi kuwa baridii.

Mhitaji extraa:

Hapa ni kulingana na ufundi na uzoefu wako unaweza kuweka vitu vifuatavyo ukipenda lakini sio vyote waweza chagua kimoja

1. Tui la nazi (waweza kutumia kukandia unga badala ya maji
2. Maziwa - ukitaka kuongeza virutubisho kwenye mlo wako
3. Mayai - Na chapati inakuwa laini kama sufi, kwa sababu mayai hayafanyi chapati iwe ngumu kama ni hivyo basi hata keki zingekuwa ngumu kama jiwe.
4. Vitunguu maji - kwa ajili ya kuongeza ladha
5. Nyama ya kusaga au mboga mboga yoyote ile -kwa ajili ya kubadilisha aina za chapati sio kila siku ni chapati design ile ile tu.

Kwa basic Chapati -Stage 1:

1. Tia unga wako kwenye chombo au mashine yako ya kukandia.
2. Weka chumvi, na sukari kidogo kwa ajili ya seasoning
3. Tia mafuta kwenye unga (kwa mfano kwa unga kilo moja weka mafuta 1/4 kikombe)

4. Changanya vizuri mchanganyiko wako
5. Weka maji yako kwenye unga kidogo kidogo mpaka unga uchanganyike.
6. Unga ukishanyanganyika ukande mpaka ulainike.
7. Ukisha lainika weka kwenye friji kama nusu saa hivi, kama huna friji ufunike mahali pasipo na joto.

Stage 2:

1. Changanya unga wako vizuri kisha ukate madonge madogo madogo kiasi.
2. Chukua donge moja usukume kwenye kibao au juu ya meza iliyo safi.
3. Paka mafuta kidogo juu ya chapati yako uliyoisukuma, waweza kutumia samli au mafuta mazito kama samli.
4 Kunja chapati yako irudi katika umbo la donge tena. Hapa ndio key unaweza kufanya chapati yako ikawa ngumu au ikawa laini yenye layers.
5. Sukama tena donge lako ulilolikunja, anza na lile la kwanza.
6. Weka chapati yako kwenye chuma kikavu (frying pan) kilichopata moto, kisiwe cha baridi wala cha moto sana.
7. Ikiiva upande mmoja igeuze upande wa pili.
8. Ikishaiva pande zote weka mafuta kijiko kimoja tu kikubwa cha chakula kwenye chapati yako upande wa chini.
9. Ikunje hiyo chapati na uigeuze pande zote ipate mafuta, au waweza kuisuguasugua na kijiko chako kukahikisha upande zote zinapata mafuta na kuiva vizuri (inakuwa na rangi ya brownish)

10. Ondoa chapati yako kwenye chuma iko tayari kwa kuliwa.

Waweza kula peke yake, na chai, mchuzi wa aina yoyote ile au hata na maharagwe.

NB:
Waweza kukanda unga kwa kutumia mashine kama bread maker unachagua dough, kisha unaumonitor unga ukishakandika tu ndani ya 30 minutes unautoa ndani ya mashine na kuuweka kwenye friji kwa nusu saa. Au unaweza kukanda unga kwa kutumia mixer zile kubwa na unatoa dough maker.
Hii ni kwa wale wenye hizo mashine kama mimi. Kama huna mashine basi utaukanda unga wako kwa mikono hadi ulainike vizuri. Kulainika hapa sio kujaza maji, bali kutumia viganja vyako kuulainisha mpaka unga ukiupiga unavutika. Kisha unauacha uendelee kulainika kwa kuuweka kwenye friji.

ILANI: Mkishajaribu msinisifie mie maana hata mi nimeipata kwa KIJARUBA!
 
Ha ha ha ha, mie nikipika zinasimama kama mfuniko wa sefuria

Nikimbambula nazo mtu anapata ngeu

U made my day...upishi wa chapati kumbe majanga eeh......Once nilipita shuleni kwa mtoto na wazazi walijipikilisha nyumbani wakaleta vyakula shule. Kuna waarabu (sijui wapemba?) walileta chapati hizo zilitufanya wamama wote tujione upishi F! Walijitihadi kweli kutuelezea ufundi wake, siku zinapita nawauliza wenzangu jamani zile chapati vipi zililipa? Hakuna hata sura iliyokuwa na jibu la nuru....wallah tulitoka kapa....
 
Habari jf chefs,ninatatzo moja kila nikipika chapati za kusukuma zinakua ngumu nawakati mwingne znakatikakatika nataman nipike chapati yani ukiiweka mdomoni ufurah mwenyewe.plz nsaidieni nimsuprize huyu shemej yenu weekend hii afu namwekea na rost la maini

We mayenu chapati hizi hizi au zile nyingine! Ni PM tu mashaaalaaah.
 
Kuna njia tofauti za kukanda chapati zako zikawa laini, lakini siri kubwa ya kupata chapati nzuri ni kuukanda huo unga vizuri na ulainike.

Mahitaji basic:

1. Unga wa ngano
2. Chumvi
3. Sukari kidogo sana kwa ajili ya seasoning
4. Mafuta kidogo ya kukandia kulingana na unga wako, usijaze mafuta kibao
5. Maji - hapa inategemea na ukandanji wako mimi natumia maji ya baridi sana ikiwezekana nayaweka kwenye freeza kidogo yazidi kuwa baridii.

