Elections 2010 Channel Ten acheni uharamia dhidi ya Chadema

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Katika taarifa yao ya saa moja usiku huu, kituo cha Channel Ten kimeonekana kimewafanyia Chadema uharamia kwa kutoa footage ya mkutano wa chama hicho uliofanyika katika viwanja vya Jangwani iliyokuwa inakatika katika.

Hotuba za viongozi wa Chadema hazikusikika vizuri, na nyingine hazikusikika kabisa ingawa picha zilikuwa zinaonekana vizuri -- hasa umati mkubwa wa watu uliokuwapo.

Ingawa wameomba radhi kwa kukatika katika huko, mimi nahisi Channel Ten wamefanya kitu hkii kimakusudi tu, kwani kama tunavyojua msimamo wa Channel Ten kuhusu Chadema, na haswa viongoizi wake wakuu.

Channel Ten -- harakati zenu hizi hazifiki popote -- mpiganaji wetu lazima atinge Ikulu apambane na wamiliki wenu.
 
Ni kweli lakini mtangazaji aliomba msamaha. Post yako inaweza kuwa ya kweli lakini kuiithibitisha baada ya "apology" ni vigumu.
 
MKUTANO MMOJA TU MWALALAMA HIVYO? MLILIPA KIASI GANI ILI MPEWE HIYO FOOTAGE? gari yao mliweka hata mafuta.....? kwa nini mwataka kitu bora huku hamkushiriki katika kukifanya kiwe bora....!
 
Ngoja tuone coverage zao nyingine kuhusu mikutano ya Chadema -- iwapo mtindo uitakuwa ni huu.
 
Katika taarifa yao ya saa moja usiku huu, kituo cha Channel Ten kimeonekana kimewafanyia Chadema uharamia kwa kutoa footage ya mkutano wa chama hicho uliofanyika katika viwanja vya Jangwani iliyokuwa inakatika katika.

Hotuba za viongozi wa Chadema hazikusikika vizuri, na nyingine hazikusikika kabisa ingawa picha zilikuwa zinaonekana vizuri -- hasa umati mkubwa wa watu uliokuwapo.

Ingawa wameomba radhi kwa kukatika katika huko, mimi nahisi Channel Ten wamefanya kitu hkii kimakusudi tu, kwani kama tunavyojua msimamo wa Channel Ten kuhusu Chadema, na haswa viongoizi wake wakuu.

Channel Ten -- harakati zenu hizi hazifiki popote -- mpiganaji wetu lazima atinge Ikulu apambane na wamiliki wenu.

TBC1=ITV=STAR TV=CHANNEL 10=MLIMANI TV
UHURU=MTANZANIA=RAI=THE AFRICAN=NIPASHE=MAJIRA=JAMBO LEO=IJUMAA=IJUMAA WIKIENDA=KIU

TBC FM=RADIO UHURU=CLOUDS=TIMES FM=RFA= RADIO ONE
=
=
=

98% ya Media ya Tanzania ni CORRUPT!
 
TBC ndiyo ilikuwa kituko kabisa walimwonyesha Slaa passoprt siza hata mtu mmoja hakuonekana. Haki ya nani Tido!
 
ni kweli lakini mtangazaji aliomba msamaha. Post yako inaweza kuwa ya kweli lakini kuiithibitisha baada ya "apology" ni vigumu.

hawa ata wake zao wakiomba msamaha wanalala na uchungu jifunze kusamehe na kusahau kama unashindwa kusamehe kwenye tv nyumbani kwako utaweza???sikiliza ndugu akuna alie perfect na hii nikutoka kwa wachungaji sasa kama mkeo anarudia matatizo akirudia utasema hii makusudi walahi anarudi kwao jumatatu na jumapili akikaa sijui mtabaki mlihudhuria arusi jifunze kusamehe
godbless u
 
hicho ni chombo binafsi.....waalike,walipie usafiri na posho za kujikimu uone kama hawatacover unachotaka.........ZILE PESA ZA CHANGIA CHADEMA HAPA NDO MAHALA PAKE ATI........ACHA KULIA LIA LABDA HAKUKUWA NA CHA UMUHIMU KUKIRUSHA
 
nimepotea njia....nilidhani niko kule kwenye TBC 1 THREAD........
 
MKUTANO MMOJA TU MWALALAMA HIVYO? MLILIPA KIASI GANI ILI MPEWE HIYO FOOTAGE? gari yao mliweka hata mafuta.....? kwa nini mwataka kitu bora huku hamkushiriki katika kukifanya kiwe bora....![/QUOTE]

...duuu hata kama mtu akiwa mpuuzi anatakiwa afiche kidogo watu wasijuwe???? sidhani kama watoto wako au watu wanaokuheshimu wanaweza kuamini maneno haya yamtoka kwako!!!!

kwa kifupi mtu alazimishwi kufungua televisheni au media ....ila akishafungua kinakuwa chombo cha jamii.......kinachotakiwa kubalance story .........sio msaada bali wanalazimika kutoa habari zenye ubora!!
 
