Chanzo cha matatizo yote ya Tanzania ni JK

Si kweli Rais hawezi kulinda waovu lakini pia Serikali haiongozwi na kila mtu akiamka simamisheni Jaifo, Lumbanga, Mponda kuna taratibu zake kwani kuna mihimili 3 Mahakama, Bunge na Serikali hivi haviingiliani.Lakini kila Kikao kikao cha Bunge lazima hoja lazima kiongozi aambiwe JIUZULU kazi ya Bunge ni kutunga Sheria na kushauri sio kulazimisha au kusema Waziri Mkuu jiuzulu itafuata sasa Rais ambapo naye atavunja Bunge hapo lengo ni nini? Wabunge wengi wamesoma Public Law hata kidato cha 2 somo la Uraia, Magazeti leo yamedokeza Mtaalam wa Siasa UDSM Bw Bana.amesema Bunge ni kutunga. Sheria ntalifuatilia Gazeti hilo namalizia nihukumiwe lkn sio Wabunge wawasimamishe Waziri mkuu au Mawaziri wote 8 wao ndio wamewachagua? Rais atalibadili tu baadhuu ya sura hilo Baraza kabla ya June 12

Mkuu hiyo mihimili unayosema zipo kinadharia tu, kiuhalisia tayari uhuru wao umeshabakwa na mtu moja ambaye ni rais anayetuhumiwa katika kila idara.
Hizo taratibu unazozisema kwamba lazima zifuatwe ingekuwa sawa kama mihimili yote ina uhuru wa kutoa maamuzi.
Kilichopo ni kwamba rais anajua hata kama utaenda kushtaki mahakamani, mahakama inatoa hukumu kwa maelekezo ya rais.

Amka Mkuu umeshaliwa mchana kweupe
 
Msitafute mchawi, raia milioni 40 tushindwa kumuwajibisha mtu 1?!. Tuendelee kutulia tunyolewe mana WOGA WETU NDIO UMASIKINI WETU
 
Kinachotakiwa ni viongozi wa kisiasa waache woga wawaambie wananchi nini cha kufanya ili kuondoa haya majambazi, dr.slaa, lipumba, mbatia wasimumunye maneno watamke wazi.Nchi inaangamia kwa kukosa maarifa

Naamini wanakusikia. Lipumba elewa tatizo sio malipo ya pili ya korosho tu kule Tandahimba. Tatizo ni mfumo mzima unaolea wezi na mmiliki wa huo mfumo. Ili kuua huu mfumo inabidi kuanza na umiliki na kisha mfumo.

Hebu Basi, Slaa W.P, Lipumba I, Mbatia J. Lyatonga M.A. fanyeni hima kuwaamsha watu, nchi inabaki mifupa, rasilimali zinabebwa mchana kweupe.

Msipofanya haya sasa, pindi mnapoingia madarakani mtakuta rasilimali zote wamebeba.
 
Nauunga mkono hoja, Marehemu BB/ wa Taifa alisema hawezi kuongoza,pamoja na rafiki yake EL, sasa wakina Mwinyi, Ngombale, kinana nawengine, 2005 wakajifanya hawajui aliyo yasema BB/ wa Taifa mwka95 japokua Mkapa(M/kiti)wakatihuo alifurukuta lkn alizidiwa, matokeo yake tukapata kiongozi mwenye sifa ya 'SURA NZURI' Tunategemea nini? Watz wakati umefika tuamue kuwatoa kwa nguvu kutumia nguvu ya UMMA hao watawala
 
