Zipapa zipapa
JF-Expert Member
- Feb 15, 2013
- 409
- 117
Kwani mmelazimishwa kula nyama iliyochinjwa na wakristo?
1-Mkaribisheni kwenu mtu aliye dhaifu, lakini msibishane naye juu ya mawazo yake binafsi.-
2-Watu huhitilafiana: mmoja imani yake inamruhusu kula kila kitu; lakini mwingine ambaye imani yake ni dhaifu, hula tu mboga za majani.-
3-Mtu ambaye hula kila kitu asimdharau yule ambaye hawezi kula kila kitu; naye ambaye hula tu mboga za majani asimhukumu anayekula kila kitu, maana Mungu amemkubali.-
4-Wewe ni nani hata uthubutu kumhukumu mtumishi wa mwingine? Akisimama au akianguka ni shauri la Bwana wake; naam, atasimama imara, maana Bwana anaweza kumsimamisha.
5-Mtu anaweza kufikiria siku fulani kuwa ya maana zaidi kuliko nyingine; mtu mwingine aweza kuzifikiria siku zote kuwa sawa. Kila mmoja na afuate msimamo wa akili yake.-
6-Anayeadhimisha siku fulani anaadhimisha siku hiyo kwa ajili ya kumtukuza Mungu; naye anayekula chakula fulani anafanya hivyo kwa kumtukuza Bwana maana anamshukuru Mungu. Kadhalika naye anayeacha kula chakula fulani anafanya hivyo kwa ajili ya kumtukuza Bwana, naye pia anamshukuru Mungu.-
7-Maana hakuna mtu yeyote miongoni mwetu aishiye kwa ajili yake mwenyewe, wala hakuna anayekufa kwa ajili yake mwenyewe-
8-maana tukiishi twaishi kwa ajili ya Bwana; tukifa, tunakufa kwa ajili ya Bwana. Basi, kama tukiishi au tukifa, sisi ni mali yake Bwana.-
9-Maana Kristo alikufa, akafufuka ili wapate kuwa Bwana wa wazima na wafu.
10-Kwa nini, basi wewe wamhukumu ndugu yako? Nawe,
kwa nini wamdharau ndugu yako? Sisi sote tutasimama mbele
ya kiti cha hukumu cha Mungu.
11-Maana Maandiko yanasema: "Kama niishivyo, asema Bwana kila mtu atanipigia magoti,
na kila mmoja atakiri kwamba
mimi ni Mungu."
12-Kwa hiyo, kila mmoja
wetu atatoa
hoja yake mbele
ya Mungu.
13-Basi, tuache kuhukumiana, bali tuazimie kutokuwa kamwe kikwazo
kwa ndugu yetu au kumsababisha aanguke katika dhambi.-
14-Katika kuungana
na Bwana Yesu, nina hakika kwamba hakuna kitu chochote kilicho najisi
kwa asili yake; lakini, mtu akidhani kwamba kitu fulani
ni najisi, basi, kwake huwa najisi.-
15-Kama ukimhuzunisha ndugu yako
kwa sababu
ya chakula unachokula, basi mwenendo wako hauongozwi
na mapendo. Usikubali hata kidogo chakula chako kiwe sababu
ya kupotea
kwa mtu mwingine ambaye Kristo alikufa
kwa ajili yake!-
16-Basi, msikubalie kitu mnachokiona
kuwa kwenu
ni kitu chema kidharauliwe.-
17-Maana Utawala
wa Mungu si shauri la kula
na kunywa, bali unahusika
na kuwa na uadilifu, amani
na furaha iletwayo
na Roho Mtakatifu.-
18-Anayemtumikia Kristo namna
hiyo humpendeza Mungu,
na kukubaliwa
na watu.-
19-Kwa
hiyo tuyazingatie daima mambo yenye kuleta amani,
na yanayotusaidia kujengana.-
20-Basi, usiiharibu kazi
ya Mungu
kwa sababu
ya ubishi juu
ya chakula. Vyakula vyote
ni halali,
lakini haifai kula chakula ambacho kitamfanya mtu aanguke katika dhambi.-
21-Afadhali kuacha kula nyama, kunywa divai, au kufanya chochote ambacho chaweza kumsababisha ndugu yako aanguke.-
22-Basi, shikilia unachoamini kati yako
na Mungu wako. Heri mtu yule ambaye, katika kujiamulia la kufanya, haipingi dhamiri yake.-
23-Lakini mtu anayeona shaka juu
ya chakula anachokula, anahukumiwa
kama akila,
kwa sababu msimamo
wa kitendo chake haumo katika imani. Na, chochote kisicho
na msingi wake katika imani
ni dhambi.
