Channel Ten (Tz): Ushauri wa BURE

Mar 27, 2009
75
5
Kama kuna kitu kinachokera kuelekea fainali ya mabingwa ulaya mwaka huu ni matangazo yaliyotolewa na yanayotolewa na kituo cha TV cha Channel ten.

Licha ya kuonyesha unazi wa wazi kwa timu mojawapo 'MAN U' na kuitabiria ushindi hatimae kuchukua ubingwa, maneno yanayotumika katika matangazo hayo hayana ustaarabu hata kidogo!!

Mfano kusema Man U itawasambaratisha vijana "wenye sura nzuri wa arsenal". Leo hii wameibuka na tangazo linasema "baada ya kuwaoa na kuwapiga talaka tatu warembo wa arsenal mbele ya wake zao na familia zao MAN UNITED imepeleka posa BARCA".

Hivi kweli kauli hizi za matusi hazikupaswa kuepukwa na kituo kikubwa kama Channel ten? Nina imani hata kituo cha tv cha MAN TV kule UK hakiwezi kutangaza kauli kama hizi!! Nadhani hata mashabiki wastaarabu wa MAN United wameshaona tatizo la matangazo haya.

Tumesikia kuwa mafisadi papa wamekinunua kutuo hiki, nadhani hata wao wasingependa watangazaji watumie unazi na maneno machafu kwenye matangazo yanayolipiwa na wadhamini wastaarabu.

WANAHABARI MSIWE MANAZI WAZI WAZI
 
Kama kuna kitu kinachokera kuelekea fainali ya mabingwa ulaya mwaka huu ni matangazo yaliyotolewa na yanayotolewa na kituo cha TV cha Channel ten. Licha ya kuonyesha unazi wa wazi kwa timu mojawapo 'MAN U' na kuitabiria ushindi hatimae kuchukua ubingwa, maneno yanayotumika katika matangazo hayo hayana ustaarabu hata kidogo!! Mfano kusema Man U itawasambaratisha vijana "wenye sura nzuri wa arsenal". Leo hii wameibuka na tangazo linasema "baada ya kuwaoa na kuwapiga talaka tatu warembo wa arsenal mbele ya wake zao na familia zao MAN UNITED imepeleka posa BARCA". Hivi kweli kauli hizi za matusi hazikupaswa kuepukwa na kituo kikubwa kama Channel ten? Nina imani hata kituo cha tv cha MAN TV kule UK hakiwezi kutangaza kauli kama hizi!! Nadhani hata mashabiki wastaarabu wa MAN United wameshaona tatizo la matangazo haya. Tumesikia kuwa mafisadi papa wamekinunua kutuo hiki, nadhani hata wao wasingependa watangazaji watumie unazi na maneno machafu kwenye matangazo yanayolipiwa na wadhamini wastaarabu. WANAHABARI MSIWE MANAZI WAZI WAZI

Hivi kweli nilisahau hawa channel 10 wana configuration mpya nani ana number zake anisaidie.
 
te he he...:D

mtangazaji alikuwa Ephraim Kibonde nini huyo?
 
olololo..huu ni ufidhuli wala si unazi..inaonesha hawa jamaa hawakupitia skuli kuelewa professionalism aidha hawajui kitu kinachoitwa ustaarabu..na inaonekana hawana edita au producer ..kila mtu steling..ubaya tu ni kuwa hamna la kuwafanya maana hawana competitors na hakuna wa kuwakemea..ndo imetoka hiyo.
 
te he he...:D

mtangazaji alikuwa Ephraim Kibonde nini huyo?

Ha ha..Mbu hata mimi ninavyosoma hayo maneno esp. in red sauti ihahisi natoka kama ya E.Kibonde,huh!..Tusubiri jamaa aliyeleta mada atuhakikishie huyo mtangazaji..
Ati kweli Ars ni remboz? ha ha,jumalipi njema mkuu!
 
Ha ha..Mbu hata mimi ninavyosoma hayo maneno esp. in red sauti ihahisi natoka kama ya E.Kibonde,huh!..Tusubiri jamaa aliyeleta mada atuhakikishie huyo mtangazaji..
Ati kweli Ars ni remboz? ha ha,jumalipi njema mkuu!

...:D BJ mchokozi wa reja -reja sana wewe...haya, tumsubiri Ephraim wa Kibonde, mutu ya 'four-flats' atuhabarishe!
 
Kuna hili tangazo la fainali za Klabu Bingwa Bara Ulaya kati ya Bacelona na Manchester ambalo limekuwa likirushwa na kituo cha Runinga cha Chanel Ten mimi limekuwa linanikera kweli. Kwani kuna ulazima gani wa kuwaita wachezaji wa Timu ya Arsenal warembo katika tangazo hili?