Si kweli Rais hawezi kulinda waovu lakini pia Serikali haiongozwi na kila mtu akiamka simamisheni Jaifo, Lumbanga, Mponda kuna taratibu zake kwani kuna mihimili 3 Mahakama, Bunge na Serikali hivi haviingiliani.Lakini kila Kikao kikao cha Bunge lazima hoja lazima kiongozi aambiwe JIUZULU kazi ya Bunge ni kutunga Sheria na kushauri sio kulazimisha au kusema Waziri Mkuu jiuzulu itafuata sasa Rais ambapo naye atavunja Bunge hapo lengo ni nini? Wabunge wengi wamesoma Public Law hata kidato cha 2 somo la Uraia, Magazeti leo yamedokeza Mtaalam wa Siasa UDSM Bw Bana.amesema Bunge ni kutunga. Sheria ntalifuatilia Gazeti hilo namalizia nihukumiwe lkn sio Wabunge wawasimamishe Waziri mkuu au Mawaziri wote 8 wao ndio wamewachagua? Rais atalibadili tu baadhuu ya sura hilo Baraza kabla ya June 12

Wewe kweli umepinda na huwezi nyooka tena!! je unaweza niambia majukumu matano ya bunge la Tanzania...inaeleka unatunga ngonjera hapa...Ashiiii
 
Tumeacha kusikiliza ushauri wa wataalamu. Tunasikiliza ushauri wa waganga wa kienyeji....yaani Afrika tuna safari ndefu sana.
 
sehemu kubwa ya watanzania akili zimeoza na ndio chanzo cha matatizo kazi kupiga domo tu rais mmemuweka wenyewe mliona anafaa leo ooh rais ndio tatizo mambo magumu dunia yote ongezeni juhudi kupambana na umaskini

Hapana akili zetu hazijaoza umekosea tunahitaji mtu wa kutoa amri, hata vitani kuna amiri jeshi anayeruhusu sasa nchi iingie vitani.Nenda kawaambie viongozi wa upinzani waseme kitu then wanachi watafuata
 
Nashindwa kuelewa kwa nini, pamoja na ukweli wote huu ulio wazi mchana kweupe, watu wanashindwa kumsema. Hata yule aliyepitisha karatasi wabunge wenzie wasaini anajua vizuri mno kuwa Kikwete na si Pinda ndiye tatizo kuu na la kwanza, lakini kwa vile ni kabwela mwenzie, wala hajamgusa, ni unafiki mkubwa mno.

harafu wanawasingizia wazee wa dsm eti ndio wamemshauri
 
Ni kweli kabisa uliyosema, hata Dr. Slaa alionya wakati wa kampeni za 2010 kuwa kumrudisha JK ni janga kwa nchi yetu. Na mimi nasema JK ni Janga la Kitaifa.Ni utaahira tu kumpamba huyu mtu kwa sifa za kijinga.
 
Ndugu zangu ni kweli swala la kujiuzuru kwa naibu, waziri au waziri mkuu hilo halipo kabisa! hii ni kwasababu kikwete ameshauriwa na wazee wa busara pale Ikulu kwamba huo ni upepo wa kisiasa na utapita kama matukio mengine hivyo asihofu mambo yatatulia baada ya muda. Pia wameshauri wabunge wote wa CHUMBA CHA MAITI (CCM)waitwe waeleweshwe na kwa wale watakaopinga wapelekewe majina yao wao wanajua namna ya kuwatuliza. baada ya hapo hata waziri mkuu mwenyewe aliridhika kisha akapata nguvu ya kwenda kuahirisha bunge kwa kupotezea ushauri wa wabunge. naomba kuwakilisha.

Umejuaje? Ukifuatilia leadership ya Tanzania imejengwa katika misingi ya Uchief. Walikokuwa wanautoa uchief mababu zetu ndiko wanakoutoa uongozi majority ya viongozi wetu (asomaye na afahamu). Kila taifa linatengeneza misingi ya kitaifa na waliotutangulia.
 
Dr.slaa CDM tayari imeshaimarika, hatuoni haja ya yeye kuzunguka nchi nzima kwa sasa kuimarisha chama, kilcho mbele yake Dr. slaa ni kuwakumbusha watanzania kwamba" Niliwaambvia wakati wa uchaguzi kuwa kuchagua CCM ni kukaribisha maafa sasa aseme watanzania wafanye nini. Muda unatutupa mkono majambazi yanazidi kupora.DR.slaa pleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeease say just a word and so kinuke sasa hivi
 
nakuunga mkono mkuu kwa 100%,ukiona jinsi mawaziri waliotakiwa kujiuzulu walivyokuwa na confidence kukataa kujiuzulu,utagundua kabisa,this man is supporting theis corruption!

