Chanzo cha kufungiwa kwa mabasi ya Dar Express ni Ridhiwan JK

we unafikiri Pinda atakubali mabasi yake ya Sumry yafungiwe? Kama kweli Sumatra wangekuwa wametumia vigezo vya ajali basi wangeifungia Sumry ambayo mwezi uliopita mabasi yake kadhaa yalipata ajali na kuua watu kadhaa ndani ya wiki 1..
Kumbe mtoto wa mkulima ni mfanyabiashara pia?
 
Kwa maoni yangu binafsi, taarifa hii haiwezi kuwa sahihi. Haya ni majungu yenye lengo la kujenga fitna na chuki dhidi ya hiyo kampuni mpya.

Usafirishaji abiria hapa nchini unahusisha mabasi zaidi ya 1,000. Hivyo hicho kikamouni kipya na vibasi vyake 40 sio tishio mpaka wapike zengwe kwa Dar Express kufungiwa.

Kama kweli lengo la hicho kikampuni kioya ni kuweka kauzibe kwa makampuni mengine, zengwe hili lingepigwa kwa Sumry mwenye mabasi zaidi ya 100 yanayokwenda nchi nzima na nje ya nchi na sio Dar Express mwenye route moja tuu ya Moshi, Arusha!.

Sumatra wakifungia chochote, wanafunga kwa vigezo ambayo viko wazi na sio kwa majungu. Dar Express wanajua ukweli na kama wanajihisi wanaonewa, mamlaka ya rufaa ya Sumatra ni Baraza la Ushindani au waende mahakamani.

Wana jf wenzangu, ili kulinda hadhi ya jf kugeuka kijiwe cha fitna na majungu, habari kama hiza ambazo hazina mantiki ziwekwe kwenye jukwaa la jokes ili isomeke kama jokes.
Pasco acha kufuru usitetee kitu kwa kujifanya zezeta eti kijikampuni cha Ridhwani cha vijibasi 40 tu. Unalinganisha Sumry na Dar Express kwa context ipi quantity au quality, inawezekana hicho unachokisema kijikampuni kipya cha Ridwani kimeona Dar Express ndiye threat wake mkubwa kwa ubora wa huduma ukilinganisha na mabasi 200 ya Sumry yanayojaza abiria hadi madirishani, sidhani kama unaelewa huduma ya mabasi ya Dar express huwa yanakwenda kwa ratiba hayasubiri kujaza hata mkiwa abiria kumi basi linaondoka.
 
Labda tumkumbushe huu wimbo wa kitambo

MWANA ACHA WIZI – Juwata Jazz Band 1977 aka MSONDO

Majirani wenzangu,
Naomba mnisaidie,
Mkanyeni mwanangu,
Labda atakusikieni,

Nimemkanya aache wizi mwanagu kanishinda,
Labda nyie wenzangu mtaweza kunisaidia,

Asante ndugu, tutajaribu kumuelisha,
Kiasi cha uwezo wetu,
Huyu mwanetu.

Ewe mwana tulia, Tukueleze,
Tabia uliyonayo ya wizi haikufai,
Ulipelekwa shule , elimu umepata,
Ya kuweza kukusaidia
Kuliko kutaka utajiri wa harakaharaka.

(Kibwagizo)

Ehhe mwana hukusikia niliyokwambia,
Balaa kutuletea nyumbani
eeh mwana.

Wazee wenzagu pia walikuketisha chini,
Wengi walikueleza mwana acha wizi,
Nawe hukusikia ukazidisha vitendo vya wizi.

[Ngurumo]
Umevunja duka la Ushirika,
Bunduki imelia,(mama weeee)
Shaba yaingia mwilini mwako waona uchungu!

Leo uko taabani ,
Hospitali umelazwa,
Pingu ziko mikononi mwako mwanangu umefungwa!!

Ehee mwana hukusikia
Balaa kutuletea nyumbani
eeh mwana.

Wazee wenzagu pia walikuketisha chini,
Wengi walikueleza mwana acha wizi,
Nawe hukusikia ukazidisha vitendo vya wizi.

Ukiwa Jf utaburudika kwa kila namna,thanks mkuu
 
uzushi uzushi tuuu kila siku kwa faida gani lakini hamna cha kufanya yaone mabichwa yenu!!
 
uzushi uzushi tuuu kila siku kwa faida gani lakini hamna cha kufanya yaone mabichwa yenu!!

Na wewe jitizame jibichwa lako lilivo la ajabu,kama ni uzushi lete facts unazozijua wewe sio kuropoka hovyo hovyo kama mwenda wazimu
 
tunachotaka usafiri bora,wa uhakika,nauli reasonable na salama!!!!ya dar express mwachie dar express na ridhiwan mwachie ridhiwan!..........
 
namshauri Ridhiwani apeleke gari zake ktk njia inayokwenda mabasi yanayoitwa TAQWA atapata faida ya haraka sana.
Mabasi haya yanakwenda nje ya nchi kwa mfano
Dar-Nairobi-Kampala
Dar-Nairobi-Kampala-Sudan
Dar-Lusaka
Dar-Lusaka-Harare
Tanzania-Malawi
Dar-Kigali-Bujumbula
Tanzania-Congo
Tanzania-Botwana

Hakuna TAQWA linaloenda Morogoro, iringa, dodoma, Tanga, Singida na mikoa mingine ya jirani.
Heshima kuu zimfikie mwenye mabasi haya ya TAQWA.
Kwani nadiriki kumfananisha na Nyani mzee aliyekwepa mishale Mingi.
Magari ya TAQWA ni Sugu na sio ya kichina
 
Kampuni hyo mpya ina magari arobaini na inasemekana kuwa kuna kijana flani wa Songea ndo amekabidhiwa aiendeshe.... Nyeti hzo nimezpata pale toka kwa dereva wa Dar express.

Mabasi ya hawa jamaa yamejaa damu na kafara. Kwa sababu dar express anampenda Mungu na hawa wachawi wameshindwa kusababisha ajali ili wachukue damu za marehemu wameamua kufanya physical attacks. Mabasi ya Rizi!1 yataishia mto nduruma na pale Kikavu na kama ana bisha aulize iko wapi MKWEMA
 
Huyo kijana, tukipata nchi tu hapo 2015, atakuwa wa kwanza kupelekwa lupango
 
Naona sasa JF imegeuka udaku mtupu,mnatupozea ladha sasa.leteni habari zenye evidence aaaah!
 
Kwa maoni yangu binafsi, taarifa hii haiwezi kuwa sahihi. Haya ni majungu yenye lengo la kujenga fitna na chuki dhidi ya hiyo kampuni mpya.

Usafirishaji abiria hapa nchini unahusisha mabasi zaidi ya 1,000. Hivyo hicho kikamouni kipya na vibasi vyake 40 sio tishio mpaka wapike zengwe kwa Dar Express kufungiwa.

Kama kweli lengo la hicho kikampuni kioya ni kuweka kauzibe kwa makampuni mengine, zengwe hili lingepigwa kwa Sumry mwenye mabasi zaidi ya 100 yanayokwenda nchi nzima na nje ya nchi na sio Dar Express mwenye route moja tuu ya Moshi, Arusha!.

Sumatra wakifungia chochote, wanafunga kwa vigezo ambayo viko wazi na sio kwa majungu. Dar Express wanajua ukweli na kama wanajihisi wanaonewa, mamlaka ya rufaa ya Sumatra ni Baraza la Ushindani au waende mahakamani.

Wana jf wenzangu, ili kulinda hadhi ya jf kugeuka kijiwe cha fitna na majungu, habari kama hiza ambazo hazina mantiki ziwekwe kwenye jukwaa la jokes ili isomeke kama jokes.

na wewe unachokiandika huna uhakika nacho kama umesoma sababu za sumatra
kumfungia dar express ucngeandika!
haya mawazo yako danganyifu
 
kati ya dar express na sumry kampuni gani ambayo inatakiwa kufungwa kwa kupata ajali kila mara?
mbona kuna watu hawana akili kiasi hiki.......
 
namshauri Ridhiwani apeleke gari zake ktk njia inayokwenda mabasi yanayoitwa TAQWA atapata faida ya haraka sana.
Mabasi haya yanakwenda nje ya nchi kwa mfano
Dar-Nairobi-Kampala
Dar-Nairobi-Kampala-Sudan
Dar-Lusaka
Dar-Lusaka-Harare
Tanzania-Malawi
Dar-Kigali-Bujumbula
Tanzania-Congo
Tanzania-Botwana

Hakuna TAQWA linaloenda Morogoro, iringa, dodoma, Tanga, Singida na mikoa mingine ya jirani.
Heshima kuu zimfikie mwenye mabasi haya ya TAQWA.
Kwani nadiriki kumfananisha na Nyani mzee aliyekwepa mishale Mingi.
Magari ya TAQWA ni Sugu na sio ya kichina
hivi unadhani magari ya kichina ni hovyo kama bidhaa zao nyingine?
jaribu kuuliza madereva ma mikoani wakupe sifa ya magari ya kichina
 
Back
Top Bottom