Chanzo cha mto Nile kipo Tanzania?

Lakini the mammoth reservoir ya hilo lake hata kwenye ramani tu ipo Tanzania, au siyo? A bit more than half of the lake is in Tanganyika. the rest is divided between Kenya and Uganda.

TZ na Ug hazitofautiani sana. TZ ni asilimia 49, Ug 45 na Kenya wana 6%
 
Bi Faiza kila kitu ni Kikwete tu? Tayari ushaanza kupindisha mada toka source ya Nile kuwa mdahalo wa ufanisi wa Kikwete.... heeee huo sio upambe tena .... it borders on maniacal reverence!!

Just so as you know, nilinunua nyumba K'nyama 1995, kivutio kimojawapo ni kuona kuna bomba la maji nje (free public water) linatoa maji masaa 24 seven days a week!! Kwa miaka saba iliyopita, toka aingie huyo mheshimiwa madarakani, tuna bahati kupata maji mara mbili kwa wiki kwa mda usiozidi saa mbili. Tunaamka saa tisa za usiku kungojea kupump maji.

Sasa nijuavyo na nilivyosoma, source ya Nile, iko toka mto Kagera kuingia Lake Vic.
Ukiwa angani kwenye ndege, unaweza kutofautisha kabisa rangi za maji ikionesha mto unaenda katikati ya ziwa na kumalizikia Jinja, out as the white nile. Nimeona hivyo kwa macho yangu enzi za late 70's. nikiwa na mkufunzi wangu.
Maji ya mto yana rangi kidogo na ya ziwa yako more clearer!

Hiyo si kijitonyama hiyo labda kijitomboga.
 
White Nile imeanzia ziwa Victoria na Blue Nile imeanzia ziwa Tana. White Nile iko upande wa Uganda, maji yanatoka ziwa Vic toria na kuingia mtoni sijui mtu anaposema maji ya Tanzania au ya Uganda anatumia kigezo gani wakati maji hayo yanatoka ndani ya chombo kimoja ambacho ni Ziwa victoria. Kumbuka kuwa WATER ALWAYS FINDS ITS OWN LEVEL. Ukichota maji mengi upande wa Tanzania kama ilivyo bomba la kupeleka maji Shinyanga, dhahiri maji ndani ya ziwa victoria yatajirekebisha kupata LEVEL yake hivyo yatahama kutoka upande mwingine kuja kujaziliza pale yalipochotwa. Kuna alama zimewekwa ziwani zenye onyo kuwa IT IS DANGEROUS TO BEYOND THIS POINT. Ambapo ni mkondo wa maji yanapoanzia kuwa na mwendo kuingia mto Nile.
 
White Nile imeanzia ziwa Victoria na Blue Nile imeanzia ziwa Tana. White Nile iko upande wa Uganda, maji yanatoka ziwa Vic toria na kuingia mtoni sijui mtu anaposema maji ya Tanzania au ya Uganda anatumia kigezo gani wakati maji hayo yanatoka ndani ya chombo kimoja ambacho ni Ziwa victoria. Kumbuka kuwa WATER ALWAYS FINDS ITS OWN LEVEL. Ukichota maji mengi upande wa Tanzania kama ilivyo bomba la kupeleka maji Shinyanga, dhahiri maji ndani ya ziwa victoria yatajirekebisha kupata LEVEL yake hivyo yatahama kutoka upande mwingine kuja kujaziliza pale yalipochotwa. Kuna alama zimewekwa ziwani zenye onyo kuwa IT IS DANGEROUS TO BEYOND THIS POINT. Ambapo ni mkondo wa maji yanapoanzia kuwa na mwendo kuingia mto Nile.

Dangerous to what?
 
Chanzo cha mto nile ni ziwa Victoria, ziwa Victoria limegusa hadi Uganda, so ukisema mto nile unaanzia Uganda upo sahihi coz umeanzia ziwa Victoria na ziwa Victoria limegusa sehemu ya Uganda, matumizi ya maji ya mto nile kwenda Shinyanga nafikiri ilikuwa hofu ya wa misri kuwa kutokana na bonde la ufa huenda maji mengi yakatiririka kuelekea mikoa ya shinyanga, singida na Dodoma hivyo kusababisha kupungua kwa kina cha maji cha mto nile kule misri ambao ndo roho ya wa misri,
 
Kwa nini Watanzania wengi hatuwezi ku-explain masuala scientifically bila kumhusisha Mungu? Kwenye huu uzi tumeambiwa Mungu ana-reside Tanzania. Tukaambiwa chanzo cha mto Nile ni ziwa Victoria.

Halafu tukaambiwa kuwa Kikwete ndo aliyefanya "ubabe na kuyavuta [maji ziwa Victoria na] kuyapeleka Shinyanga na Sasa Tabora na kwingine....Kikwete ... akasema aahh, ujinga huu, watu wetu wana shida ya maji, maji yako kwetu, halafu tusiwapelekee? akaamuru miradi ianzishwe na watu wapelekewe maji. Naam, sasa hivi tunaona maji yakisambazwa kutokea Victoria kwenda Shinyanga na Tabora kwa ubabe wa Kikwete."