you are very right br. Huyu jamaa amekuwa ni chanzo cha nchi yetu kuzidi kudidimia kiuchumi. Yeye na watendaji wake wako kwenye ziwa la utajiri wetu wakitafuna nchi huku taifa na wananchi wakigugumia kwa maisha magumu. Vielelezo ambavyo hata layman ataviona kuhusu jk alivyo na awkward leardeship ni;

kukosa uaminifu kwa taifa na kuteuwa watafuna nchi badala ya waleta maebndeleo.

1. Baraza la mawaziri walinaoliangamiza taifa ni chaguo la raisi na anawalinda. Katika hili tumeshuhudia mara nyingi anavyowatetea wakati ukweli ukiwa wazi. Anamkomoa nani ktk hili? Mwananchi mtanzania

2. Makatibu wakuu wote waloikubuhu kwa ufisadi wa kutisha ni chaguo la jk . Kashfa nyingi zimeripotiwa kuhusiana na makatibu mbalimbali wa wizara na idara mbalimbali nani atakayewatoa angali wanalindwa na jk?

3. Wakurugenzi wa mashirika,halimashuri,taasisi za serikali na mamlaka mbalimbali ni chaguo la jk. Tunazo kashfa ngapi zinazohusiana na hawa ngudu? Because of jk, hakuna kuwawajibisha.

4. Wenyeviti wa bodi mbalimbali na mamlaka -wateule wa huyu huyu dhaifu

5. Wengine wamepewa/kuajiriwa kwa upendeleo wa kumjua huyu hyu mtu na ndo wameboronga mpaka sasa nchi inaangamia. Wantoa sababu za kijinga e.t mdororo wa uchumi duniani,mara mfumuko wa bei, mara hichi mara kile, kini still chanzo ni nini?
Jk na serikali yake dhaifu. Hana uwezo wa kupambanua mambo zaidi ya kuongea kama taahira akitakiwa kuongelea mambo ya msingi
mfano ni pale aliposema hajui kwa nini tanzania ni maskini, maisha bora kwa kila mtanzania, ari zaidi,kasi zaidi,nguvu zaidi, failed kilimo kwanza, e-laerning kwa shule zote za tanzania, good governance, na mengineyo manyoyajua.
Katika hili kwa mwenye akili timamu ni lazima atekeleze alichokitamka na anachokisimamia.
 
sehemu kubwa ya watanzania akili zimeoza na ndio chanzo cha matatizo kazi kupiga domo tu rais mmemuweka wenyewe mliona anafaa leo ooh rais ndio tatizo mambo magumu dunia yote ongezeni juhudi kupambana na umaskini
Kuwa Great thinker japo kidogo. Mbona inapotokea mambo yanakwenda vema duniani huwa hatuoni matokeo yake nchini kwetu? Ila yakienda kombo utasikia "Hii hali ni kwa sababu ya msukosuko wa uchumi duniani kote". To HELL!! Hebu jiulize

  • Kupakia Twiga, Tembo n.k kwenye ndege ni kwa sababu ya mambo magumu duniani,
  • Kuua reli ili malori yenu yapate kazi ya kusafirisha mizigo ni kwa sabubu ya mambo magumu duniani,
  • Kuua bandari a Tanga ili wajanja wa Dar waendelee kutesa ni kwa sabubu ya mambo magumu duniani,
  • Kuuza bandari ya Mtwara ni kwa sabubu ya mambo magumu duniani,
  • Jairo na Uwajibikaji ni kwa sabubu ya mambo magumu duniani,
  • Richmond ni kwa sabubu ya mambo magumu duniani,
  • Meremeta, TanGold, Kagoda ni kwa sabubu ya mambo magumu duniani,
  • Ufisadi kwenye Tamisemi ni kwa sabubu ya mambo magumu duniani,
  • Safari zisizo na ukomo za Rais wako ni kwa sabubu ya mambo magumu duniani,
  • Kuua shirika la ndege wakati Precision ikistawi katika mazingira hayo hayo ni kwa sabubu ya mambo magumu duniani,
  • Mrahaba mdogo kwenye madini ni kwa sabubu ya mambo magumu duniani,
  • Stimulus package fraud ni kwa sabubu ya mambo magumu duniani,
  • Mabilioni ya JK ni kwa sabubu ya mambo magumu duniani,
  • Ukosefu wa madawati wakati 50% ya nchi ni misitu ni kwa sabubu ya mambo magumu duniani,
  • Ukosefu wa walimu wakati nchi ina rasilimali watu zaidi ya milioni 40 ni kwa sabubu ya mambo magumu duniani,
  • Na mengine mengi............