?
Kwenye kipindi kilicho rushwa na chaneli ten mzee wa Upako ameonyesha kushangazwa na viongozi wa kikristo wanao ng'ang'ania kuchinja. Amesema ""nawashangaa sana wachungaji wenye hoja za kipumbavu eti nani achinje"
"Wanamsumbua waziri mkuu eti kujadili nani achinje wakati nchi ina matatizo lukuki, kwani waislamu walipo kuwa wana chinja ilikuwaje?"
Akaendelea kusema "Tuombee amani tuache hoja za kijinga eti nani achinje nani asichinje".
Aliongea mengi kuonyesha namna ambavyo amani yetu inaweza kutoweka kwa ajili ya mawazo ya kijinga! Amewaomba wakristo kusoma Warumi 14 mstari 1 na 31.
Naomba mwenye biblia atuweke mstari huo unasemaje.
Waislamu wengi tunafuatilia kwa karibu mafundisho yenu. Kuna wachungaji wanaohubiri mafundisho mema kwenu kama Mzee wa Upako na Mchungaji Kakobe!
Naanza kwa kusema mimi sio mshabiki wa mzee wa upako.
Wakristo sasa tunataka kuanza kuendekeza mambo ya kimwili. Hili suala la kuchinja sidhani kama linamjenga mkristo kiroho. Kama tukifikia muafaka kwamba nyama ya mkristo ichinjwe na mkristo na nyama ya muislamu ichinjwe na muislamu ina maana hili litakuwa anguko kubwa sana katika amani ya nchi yetu na kazi ya kuwafikia watu waache dhambi na waje kwa Kristo Yesu aliyesulubishwa kwa ajili yao itakuwa ngumu.
Pata picha, ina maana shughuli (mf. harusi, msiba, n.k ambayo itahusu na kula) ya mkristo itabidi ihudhuriwe na wakristo tu na hivyo kwa upande wa waislamu. Tukitoka hapo, tutafuata na mambo mengine kama wimbo wa taifa n.k.
Walioanzisha huu mjadala wa nani achinje walitakiwa wajue pia madhara yake ya muda mrefu.
Na wale wanaoona kwamba hawawezi kula nyama ilichinjwa na mwislamu wajichinjie wenyewe kimya kimya na sio kuhamasisha wengine katika suala litakalotenganisha Taifa letu. Na tena kwa kuwa wamegundua ni dhambi, basi wanatakiwa watubu kwa ajili ya zile nyama walizokula siku za nyuma (hata kama walikuwa hawajui kwamba ni dhambi) pamoja na dhambi nyingine kama kuzini, kudanganya, kuiba, kufanya uasherati, kusengenya, kumatamani mtu kimapenzi, n.k. Hapo ndio wataonekana wapo makini na sio kung'ang'ania kuchinja tu.
Kwa hiyo basi, tufanye kila juhudi tutimize yale yaletayo amani na kujengana. Usiiharibu kazi ya Mungu kwa ajili ya chakula. Vyakula vyote vinafaa, lakini ni kosa kula kitu ambacho kinamfanya mwenzako kujikwaa. Ni afadhali usile nyama wala kunywa divai au kufanya jambo lingine lo lote litakalomfanyandugu yako aanguke. Unavyoamini kuhusu mambo haya, iwe ni siri yako na Mungu. Amebarikiwa mtu ambaye hajisikii kuhukumiwa afanyapo jambo analoamini kuwa ni sawa. Lakini mtu mwenye mashaka kuhusu anachokula, amehukumiwa ikiwa atakula, kwa sababu kula kwake hakutokani na imani. Kwa maana jambo lo lote ambalo halito kani na imani, ni dhambi (Warumi 14:19-23)
Naelewa wana hoja ya msingi, ila sio kipaumbele cha muhimu kwa sasa na sioni sababu ya kuhasisha wakristo wote katika suala kama hili. Yaani mwisho wa siku, kama ikiamuliwa kuwe na mabucha ya kikristo na kiislamu utakuwa ni mwanzo wa utengano wa kudumu. Haya mambo hayataaishia hapa jamaniNdugu, umesoma hoja ili kujua ni nini hasa ambacho wakristu hawataki?