Sasa wewe unasema chanzo cha mto Nile ni "topic nzito Sana and it needs a bible of explanation". Sitashangaa wewe au mtu mwingine kuja na bible explanation hapa kuwa Bibilia inasema pia mto Nile utakauka kwani ni kweli Bibilia inasema hivyo (Isaiah 19:5, Ezekiel 30:12, Zechariah 10:11).

Utakauka kivipi? Atadai Bibilia inasema ziko njia nyingi za huo mto kukauka (Isaiah 11:15). Kwamba Mungu mwenyewe anayedaiwa ku-reside Tanzania anaweza kuukausha mwenyewe au atatokea mtu na kubadilisha mkondo wa mto kama historia inavyoonyesha pale Darous alivyovamia Babylon na kubadilisha mkondo wa Euphrates.

Au kama Hezekiah alivyofanya kwenye 2 Chronicles 32:3 (He consulted with his officials and military staff about blocking off the water from the springs outside the city, and they helped him).

Hapa wanaotumia "bible explanation" waunganisha dots na kutakuta kwamba lawama zote za kukauka kwa Nile zinaweza kumwangukia Kikwete kwa kuwa mbabe kuyavuta maji na kuyapeleka Shinyanga, Tabora na kwingineko.

Halafu utakuta wanatoa hiyo "bible explanation" wanatoka huko huko S
hinyanga, Tabora na kwingineko Kikwete alikovutia maji kutoka chanzo cha mto Nile na kusababisha huo mto kukauka.

labda watasema litajitokeza lishetani likubwa sana na litakunywa maji yote ya ziwa Victoria hadi likauke, (dini ni chombo cha kupumbaza akili za watu)
 
Bibie FaizaFoxy maneno mazito sana karibu yanitoe machozi.Tunakosa uongozi laiti tungefanikiwa kupata uongozi bora hakika tungekuwa mbali sana.

Kuna Mjapan mmoja alikuja Tanzania katika kutayarisha dissertation yake ya PhD kuhusu anthropology, ilikuwa akae miezi sita akakaa miaka 6. Aliporudi kwao akaulizwa, vipi Tanzania mbona umekaa sana? Akasema, Tanzania ni nchi ya ajabu sana, kwanini? akajibu nilipotoka Japan kwenda Tanzania nilikuwa siamini kama Mungu yupo, sasa naamini Mungu yupo tena yupo Tanzania...
 
Last edited by a moderator:
Kuna kipindi tz ilitaka kuyatumia maji ziwa victoria kwa ajili ya matumizi ya majumbani basi nchi ya misri na sudani pamoja na ethiopia zikazua vikwazo sasa wewe unayebisha source ya nile ni victoria haya tuelezeni source zenu

Hao uliowataja hapo ni kweli walilalamika, but hilo haliwezi kuwa hitimisho kwamba source ya mto nile ni lake victoria.

Na wao kukataza maji kutumika sana sio kosa kwa vile maji yakipungua sana ziwa victoria itafanya amount fulani ya maji kutokwenda kule but hiyo haitakua na maana kwamba maji ya ziwa victoria yasipokwenda kule ule mto utakauka!!!!!

Just jiulize maji ya ziwa victoria yanakuwaje chanzo cha ule mto?

Na kama victoria ni chanzo, kwanini na Kenya isijitangaze kuwa ni source ya ule mto? Au Kenya haihusiani na ziwa victoria?

Ivi haujiulizi kwamba Uganda inajitangaza ni source but licha ya kujitangaza kwao hawasemi Lake Albert ndio source? Unajua kwanini? hicho chanzo kiko kilomita kadhaa kabla ya lile ziwa. After all Lake Albert lenyewe likijaa linapeleka maji kwenye vile vyanzo.

Na jee haujiulizi Kwanini Uganda haisemi source ya mto nile iko lake kyola? wakati lake kyola likijaa ndio linapeleka maji ziwa Albert!!!!!

Sasa Ziwa vitoria likijaa ndio kwanza linapeleka maji Lake kyola.

Si umeona mzunguko huo??????

Angalia na picha.

327px-River_Nile_map.svg.png


Before lake Albert, kutoka juu (north lake albert) ndio kuna chanzo cha moja kwa moja kinachopeleka maji mto nile, chanzo hicho hakitegemei maji kutoka lake albert, lake kyola wala lake victoria ingawa maziwa hayo YAKIJAA ndio yanapeleka maji kwa hiko chanzo kinapeleka maji.

Sipendi kuhitimisha but kusema kina Egypt, Sudan na Ethiopia walilalamika haifanyi Ziwa victoria kuwa chanzo.

Unless uelezee vizuri, na sio tu kulazimisha watu waamini coz of malalamiko huku mwenyewe ukilalamika watu sio waelewa. Hapa hatubishani, ukiwa na data weka utaeleweka tu.
 
Bibie FaizaFoxy maneno mazito sana karibu yanitoe machozi.Tunakosa uongozi laiti tungefanikiwa kupata uongozi bora hakika tungekuwa mbali sana.

Naam, hata nilipolileta hapa si wengi walionielewa.

Naona hata wewe dhanna yake imekupiga chenga, haihusiani na viongozi wala uongozi, na huo ndio ujinga wa Watanzania wengi, kutegemea uongozi na viongozi wawafanyie kila kitu, hayo ni mawazo yaliyojazwa (brain washed) na ambao walikuaminisha na wewe umeamini mpaka leo hii kuwa lazima uwe na kiongozi, kwanini wewe mwenyewe usiwe kiongozi wako?

Kuna uongozi zaidi ya Mwenyeezi Mungu? Fikiri.
 
JAMANI, kuna vigezo vingi vya kutumia ku-define source ya Mto; ukitaja Nile ndo unaongeza confussion zaidi kwani mto huo unajulikana kuwa unatoka ziwa Victoria na Exit point iko Uganda.
Lakini, ziwa limeanzia wapi? au mtiririko wa maji yaendayo Nile umeanzia wapi? Je ni mwisho wa ziwa? au mwanzo wa mto unaotiririsha maji mengi?
Kwa kanuni za kijiografia Chanzo cha Mto Nile kiko Burundi. Ndio farthest point ya mto unaotiririsha maji kupitia mito ya Ruvuvu pale Ngara na mto Kagera hadi ziwani. UNFORTUNATELY HUU NDIO UKWELI. Ulichotueleza wewe ni hao wazungu bila shaka kufika mwisho wa ziwa in relation to the Nile exit point (unavyotoka ziwani). Hakuna cosideration ya mito inayoingia ziwani hapo.
Kuhakikisha ninachosema, ukibahatika kupita juu ya ziwa hilo kwa ndege hasa wakati wa mvua (mfano ukitokea Kinshasa- Nairobi) utaona jinsi maji yenye rangi ya udongo ya mto Kagera yanavyopita ziwani moja kwa moja kuelekea exit point ya Nile karibu na Entebe ambayo waganda wanasema ndio source ya Nile.
Ukweli hapana, Source ya Nile ipo milima ya Burundi. Ndio maana hata Buja kuna hoteli kubwa inayoitwa SURCE DU NILE (source of Nile)
Nawasilisha Mkuu.
 
Ukisoma historia ya chanzo halisi cha mto Nile hakuna jibu sahihi isipokuwa utapata vyanzo vikuu viwili ambavyo ni White n' Blue Nile na mlolongo wa nchi...

Kwa kuzingatia hilo ndio maana kuna mapatano ya nchi zote za bonde la mto Nile hata zile ambazo mto umepita tu...

Wanajiografia wanapoongelea chanzo cha mto wanaongelea tributary ndefu zaidi. Kwa hivyo, katika kuongelea chanzo cha mto Nile, chanzo kinachotafutwa ni cha White Nile, sio Blue Nile.
 
Mto Kagera ndo chanzo cha mto Nile,mito mingi midogo midogo iliyoko kagera kwa upande wa Tanzania kama Mto ngono na mito midogo midogo kwa upande wa Burundi na Rwanda ndiyo uingia mto Kagera kisha Nile.Kwa wale ambao wameishafika sehemu ya Lukunyu mto Kagera unapoingilia Ziwa victoria watakubaliana na mimi kuwa mto huu umejitenga na na unaonekana jinsi unavyotambaa juu uso wa maji ya Ziwa Victoria.Maji ya Mto Kagera yanakusanya uchafu mwingi na ragi ya udogo hivyo utayona yakipita juu ya ziwa hilo,hata wavuvi ukuta na mto huu katikati ya Ziwa.Mto huu utokea upande wa Uganda pale Jinja.Ndo maana hata mkataba wa Cairo wa utumiaji wa maji ya mto Nile umejumuisha mto Kagera
 
ETM kuna tofauti kati ya bible explanation na Biblical explanation. Jamaa alitumia bible explanation akimaanisha bulkness of information.
 
River Nile unajazwa na mikondo mingi na mitiririko mingi na vyanzo vingine vya maji kama milimani na mabonde lakini chanzo chake kila explorer anakuja na yake mnamo mwaka 140 CE Ptolemy alisema umeanzia milima ya Ruwenzori Uganda halafu John Speke akasema umeanzia lake Victoria sasa dawa ni kuchukua mtumbwi nianzie Egypt najua ntafika tu kwenye chanzo
 
Point hapa ni hii Uganda wanajitangaza na wanapata watalii wengi kwenda kuona chanzo cha Nile
sasa kama tunacho sisi mbona tuko kiimya?

hadi wazungu ndo waseme?
hatuoni faida za hili jambo kitalii?

Ngoja wakitoka huko Zanzibar kwenye kikao chao cha kujadili ulaji mwingine wa Octoba halafu wakapitia hapa huenda wakakupa jibu!
 
Back
Top Bottom