Chanzo cha kufungiwa kwa mabasi ya Dar Express ni Ridhiwan JK

Nicas Mtei

JF-Expert Member
Dec 21, 2010
11,556
7,085
Kuna taarifa ambazo nimezipata toka kwa chanzo makini kuwa kuna kampuni mpya ya usafirishaji abiria ambayo ni ya Riz 1 inatarajiwa kuanza mnamo tarehe 6 november. Inasemekana kuwa kampuni hyo imeanza fitna ili wengne wafungiwe ili wafanikiwe kupata wateja ndipo wameanza na Dar Express kwa njia ya Dar to Arusha..

Inasemekana kuwa pia fitna hzo zimegonga mwamba kwa mmiliki wa Kilimanjaro amcpo yeye alitumia nguvu kubwa alonayo serikalini..

Naona sasa JF imegeuka udaku mtupu,mnatupozea ladha sasa.leteni habari zenye evidence aaaah!

Sumatra yasitisha mabasi 14 Dar- Arusha

Tuesday, 01 November 2011 20:30
Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafirishaji wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imesitisha safari za mabasi 14 ya kampuni za Dar Express kutoa huduma kati ya Dar es Salaam- Arusha na Arusha-Tanga kuanzia kesho.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Sumatra jana, mamlaka hiyo kupitia kifungu namba 15 cha Sheria ya Sumatra namba 9 ya mwaka 2001, imeiagiza Kampuni ya Dar Express kusitisha utoaji huduma kwa magari yake yote yanayotoa huduma ya usafiri kati ya Dar - Arusha na Arusha- Tanga kuanzia kesho.

"Kutokana na kuwapo kwa matukio mengi ya ajali yaliyohusisha mabasi yanayomilikiwa na kampuni hiyo kwa kipindi kisichozidi miezi 10, mamlaka inatilia mashaka sifa za madereva wa mabasi ya Kampuni ya Dar Express," inaeleza taarifa hiyo.

Pia, taarifa hiyo ilieleza kuwa imebainika Kampuni ya Dar Express imekiuka Kanuni namba 22 ya Kanuni za Ufundi na Usalama na Ubora wa Huduma kwa Magari ya Abiria za 2008.

"Kuanzia Januari 2011 hadi sasa, mabasi ya Kampuni ya Dar Express yamehusika katika matukio ya ajali maeneo mbalimbali ambayo kampuni hiyo inatoa huduma za usafirishaji abiria. Matukio hayo ni kama lile la Januari 4, mwaka huu basi la Dar Express lilimgonga mpanda pikipiki na kusababisha kifo maeneo ya Kifaru- Mwanga, mkoani Kilimanjaro. Kwa mujibu wa taarifa za polisi chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi," ilieleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo inaeleza pia kuwa Septemba 22, mwaka huu, basi la Dar Express likitokea Arusha kwenda Tanga lilimgonga mtembea kwa miguu Ramadhani Hassan na kusababisha kifo eneo la Mkumbara - Mombo na Oktoba 24, basi jingine la kampuni hiyo liligonga gari jingine kwa nyuma kisha kuacha njia na kupinduka maeneo ya Kitumbi - Korogwe. Katika ajali hiyo watu tisa walijeruhiwa [/quote]

Kampuni hyo mpya ina magari arobaini na inasemekana kuwa kuna kijana flani wa Songea ndo amekabidhiwa aiendeshe.... Nyeti hzo nimezpata pale toka kwa dereva wa Dar express.

Mmmmmmhh, this will be another issue, why mabasi ya Dar Express? ktk nyanja ya usafirishaji Tz jamaa wanajitahidi kwa kweli. Ila kwa alivo dogo huyo inawezekana!

kwa maana hiyo leo hii hakuna mabasi ya dar express yanayotoa huduma ? na kama wamefungiwa ni kwa kigezo gani?

