Elections 2010 Changia kesi dhidi ya Mahanga vs Mpendazoe

Hivi bado ipo ile sheria sijui ukitaka kupinga matokeo ya ubunge unatakiwa kuweka dhamana ya shilingi milioni 15?

Naomba kuelimishwa
Bado ipo na ndiyo inayosumbua. Na inatakiwa kulipwa ndani ya siku 14 tangu mlalamikaji anapokabidhiwa gharama za kesi. Hapo ndo kununua haki!
 
tutachangia sana tu, pia naomba siku kesi ikianza utuambie ila tuweze kuhudhuria kwa wingi.

mabadiliko lazima...
 
Bwana Quality na wengine ambao wanaweza kututumia mchanganuo ufuatao utatusaidi wengine tulio nje ya Tz kuweza kuwakilisha michango yetu pia.

BANK NAME:
BANK ADDRESS:
ACCOUNT NAME:
SWIFT CODE:
ACCOUNT NUMBER, ACCOUNT TYPE
ROUTING NUMBER & BRANCH NUMBER
Na kama kuna IBAN itasaidia pia japo kuwa nashaka kuwa Tz huwa hatutumii IBAN as such.
Kwa kifupi maelekezo ya kutosha kumwezesha mtu kutuma pesa moja kwa moja kwenye akaunti kutoka nje ya Tz.

Aluta continua...
 
Umenena kaka japo haukubisha hodi, weka full mapambano sio lazima yaanzie home...we all Mpendazoe love you....Go hommie mpaka kieleweke man...
 
Nashukuru kwa kunikaribisha jamvini wana JF japokuwa sikubisha hodi.
Ni matumaini yangu kuwa kutokana na jamvi hili nchi yetu ya Tz itaweka historia ambayo vizazi vijavyo vitaithamini na kuienzi.
Tutaendeleza mapambano ndani ya jamvi na zaidi zaidi tunakoishi ili kuhakikisha kizazi chetu hiki hakipiti kabla tanzania yenye neema kupatikana.
ANY
 
Hakuna ujambazi unaozidi aliyeiba kura halali za watanzania, na anajiona sio mwizi. anataka watu wenye vichwa-zero kama wewe ili wawatawale maisha yao yote!

Kama unashindwa kutambua kuwa Mpendazoe kawekwa ktk target tu ya kwamba anatumia gari 'inayohisiwa ya wizi' kama njama za hao manyang'au, wezi wa kura ambao wameiba ubunge wa Segerea na wanaogopa kesi iliyo mahakamani.
Utambue kuwa dawa ya moto ni moto. Ujanja wa kutumia polisi ili kuyumbisha upatikanaji wa haki ni kufillisika. Ndio CCM ipo hapo.

Fred tutamchangia, jimbo litarudi kwa washindi halali, na huyo 'naibu waziri' feki na fisadi wa elimu atarudi mtaani kumiliki baa zake alojenga kwa kukwapua viwanja vya wazi na maeneo ya kuchezea watoto.

Inatia hasira sana kuona mijitu inatetea uozo na hawana fikra halisi.
Well said bro/sisy,magazeti ya leo yamereport kuwa polisi imemsafisha mpendazoe ni baada ya kumsingizia gari la wizi.hii ina maana ilikuwa ni mbinu chafu inayotumiwa na mpinzani wake kumpunguza nguvu ila atashindwa tu na unaibu waziri ataucheua
 
Wansoga wa JF wengine haswa wale wapenzi wa Chadema, mara zingine ukiwaambia kupeleka malalamiko yao mahakamani, husema hawana imani na mahakama za Tanzania, kwa nini? kwa sababu serikali ni ya CCM! Sasa hapa naona wengine, au sijui ndio haohao, wanataka mchango wa kesi. Sasa hiyo kesi wataifungulia mahakama ipi? au dili hii?
 
Changia kesi dhidi ya Mahanga vs Mpendazoe ?

Kichwa kiko sawa hiki? Unachangia kesi dhidi ya Mahanga vs Mpendazoe ? Ina maana kuna hii kesi ya Mahanga vs Mpendazoe, halafu kuna mchango kwa ajili ya kesi dhidi ya kesi hii?

Nikisoma maelezo ya post na kichwa naona haviendani.
 
Sijasikia kesi pale Sumbawanga mjini - yule Mwalimu wa Chadema walimchakachua kweli kweli - kuna nafasi kubwa ya kushinda kesi na uchaguzi ukirudiwa. Au wamemalizana kimyakimya!
 
tutachangia sana tu, pia naomba siku kesi ikianza utuambie ila tuweze kuhudhuria kwa wingi.