Mhitaji extraa:

Hapa ni kulingana na ufundi na uzoefu wako unaweza kuweka vitu vifuatavyo ukipenda lakini sio vyote waweza chagua kimoja

1. Tui la nazi (waweza kutumia kukandia unga badala ya maji
2. Maziwa - ukitaka kuongeza virutubisho kwenye mlo wako
3. Mayai - Na chapati inakuwa laini kama sufi, kwa sababu mayai hayafanyi chapati iwe ngumu kama ni hivyo basi hata keki zingekuwa ngumu kama jiwe.
4. Vitunguu maji - kwa ajili ya kuongeza ladha
5. Nyama ya kusaga au mboga mboga yoyote ile -kwa ajili ya kubadilisha aina za chapati sio kila siku ni chapati design ile ile tu.

Kwa basic Chapati -Stage 1:

1. Tia unga wako kwenye chombo au mashine yako ya kukandia.
2. Weka chumvi, na sukari kidogo kwa ajili ya seasoning
3. Tia mafuta kwenye unga (kwa mfano kwa unga kilo moja weka mafuta 1/4 kikombe)

4. Changanya vizuri mchanganyiko wako
5. Weka maji yako kwenye unga kidogo kidogo mpaka unga uchanganyike.
6. Unga ukishanyanganyika ukande mpaka ulainike.
7. Ukisha lainika weka kwenye friji kama nusu saa hivi, kama huna friji ufunike mahali pasipo na joto.

Stage 2:

1. Changanya unga wako vizuri kisha ukate madonge madogo madogo kiasi.
2. Chukua donge moja usukume kwenye kibao au juu ya meza iliyo safi.
3. Paka mafuta kidogo juu ya chapati yako uliyoisukuma, waweza kutumia samli au mafuta mazito kama samli.
4 Kunja chapati yako irudi katika umbo la donge tena. Hapa ndio key unaweza kufanya chapati yako ikawa ngumu au ikawa laini yenye layers.
5. Sukama tena donge lako ulilolikunja, anza na lile la kwanza.
6. Weka chapati yako kwenye chuma kikavu (frying pan) kilichopata moto, kisiwe cha baridi wala cha moto sana.
7. Ikiiva upande mmoja igeuze upande wa pili.
8. Ikishaiva pande zote weka mafuta kijiko kimoja tu kikubwa cha chakula kwenye chapati yako upande wa chini.
9. Ikunje hiyo chapati na uigeuze pande zote ipate mafuta, au waweza kuisuguasugua na kijiko chako kukahikisha upande zote zinapata mafuta na kuiva vizuri (inakuwa na rangi ya brownish)

10. Ondoa chapati yako kwenye chuma iko tayari kwa kuliwa.

Waweza kula peke yake, na chai, mchuzi wa aina yoyote ile au hata na maharagwe.

NB:
Waweza kukanda unga kwa kutumia mashine kama bread maker unachagua dough, kisha unaumonitor unga ukishakandika tu ndani ya 30 minutes unautoa ndani ya mashine na kuuweka kwenye friji kwa nusu saa. Au unaweza kukanda unga kwa kutumia mixer zile kubwa na unatoa dough maker.
Hii ni kwa wale wenye hizo mashine kama mimi. Kama huna mashine basi utaukanda unga wako kwa mikono hadi ulainike vizuri. Kulainika hapa sio kujaza maji, bali kutumia viganja vyako kuulainisha mpaka unga ukiupiga unavutika. Kisha unauacha uendelee kulainika kwa kuuweka kwenye friji.

ILANI: Mkishajaribu msinisifie mie maana hata mi nimeipata kwa KIJARUBA!

Asante kwa somo zuri, japo bachelor ila ntajaribu
 
Yaani mimi hakuna mlo naupika fasta na fresh kama chapati!
just maji ya baridi,mafuta ya baridi,chumvi kiasi,pilipili manga ukipenda,kijiko kimoja cha blue band,unga kg 1

mix vyote,weka maji nusu kikombe(unaweza kukandia tui la nazi kwa ladha ya ukweeen!)kanda kwa dk kadhaa!

ukishalainika uache kidogo kama dak 10 hv!
gawa madonge(kg ya unga inatoa chapati 9 kubwa)
kisha sukuma huku thn weka mafuta yasambaze kwa kijiko kisha kunja kama tairi hvi!

maliza madonge yote thn anda chuma chako(kwa uzoefu wangu kile chuma cheusi kile ndo hatareee kwa chapati nzuri sio fyrn pan zenu zile za supermarket)
weka chapati yako kavu bila mafuta,ikishageuka rangi pande zote mbili weka mafuta,mafuta kidogo wakati wa kupika ndo ulaini wa chapati utakavokuwa long last!)

NB
unga unavokuwa mlaini ndo chapati zinakuwa ngumu!
ukiwa mgumu ndo chapati zinakuwa laini!

maji ya moto yaivisha unga unakuwa kama umechemshwa!(nionavyo mimi)
unga ukiwa wa kuvutika unatengeneza chapati zinakuwa kama unakula bg gee!kwa mpishi unajua tu nimechemsha!
wasalaam!
 
Chapati hapikwi, ya kaangwa
Chapati yachomwa haikaangwi. Nacheka na jibu la kongosho eti mfuniko wa sufuria akikupiga nao unatoka ngeu. Chapati ni mlo rahisi na mwepesi kuandaa ukifuata instructions. Mimi kila jumamosi napika chapati za kifungua kinywa jumapili asubuhi na mlo wa jioni siku ya jumatatu baada ya kazi.
 
Nataka kujua kupika chapati za kusukuma zenye backing powder mayai na blue bend kuna sehemu nilikula zilikuwa nzuri sana ila sijui kuzipika.
 
Similar Discussions

14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom