Maarko
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 1,189
- 602
Kwa maoni yangu binafsi, taarifa hii haiwezi kuwa sahihi. Haya ni majungu yenye lengo la kujenga fitna na chuki dhidi ya hiyo kampuni mpya.
Usafirishaji abiria hapa nchini unahusisha mabasi zaidi ya 1,000. Hivyo hicho kikamouni kipya na vibasi vyake 40 sio tishio mpaka wapike zengwe kwa Dar Express kufungiwa.
Kama kweli lengo la hicho kikampuni kioya ni kuweka kauzibe kwa makampuni mengine, zengwe hili lingepigwa kwa Sumry mwenye mabasi zaidi ya 100 yanayokwenda nchi nzima na nje ya nchi na sio Dar Express mwenye route moja tuu ya Moshi, Arusha!.
Sumatra wakifungia chochote, wanafunga kwa vigezo ambayo viko wazi na sio kwa majungu. Dar Express wanajua ukweli na kama wanajihisi wanaonewa, mamlaka ya rufaa ya Sumatra ni Baraza la Ushindani au waende mahakamani.
Wana jf wenzangu, ili kulinda hadhi ya jf kugeuka kijiwe cha fitna na majungu, habari kama hiza ambazo hazina mantiki ziwekwe kwenye jukwaa la jokes ili isomeke kama jokes.
Hujui usemalo wewe,pengine ndiyo miongoni mwa wale mafisadi wanayoihujumu nchii,wewe kama ulishawahi kufanya Biashara usingesema haya madudu,fitina katika biashara huwa ipo,na kampuni ya Dar Express kwa mikoa ya kaskazini ni tishio kutokana na ubora wa huduma anayotoa.Swala hapo siyo wingi wa mabasi bali ni ubora wa huduma itolewayo na kampuni husika.
Huyo kijana wa muheshimiwa siyo Kampuni ya kwanza kaumiliki hapa nchini,kuna kampuni moja ya malori ya kubeba mafuta ama ni ya kwake100% au ana hisa katika kampuni hiyo. yapo mengi tu lakini kama alivyosema mjumbe mmoja ni swala la wakati tu mtakuja kuyaona na kuyajua vizuri.