Napenda sana chapati

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,801
59,274
Nazitamani chapati. . .chapati za kusukumwa wala so za mayai. . .
Za kupika mwenyewe. . .wala so za jirani hata kama zimepikiwa chai. .

Bwana akishaenda shamba. . nami nifunge kibwebwe. .
Nende lilipo duka. . . .

Ahhhhh vina haviji ila nazitamanije. Natamani ningekaa chini nikande unga lainiiiii ulotiwa chumvi kidogo na maji ya uvugu vugu tu basi. Niuchanganye mpaka niridhike.

Nitie mafuta kwenye bakuli na kijiko ndo nianze kukata kipande kimoja kimoja na kusukuma, nikimaliza nikipake mafuta king'ae. Nikisukuma yasimwagike mwagike maana sijazidisha. Nivipange vipande vilosokotwa kwenye sahani au sinia lilonyunyuziwa unga kwa mbali.

Nikishasokota zote niandae chakugeuzia pia chakuwekea na kufunikia. Niwashe jiko langu kisha niweke frying pain yangu juu yake. .
Nianze kusukuma tena na kuziweka jikoni moja moja. Zikianza kupata rangi nizipake na mafuta. . .nizigeuze mara mbili mpaka rangi ipendeze. Niziweke kwenye chombo kisha nifunike kwa muda. Zilainike vizuri ndio nijisevie kwa mchuzi wa nyama au maharage yaloungwa kwa nazi. Nikizikata zichambuke mpaka nione raha.

Haki ningekua sijajikata kidole leo ningezikaanga hata usiku.

Wapi wapenzi wa chapati. . . . . .?
 
Lizzy karibu kwangu hiyo menu inahusika sana leo. Napenda sana chapati. Si asubuhi, mchana ama jioni. I just love them!

Amy embu niambie umepika na mboga gani. . .
Na kama ni chai usiache kutia viungo.
 
Last edited by a moderator:
Kupika sijui. Napenda kuzila tu. Chapati tamu sana.
tangu lini ukajua kula chapati mbara wewe?
kisha muulize Lizzy kuhusu mapishi ya chapati kama anayaweza kweli au anapiga talalalila tu hapa maana ni shughuli pevu yahitaji olive oil ili mapishi yawe muruwa.
 
Last edited by a moderator:
tangu lini ukajua kula chapati mbara wewe?
kisha muulize Lizzy kuhusu mapishi ya chapati kama anayaweza kweli au anapiga talalalila tu hapa maana ni shughuli pevu yahitaji olive oil ili mapishi yawe muruwa.

Bishanga shughuli yake naifahamu. . .siku nikipika lazima naniii awepo ili massage iweke kiuno na mgongo sawa.
 
Last edited by a moderator:
chapati zipi?

Mie nataka mkate wa kumimina
nikipata na chai ya mchaichai ya maziwa

natoa mkeka varandan
chakula kifunikwe kwa kawa lenye urembo

mlaji avae msuli na fulana
rahisi kwa kupitisha hewa

ale huku nikimpepea
na vicheko vikiendelea

mkate wa kumimina kiboko.
 
chapati zipi?

Mie nataka mkate wa kumimina
nikipata na chai ya mchaichai ya maziwa

natoa mkeka varandan
chakula kifunikwe kwa kawa lenye urembo

mlaji avae msuli na fulana
rahisi kwa kupitisha hewa

ale huku nikimpepea
na vicheko vikiendelea

mkate wa kumimina kiboko.

Chai ya mchai chai tu ngoja nikakupikie. . .mkate ntakununulia.
 
kweli nipikie jamani.

Akipatikana kuku wa kienyeji rost itakuwa bonus.

Inakuja sasa hivi Konnie. . .
Alafu hivi mjini (Dar, Atown, sijui na wapi wapi) unaweza ukapata mchai chai? Alafu kuku wa kienyeji. . . .dah lazima kesho nile maini ya kuku.
 
Kila ninapoishi lazima kuwe na ndoo nimepanda mchai chai, miti angalau 3 ya mipapai, na kuku hata 10 tu lol.

Inakuja sasa hivi Konnie. . .
Alafu hivi mjini (Dar, Atown, sijui na wapi wapi) unaweza ukapata mchai chai? Alafu kuku wa kienyeji. . . .dah lazima kesho nile maini ya kuku.
 
Back
Top Bottom