Kama ni kweli huyu bwana mdogo anazidi kujitafutia shida. Wasipopanda hayo ya kwake atayapeleka Bagamoyo au?

mi nimeshangaa kuna mabasi yana viwango kama dar express eti leo unayasimamisha?hivi hawa wana akili kweli waacha mikweche kama mbazi express kuifungia wanahujumu dar express.huyu dogo aangalie jibsi gadafi alivotiwa vijiti matakoni ndo atajua hayo anayofanya yana mwisho

hayo magari ya riz1 labda yafanye safari za songea na bagamoyo

Hyo imejulikana baada ya wadau kuhoji vigezo vya Dar Express kufungiwa kibali cha kusafirisha abiria, Sumatra wanadai et magari hayo yamekuwa yakipata ajaji mfululizo tangu mwezi january lakini rekodi halisi hazionesh kuwa kuna ukweli.. Safari zilizofungwa ni Dar to Arusha, Arusha to Tanga. .

Umbea, umbea. Ina maana magar ya Dar Arusha ni Dar Express pekee, au wao wana nini cha zaidi. Huo ni uongo mkubwa. Umetumwa kuwafanyia promo Dar Express.

Na pia mchakato mzima wa kupata madereva umekuwa na zengwe kutokana na wakala alyekabidhiwa hiyo kazi, wakala huyo amepewa maagizo ya kutafuta madereva wanachama wa ccm tu. Tusubiri taarifa zaidi.

Hyo imejulikana baada ya wadau kuhoji vigezo vya Dar Express kufungiwa kibali cha kusafirisha abiria, Sumatra wanadai et magari hayo yamekuwa yakipata ajaji mfululizo tangu mwezi january lakini rekodi halisi hazionesh kuwa kuna ukweli.. Safari zilizofungwa ni Dar to Arusha, Arusha to Tanga. .

habari zako sio za kweli. Mbona leo magari yapo barabarani.

Na pia mchakato mzima wa kupata madereva umekuwa na zengwe kutokana na wakala alyekabidhiwa hiyo kazi, wakala huyo amepewa maagizo ya kutafuta madereva wanachama wa ccm tu. Tusubiri taarifa zaidi.

habari zako zimekaa kimbeambea.

..........wabongo!wabongo!wabongo! ukishakuwa mtoto wa mkubwa tu kichwa unakipeleka likizo, wapambe wanaanza kufikiri badala yako, mbaya zaidi wao hawatumii tena kichwa kufikiri,wanatumia matumbo yao, washibe, wao na watoto wao. Pengine wanatumia kichwa mara moja moja pale wanapotafuta nini unapenda kukisikia kutoka kwao, basi!!!!!!!!!, R1, R1, R1, R1 ni suala la wakati tu; walikuwepo akina Bokassa, akapita. Mobutu Sesseko Kuku wa Kubanga, akapita. Saddam, akapita. Gaddafi, (kwa uchache) akapita sembuse............!!!!!!!!!! ni suala la wakati tu, mbaya zaidi hata walichojilimbikizia hawakufaidi kwa kiwango walichodhania.

Kwa maoni yangu binafsi, taarifa hii haiwezi kuwa sahihi. Haya ni majungu yenye lengo la kujenga fitna na chuki dhidi ya hiyo kampuni mpya.

Usafirishaji abiria hapa nchini unahusisha mabasi zaidi ya 1,000. Hivyo hicho kikamouni kipya na vibasi vyake 40 sio tishio mpaka wapike zengwe kwa Dar Express kufungiwa.

Kama kweli lengo la hicho kikampuni kioya ni kuweka kauzibe kwa makampuni mengine, zengwe hili lingepigwa kwa Sumry mwenye mabasi zaidi ya 100 yanayokwenda nchi nzima na nje ya nchi na sio Dar Express mwenye route moja tuu ya Moshi, Arusha!.

Sumatra wakifungia chochote, wanafunga kwa vigezo ambayo viko wazi na sio kwa majungu. Dar Express wanajua ukweli na kama wanajihisi wanaonewa, mamlaka ya rufaa ya Sumatra ni Baraza la Ushindani au waende mahakamani.

Wana jf wenzangu, ili kulinda hadhi ya jf kugeuka kijiwe cha fitna na majungu, habari kama hiza ambazo hazina mantiki ziwekwe kwenye jukwaa la jokes ili isomeke kama jokes.

Back
Top Bottom