Je huyu Mtangazaji au mwandaaji wa tangazo hafikirii kuwa Runinga ni chombo ambacho kinatazamwa na Jamii mchanganyiko na kuwa maneno kama hayo kuwaita wanaume wenziyo ni kero. Na hata kama ni suala la urembo kuna mchezaji gani wa Arsenal ambaye anaweza kumfikia Berbetov, Ronaldo, Nani, Anderson na wengine wengi? After all Arsenal haichezi fainali, au ndo tu kwamba aliyeandaa tangazo anamapenzi makubwa na Man United kiasi kwamba ameona lazima awakwaze mashabiki na wapenzi wa Arsenal?

Je sisi ambao siyo wapenzi wa Arsenal au Man. United tumewekwa kundi gani.

Ni vema uongozi wa Chanel Ten wangeliondoa tangazo hilo na kuweka tangazo lenye maneno ya heshima na staha kwa umma.
 
Kuna thread nyingine ya hii kitu pia! Huu sio ustaarabu kabisa, Channel ten wanafanya business na wateja wao si wote ni fans wa Man, wapo wa Arsenal na timu nyinginezo na wapo ambao ni neutral kabisa!

Tangazao lile linawakwaza si tu fans wa Arseanal lkn pia hata wananchi wengine kwakuwa linatia kinyaa, so better waliondoe mapema na kuapologise kwa matumizi mabaya ya lugha!!
 
Kwa kweli ahta mimi ingawa si mpenzi wa Man U wala Arsenal, hili tangazo linanikera sana hasa ukizingatia mimi ni mpenzi mkubwa wa kutazama channel 10, pamoja na mambo yao ya LIVE bila chenga! ............Channel 10, huu ni ushauri wa buuuuuuure!
 
ujue ndio tatizo la kutokuwa na wataalamu wa masoko waliobobea ili kujua ni ujumbe gani ufike kwa wananchi. Hivi wakifungua kesi ya kudhalilishwa wataweza kulipa? Manake nana ni kashfa. Wanasheria mtusaidie kwa hili
 
kweli kabisa, kama vile ulikuwa kwenye mawazo yangu, maana nilifikiria kumtafuta msiba awaambie wenzake hilo tangazo halifai kwa jamii, ni la kitoto sana, ukitazama kwa undani inawashushia heshima channel ten, na kuashiria kwamba hawana msimamizi thabiti, kila mtu anaweza akafanya atakavyo, kwa kifupi washika bunduki wametoka ni bora tangazo liwahusishe walioingia finali tu, tukirudi kwenye game yenyewe, naamini itakuwa ngumu kuliko mashabiki wa man wanavyofikiria na tegemea man watacheza mpira, badala ya kuzuia tu..
 
Unapokuwa na wajinga, wapuuzi na washabiki wasiofanya kazi kuzingatia weledi us$%*# kama huo lazima utokee. Hicho kituo kama kijiwe cha watu waliokosa nafasi sehemu za maana. Mzee Hamza Kasongo ndio anaongoza upuuzi huo SHAME ON HIM
 
Wakuu nimekuwa nikiwinda lile tangazo dhalimu la hawa jamaa hatimae nimelipata na nimeattach so mtaweza kusikiliza uozo huu na kutoa hukumu/mawazo yenu. Channel ten kama sio sikio la kufa nao wapime uzito wa maoni yenu wadau!!

NIAMBIENI UHALALI WA TANGAZO HILI!!!

[mp3]https://www.jamiiforums.com/attachments/michezo-sports-games/4577d1242673957-channel-ten-tz-ushauri-wa-bure-chten.mp3[/mp3]
 

Attachments

  • chten.mp3
    1.1 MB · Views: 75
Pata Freq za channal zetu Tanzania. Sat- Intelsat 906 at 64.2 East. .ITV Tr 3642 Sr 13333-Hor-. Channel Ten Tr 3908 Sr 2849.-Vert- TvT Tr 3891 Sr 4444.--Vert--Star Tv Tr 3884 Sr 3272.-Vert- Agape Tr 3900 Sr 3800-Ver-.
 
...Nilidhani ni mimi peke yangu tu ambaye tangazo lile linaniudhi. Ukweli ni jambo la ajabu sana kituo kikubwa kama channel 10 kinaweza kuruhusu upuuzi kama ule kurushwa hewani tena katika tangazo ambalo eti ni la kutafuta watangazaji biashara!! Ni ushahidi tosha wa jinsi vyombo vyetu vya habari vinavyoendeshwa kienyeji!!
 
Wakuu nimekuwa nikiwinda lile tangazo dhalimu la hawa jamaa hatimae nimelipata na nimeattach so mtaweza kusikiliza uozo huu na kutoa hukumu/mawazo yenu. Channel ten kama sio sikio la kufa nao wapime uzito wa maoni yenu wadau!! NIAMBIENI UHALALI WA TANGAZO HILI!!!

Mkuu,

Asante kwa tangazo hilo. Jamaa wametukana live na hakuna maadili yoyote humo. Hata kama ni ushabiki, hawa naona wamekwenda an extra mile...
 
Back
Top Bottom