hicho ni chombo binafsi.....waalike,walipie usafiri na posho za kujikimu uone kama hawatacover unachotaka.........ZILE PESA ZA CHANGIA CHADEMA HAPA NDO MAHALA PAKE ATI........ACHA KULIA LIA LABDA HAKUKUWA NA CHA UMUHIMU KUKIRUSHA

Kama hakukuwa na kitu muhimu cha kurusha, kwanini waliingiza coverage ya huo mkutano kwenye news cast yao? Naona tunaingiza hoja nyingine ambazo hazina mashiko.
 
hicho ni chombo binafsi.....waalike,walipie usafiri na posho za kujikimu uone kama hawatacover unachotaka.........ZILE PESA ZA CHANGIA CHADEMA HAPA NDO MAHALA PAKE ATI........ACHA KULIA LIA LABDA HAKUKUWA NA CHA UMUHIMU KUKIRUSHA

Je TBC1 ni chombo binafsi kuuanzia Tido Mhando alipoletwa pale?. Kodi za watanzania mbona ndiyo bado zinatumila kuiendeshe? CCM wanalipia hapo TBC1 ndiyo habari zao zinarushwa kamili. Je Lowasa na Kikwete nao wanatolewa pasipoti TBC1 kama alivyototewa Dr. Slaa?.
 
kuna comment za watu zimetolewa hapo juu.... kuwa ukitaka coverage kwenye habari (news) lazima ulipie zimenifanya nifikiri mara mbili kama nilikuwa JF au ..... ngoja nisiseme kwa sasa.

News ni news ... haiitaji kulipia ili ioneshwe, yaani kama TV ikiamua kuonesha habari ya ajali pale daraja la wami, hakuna mtu yeyote aliyepata ajali atahitajika kulipia ili watu wa TV waoneshe hiyo habari.

TV zinapimwa kwa vitu gani zinavipa kipaumbele wakati wa matangazo ya habari (ambazo nyingi kama sio zote) bure na ambazo haziitishi malipo toka kwa wahusika ili zioneshwe. Kama TV itaonesha watoto wa mnata wakicheza chandimu wakati kuna habari kubwa (kama ya ajali ya MV Bukoba) imetokea, basi ujue kuna jambo kwenye waamuzi wa habari zipi zitangazwe.

BTW, TV nyingi zinatumia airwaves za public (zinahitaji ruhusa ya serikali kufanya hivyo) hapo Tanzania. Huwezi kuziita 100% private. Ndio maana hawawezi kuonesha ngono kwenye TV maana watafungiwa (kama vile magazeti yanavyofungiwa).
 
hicho ni chombo binafsi.....waalike,walipie usafiri na posho za kujikimu uone kama hawatacover unachotaka.........ZILE PESA ZA CHANGIA CHADEMA HAPA NDO MAHALA PAKE ATI........ACHA KULIA LIA LABDA HAKUKUWA NA CHA UMUHIMU KUKIRUSHA

Hapana, mojawapo ya masharti ya kupata leseni ya utangazaji ni kutoa habari ambazo haziko biased. Ni makosa kutumia leseni ya utangazaji kutangaza habari ulizolipiwa, ndiyo maana kipindi fulani kulikuwa na mgogoro baina ya Mbunge Malima na Mfanya Biashara Mengi kutokana na madai kuwa ITV ilikuwa inaonyesha habari nyingi zinazomhusu Mengi tu badala ya zile za kitaifa.
 
Wewe MAHESABU ni bora utoe picha ya Nyerere kwenye utambulisho wako, maneno yako ni kejeli na fedheha kwa hiyo picha, hata umri wako haukuruhusu kuwa na maneno ya namna hiyo-
 
This is 21st centuary, hao jamaa wa vyombo vya habari vya kifisadi, wasitake kufikiri kwamba wanaweza kuzuia information kwa mtindo huo wa kizamani.

You corrupted media people, you need to know that you can fool people once but not twice in such type of arogant behaviors.

When you feed your stomach with corrupted practices, you need to ask whether your childrens and grandchildrens will be able to do so and what future of the nation are you building.
 
Mimi nilishawashtukia Channel Ten, coverage ya Dr. Slaa ni ndogo sana kiasi kuwa inashangaza, Nilikuwa mmoja wa watu wanopendelea kuangalia News Editions zao hasa saa moja Usiku lakini sasa hivi Bora Niangalie Katuni. Sijawahi kuona chombo cha habari ambacho kinatoa coverage kubwa ya uteuzi wa madiwani na kuacha habari za Wagombea Urais. Anyway, "TIME WILL TELL"
 
MKUTANO MMOJA TU MWALALAMA HIVYO? MLILIPA KIASI GANI ILI MPEWE HIYO FOOTAGE? gari yao mliweka hata mafuta.....? kwa nini mwataka kitu bora huku hamkushiriki katika kukifanya kiwe bora....!

DO, wapambe mna nguvu kuliko wenye mali
 
Back
Top Bottom