Ndio haya tunayosema kuwa tatizo la pili ni wananchi wenyewe kuwa bongo lala. Tunasumbuliwa na ujinga tu. Ukishapewa Ukatibu kata basi huo ni mtaji tosha wa kukuwezesha kudai rushwa na mfumo huu ni safi kwako.
 
Si kweli Rais hawezi kulinda waovu lakini pia Serikali haiongozwi na kila mtu akiamka simamisheni Jaifo, Lumbanga, Mponda kuna taratibu zake kwani kuna mihimili 3 Mahakama, Bunge na Serikali hivi haviingiliani.Lakini kila Kikao kikao cha Bunge lazima hoja lazima kiongozi aambiwe JIUZULU kazi ya Bunge ni kutunga Sheria na kushauri sio kulazimisha au kusema Waziri Mkuu jiuzulu itafuata sasa Rais ambapo naye atavunja Bunge hapo lengo ni nini? Wabunge wengi wamesoma Public Law hata kidato cha 2 somo la Uraia, Magazeti leo yamedokeza Mtaalam wa Siasa UDSM Bw Bana.amesema Bunge ni kutunga. Sheria ntalifuatilia Gazeti hilo namalizia nihukumiwe lkn sio Wabunge wawasimamishe Waziri mkuu au Mawaziri wote 8 wao ndio wamewachagua? Rais atalibadili tu baadhuu ya sura hilo Baraza kabla ya June 12

Mkuu kasome tena katiba vizuri, serikali inawajibika kwa wananchi wanaowakilishwa na wabunge. Yanayofanywa na serikali hayalidhishi, watuwezi kuendelea kunyamaza. Kelele za wabunge ndo kilichopo mioyoni mwa wananchi,wabunge wanatusemea tu. Hivyo kuto kusikiliza wabunge ni kutosikiliza wananchi wenye nchi yao, kitakachofuata ni yale ya Tunisia. Tunaanza na maandamano kila kijiji.......
 
sehemu kubwa ya watanzania akili zimeoza na ndio chanzo cha matatizo kazi kupiga domo tu rais mmemuweka wenyewe mliona anafaa leo ooh rais ndio tatizo mambo magumu dunia yote ongezeni juhudi kupambana na umaskini

Hapo kwenye Red, Mbona siku mambo yakiwa mazuri duniani kote hayafiki Tanzania? Ni pale yanapokuwa magumu tu!

Hatuwezi kupambana na umaskini bila uwajibikaji. Ni lazima kila mmoja awajibike katika nafasi yake. Tuondoe matatizo ya wizi.
 
Chanzo cha matatizo yote haya ni wanawake....wanawake wengi walijitokeza kumpigia kura JK kwa sababu ya sura yake....wanawake ni wengi kuliko wanaume,wanawake wengi wako idle hivyo wana muda wa kupiga kura...wanawake wengi sio watu wa kukata tamaa kwenda kupiga kura kama wanaume....wanawake wana moyo wa huruma,walimhurumia JK amalizia muda wa miaka kumi...wanawake waliahidiwa maisha bora na JK...chezea wanawake wewe....wanachagua chagua tu coz hawaujui ugumu wa maisha but kuna wachache wanaojitambua na kuna wanaume wanaopenda vya kupewa nao hupigia CCM ili waendelee kula vya bure....hawa ndio chanzo..JK ni matokeo tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom