Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHANGIA JF: Mkono mtupu haulambwi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sikonge, Jan 9, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,294
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 48
  Wana JF,

  Kwa maana hii mchango na mimi mwaka huu naanza kuchangia.
  Invisible nilikuahidi kuwa ntaleta mchango wangu mwenyewe nikiwa Dar ila naona sintaweza au nikaja mwisho wa mwaka. Pesa kidogo tayari zipo Dar na hapo Sister wangu atakuleteeni. Unaweza kunitumia anwani yenu na nani wa kumuona ili akija akupatieni hako kamchango kiduchu!!!Niandikie kwenye PM.

  NB:- Mods, baadaye waweza zichanganya na ile ya Kichuguu.

  Quote:
  Napenda kuapa kuwa JF ni forum ambayo inaendeshwa vizuri sana. Admin wa JF ana-respond kwa kila ombi in time. Kukitokea out-of-direction thread, anaishugulikia ipasavyo kabla hijawa kero kwa forum nzima. Ilivyofika wakati wa kipindi cha holidays ali-respond vizuri tukawa na skin ya Chrsimas halafu ikaja skin ya New Year na leo skin yetu ya Tanzania Tanzania Nakupenda kwa Moyo Wote imerudi tena. Nahisi amejenga system nzuri sana kwa kutumia OOP akaweka na objetcs nzuri sana kiasi kuwa haoni ugumu kubadili mambo ikiwa lazima.

  Kwa vyovyote vile, ameweka muda wake mwingi ili kuifanya JF iwe sehemu nzuri ya mtu kutumia muda wake hata kama hupendezwi na yanayoongelewa. Mod anastahili pongezi nyingi sana.
   
  Last edited: Oct 3, 2009
 2. m

  msabato masalia JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 121
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 16
  Sina wasi wasi na JF.Ongera ya maneno haitoshi.Binafsi ndo nimekuja huku kupiga boksi,nikisimama mchango wangu utafika.Hii ni sehemu ambayo unaweza dhani uko pale sinza Corner bar unaongea na washikaji.You really feel to be home though you're away.
  Thank you JF.
   
 3. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,294
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 48
  Kweli kabisa Msabato,
  Na unaanzia kuanzia dola kumi kwa mwaka, na kuendelea. Ukitoa hata ...... kwa mwaka ni nyongeza kubwa sana katika kuweka Tbites kadhaa ndani ya Hard disc ya JF, maana kila tunavyoandika, viaenda kutunzwa sehemu na hiyo inabidi isiwe moja maaja ikianguka moja basi ipo ya akiba. Hii shule imenifungua mengi na kunikutanisha na wengi. Humu tumeshakuwa jamii moja kubwa sana. Ila wanasema "hakuna mtu atakupa ugali wa bure". Tujipigepige hivyohivyo na tuwasaidie wenzetu. Ikifika sehemu waweze kusimama wenyewe kwa matagazo ya biashara, hapo tunaweza kusema sasa endelea mwenyewe. Penye nia pana njia, zitapatikana tu.
   
 4. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #4
  Jan 9, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,667
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 63
  Mkuu wangu Sikonge,

  Ukweli ni kuwa siku za nyuma tulijaribu sana kuwafahamisha members kuwa JF haiendeshwi kwa fedha za watu flani bali kwa kujitolea.

  Tukatanabaisha wazi kuwa wanachama na wote wenye mapenzi mema inabidi watambue kuwa tuna mzigo mkubwa wa kubeba kwa niaba yao.

  Nyakati hizo tulikuwa na wanachama waliojisajili karibia 2,000 hivi na tukasema endapo kila mwanachama (aliyejisajili) angechangia Tshs 10,000/= basi ilimaanisha kuwa tungepata Tshs 20,000,000/= ambayo kwa wakati huo ingetosheleza kuiendesha JF kwa karibia mwaka mzima bila wasiwasi.

  Maisha yakabadilika, Server tuliyokuwa nayo ilikuwa ndogo sana kumbe kulinganisha na uhitaji wa watanzania, balaa lilionekana wazi Mwezi Februari 2008 pale Mhe. Lowassa alipokuwa akijieleza Bungeni... Server ikachemsha kubeba mzigo mkubwa.

  Kwa wakati huo tukaona ni vema tukaangalia namna ya kuweza kuwashirikisha wanachama juu ya ugumu tunaokumbana nao... Tukalazimika kununua server kubwa zaidi mbili na zenye back up za kila baada ya masaa 6 kwa nyakati tofauti.

  Hilo likasaidia japo kwa gharama ambazo zilitoka mfukoni mwa mwanachama mmoja! Ndiyo, kulipia server hizo kila mwezi ni $940 na ameendelea kufanya hivyo kwa imani kuwa kuna siku mambo yataenda sawa.

  JF inahitaji SANA michango ya watanzania na wote wenye mapenzi mema.

  Kuna wanachama ambao humu mnawaona wana usernames ambazo ni bolded, hawa ni Premium Members. Hawa walau wamechangia kwa kiwango cha kuanzia $5 na wawili walau $300 tangu JF inaanzishwa mwaka 2006 (ikijulikana kama JamboForums).

  Tangu JF inaanza (2006) mpaka sasa Januari 9, 2009, tumekwishapokea jumla ya US$ 1,450/= toka kwa wanachama waliojisajili na wasiojisajili.

  Wengi wa waliohitaji kuchangia walikuwa wanatuma barua pepe nasi tunawapa maelekezo juu ya namna ya kutufikishia michango hiyo.

  Ukweli ni kwamba kwa wasio wanachama wa JF wakiwa wanasoma hapa wanaona matangazo mengi ya Google kuliko wanachama waliojisajili.

  Dhamira yetu si kuweka matangazo haya ya Google kwani hayaingizi kwa kiwango kikubwa hivyo, watu hawabonyezi matangazo hayo na hivyo income yake inategemea pale mtu atakapokosea akabonyeza tangazo ndipo tupate vijisenti kidogo kwa clicks hizo. Gharama za uendeshaji bado zinatoka mfukoni mwa mtu mmoja mpaka sasa na baadhi ya Premium Members ambao wameendelea kuona umuhimu wa kufanya hivyo.

  Mpaka sasa JF ina wanachama waliojisajili zaidi ya 35,000. Endapo waliojili hawa wangechangia walau Tshs 10,000/= kwa mwaka basi inamaanisha JF ingetengeneza Tshs 350,000,000/= kwa mwaka na hivyo tusingeweka matangazo KABISA na tungejitahidi kupata moderators ambao watakuwa wanalipwa kwa kazi yao na wangeifanya kwa umakini mkubwa zaidi.

  Ukiangalia katika historia ya Forums nyingi, huwa zinashindwa kuhimili traffic inapokuwa kubwa kutokana na servers kuhitaji umakini zaidi na Forum owners hujikuta wanaona ni mzigo usio na faida hivyo forums hizo kufa.

  Tumshukuru Maxence kwa kuendelea kulipia gharama hizi kila mwezi kwa kujitolea mpaka sasa huku akilipia na Chat Server (IRC Server).

  Wapo wanachama kama Ogah, Nyambala, SteveD, FairPlayer, Mchukia Fisadi na Phillemon Mikael ambao huchangia walau kila wanapopata wasaa... Hawa nao wamesaidia kwa kiwango kikubwa katika jitihada za kuhakikisha JF inakuwa hewani. Bila kuwasahau wadau waliochangia walau $200 hivi initially kama Mtanzania, Field Marshal ES na Halisi.

  Ninachoamini binafsi ni kitu kimoja, Tshs 5,000/= kwa mwaka (12months, walau 450 kwa mwezi) inawezekana kabisa kwa watanzania tulio na uwezo wa kuingia mtandaoni. Na uzuri, benki zetu Tanzania zinaruhusu mtu ku-deposit Tshs 5,000/= kama kiwango cha chini.

  Endapo kuna mwanachama anaguswa (kutoka moyoni) na angependa kuiwezesha JF kuendelea kusimama imara na kufanya vema zaidi bila mizengwe ya kifedha, basi anaweza kukubali kuchangia Tshs 5,000/= walau kwa mwaka.

  Benki zetu (hapa naongelea walau NBC na CRDB kwa haraka) hazikulazimishi unayetuma hela kuandika jina lako la kweli bali lile ambalo ungependa mpokeaji alitambue.

  Kwa walio Tanzania wanaweza kuichangia JF kwa kutuma katika akaunti za NBC au CRDB.

  Akaunti ambazo tangu awali tulipendekeza zitumiwe ni za Maxence Melo (as the JF Founder) na tukawaomba wanaotuma waandike Nicks za kuweza kutanabaisha kuwa wao ndio walotuma.

  =================================

  Michango inaweza kutumwa kwa njia kuu nne:

  1. Paypal users:

  Details will follow

  2. Njia ya pili ni kutumia Western Union au Money Gram na kutuma kwenda kwa Maxence Melo Mubyazi wa Dar es Salaam.

  3. Njia ya tatu ni kutumia Bank accounts za Maxence kama ifuatavyo:

  CRDB:

  Account Name: Maxence Melo Mubyazi
  Bank: CRDB Pugu Road Branch
  Swift Code: CORUTZTZ
  Acc No: 01J2092391800

  4. Njia ya nne:

  Unaweza kutuma recharge vouchers za tiGO, Zain, VodaCom au Zantel au ZAP (0784526444), M-PESA (0755642929), tiGO PESA, Z-PESA n.k kwenda kwa Maxence - 0713444649 naye atakufahamisha kuwa kazipokea. Namba za ZAP, M-PESA na Z-PESA anaweza kukupa ukiwasiliana naye.

  =================================

  Ikumbukwe, SI LAZIMA kuandika jina lako la kweli na SI LAZIMA kwenda mwenyewe bank kutuma pesa hizo (kwani unaweza kumpa unayemwamini na kumpa account details na jina lako ambalo ungependa aandike).

  Tunaweza kuandika mengi lakini ukweli unabakia pale kuwa JF inahitaji michango yenu kwa sana tu.

  Kwa wenye maswali zaidi wanaweza kuwasiliana na Maxence kupitia namba yake ya simu +255713444649.

  Nasikitika kuwa yawezekana hata hivi natembeza bakuli :)
   
 5. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,146
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wadau na wapenzi wote wa JF.....! Heshima mbele!

  Wakuu mbona haka kathread tunakasahau sana? Tunalipenda jamvi sana kwa sababu mbalimbali (sitaki kuzieleza, hope kila mmoja anazifahamu), lakini founders wa hii kitu wanaumia sana kuhakikisha jamvi linakuwa hai katika hali tunayoifurahia. Wanaumia,techinically and financially wakuu!

  Sisi wadau wengine tunaweza tukashindwa kusaidia technically directly but we can do that financially...na kwa maoni yangu silazima uchangie mamilioni wakati huna uwezo wakufanya hivyo, kila mmoja wetu (members) ambao ni registered akitoa Tshs 1,000..kwa mwaka, tunaweza kufanya makubwa kwa kuwasaidia kina Robot na founders wengine kutuboreshea zaidi jukwaa hili kwa manufaa yetu sote!

  I hope hakuna mtu angependa kusikia ati anaamka asubuhi kujaribu kupata breaking news hapa JF au kasikia tetesi sehemu fulani anataka kuja apate uthibitisho hapa ....unaambiwa the web you are browsing is not found....yaani JF haiko hewani.....! No one will like this to happen! But nina uhakika kama hatuisupport JF one day hii kitu itafungwa kabisa!

  Kwa hiyo wandugu kwa wote wenye mapenzi mema na JF pamoja na nchi hii, let us join our hands...tuchangie JF kwa moyo wote!

  Admin please wakumbusheni members hali halisi ya gharama za kuiendesha JF na umuhimu wa michango yao! Ningeshauri pia, mngewajulisha members direct costs za kuimanage JF kwa mwaka...then labda tufungue thread special kwaajili ya members kuweka Pledges zao za hali na mali zitakazowezesha atleast kucover direct running costs za JF kwa mwaka!

  Kwa kuanzia kule VIP mimi nimeahidi kuirusha kwa Max Tshs 30,000 wiki ijayo.....so wadau mnaweza endeleza hapo!

  Cheers!
   
 6. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,208
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 36
  Nashangaa sasa limekuwa jukwa la kutukana matusi na kuwakashifu waislamu mtindo mmoja na hatuwa hazichukuliwi kwa wahusika au ndo wenye jukwaa hao?
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,187
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Usiharibu thread tfadhali.....hapa sisi tunataka michango kunusuru JF...malalamiko yako si hapa...andikia mods! Hapa tupishe...
   
 8. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #8
  May 20, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,146
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkuu Junius, kwanza kabisa kumbuka kuwa umeweza kuandika ulichoandika kwa sababu tu kuna watu wamekuwezesha kufanya hivyo hapa JF.....! Sasa kama unataka uendelea kuwezeshwa kufanya hivyo, please tunaomba pledge yako ya hiari kuisaidia JF kuwa hewani!

  Pili, ungeweza kutoa dukuduku zako kule kwenye compaints na ungesaidiwa vizuri sana mkuu! Hii thread ni kwa ajili ya fund raising na kutoa maoni ya jinsi ya kuiwezesha JF ijiendeshe mkuu!
   
 9. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2009
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 3,360
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 48
  Kuna wakati kama vile speed ya wanajamii kuchangia ilikuwa inaridhisha. Lakini ghafla kumekuwa na kuzorota tena kwa muda mrefu sasa.

  Ninafahamu kwamba mchangiaji/mwendashaji mkuu (90%) wa JF ni mmoja tu. Sisi wanachama zaidi ya 5000, mpaka leo waliochangia hawazidi hata 50! Chini ya asilimia moja!

  Inasikitisha. Kama sisi ndio wasomi, tena wenye uelewa wa hali ya juu, na kipato fulani, tunashindwa kusaidiana mzigo huu wa kifedha, mmmmhhhh!
   
 10. Ndamwe

  Ndamwe JF-Expert Member

  #10
  May 20, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 16
  Wana JF salaam wote,

  Yaani hii forum mimi inanikuna sana. Naomba nishauriwe kwa kuchangia kwa njia ya euro moja kwa moja, nifanyeje bila ya peleka kwa a/c za CRDB au NBC ambazo zitahitajika gharama zingine za kutuma michango Tanzania. Kama kuna namna ya kuwakilisha mchango kama euro hapa Netherlands moja kwa moja kwa a/c ya JF nifahamishwe.
  Asanteni
  Amandla!
   
 11. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #11
  May 20, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 4,348
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 48
  Mimi naahidi kutoa Tshs 100,000 before 17th June! Ila nahitaji mtu wa kunikumbusha!

  Sii kwamba hatupo tayari kuchangia..sema saa ingine pia tukumbushane mara kwa mara!

  Nakubaliana na utaratibu wa kutoa ahadi..na baadhi yetu basi wafuatilie hizo ahadi through PM!

  Tunawapongeza wote JF kwa kazi nzuri ya kujenga spirit ya uzalendo ktk nchi yetu!
   
 12. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #12
  May 21, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,146
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ubarikiwe sana Mzalendohalisi......! Mkuu don't worry tutakumbushana tu mkuu.......!
   
 13. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #13
  May 21, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,146
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkuu Ndamwe,

  Mungu aendelee kukubariki kwanza kwa kuwa na moyo wa kuchangia JF! Kuhusu namna ya kuchangia, kuna njia nyingi ikiwa ni pamoja na Paypal, debit cards & Credit cards au Western union or Money gram (soma post ya Invisible hapo juu) lakini zaidi ya hayo wadau kina Max watakusaidia, hakuna kisichowezekana duniani siku hizi!

  Cheers
   
 14. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #14
  May 21, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 944
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 28
  Mbona nikisoma Post # 4 naona maelezo yako wazi tu.

  Mimi siahidi, nshatuma Tshs 10,000/= kwa Max kwa njia ya sms. Nitakuwa nachangia kiasi hicho kila mwezi. Naomba msinipe Premium member pls

  Dr.
   
 15. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #15
  May 21, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,542
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 48
  Hata mimi ni victim wa msaada wa Invisible
  Ingawa sijawahi kumuona ila alinisaidia sana kwa kunitafutia watabibu wa technical probe yangu.
  Nimekuwa mchoyo wa fadhila na dhambi inanisuta hapa ila LAZIMA nitafunga mkanda kukatisha mlo wa familia japo kwa siku moja nichangie JF ili wengi wapone

  Shime jamani
   
 16. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #16
  May 21, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,146
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ni kweli mkuu, ila kumbuka wakati mwingine huwa mtu anakuwa busy sana, so anaenda mojakwa moja kwenye last post, zile za mwanzo anakuwa hajazisoma pengine due to time factor etc...so wacha tusaidiana kueleweshwa tu!

  Mkuu hiyo ni ahadi kubwa sana....haba na haba hujaza kibaba 10,000*12=120,000 kwa mwaka! Mungu akubariki sana.....!

  Ni vizuri ukawa identified kama Premium member, ili kwanza kabisa kutoa hamasa na kwa wengine kuchangia chochote ....hata jero (500) kwa mwezi! Pili, itasaidia sana members wengine kujua kuwa JF iko supported na members wenyewe na si fisadi fulani au kampuni fulani au kikundi fulani cha watu, na hivyo kuifanya iwe huru zaidi katika mijadala yake.....where we dare to talk openly..! Hii inawezekana tu kwa kuwa JF iko supported na JF members wenyewe..vinginevyo kungekuwa na masharti mengi sana....na wengi pengine tungekimbia!

  Mods ...please mpeni upremium Dr.
   
 17. senator

  senator JF-Expert Member

  #17
  May 21, 2009
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,937
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 36
  Kauli yako inafanana na jinalo!! Naamini utafanya kweli na watoto wataenda tu msalani..Naahidi Tsh 20,000/- kwa njia SMS
   
 18. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #18
  May 21, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,146
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkuu Senator,

  God bless you....please saidia pia kucampaign na kwa wadau wengine wasaidie jahazi lisizame tukakosa uhondo!

  Mkuu Max, I trust utakuwa unamark sehemu hizi ahadi zote wadau wanatoa hapa, ili iwe rahisi kuzifuatilia...!
   
 19. senator

  senator JF-Expert Member

  #19
  May 21, 2009
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,937
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 36
  Shaka la Hofu Ondoa Next Level utapata updates through Max....Kampeni zitafanyika lakini sio zile za Busanda!!
   
 20. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #20
  May 21, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,468
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 38
  Kama watu mia tukiamka na spirit hii ya kusaida jf nawambia Max hawezi kuwa na kilio kabisa. Tutaendelea kuwafunga pingu mafisadi ingawa wanasema kelele za mlango haziwazuii kulala.
  Nimeshaona zinaanza kuwaamsha na wanakosa usingizi.
   
Thread Status:
Not open for further replies.

Share This Page