Naelewa wana hoja ya msingi, ila sio kipaumbele cha muhimu kwa sasa na sioni sababu ya kuhasisha wakristo wote katika suala kama hili. Yaani mwisho wa siku, kama ikiamuliwa kuwe na mabucha ya kikristo na kiislamu utakuwa ni mwanzo wa utengano wa kudumu. Haya mambo hayataaishia hapa jamani
Kwa hiyo mzee wa upako ndo umemwona anawakilisha imani sahihi ya kikristo? na kwa nini unataka wakristo peke yao ndo waridhie kila kitu ila isiwe waislamu. Kama waislamu wanaona wakristo wakichinja inawaathiri imani yao, vivo hivyo na kwa wakristo kwani wamekatazwa kutumia vyakula vilivyotolewa sadaka kwa miungu wasioijua.Ukiniona MZIMU nimemkubali Mtu, jua huyo mtu anastahili. Jamani kwa watu wenye akili, hakuna suluhu nyengine itakayo linda Amani ya Nchii hii zaidi ya hiyo alioitoa Mchungaji Antony Lusekelo. Kwani hayo hayo ndio anayo yaongelea Mzee Pinda na Mzee Steven Wasira.
Kama kuna mkristo yoyote anapingana na huyu mchungaji, hakika huyo ndio asie itakia Mema Nchi hii.
1-Mkaribisheni kwenu mtu aliye dhaifu, lakini msibishane naye juu ya mawazo yake binafsi.-
2-Watu huhitilafiana: mmoja imani yake inamruhusu kula kila kitu; lakini mwingine ambaye imani yake ni dhaifu, hula tu mboga za majani.-
3-Mtu ambaye hula kila kitu asimdharau yule ambaye hawezi kula kila kitu; naye ambaye hula tu mboga za majani asimhukumu anayekula kila kitu, maana Mungu amemkubali.-
4-Wewe ni nani hata uthubutu kumhukumu mtumishi wa mwingine? Akisimama au akianguka ni shauri la Bwana wake; naam, atasimama imara, maana Bwana anaweza kumsimamisha.
5-Mtu anaweza kufikiria siku fulani kuwa ya maana zaidi kuliko nyingine; mtu mwingine aweza kuzifikiria siku zote kuwa sawa. Kila mmoja na afuate msimamo wa akili yake.-
6-Anayeadhimisha siku fulani anaadhimisha siku hiyo kwa ajili ya kumtukuza Mungu; naye anayekula chakula fulani anafanya hivyo kwa kumtukuza Bwana maana anamshukuru Mungu. Kadhalika naye anayeacha kula chakula fulani anafanya hivyo kwa ajili ya kumtukuza Bwana, naye pia anamshukuru Mungu.-
7-Maana hakuna mtu yeyote miongoni mwetu aishiye kwa ajili yake mwenyewe, wala hakuna anayekufa kwa ajili yake mwenyewe-
8-maana tukiishi twaishi kwa ajili ya Bwana; tukifa, tunakufa kwa ajili ya Bwana. Basi, kama tukiishi au tukifa, sisi ni mali yake Bwana.-
9-Maana Kristo alikufa, akafufuka ili wapate kuwa Bwana wa wazima na wafu.
10-Kwa nini, basi wewe wamhukumu ndugu yako? Nawe,
kwa nini wamdharau ndugu yako? Sisi sote tutasimama mbele
ya kiti cha hukumu cha Mungu.
11-Maana Maandiko yanasema: "Kama niishivyo, asema Bwana kila mtu atanipigia magoti,
na kila mmoja atakiri kwamba
mimi ni Mungu."
12-Kwa hiyo, kila mmoja
wetu atatoa
hoja yake mbele
ya Mungu.