Mabadiliko lazima...

i will inform all of you through jamii forum. Nafuatilia kwa karibu sana kesi hii na zingine
 
Wansoga wa JF wengine haswa wale wapenzi wa Chadema, mara zingine ukiwaambia kupeleka malalamiko yao mahakamani, husema hawana imani na mahakama za Tanzania, kwa nini? kwa sababu serikali ni ya CCM! Sasa hapa naona wengine, au sijui ndio haohao, wanataka mchango wa kesi. Sasa hiyo kesi wataifungulia mahakama ipi? au dili hii?

hakuna nia nyingine ya shughulikia suala hili bila kwenda mahakamani. ziko na kesi nyingine zimefunguliwa za wabunge na madiwani.

Halafu suala la dili linatoka wapi? Inaelekea hata magazeti hausomi maana hii kesi ilikuwa magezetini hivi karibuni.
 
Bwana Quality na wengine ambao wanaweza kututumia mchanganuo ufuatao utatusaidi wengine tulio nje ya Tz kuweza kuwakilisha michango yetu pia.

BANK NAME:
BANK ADDRESS:
ACCOUNT NAME:
SWIFT CODE:
ACCOUNT NUMBER, ACCOUNT TYPE
ROUTING NUMBER & BRANCH NUMBER
Na kama kuna IBAN itasaidia pia japo kuwa nashaka kuwa Tz huwa hatutumii IBAN as such.
Kwa kifupi maelekezo ya kutosha kumwezesha mtu kutuma pesa moja kwa moja kwenye akaunti kutoka nje ya Tz.

Aluta continua...

Nitakutumia mara baada ya kupata info toka kwa Mpendazoe mwenyewe
 
hakuna nia nyingine ya shughulikia suala hili bila kwenda mahakamani. ziko na kesi nyingine zimefunguliwa za wabunge na madiwani.

Halafu suala la dili linatoka wapi? Inaelekea hata magazeti hausomi maana hii kesi ilikuwa magezetini hivi karibuni.

Sasa kama mahakama zipo, na hao majaji wanateuliwa na Rais ambae mnasema hakuchaguliwa kwa haki, nashindwa hata kuwaelewa, contradictions tupu. Hamjuwi mlifanyalo mnatapa-tapa kama wafa maji.

Ushauri: kama mnaikubali mahakama basi mkubali na matokeo ya uchaguzi, msipoteze wakati. Mlikuwa na wasimamizi vituoni, hamuwaamini? Na ikiwa hata hao wasimamizi wenu hamuwa amini, ni kweli mtaweza kukubali hukumu zitazotolewa na mahakama ambayo majaji wake wanateuliwa na Rais msiemkubali? Hamueleweki.

Wacheni Jazba, nendeni bungeni mkachape kazi, jifunzeni kwa wenzenu wa CUF, walijaribu mbinu zote hizo, matokeo, kuvunjika kwa amani. Walipoamuwa kukaa chini na kusikilizana, na JMK ni msikivu, wakakubaliana yakaisha na sasa wanakula matunda ya uhuru.
 
Huyu Mpendazoe alimuiga Augustine Mrema, akapiga kelele bungeni, akajitoa CCM akifikiri atagombea urais Chama cha Jamii matokeo yake kajikuta anahangaika, siasa hesabu. Asingejitoa CCM leo si angeendelea kuwa mbunge, mwacheni aendelee kuumia

Mijitu mingine, nyoo kama huna la kusema si unyamae
 
Mimi niko safarini, nikitia timu kesho nitachanga kupitia tigo Pesa, tuko pamoja mpaka kieleweke
 
wewe kama nani? Au unataka tukuchangie wewe?

Emma hujaambiwa wewe, tumeambiwa sisi wapenda haki na mabadiliko, binafsi nakufahamu tena ulikuwa mmoja wa mawakala wa sisiem jimboni segerea katika uchaguzi huu.
 
Ahsante kwa maneno yako mazuri. Taarifa hii ni ile ile iliyokuwa katika gazeti la Tanzania Daima Uk 3. So haunichangii mimi. Lakini unaweza kumpigia katika simu zilizoko katika gazeti na kupata maelezo zaidi. Ahsante sana

Quality tuko mbali na magazeti tuwekee hizo namba za simu...hao wasiochanga labda wanatafuta bado kazi....lakini usiwe nao na hasira wewe tupatie taarifa na siku nao wakikwama watakuja humu tutawasaidia..ni wakuwaonea huruma
 
Back
Top Bottom