Changia CHADEMA Chato ili kukata rufaa ya hukumu ya mwenyekiti wake kufungwa 5 years

Nadhani sii busara kuwa na mtizamo wa aina hii. Lakini pia, hao uliowataja hawahitaji hela za kuchangiwa kulisha matumbo yao. Hivi wewe pia unaishi kwa kuchangiwa kulisha tumbo lako? Yakupasa ukue na uone upeo unaozidi umbali unaokojoa.
 
Kuna mambo mengine viongozi wanatakiwa kuwa makini sana,wananchi wameshakata tamaa vijijini hivyo kiongozi lazima atumie busara zaidi na asiwe na kauli za kuchochea.

Kuna kipindi nilisafiri hadi Bariadi nilikuta kitu kama hiki kimetokea kwa mganga wa kienyeji kuvamiwa usiku na kijiji,ng'ombe 40,magunia ya mahidi 30,20 mpuga pamoja na nyumba kadha wa kadha kuteketezwa japo familia ilinusurika kwa kutoroka kabla ya tukio.

Kisa mganga anazuia mvua kunyesha kijijini,je,hii ndo ilikua adhabu stahili? Katika masuala ambayo katiba haiyatambui ni hili la uchawi/ushirikina na kama unaamini katika ushirikina nawe ni vizuri kumalizana na mbaya wako kwa kishirikina.

Pia la sivyo katiba haitokuacha ukitamba mtaani,suala la chato sijajua chanzo chake lakini kama lilifanyika katika mazingira kama la bariadi tuache jamani sheria ifanye kazi na tusiwe wepesi wa kusema eti hukumu ziko kisiasa,kama chama.

Chadema wahatakiwi kulea mtu wanayeona anavunja sheria na haki za binadamu lakini kama watakumbatia kila mmoja kwa kuitana makamanda ata wakati mnavunja sheria tutakuwa tunakosea sana tunakiua chama chetu ambacho ndo tunaona taa ya kijani imeweka wakati vingine vyote akiwemo Mabwepande wametuwashia taa nyekundu kabisa.
Kwa maelezo haya, basi ni vyema kupata kauli ya msemaji mkuu wa chama. Na mchango uratibiwe na katibu mkuu wa CDM. Hii itakuwa rahisi kunyanyua imani ya wapenzi wa CDM kuhusu hili suala. halafu chama kina mawakili kwa ajili ya kitu kama hiki.
 
Kama mlivyosikia kwenye vyombo vya habari kuwa

MAHAKAMA ya Wilaya ya Chato, mkoani Geita, imemhukumu kifungo cha miaka mitano jela, mwenyekiti wa kijiji cha Minkoto, Alphonce Kanungu (44), na wenzake wawili baada ya kupatikana na hatia ya kuhamasisha vurugu, kuchoma nyumba na kuwakatakata ng’ombe 30 na mbuzi 20 kinyume cha sheria.


Wengine waliohukumiwa kifungo kama hicho ni Marco Elias (36) na Cosmas Kanungu (30) wote wakazi wa kijiji cha Minkoto, kata ya Bwanga.


Habari kutoka Chato zinaeleza kuwa mbali na kifungo hicho, washtakiwa hao wametakiwa kulipa fidia ya sh milioni 38 kwa mlalamikaji, Paul Mhunda.


Akitoa hukumu hiyo mwishoni mwa wiki, Hakimu Khasan Koja alisema ametoa adhabu hiyo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka ukiongozwa na Mwendesha Mashtaka Mkaguzi wa Polisi, Mkwasi Rashid.

Washtakiwa hao walidai kuwa April 3, mwaka huu, majira ya saa 2 usiku waliongoza kundi la wananchi, kwenda kufanya uharibifu mkubwa wa nyumba, mifugo na mali ya Paul Mhunda na kusababisha hasara ya sh milioni 38.

Response

Kwa imani na ushahidi mkubwa kuwa hukumu hii imetolewa kwa kuihusanisha na siasa, wanaharakati na wapenda Chadema wa Chato wameamua kuchanga mchango wa hiari ili kuwezesha kukata rufaa. Hadi hivi sasa tayari mwanasheria amemwandikia hakimu kutoa nakala ya hukumu ndani ya siku kumi ili tuweze kusonga mbele.

Kwa mwenye kuweza kuchangia aliyeko Chato amuone bwana Mange ambaye ni Katibu wa Chadema Chato au mchango kwa M pesa kwa

FAUSTINE KITASANJA - 0753 277741 - Katibu wa Tawi Chato

COSMAS MAKUNE - 0753 945 888 - Mwanaharakati

Appreciation itatolewa kwa wote watakao husika na jumla ya kiasi kilichochangwa kitatajwa kwa wahusika wote.

Asanteni........by Ta Muganyizi - Activist Kagera

poa ngoja
 
Ni huyo aliyeshitaki anatakiwa asikilizwe maelezo yake pia, ili kubalance na kufanya maamuzi ambayo hayatamuonea yeyote.
-Upo uwezekano pia CCM bado inakinyongo na wanaharakati wote wa CDM
-Lakini upo uwezekano pia ukawa mwanaharakati mzuri wa chadema, ila bado una sifa ya kuwa uhalifu
 
Back
Top Bottom