Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,319
- 33,125
Burhani Yakub,
Tanga
SERIKALI imesema katika kipindi cha miaka mitano
ijayo, Serikali yake itaelekeza nguvu zake kupambana na tatizo la kansa ya shingo ya kizazi ili kuokoa vifo vingi kwa wanawake.
Hayo yalisemwa na Rais Jakaya Kikwete wakti akitoa ahadi hiyo jana alipokuwa akizungumza na wakazi wa Jiji la Tanga wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mkwakwani.
Alisema kutokana na kansa ya shingo ya kizazi kwa kuwa ni tatizo kubwa, Serikali imeamua kuelekeza nguvu zake katika
kutafuta chanjo ya uhakika ili kuonda kabisa tatizo hilo.
Chanjo ya kansa ya shingo ipo,katika nchi za wenzetu,hivyo na sisitumeona hatuwezi kuachia wanawake wazidi kuteketea tutaifuata iliko ili tatizo hilo baadaye liweze kutoweka nchini,alisema Kikwete.
Alisema matayarisho ya kutoa chanjo hiyo, imeanza na kwamba ifikapo mwakani wanawake wataanza kuchanjwa ili wasiweze kupata maradhi hayo.
Rais Kikwete alidokeza kuwa Serikali imejenga maabara kubwa na ya kisasa katika hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo ambayo ina uwezo wa kupima aina mbalimbali za magonjwa.
Maabara ya Bombo ni kubwa na ya kisasa yenye uwezo wa kupima magonjwa mbalimbali,alisema.
Alisema maabara hiyo imetolewa kwa msaada wa taaisi ya ABBOT ya Marekani na Serikali kuamua ijengwe katika Hosptaliya Bombo.
Kuhusu ugonjwa wa malaria, Rais Kikwete alisema tayari serikali imepokea idadi ya vyandarua 14,000,000 na
kwamba itahakikisha kila kaya inapewa ili kutokomeza ugonjwa wa
malaria.
chanzo : Serikali kutafuta dawa ya kansa ya kizazi