Channel 10 wametishwa na serikali kuhusu kipindi maalumu cha Mwangosi

Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
12,013
10,167
Channel 10 siku kadhaa zilizopita walitangaza kwamba siku ya jumamosi ambayo ni leo majira ya saa 2 usiku watakuwa na kipindi maalumu kuhusu mauaji ya mwandishi wa habari Iringa, ajabu mida hii wanaonyesha kipindi cha bongo fleva hapa sijui inamaanisha nini tena au SERIKALI IMEWAPIGA MKWARA?
 
Ao wadhamini wa kipindi kaka,kuwa na subira ndo tunaweka sawa mambo apa kuanza rasmi tamthilia yetu ya mwango
 
Wasipoweka, tutajua wamemsaliti mwenzao. Hakuna kesi iliyokuwa mahakamani, hoja hakuna na kama Tume, nao wangekaa chini kufuatilia kama sisi
 
Kipindi kilichoko hewani ni 'Kutoka Zanzibar'. Tunaomba wahusika watuambie sababu ya kuahirisha kipindi tulichoadiwa. Hata hivyo siku chache zilizopita kulikuwa na link iliyokuwa inaonyesha kupindi hicho.
 
kawaida ya television station zetu hazipendi kukwaruzana na serikali ,sijui kama watarusha hicho kipindi huenda wakasema kinahatarisha usalama wa nchi tusubiri tuone....
 
Nilikaa nasubiri kwa hamu kipindi hiki! Channnel 10 wameniangusha.
Walipaswa hata kutoa taarifa kwamba kipindi kimeahirishwa na kwa sababu zipi!!
 
Mbona tulikiona tayari kwenye You Tube! Kuna mwana JF alitupia humu link za mahojiano hayo mapema katikati ya wiki.
 
Hawa channel 10 wasitufanye sisi watoto tokea saa moja niko kwenye kideo
 
nimekisubiri kipindi hicho kwa hamu...nikaishia kusikiliza majadiliano ya mpira wa miguu...nikachoka kabisa.
 
Kweli wamekosea kubadilisha kipindi bila taarifa, lakini yote hii inaweza kuisha kama wakitoa taarifa na kukiweka/kukirusha Kipindi Maalum, otherwise watakuwa:
-Wasaliti kwa D.Mwangosi(R.I.P)
-Hawana Utu kwa familia ya D.Mwangosi(R.I.P)
-Dharau kwa watazamaji wake.

Anyway, tuwe na subira tuone itakuwaje.
 
kila siku mwenyekiti wa chadema anasema "WATANZANIA ACHENI UOGA WA KUONGEA KILE MNACHOKIAMINI KUWA KINA UKWELI, WATANZANIA ACHENI WOGA WA KUDAI HAKI ZENU"
 
Kipindi chenyewe kilisharushwa tangia juzi yalikuwa ni mazungumzano ya Nchimbi na waandishi wa habari humo ndo aliunda kamati baadae katibu wake kasema ni kamati. Tz bwana mi sijui kama jina ndo lina maana kuliko kazi za kamati au tume. Haya ndo hivo poleni kama umeme ulikuwa umekatika maana ni uhalisia wetu
 
Namwona mzee wa upako lusekelo akitaja namba za m-pesa,tigo pesa,airtel maney na namba za nbc waumini wa2me sadaka
kipindi nadhani hakuna
 
Mbona tulikiona tayari kwenye You Tube! Kuna mwana JF alitupia humu link za mahojiano hayo mapema katikati ya wiki.

Hicho walirusha sawa lakini wakawa wanatangaza usikose kipindi maalumu siku ya jumamosi saa 2 which means ni kipindi ambacho ni exclusive na watu tukaweka reminder kabisa kwenye simu zetu tusisahau ajabu kufika saa 2 kipindi kilichokuwepo ni mafanikio ya ujenzi wa barabara ya kusini, mara bongo flava na mara kutoka zanzibar, unless kama wana channel two kama TBC
 
Kipindi chenyewe kilisharushwa tangia juzi yalikuwa ni mazungumzano ya Nchimbi na waandishi wa habari humo ndo aliunda kamati baadae katibu wake kasema ni kamati. Tz bwana mi sijui kama jina ndo lina maana kuliko kazi za kamati au tume. Haya ndo hivo poleni kama umeme ulikuwa umekatika maana ni uhalisia wetu

Walitangaza kwa msisitizo kwamba tusikose kipindi maalumu siku ya jumamosi saa 2 hivyo vyote nimeviona na kwa jinsi walivyokinadi hicho kipindi maalumu watu walitegemea kuna mambo mengi mazito ambayo hayawa covered, kuwasha TV ndio hivyo tena bongo fleva na kutoka zanzibar
 
Back
Top Bottom