13-Basi, tuache kuhukumiana, bali tuazimie kutokuwa kamwe kikwazo
kwa ndugu yetu au kumsababisha aanguke katika dhambi.-
14-Katika kuungana
na Bwana Yesu, nina hakika kwamba hakuna kitu chochote kilicho najisi
kwa asili yake; lakini, mtu akidhani kwamba kitu fulani
ni najisi, basi, kwake huwa najisi.-
15-Kama ukimhuzunisha ndugu yako
kwa sababu
ya chakula unachokula, basi mwenendo wako hauongozwi
na mapendo. Usikubali hata kidogo chakula chako kiwe sababu
ya kupotea
kwa mtu mwingine ambaye Kristo alikufa
kwa ajili yake!-
16-Basi, msikubalie kitu mnachokiona
kuwa kwenu
ni kitu chema kidharauliwe.-
17-Maana Utawala
wa Mungu si shauri la kula
na kunywa, bali unahusika
na kuwa na uadilifu, amani
na furaha iletwayo
na Roho Mtakatifu.-
18-Anayemtumikia Kristo namna
hiyo humpendeza Mungu,
na kukubaliwa
na watu.-
19-Kwa
hiyo tuyazingatie daima mambo yenye kuleta amani,
na yanayotusaidia kujengana.-
20-Basi, usiiharibu kazi
ya Mungu
kwa sababu
ya ubishi juu
ya chakula. Vyakula vyote
ni halali,
lakini haifai kula chakula ambacho kitamfanya mtu aanguke katika dhambi.-
21-Afadhali kuacha kula nyama, kunywa divai, au kufanya chochote ambacho chaweza kumsababisha ndugu yako aanguke.-
22-Basi, shikilia unachoamini kati yako
na Mungu wako. Heri mtu yule ambaye, katika kujiamulia la kufanya, haipingi dhamiri yake.-
23-Lakini mtu anayeona shaka juu
ya chakula anachokula, anahukumiwa
kama akila,
kwa sababu msimamo
wa kitendo chake haumo katika imani. Na, chochote kisicho
na msingi wake katika imani
ni dhambi.
?
Romans 14 haina verse 31
nimewahi kusikia haya kwenye mahubiri ya wa Upako kupitia channel ten "nina magari sita siyo ya japan, nina Range Rover sport, nina BMW X5, nina Landrover Discovery....nikiamka asubuhi naangalia kwenye parking niendeshe lipi!!! halafu nilivyo na mkwara kwenye gari nakua peke yangu, kama wewe unakuja kanisani kwangu na haujafanikiwa umekaa mwaka wa kwanza,wa pili na haujanunua usafirii! basi wewe hutoi dhaka, hutoi fungu la kumi ndo maana hufanikiwi, Yesu hakutembea na malofa...."~Mzee wa upako aka SMG, ha ha haaaa.
Namsikiliza Mchungaji Antony Lusekelo Chanel Ten sasa hivi. Nimemkubali huyu kweli ni kiongozi sahihi katika Imani ya Kikristo. Tukiwa na Viongozi wa kama hawa Amani yetu ya inchi haiwezi kutetereka.
Heshima kwako Mchungaji. Natamani Wachungaji, Mapdre na Maaskofu pamoja na Makidanali wote Muwe na upeo mkubwa wa kufikiria kama huyu Mchungaji. Huyu ni Tunu ya nchi.
Kwa ufupi tu, Mchungaji Antony Lusekelo Ameshangaa kulikoni leo Mashekhe na Maaskofu au Mapadre au Wachungaji wagombane wakati waliishi kwa amani tangu zamani. Kama ni suala la kuchinja, mbona suala hilo tangu enzi ya wazee wetu, walikua wanachinja waislamu wanakula wote. "Kama tukichinja sisi waislamu hawali, basi wachinje waislamu tule wote. Kuchinja isiwe ndio sababu ya kuvunja amani ya nchi yetu".
Ameeleza kwa kirefu suala hilo. Hiyo ndio ilikua mada ya kipindi.
Huyu nimekua nikifuatilia mahubiri yake, huyu kweli anawakilisha imani sahihi ya kikristo. Mimi sio Mkristo mimi ni Muislamu, ila hua tuna wapenda viongozi kama hawa katika jamii. Sio vizuri sisi watanzania kutengana kimisingi ya dini. Ni vibaya na hatari sana. Familia nyingi ni mchanganyiko.